Katika makala haya, tutaangalia jinsi
wanasayansi wa kawaida, tena ambao walikuwa hawaamini kabisa kwamba
kuna Mungu au shetani, katika utafiti wao ambao haukuwa na uhusiano
wowote na masuala ya rohoni, walijikuta wanagundua mambo ambayo
yaliwatia hofu hadi wengine kukimbia kazi. Waliweza kusikia waziwazi
sauti za vilio vya mateso kutokea katikati ya dunia! Sauti hizo
walizirekodi; na mwisho wa makala haya utaona anwani inayoweza
kukupeleka kuzisikia sauti hizo za kutisha na kusikitisha mno, mno!!
Ni nani ambaye hajasikia habari za
kwamba wanga huenda baharini, wakatupa mayai viza kisha malango
yanafunguka nao wanashuka hadi kuzimu? Bila shaka habari hizi si ngeni
masikioni mwa wengi wetu? Ni mambo ambayo ni rahisi kuaminika katika
ulimwengu wa kawaida lakini unapoyaongelea kwa mtazamo wa Biblia, hapo
watu wanaanza kukosa imani na kudhani kuwa si za kweli.
Makala haya yanatokana na habari ambayo iliandikwa katika gazeti la Ammennusatia la kule Finland katika toleo lake la Julai 1989.
Sehemu ya gazeti
Kikundi kimoja cha wanajiologia (wana
elimu ya miamba) wa Kirusi walikuwa katika mradi wa kutoboa tundu katika
eneo la Kola, karibu na Murmansk; maili takriban 150 kaskazini mwa
Duara la Aktiki, nchini Siberia. Watafiti hao waliweza kutoboa tundu
ardhini lenye urefu wa kilometa 14.4 kwenda chini.
Dr Azzacov, ambaye alikuwa ndiye meneja
wa mradi alisema kuwa wakati wa kutoboa, ghafla drili ilianza kuzunguka
bila utaratibu, hali iliyoonyesha kwamba drili imefika kwenye sehemu
iliyo na uwazi.
“Taarifa tunazokusanya ni za kushangaa
sana, kiasi kwamba kwa kweli tumeingiwa na hofu maana hatujui kile
tunachoweza kukikuta huko chini,” alisema Dr Azzacov.
“Jambo la pili lililotushangaza lilikuwa
ni kiwango cha joto tulichokigundua katikati ya dunia. Mahesabu
yanaonyesha kuwa joto hilo lilikuwa takribani nyuzi 1,000 za Selsiasi,”
aliongeza kusema Dr Azzacov. “Hii ni zaidi ya kile tulichotegemea.
Inaonekana ni kama moto wa jehanamu unawaka kwa nguvu sana humo ndani,
katikati ya dunia!”
“Ugunduzi wa mwisho ndio uliokuwa wa
kushitua sana masikioni mwetu kiasi kwamba wanasayansi wana hofu kubwa
ya kuendelea na mradi huu. Tulikuwa tukijaribu kusikiliza mjongeo wa
dunia kila baada ya muda fulani kwa kutumia vinasasauti vya hali ya juu
sana (supersensitive microphones), ambavyo tulikuwa tukivishusha hadi
chini kupitia kwenye tundu
tulilotoboa.”
Dr Azaccov anaendelea kueleza kwamba,
“Kile tulichosikia, wanasayansi hawa ambao wamezoea tu kuamini mambo
yanayoleta mantiki akilini, kiliwafanya kutetemeka kwa hofu kubwa mno!
Wakati mwingine hicho tulichokisikia kilisikika kwa sauti ya chini
lakini kali ambayo mwanzoni tulidhani inatokana na vifaa
vyetu.”
“Lakini baada ya kuvirekebisha,
tulibaini kwamba zilikuwa ni sauti zilizotoka katikati ya dunia kabisa.
Hatukuamini masikio yetu. Tulisikia sauti ya mwanadamu akipiga kelele
kwa maumivu. Japokuwa sauti moja ilikuwa inasikika kwa uwazi zaidi,
tuliweza kusikia kwa nyuma sauti za maelfu, na huenda mamilioni ya watu
wakilia kwa mateso na maumivu.
