Jumatano, 30 Oktoba 2013

NDOTO NA MAONO.



Friday, June 28, 2013

NDOTO NA MAONO.

Mwl Sospeter Simon S. Ndabagoye
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.


Kama ilivyoandikwa katika (Matendo ya Mitume 2:17)”Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu ,nitawamwagia watu Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto”. LEO TUTAJIFUNZA JUU YA NDOTO NA MAONO.

Dhana ya Ndoto.
Ni picha zinazoambatana na sauti kama sinema ambazo mtu huziona anapokuwa amesinzia. (Mwanzo 28:10-15).
Maono- ni picha ambazo mtu huziona anapokuwa macho yaani akiwa hajasinzia.
Tofauti iliyopo baina ya hivi vitu viwili ni kuwa, kimoja hutokea usingizini wakati kingine hutokea katika hali ya kawaida pasipo kuwa usingizini.
Sifa kuu ya Ndoto na Maono ni kuwa ni Mafumbo. Hii ina maana kwamba, mawasiliano haya ya kiroho huja kwa namna isiyo ya kawaida, hivyo hayawi na tafsiri ya moja kwa moja. (Hesabu 12 :5-8). Aidha, hakuna kanuni maalumu katika kutafta tafsiri zake (Mwanzo 37 :5-7), japo watu wa Mungu wanaweza kufunuliwa maana ya ndoto, kumbuka Yusufu alivyotafsi ndoto akiwa gerezan. izingatiwe kuwa wakati mwingine, ndoto zaidi ya moja,zinaweza kumaanisha kitu kimoja (Mwanzo 41 :1-7,14-16,25-38)
Mfano: Kornelio aliona maono saa tisa mchana (Matendo 10:1-6)
Petro aliona maono saa sita mchana (Matendo 10:9-16)
Paulo aliona maono alipokuwa njiani kwenda Dameski ilikuwa adhuhuri (Matendo 26:12-16)
Musa alipewa maono alipokuwa akichunga kondoo wa mkwewe Yethro mchana (Kutoka 3:1-3)
Hata hivyo, kuota si kwa watu waliookoka tu, bali hata ambao hawajaokoka wanawezakuota ndoto na kuona maono ya kimungu.
Mfano wa watu ambao hawakuwa wacha Mungu lakini waliweza kuota na kuona maono ya kimungu ni kama ifuatavyo:
Farao (Mwanzo 41:1)
Nebukadreza (Daniel 4:4-5)
Mkewe Pilato Mathayo (27:17-19)
Kornelio (Matendo 10:1-4).
Kutokana na Mifano hiyo hapo juu tunaona kuwa,mtu yeyote anaweza kuota na kuona maono ya kimungu.
Tatizo ni namna ya kupata maarifa ya kupambanua au kutafsiri ndoto hiyo au maono hayo. Hapa inatokana na kuwa ndoto au maono hayana jibu moja, na wala si kila ndoto inatoka kwa Mungu. Na hapa ndipo Hosea anapoliasa kanisa juu ya kuwa na maarifa (Hosea 4:6).
AINA ZA NDOTO.
Aina ya ndoto hutegemea chanzo chake.
VYANZO VYA NDOTO NA MAONO.
Kuna vyanzo vikuu vitatu vya ndoto/maono.
(i) Ndoto au maono yatokanayo na nafsi ya mtu mwenyewe.
Hii hutokana na shughuli alizokuwa akizifanya kutwa nzima,hivyo anapoenda kulala,matukio ya siku nzima hujirudia kutokana na picha zilizohifadhiwa katika ubongo wake. (Mhubiri 5:3)
Kwamaana ndoto huja kwasababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya maneno.
Vilevile, mtu anapotafakari kitu kwa muda mrefu. (Isaya 29:8)
Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe anakula ; lakini aamkapo,nafsi yake haina kitu…
(ii) Ndoto au maono yanayotoka kwa shetani.
Ndoto hizi,huambatana na vitisho,hutuondolea amani, kuogofya na kutuacha katika hali ya taharuki ya woga. Ndoto hizi huchosha mwili na akili. (Ayubu 7 :14) Biblia inasema « ndipo unitishapo kwa ndoto,na kunitia hofu kwa maono ».
Hizi ndoto hazitoki kwa Mungu kwa kuwa Mungu kamwe hawezi kutupa ndoto za namna hii (2Timotheo 1 :7) « Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi »

MAKUSUDI YAKE NI NINI ?


Kutupoteza na kutupeleka mbali na neno la Mungu.

(Zaburi 119 :95,Ufunuo2 :20 1Yohana2 :26)
Kutuonea. (Matendo 10 :38)
Kututesa. (1Petro 5:8-9)
Kutushambulia kwa kutumia sura za kutisha. (Ayubu 16:14).
Kuitichafua miili yetu kupitia ndoto za uasherati na uzinzi na mapepo au watu/mizimu Yuda (1:6-8)
Kututisha na kutupa hofu ili tusiendelee.(Ayubu 7:13-15)

(iii) Ndoto au Maono Yanayotoka Kwa Mungu.(Mwanzo 20:3,Kutoka 3:2)

Tofauti ya zile za Shetani, hizi huambatana na amani ya Mungu!hii ni kwa kuwa Mungu ni wa amani wala si wa machafuko. Hivyo, ndoto yoyote unayoona inaleta machafuko,ujue si ya Mungu.

MAKUSUDI YA NDOTO HIZI NI YAPI ?


Mungu, hutumia njia hii kuwasiliana na watu wake. Mawasiliano haya huwa na shabaha anuwai (Ayubu 33 :14-15) kama ifuatavyo :

Kutupa maelekezo (Mathayo 2:13, Matendo 9 :10-12,Mwanzo 20 :3-7)
Kutuonya/Kututahadharisha juu ua hatari (Matahyo 2:12, Mwanzo 31:24)
Kufanya mawasiliano nasi na kutueleza au kutulewesha mambo mbalimbali Mwanzo 28:10-16,1Wafalme 3:5-15)
Kutuondolea mashaka na wasiwasi juu ya jambo ie kutuongoza palipo sahihi.
(Mathayo 1:20,Matendo 16:6-10)
Kumshughulikia mtu ili kuubadiri mwelekeo wake usio sahihi pengine. (Mathayo 27:19)
Hutuonyesha mambo tusiyoyajua kwaajili ya kanisa au sisi binafsi (Ufunuo 1:1)

Namna ya Kupata tafsiri ya Ndoto au Maono yatokanayo na Mungu.

Kama nilivyotangulia kusema, hakuna kanuni maalum wala taaluma inayohusiana na vitu hivi, hivyo kwa kutumia mawazo yetu au hekima zetu wenyewe si rahisi kupata tafsiri sahihi. Tutajidanganya wenyewe na hapo ndipo tunapopaswa kukumbuka (Mwanzo 40:8) Wakamwambia, tumeota ndoto wala hapana awezaye kufasiri.Yusufu akawaambia, kufasiri ndoto si kazi ya Mungu?Tafadhari mniambie.
HATUA KATIKA KUPATA MAJIBU YA NDOTO/MAONO.
1. Mara tu, baada ya maono au ndoto kuisha, muda ule ule, unapaswa kutulia kimya na kutafakairi kwa muda, na hapo ndipo roho wa Mungu anapoweza kutupa maelezo ya maono/ndoto hiyo (Matendo 10:9-20).izingatiwe kuwa si lazima Mungu afanye hivyo kwa muda huo, hivyo endapo hatafanya hivyo, ni vema sasa ufuate hatua ya pili ambayo ni hii ifuatayo.

2. Kumwomba Mungu tafsiri moja kwa moja.

Baada ya kutulia kwa muda,kama hujapata tafsiri, tunapaswa kumwomba Mungu mwenyewe atafsiri (Daniel 2:16-19). Na endapo hatujapata majibu bado, tunapaswa kulala na hata kuisahau ndoto hiyo,hapo Mungu huweza kukuletea ndoto ile ile tena huku akiifafanua kwa namna flani. Anaweza kuleta moja au hata zaidi. Tunapaswa kuwa na subira pia (Mwanzo 41:17-23) kwani pengine, anawezaa kukukumbusha juu ya matukio utakayo yaona katika maisha yako siku zitakazofuata. (Waamuzi 7:7-15)
3. Kuuliza Katika Maono au Ndoto.
Hatua hii, hutumika mara unapokuwa unapewa maono moja kwa moja kutoka kwa wale watu au viumbe wanaokuwa wanakupa ujumbe huo. Mara zote, kiumbe yeyote atakaye kuja kwako, atajitambulisha kuwa yeye ni nani na ametumwa na nani kwako, kisha ndiyo atatoa ujumbe aliotumwa kwako. Kama ni malaika wa Mungu, kwanza atakusalimia kwa salamu ya Usiogope na hapa utajisikia amani sana moyoni mwako (Daniel 10 :19, Luka 1 :13, 30) na endapo utaendela kuogopa kemea kwa jina la Yesu, huyo hatakuwa Malaika. Matokeo ya kukemea yatakuthihirishia kuwa huyo ni nani.
Angalizo ; malaika yeyote atakayetumwa kwako atakapojitambulisha, atakachokwambia utapaswa kukipima kulingana na neno la Mungu. Mfano, akikwambia umechanguliwa kuliko wanawake wote duniani kuwa utamzaa masihi wa Bwana.Lazima ujue kuwa hiyo si kweli, kwani masihi alisha kuzaliwa miaka zaidi ya 2000 iliyopita.

Izingatiwe kuwa, Mungu huweza kutuma ujumbe kwako kupitia malaika wake au watu walio hai wala si watu waliokufa kama vile mitume n.k. mfano, ukisikia mtu anajitambulisha kwako akikwambia kuwa yeye ni Paulo,Ayubu,Bikra Mariam n.k. ujue huo ni ujanja wa shetani anataka akutapeli kwa kukudanganya.

Tahadhari : wakati mwingine unaweza ukatokewa na kiumbe atakayejitambulisha kwako kama « Malkia wa Mbingu » huyu kiumbe alikuwepo tangu enzi zile za nabii Yeremia huko Misri (Yeremia 6 :18 )na kwa kuwa hujitambulisha kama mtakatifu, bais amewapoteza watu wengi wa Mungu kwa kutolijua neno hili. (Yeremia 44 :17-19,25).
Kiumbe huyu ndiye aliye watokea watoto wa Fatma yaani Lusia, Franscis na Yasinta akijitambulisha kuwa yeye ni Bikra Maria na kuwafundisha wasali rozali. Izingatiwe kuwa Yesu, alisha tufundisha namna ya kuomba, kuwa ni kupitia jina lake tu, pia akasema kuwa yeye ni mwanzo na mwisho (Ufunuo 22 :13) hivyo, hatutegemei kusikia mtu mwingine atakaekuja kwa lolote badala yake. Lakujihadhari sana ni kuwa, pepo huyu anauwezo wa kufanya miujiza kama ya Yesu, hivyo ni lazima kuwa makini ili asije akaliteka kanisa.