“Baada ya ugunduzi huu wa kutisha, nusu
ya wanasayansi waliachana na mradi huo kutokana na hofu. Ni matumaini
yangu kuwa hicho kilichoko huko chini kitabia hukohuko,” aliongezea Dr
Azzacov.
“Na kilichowamaliza kabisa nguvu hawa
wanasayansi wa Kisovieti, mbali na hizo sauti walizozisikia, ilikuwa ni
kutokea usiku uleule kwa gesi inayong’aa kutoka kwenye tundu lile
walilokuwa wamelitoboa; na katikati yake alijitokeza kiumbe mwenye
mabawa kama ya popo pamoja na maneno yaliyokuwa yameandikwa kwa Kirusi
‘Nimeshinda’.”
Baada
ya mkasa huo, Dr Azzacove alisema, “Mimi kama mkomunisti, siamini juu
ya mbingu au Biblia, lakini kama mwanasayansi, hivi sasa naamini juu ya
kuwapo kwa kuzimu. Ni kweli tuliogopa sana kutokana na ugunduzi huo.
Lakini tunajua fika kile tulichokiona na kukisikia. Tunaamini kabisa
kuwa tulitoboa tundu kwenye lango la kuzimu yenyewe!”
MAELEZO YANGU MIMI JIMMY
Hili lilikuwa ni tukio ambalo
liliwatokea watu ambao hawaamini kabisa habari ya Mungu. Wengi
tunakumbuka kwamba kabla ya kusambaratika kwa Urusi ya zamani, ambayo
ilikuwa ni dola kubwa ya umoja wa nchi za kisovieti, itikadi ya kisiasa
ya dola hiyo ilikuwa ni ya kikomunisti ikiongozwa na falsafa za akina
Marx, Lennin, Angels na Stalin.
Wao waliamini katika uyakinifu
(materialism), yaani kwamba mwanadamu pamoja na ulimwengu wote ni kile
tu kinachoonekana kwa macho au kuthibitika kisayansi. Suala la Mungu,
shetani na chochote cha kiroho kwao kilikuwa ni uzushi. Na yeyote
aliyejaribu kueneza itikadi za kidini, alishughulikiwa na dola ipasavya.
Karl Marx, kwa mfano , alisema, “Religion is an opium dose of the people.” –
kwamba, “Dini ni dozi ya afyuni (dawa za kulevya) kwa watu.” Hii
ikimaanisha kwamba dini ni kama ulevi wa kupumbaza akili za watu na
kuwafanya wasiendelee.
Kwa hiyo, haingewekana kabisa
wakomunisti hawa waanze kueleza mambo ya rohoni ambayo maishani mwao
mwote, tangu wakiwa watoto, waliaminishwa kwamba hakuna Mungu wala
shetani, kama anavyokiri Dr Azzacov mwenyewe kwenye maneno yake ya
mwisho.
Sasa je, ugunduzi wao huo uliowajia bila kutegemea una uhusiano wowote na Biblia?
Biblia inasema kwamba Yesu amepewa
heshima kubwa na Mungu: “… ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la
vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi.” (Wafilipi
2:10). Chini ya nchi hapa ni kuzimu!
Katika kuongelea kuhusu kupaa kwa Bwana
Yesu, maandiko yanasema: “Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama
siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za
nchi?” (Waefeso 4:10). Pande zilizo chini za nchi hapa ni kuzimu!
Je, Yesu alienda kufanya nini huko?
Biblia inasema kwamba Yesu
alipoteswa: “… mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, ambayo kwa
hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri.” (1 Petro
3:18-19). Yesu hakuhubiri tu duniani, bali kwa zile siku tatu alizokaa
kaburini, alienda kuwahubiria wale wote waliokuwa wamekufa tangu Adamu
hadi wakati huo Yeye alipokufa.Kifungoni hapa ni kuzimu!
Maandiko haya matatu (japo yapo na
mengine), yanatuonyesha kwamba ni kweli chini ya dunia ndiko iliko
sehemu inayoitwa kuzimu; ambayo ndiyo makao ya shetani na mapepo au
majini; ambako watu wanaokufa katika dhambi wanaenda kuanza mateso wakisubiri siku ya mwisho wa ulimwengu.
HITIMISHO
Licha ya kwamba kuzimu kuna mateso makali yasiyoelezeka, lakini ukae ukijua kwamba kuzimu si jehanamu!