4. Kutosumbuka tusipopata tafsiri ya Ndoto.

Kama Mungu ametuma ndoto kwako, hakika atakupa na tafsiri yake. Endapo utazingatia vigezo vyote hapo juu bado usipate majibu tulia, Mungu mwenyewe atashughulika na tafsiri ya ndoto hiyo.(Luka 12 :25-26). Hii inatokana na kwamba, ndoto hii inaweza ikawa imetokana na nafsi zetu wenyewe, au shetani au pengine ikawa ni ya muda mrefu sana ujao, hivyo tafsiri yake si ya lazima kwasasa. Lamsingi, tunapaswa kutunza kil akitu kwenye kumbukumbu sahihi. (Habakuki 2 :2-3, Daniel 10 :14)
HITIMISHO.
Tunapaswa kuzipinga ndoto na maono ya kufarakanisha kwani hazitoki kwa Mungu hizo. Shetani ni mfitini, hutumia ndoto na maono ili kutugombanisha. Hapendi aone upendo, amani na ushirikiano baina yetu,hivyo huchukua mwanya wa maono na ndoto kuonesha madhaifu ya wenzetu ili tudhoofishane, tusiaminiane. Tuwaone wenzetu watenda maovu kama vile wachawi,wazinzi,n.k. ili kupanda mbegu ya chuki miongoni mwetu. Ndoto kama hizi tunapaswa kuzitupilia mbali kwani ni za baba wa uongo si za Mungu.Kamwe Mungu hawezi kutuonyesha ubaya wa wengine bali hutuonyesha ubaya wetu wenyewe ili tuweze kutubu (Mithali 6 :16, Yakobo 3 :15-17 ;Daniel 5 :1-6).

Mwl Sospeter Simon S. Ndabagoye

New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.

DALILI ZA KUVAMIWA NA MAPEPO



DALILI ZA KUVAMIWA NA MAPEPO


      


Mapepo ni hali ya utendaji kazi wa shetani.
Ni viumbe wa kiroho wanaomwingia mwanadamu na kumfanyisha au kumsaidia kufanya uovu mbele za MUNGU. Ndugu jichunguze na kama una baadhi ya dalili hizi hapo chini hakikisha unavunja kwa maombi mpango huo wa shetani kwa jina la YESU KRISTO(1 Yohana 3:8b) Kwa kusudi hili MWANA wa MUNGU alidhihilishwa ili azivunje kazi za ibilisi.

DALILI 13 ZA KUVAMIWA NA MAPEPO.

1: Kukosa amani ghafla au kuhisi vitu vinatufanya tuwe na hofu na woga. 2 Timotheo 1:7 ''Maana MUNGU hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.'', na katika 1 yohana 4:18 ''Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo''.

2: Kukosa uhuru wa kufanya tunavyotaka na kulazimishwa kufanya tusiyotaka kutokana na nguvu fulani kutoka ndani mwetu. 

3: Kuota ndoto usiku ambazo hutufanya tuwe na kichwa kizito sana wakati wa kuamka, kuota majitu ya kutisha kwa namna ya kivuli yakitaka kutukaba au kutudhuru.

4: Kukosa usingizi kabisa na akili yetu kufunikwa na mawazo mfululizo.

5: Vitu kutembea mwilini, kuhisi mwili unawaka moto.

6: Kusahau kusiko kwa kawaida na kuwa na uzito kichwani.

7: Kupiga miayo hovyo tena mfululizo tena bila kuchoka chochote.

8: Kuchukia mme/mke bila sababu yoyote.

9: Hali ya kubebeshwa mzigo kichwani ,kifuani,mgongoni au sehemu nyingine lakini mzigo huo hauonekani kwa macho.

10: Kuwa na hali ya kuogopa vitu vidogo vidogo kama kivuli, au kuogopa kuwa pekeyako chumbani, kuogopa kuvuka daraja au barabara.

11: Kukosa uwezo wa kufikiri, kupenda kuongea wakati wote hata ukiwa peke yako na kukosa kusikiliza wengine. Kuwa na hali ya kulewa bila kunywa kileo chochote.
12: Kwa hali isiyo ya kawaida kuona watu wanakuja kufanya uasherati na wewe ndotoni, kuota unapelekwa porini, kunyweshwa madawa ya uganga ndotoni, pia kuota ndoto za watu waliokufa wakifanya mazungumzo na wewe.

13: Kusisimka mwili ghafla na nywele kusimama.
Ayubu 4:15.

''Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama. ''
Ndugu kama una moja ya dalili hizo hakikisha unafanyiwa maombezi na umpokee BWANA YESU maishani mwako ili uwe mbali na uonevu huu wa mapepo ambao ni mawakala wa shetani.  Na katika BIBLIA kitabu cha zaburi 68:20 pia Zaburi 50:15
MUNGU akubariki sana na kama hujaokoka mpokee BWANA YESU leo maana wokovu ni sasa.
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.

WANASAYANSI WASHANGAZWA KUKUTA MAANDISHI YA AMRI KUMI ZA MUNGU KATIKA SAYARI YA MARS YAMEANDIKWA KWA LUGHA 7 TOFAUTI



Wednesday, July 24, 2013

WANASAYANSI WASHANGAZWA KUKUTA MAANDISHI YA AMRI KUMI ZA MUNGU KATIKA SAYARI YA MARS YAMEANDIKWA KWA LUGHA 7 TOFAUTI

 



wanasayansi wa anga za juu wa kampuni ya NASA ya Marekani wameshangazwa na kukuta maandiko ya amri kumi za Mungu na andiko la Yohana 3:16. 

wanasayansi hao waliingia kwenye pango moja kujalibu kutafuta maji na  kukuta maandiko hayo kwenye pango katika sayari ya Mars yakiwa yameandikwa kwenye mawe.
maandishi hayo yaliyoandikwa kawa  lugha 7 tofauti nazo ni English, Spanish, Chinese, Basque Hebrew na lugha yingine hazikutambulika.


wanasayansi hao wameshangwazwa na jambo hilo na kuwafanya wao waamini kuwa ni dini ya kikristo tu ndiyo ndini ya kweli kutoka kwa Mungu.


kati ya wanasayansi hao ambaye yeye ni muautralia na anafanya kazi NASA ambao wako huko tangu Agosti mwaka jana, wameshangaa maandiko hayo yamefikaje huko zaidi ya kuona kuwa kweli MUNGU yupo,


 wanasayansi hao wako huko kuchunguza sayari hiyo ili kuona kama kuna uwezekano wa binadamu kuishi huko jambo mpaka sasa inasemakana kuna uwezekano wa viumbe hai kuishi kuko kutokana na vitu vingi kushabihiana na huku Duniani.


source:martblog

yohana 3:16 BIBLIA inasema ''kwa maana jinsi MUNGU
aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Amri Kumi za Mungu kwa kiswahili

  1. Mimi ni Bwana Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi.
  2. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani,wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; Kwa kuwa mimi Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kizishika amri zangu.
  3. Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
  4. Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mnyama wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.
  5. Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
  6. Usiue
  7. Usizini
  8. Usiibe
  9. Usimshuhudie jirani yako uongo.
  10. Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake,wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako.

IKIMBIE ZINAA



Saturday, December 1, 2012

IKIMBIE ZINAA

MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE
Je! Unaamini ya kuwa Mungu anaweza kusema na watu kwa njia ya ndoto? Najua ni rahisi kuamini kuwa Mungu alisema na watu zamani kwa njia ya ndoto kama tunavyosoma katika Biblia; lakini je! Unaamini ya kuwa Mungu anasema na watu kwa njia ya ndoto siku hizi? Najua kuna watu wanaoamini na wengine hawaamini. Sijui wewe uko upande gani. Lakini nataka nikueleze hivi; Kufuatana na Biblia kuna ndoto za aina tatu; (a) Kuna ndoto kutoka kwa Mungu. Soma kitabu cha Hesabu 12:6, na Yoeli 2:28. (b) Kuna ndoto zinakuja kwa sababu ya shughuli nyingi. Soma kitabu cha Mhubiri 5:3. (c) Kuna ndoto za uongo zinazotoka kwa shetani aliye baba wa uongo. Soma kitabu cha Yeremia 23:52 na Yohana 8:44. Unaweza kutofautisha kwa namna gani tofauti iliyopo kati ya hizi ndoto? Na utajuaje kuwa ndoto uliyoiota imetoka kwa Mungu? Kila ndoto lazima ipimwe na Neno la Mungu. Ikiwa imetoka kwa Mungu, ni lazima utakuta neno la Mungu ambalo linaeleza maana yake. Mara nyingine ndoto toka kwa Mungu huja kama fumbo; lakini Roho Mtakatifu ajuaye kuyafumbua mafumbo ya Mungu (1 Wakorintho 2:10,11), atalifunua fumbo hilo kwa kukuonyesha neno la Mungu linalofanana na ndoto hiyo. Si busara kuzikubali ndoto zote unazoota bila ya kuzipima katika Neno la Mungu. Na pia si busara kuzikataa ndoto zote bila kuzipima katika Neno la Mungu. Nimeona nianze kwa kukueleza haya kwa kuwa chanzo cha kuandika kitabu hiki, ni ujumbe wa Mungu ulionijia kwa njia ya ndoto. Ndoto yenyewe ilikuwa hivi: Niliona katika ndoto mtu mmoja mkristo, tena aliyeokoka akifanya mambo ya zinaa bila hata kuogopa. Na wakati nilipokuwa nikimtazama na kusikitika, nikasikia sauti toka juu yangu ikisema; “ NITACHUKULIANA MPAKA LINI NA MWANADAMU AFANYAYE MAMBO YA JINSI HIYO?” Baada ya kusikia maneno hayo nikaamka. Wakati huo ulikuwa ni alfajiri, na ndoto hiyo ilinipa maswali na masononeko mengi moyoni mwangu. Na niliamua kumshirikisha mke wangu Diana juu ya ndoto hiyo. Mke wangu akaniuliza; “ Maana yake nini ndoto hiyo?” Nilipotaka kufungua kinywa ili nimjibu uchungu mzito ulijaa moyoni mwangu, nikasikia kuugua rohoni, na mara nikaanza kulia! Unaweza ukaniuliza; “Mwakasege kwa nini ndoto ikulize machozi?” Hili ni swali zuri. Hata mimi nilijiuliza kwa nini nitoe machozi kwa ajili ya ndoto. Lakini baada ya kulifuatilia jambo hili katika maombi na katika neno la Mungu nilielewa sababu yake. Je! Unafahamu matokeo ya Mungu kusema “Nitachukuliana mpaka lini na mwanadamu afanyaye mambo ya jinsi hiyo?” Ukisikia maneno ya jinsi hii ujue Mungu amekasirika na kuna maangamizo mbele. Hebu na tulifuatilie jambo hili katika biblia ili tulione uzito wake. Nuhu na Gharika. Ni vizuri ukumbuke ya kuwa gharika ilitokea wakati wa Nuhu kwa sababu ya zinaa. “Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliona hao binti za wanadamu – ni wazuri; WKAJITWALIA WAKE WO WOTE WALIOWACHAGUA. Bwana akasema, ROHO YANGU HAITASHINDANA NA MWANADAMU MILELE, kwa kuwa yeye ni nyama; basi siku zake zitakuwa mia na ishirini. Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile, tena baada ya hayo, wana wa Mungu WALIPOINGIA kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa. BWANA AKAONA YA KUWA MAOVU YA MWANADAMU NI MAKUBWA DUNIANI NA KWAMBA KILA KUSUDI ANALOWAZA MOYONI MWAKE NI BAYA TU SIKU ZOTE. BWANA AKAGHAIRI KWA KUWA AMEMFANYA MWANADAMU DUNIANI, AKAHUZUNIKA MOYONI. Bwana akasema, Nitamfutilia usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambulisho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana.” (Mwanzo 6:1-8) Ukiendelea kufuatilia habari hii katika Biblia utaona ya kuwa baada ya gharika ya maji walibaki watu nane tu! Wanadamu wengine wote waliangamia kwa sababu ya nini? – Zinaa! Sodoma na Gomora Wasomaji wa Biblia wanafahamu kabisa ya kuwa miji ya Sodoma na Gomora iliteketezwa kwa moto baada ya Mungu kuihukumu kwa sababu ya uasherati uliokuwa ukifanyika ndani yake. Soma Mwanzo 19:4-25. Na pia katika kitabu cha Yuda 1:7 tunasoma hivi: - “Kama vile Sodoma na Gomara, na miji iliyokuwa kando kando, waliofuata UASHERATI kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.” Ikiwa Mungu aliwatenda hivi watu wa Sodoma na Gomora, ni kitu gani kinamfanya mwanadamu wa siku hizi adhani ya kuwa Mungu amebadilika juu ya kuadhibu wale wote wafanyao uasherati? Katika miji hiyo miwili ni watu watatu tu waliobaki – Lutu na watoto wake wawili! Wanadamu wengine waliokuwa katika miji hiyo waliteketezwa kwa sababu ya nini – Zinaa! Kuhani Eli na watoto wake. “Basi Eli alikuwa mzee sana, naye alisikia habari za mambo yote ambayo wanawe waliwatenda Waisraeli; na jinsi WALIVYOLALA NA WANAWAKE waliokuwa wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania.” (1Samweli 2:22) Hata baada ya baba yao kuwaonya hawakusikia, na matokeo yake ni:- 1. Watoto hao wawili, Hofni na Finehasi walikufa wote siku moja; 2. Wana wa Israeli walipigwa na adui zao Wafilisti na Sanduku la agano likatekwa; 3. Kuhani Eli alikufa. Yote haya yalitokea katika taifa ambamo watoto wawili wa kiongozi waliuwa wakifanya mambo ya Zinaa bila hata kujali maonyo. Je! Bado unajiuliza kwa nini nilitoa machozi baada ya kusikia sauti ya Mungu katika ndoto ikisema “Nitachukuliana mpaka lini na mwanadamu afanyaye mambo ya jinsi hiyo?” Siku za Mwisho. “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi…….Kwa maana katika hao wamo wale WAJIINGIZAYO KATIKA NYUMBA ZA WATU, NA KUCHUKUA MATEKA WANAWAKE WAJINGA WENYE MIZIGO YA DHAMBI, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi. (2 Timotheo 3:1,26). Je! Siku hizi wanawake hawatekwi mateka na wanaume ili wafanye mambo ya zinaa? Vishawishi vimekuwa vingi, na wanawake wengi wameanguka katika mitego hiyo ya kupenda fedha na anasa, na mwisho wake ni kufanya uzinifu. Kwa nini wanaume wengi wamekosa akili juu ya jambo hili. Ni kitu gani kimewapofusha macho wasione ya kuwa uzinifu ni mbaya? Biblia inasema; “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomangamiza nafsi yake.” (Mithali 6:32) Ni dhahiri ya kwamba palipo na zinaa pana uharibufu, na wengi wanaangamia. Na nataka nikuambie ya kuwa Roho Mtakatifu akikuwekea mzigo huo ndani yako na kuliona jambo hili jinsi linavyomhunish Mungu, hakika hutatulia; na hapana budi macho yako yatajaa machozi juu ya kizazi hiki kinachojiangamiza chenyewe kwa sababu ya zinaa. Sababu ya mambo haya kuandikwa. Mambo haya hayakuandikwa kwa bahati mbaya, wala si kwa ajili ya kuonyesha historia ya watu Fulani tu. Bali yaliandikwa kwa kusudi maalumu na muhimu. “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili KUTUONYA SISI, tuliofikiriwa na miisho ya zamnai – Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.” (1 Wakorintho 10:11,12) Na mimi nimependa kuyaonyesha wazi ili tujue tunapozungumza juu ya zinaa, Bwana Mungu anakuwa na mawazo gani juu yake. Nafahamu si mara kwa mara hata katika mahubiri na mafundisho, jambo hili huguswa kwa undani. Lakini naona umefika muda wa kulichambua jambo hili kwa undani zaidi. Hali ilivyo sasa. Mtu mmoja aliniuliza “Je, mtu aliyeokoka anaweza kufanya mambo ya uasherati – je, anaweza kuzini?” Nikamwambia, “Mtu aliyeokoka hatakiwi kufanya mambo ya uasherati, kwa kuwa kufanya hivyo ni dhambi, lakini asiposimama katika Kristo sawasawa anaweza kuzini.” Halafu huyo mtu akaendelea kuuliza, “Je, Unamfahamu Fulani? (Akamtaja jina lake). “Ndiyo namfahamu.” Mimi nilimjibu, na nikaendelea kusema; - “ kuwa ni mtumishi wa Mungu, ingawa sijamwona muda mrefu umepita sasa”. Ndipo akasema, “Unafahamu ya kuwa alianguka na akazini na msichana Fulani (akamtaja jina lake) ambaye pia ameokoka, na sasa yule msichana amezaa?” Mimi nilishangaa na kushutushwa na habari hizo. Nikamuuliza “Unasema kweli ndivyo ilivyotokea?” Akasema, “Ndiyo” Ndipo Roho wa Mungu aliponikumbusha ndoto ile aliyonipa. Katika ujumbe ule wa ndoto, Mungu alinionyesha mkristo aliyeokoka akifanya mambo ya uasherati. Kwa mtu asiyeokoka siwezi kushangaa akifanya uzinzi, kwa kuwa bado yuko gizani, na yuko chini ya mkuu wa giza, ibilisi – kwa hiyo anaweza kufanya lo lote lile. Ndiyo maana mtu anaweza kusema yeye ni mkristo, na huku anazini mara kwa mara. Mkristo wa kweli aliyeokoka hatakiwi kuzini, wala kushindwa na dhambi. Kwa nini? Kwa kuwa ndani yake ametengwa mbali na dhambi, na amepewa ushindi juu ya dhambi. Ushindi dhidi ya dhambi Uhusiano wako na dhambi unakuwaje baada ya kuokoka, na kufanyika kiumbe kipya ndani ya Kristo? Watu wengi wakiisha-okoka, huwa bado wanasumbuliwa na kuanguka katika dhambi mara kwa mara, na hasa katika zinaa. Na hii inatokea kwa kuwa hawapati mafundisho ya kutosha ya neno la Mungu juu ya jinsi wanavyotakiwa kuenenda katika maisha mapya waliyopita. Kaini aliambiwaje na Mungu? Bwana alimwambia hivi; “ kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa UISHINDE” (Mwanzo 4:7) Na ndivyo ilivyo hata sasa. Bado tumo ulimwenguni humu, ingawa aliyezaliwa mara ya pili yeye si wa ulimwengu huu (Yohana 17:16). Lakini kwa kuwa bado tumo katika ulimwengu uliojaa dhambi inayotutamani kila siku, na tusije tukajisahau. Inatupasa tuishinde. Yanenaje maandiko? Imeandikwa katika kitabu cha (Warumi 6:12-14) “Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi, bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi, bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki. Kwa maana DHAMBI HAITA WATAWALA NINYI, kwa sababu hamuwi chini ya sheria, bali chini ya neema”. Ikiwa tunaambiwa ya kuwa “Dhambi haitawala ninyi …….” inakuwaje basi wengine wanatawaliwa nayo? Inakuwaje mtu wa Mungu, aliyepakwa mafuta kwa Roho Mtakatifu aanguke katika zinaa? Kitu gani kinampofusha macho ya rohoni? Je! Ni halali kwa mtu anayekaa ndani ya Kristo kutenda dhambi? Yanenaje maandiko? “Kila akaaye ndani yake (Yesu Kristo) HATENDI DHAMBI; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtamua….atendaye dhambi ni wa ibilisi; kwa kuwa ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.” (1 Yohana 3:6,8) Je! Unaona maneno haya yalivyoandikwa kwa ajili yetu? Sidhani kama unapenda tena kuwa Ibilisi kwa kuwa “Apendaye dhambi ni wa Ibilisi” Kwa hiyo ni muhimu ujilinde usitende dhambi. Tena imeandikwa: “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu UZAO WAKE WAKAA NDANI YAKE; WALA HAWEZI KUTENDA DHAMBI KWA SABABU AMEZALIWA KUTOKANA NA MUNGU.” (1 Yohana 3:9) Ikiwa umezaliwa mara ya pili kwa Roho wa Mungu, ujue hakika UZAO WA MUNGU unakaa ndani yako. Na uzao huu wa uungu ni Mtakatifu, na unakaa ndani yake bila kutangatanga unakuwezesha kuishi bila kutenda dhambi. Je! Si jambo la kumshukuru Mungu hilo. Si kwamba anatuambia tusitende dhambi bila kutupa njia ya kutusaidia. Anajua sisi wenyewe hatuwezi kuishinda dhambi, BALI YEYE AKIKAA NDANI YETU NA SISI NDANI YAKE TUNAWEZA KUISHI KATIKA USHINDI DHIDI YA DHAMBI NA MITEGO YAKE YOTE. Tena imeandikwa; “Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu HATENDI DHAMBI; bali yeye aliyezaliwa na Mungu HUJILINDA, wala yule mwovu HAMGUSI.” (1 Yohana 5:18) Ee, mtu wa Mungu, jilinde basi kwa kuwa umezaliwa na Mungu, kwa nini tamaa ya uasherati ikusonge? Je?! umesahau ni uzao wa namna gani ulio ndani yako? Ni kweli kwamba mtu akitenda dhambi na akatubu, Bwana atamsamehe, (1 Yohana 1:9). Lakini hatutakiwi kutenda dhambi. Ndiyo maana imeandika; “Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba MSITENDE DHAMBI”…. (1 Yohana 2:1) Sasa naona unaweza kuelewa kwa nini inashtusha na kusikitisha unaposikia mtu wa Mungu ameanguka katika dhambi ya zinaa. Ikiwa maisha ya wokovu yatakuwa ni ya kuanguka na kusimama, halafu tena kuanguka na kusimama mara kwa mara; basi ina maana ya kuwa ushindi wa kutosha haukupatikana pale msalabani. Lakini nataka nikuambie hivi, ushindi kamili ulipatikana pale msalabani bila kubakiza kitu! Ndiyo sababu Yesu Kristo alikuwa na ujasiri wa kusema ‘IMEKWISHA’ pale msalabani.
MAMA DIANA MWAKASEGE AKIONGOZA MAOMBI KWENYE KONGAMANO LA MAOMBI DODOMA

Hatari ya Ndoto



Monday, September 2, 2013

Hatari ya Ndoto

Photo: Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima akifundisha somo la "UFALME WA MAJINI" katika ibada ya jumapili ufufuo na uzima.

Akifundisha alisisitiza kuwa majini/mashetani wanaweza kumzuia mtu asifanye chochote, akitoa mfano katika 2 Wathesalonike 2:8, alisema mtume Paulo alikua amepakwa mafuta na Mungu kutenda mambo makubwa lakini shetani aliweza kumzuia kwenda Thesalonike kuifanya kazi ya Bwana. Alisisitiza mashetani wapo na ili uwashinde yakupasa kushindana nao kwa kutumia jina la Yesu.

Ibada hiyo iliambatana na uweza wa Mungu na udhihirisho wa ishara za kupita kawaida ka jina la Yesu.
GLORY TO JESUS
Na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima|Kawe Tanganyika Packers|Dar es Salaam

1.0 Utangulizi

Leo nitafundisha kwa habari ya ndoto. Neno ndoto limeandikwa ndani ya Biblia zaidi ya mara 86. Katika kitabu cha mwanzo pekee neno ndoto limeandikwa zaidi ya mara 30. Katika kitabu cha Daniel neno ndoto limejitokeza zaidi ya mara 22.Kwa kawaida kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho.

Nitafundisha hatari ya ndoto leo kwa mifano ya ndoto za wafalme wawili. Mfalme wa kwanza Nebukadreza aliyekuwa mfalme katika mashariki ya kati. (Danieli 2:1-6) Nebukadreza alitawala kipindi ambacho ufalme wake ulikuwa mkubwa mashariki ya kati yote na dunia yote. Mfano wa pili ni mfalme wa Misri Farao, huyu alikuwa mfalme katika Afrika (Mwanzo 41:1-8).

Daniel 2: 1-6, tunajifunza habari ya ndoto iliyootwa na Mfalme Nebudkadreza. “ Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi ukamwacha….”

1.1 Ndoto ni nini?

Ndoto ni jambo linalotakiwa kumpata mtu siku chache zijazo. Ndoto ni kipimo cha hali ya rohoni ya mwotaji. Mfano mtu akiota anakimbizwa na ng’ombe inaamanisha kuwa kiwango cha nguvu zako za rohoni kimeshuka. Endapo utaota wewe ndio unamkimbiza adui inamaana nguvu zako za rohoni zipo juu. Ndoto ni bayana.


2.0 Msisitizo wa Hatari ya ndoto

Ikiwa ndoto inamfadhaisha mfalme ambaye ni mkuu wan chi, je nini mimi na wewe? Hii inatuonesha kuwa kitendo cha mfalme kutaka kufahamu tafasiri ya ndoto inamaanisha kuwa ndoto ni bayana.

2.1 Mambo ya kufanya ukiota ndoto

(i) Jambo la kwanza la kufanya baada ya kuota ndoto ni kuindika hiyo ndoto
Habakuki 2:2-3; BWANA akanijibu akasema, iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili kila aisomaye apate kuisoma kama maji.

(ii) Baini je ndoto uliyoota ni ya mema au ya mabaya

(iii) Ukiota ndoto ukabaini ni ya mabaya anza kuomba mara baada ya kustuka toka ndotoni. Usisubirie kukuche. Omba kinyume cha hiyo ndoto. Batilisha hiyo ndoto.

2.2 Maandiko yanayofanya baadhi ya watu wapuuzie ndoto

Mhubiri 5:3; “kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi…”
Zekaria 10:2; “kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo…”

Yeremia 23:25; “Nimesikia waliyosema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema nimeota ndoto nimeota ndoto.”

Watu hupuunza ndoto kwa kuwa ndoto huja kwa shughuli nyingi na pia hupuuza ndoto kwa kuwa zipo ndoto za uongo. Kimsingi kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho. Uwepo wa maandiko mawili yanayofanya baadhi ya watu wapuuzie ndoto hauwezi kupuuza ndoto zaidi ya 80 ambao zilikuwa bayana, na Mungu alisema na watu katika ndoto.

3.0 Baadhi ya maandiko yanayotufanya tuzishughulikie ndoto tunazoota

Mwanzo 20:3-5; “Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku…”

Mwanzo 28:12 Ndoto ya Yakobo “…akaota ndoto na tazama ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena tazama malaika wa Mungu wanapanda na kushuka juu yake….”

Mwanzo 31:11”Na malaika wa Mungu akiniambia katika ndoto…”

Mwanzo 31:23-24 “…Mungu akamjia Labani Mshami katika ndoto ya usiku…”

Mwanzo 37:46; ndoto ya Yusuph

1 Falme 3:5-10; Ndoto ya Suleiman

Ayubu 7:14; Ndoto ya Ayubu

Viumbe na Maumbile ya Kichawi



Monday, July 15, 2013

Viumbe na Maumbile ya Kichawi



Katika dunia tunayoishi imegawanyika katika sehemu mbili, yaani Ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili. Ulimwengu wa mwili ni ulimwengu ambao unaonekana kwa macho ya nyama. Ulimwengu wa roho, wenyewe una tabia tofauti,
i) ni ulimwengu usioonekana kwa macho ya kawaida.
ii) vitu vyote vilivyoko humo ni roho.
iii) kuna viumbe mbalimbali vya rohoni.

Leo tunaangalia kuhusu Viumbe vya Rohoni. Tukirudi katika Biblia, tunaona kwa habari ya wamisri na vyura, (kutoka 8:2-7) katika mstari wa saba, tunagundua kuwa na waganga nao walifanya vilevile kwa kuleta vyura duniani kama Musa alivyofanya. Kumbe, hata wachawi wanaweza kutengeneza viumbe mbalimbali vya rohoni na kuvidhihirisha katika ulimwengu wa mwili.

Mambo ya Walawi 13:11, hapa tunaona baadhi ya ndege ambao Mungu alikataza kuwa wasiliwe. Utajiuliza kwanini? Jibu ni kuwa kwa kipindi cha agano la kale Yesu alikuwa hajafa bado, hivyo hakukuwa na damu ya utakaso kwa wanyama hao. Mungu alikuwa anatumia njia hiyo ya sheria kuwaokoa wana wa Israeli wasijinajisi na wanyama hao. Kumbe viumbe vya kichawi vilikuwepo tangu agano la kale.

Ndio maana Ayubu 41:1, Luka 10:19, Ufunuo 6:4, Ayubu 39:9, biblia inatumia wanyama kwasababu, Mungu anataka tujue uwepo wa viumbe hivyo vya kichawi katika ulimwengu wa roho. Hivi vyote ni viumbe vya rohoni vinavyotenda kazi dhidi ya maisha ya watu.

Kama vile malaika walivyovaa mwili na kuja kuiangamiza Sodoma na Gomora, vilevile na mapepo wachafu nao huvaa maumbo mbalimbali. Ufufuo 12:7, shetani naye anaweza kujibadili maumbo ya namna mbali mbali ili kuangamiza maisha ya watu. Ndio maana unaweza ukapita mahali, ukasikia kifuu cha nazi kimekusemesha, kwa hakika kile sio kifuu bali ni pepo amejigeuza na kuwa kifuu cha nazi. Mashetani wana tabia za kujibadili maumbo ya aina mbalimbali.

Ni muhimu kuomba kabla ya kutumia vitu ambavyo ama unapewa na mtu, 1Wakorintho 10:31. "31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu." Kumbe kila jambo unalotenda au kabla ya kununua au kuuza unatakiwa ufanye kwa utukufu wa Mung-Pastor Josephat Gwajima

JINSI YA KUSIKIA SAUTI YA MUNGU



Friday, November 16, 2012

JINSI YA KUSIKIA SAUTI YA MUNGU

WATU WA MUNGU WAKIMWABUDU MUNGU

MUNGU ANAONGEA NA WATU KWA NJIA ZIFUATAZO;                                                                                                                           1.kwa njia ya malaika; Alimtokea Dideoni Waamuzi 6:11-14 2, pia alimtokea Mariam  Luka 1:26-37, pia alimtokea Petro gerezani  Matendo 12:7-11.     2.Kwa sauti ya wazo; MUNGU alisema na Yahazieli  kwenye kundi la watu 2Nyakati 20:12-17.                                                                                          3.Kwa njia ya watumishi wake; Waebrania 1:1-2 {MUNGU ambaye zamani alisema na baba zetu katika manabii na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika MWANA ambaye amemweka kuwa mrithi wa yote tena kwa yeye aliufanya ulimwengu} pia MUNGU alimtuma Isaya kwa mfalme Hezekia 2Wafalme 20:12-17.                                                                          4.Kwa njia ya neno lake; alisema na Daniel kwa njia ya neno katika Danieli 9:1-4.                                                                                                                5.Kwa njia ya ndoto; alisema na Yusufu kuhusu ndoto ya Farao Mwanzo 41:15-32.                                                                                                                 6. Kwa njia ya ishara; alisema na nabii Isaya kuhusu kuzaliwa kwa YESU katika Isaya 7:14.                                                                                           7.Kwa njia ya maono; alisema ma Mtume Yohana katika Ufunuo 1:10.      8.Kwa njia ya mazingira; Katika kitabu cha Esta sura ya 2hadi sura ya 7             

JEHOVAH NI MUNGU MPONYAJI

  MAMBO YA KUZINGATIA ILI USIKIE SAUTI YA MUNGU                          A.Kwanza kabla ya kuisikia sauti ya MUNGU lazima uwe na shauku  ya kuisikiliza sauti ya MUNGU.                                                                     B.Lazima uwe mwombaji/mwana maombi;mfano ili uongee na mtu lazima uanze kumsemesha mtu huyo na kwa MUNGU ni hivyo hivyo  ila kwa MUNGU tunatumia njia ya maombi ndio maana amesema katika Yohana 14:14 kwamba tuombe chochote kwa jina la YESU yeye atajibu.                                    C.Lazima utengeneze mazingira; Maana MUNGU ni utakatifu hivyo anatutaka tuwe watakatifu na tuwe tumefanyika watoto wake kupitia YESU KRISTO yaani Tumeokoka kwa kumaanisha maana MUNGU anajua yote hata siri zote za mioyoni mwetu.                                                                                       D.lazima uwe mtii wa kile anachokisema MUNGU.


YESU KRISTO NDIYE MWOKOZI PEKEE KWA WANADAMU WOTE

Ubarikiwe sana ndugu popote ulipo na kama hujaokoka kumbuka kuwa wakati wa wokovu ni sasa hivyo tafuta kanisa la kiroho na waeleze watakusaidia kwani hakuna ajuaye kalenda ya maisha yake na BWANA YESU alikuja tuwe na uzima wa milele katika yeye kwani hakuna uzima wa milele kwingine kokote.MUNGU wa milele akubariki sana.

MUNGU AWE WA KWANZA KATIKA MAISHA YAKO YOTE