Kuzimu ni makao ya shetani na majini wake leo; lakini jehanamu ni moto
ambako mashetani au majini pamoja na watenda dhambi wote watatupwa na
Bwana Yesu baada ya mwisho kabisa wa ulimwengu.
Biblia inasema hivi: Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti. (Ufunuo 20:10).
Pia imeandikwa: Mauti na kuzimu
zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani hilo
ziwa la moto. Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa kwenye kitabu
cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. (Ufunuo 20:14-15).
Sasa, kama kuzimu tu kuna mateso yasiyoelezeka, je jehanamu itakuwa vipi?
Biblia inasema: Ni jambo la kutisha
kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai. (Waebrania 10:31). Hii ni kwa
sababu wanaoangukia mikononi mwa shetani wanaweza kupata fursa ya
kuokolewa; lakini ukiangukia kwa Mungu mwenyewe, ni nani tena wa
kukuokoa??
Ndugu unayesoma makala haya, pokea
wokovu wa Bwana Yesu muda ungalipo, maana Biblia inasema “Wakati
uliokubalika ni sasa” (si leo)! Nimeshasema mara kadhaa, dini haina
wokovu; NI YESU PEKE YAKE ANAYEOKOA! Dini bila Wokovu wa Yesu ni maagizo
tu ya wanadamu.
Habari za Dr Azzaccov na timu yake unaweza kuzisoma mwenye mtandaoni kwenyewww.diggsjourney.com. Hata hizo sauti za watu wanaoteseka kuzimu ambazo walizirekodi zimo humohumo; ni vizuri uzisikilize!!
Karibu kwenye makala nyingine kama Bwana Yesu atakuwa bado hajarudi.
25 thoughts on “Utafiti wa kisayansi uliogundua sauti za wanadamu wanaoteseka kuzimu”
Japo Mungu anataka tuishi kwa imani kwa asilimia mia moja, wakati
mwingine anaruhusu tuone, kusikia au kujua mambo kwa njia ya kimwili
ili kuimarisha imani yetu na kututia moyo kwamba yale tunayosoma kwenye
Neno lake ni ya kweli kabisa.
Bwana YESU asifiwe wapandwa.Mimi nadhani huu ni wakati ambao
hata wale wasioamini injili wanadhihirishiwa uhai uliopo katika neno la
MUNGU:Watu wanapaswa kutopuuzia biblia.Tumtafuteni MUNGU wapendwa.Mambo
haya yapo.Usipokuwa na YESU yumkini hata mimi na wewe tunaweza
kuchukuliwa
Nimeifuatilia kwa youtube na kugundua ni ukweli, ni sauti zinatisha sana!
Na ashukuriwe Mungu Baba yetu wa mbinguni kwa kujidhirisha na
kujifunua hasa kwa hawa wasioamini kweli yake ili wapate kuujua ukuu na
uungu wake tangu sasa na hata zamani zijazo,hivyo wakati wa kumwona na
kumpokea Mungu Baba ,Mungu mwana na Mungu roho mtakatifu ndio sasa.
Wapendwa,
Je, Kuzimu ndiko Jehanamu?
Aliye na uelewa mzuri anisaidie ili niweze kulielewa vizuri tukio hili!
Mpendwa CK Lwembe na wengineo,
Somo hili la kuzimu bado ni miongoni mwa mada ninazoziita zenye
mitazamo mingi baina ya wapendwa na wanazuoni wa Biblia. Fuatana nami
hapa uone maana ya kuzimu na ulinganishe na huo utafiti ambao bado hata
mimi sijauamini.
KUZIMU NI NINI AU TOFAUTI YA KUZIMU NA JEHANAMU NI IPI?
Wazo la kuzimu kwa watu wengi ni mahala pa adhabu kwa’roho
zisizopatwa na kifo’ za wabaya moja kwa moja baada ya kufa, au mahala pa
kuteswa wale ambao watakataliwa. Ni tendo letu la kusadikisha kwamba
Biblia inafundisha kuwa kuzimu ni kaburi, mahali watu wote wanakwenda
wakifa.
Ni neno lisilotumika sana katika misemo ya watu, awali katika
Kiebrania neno’Sheol’ limetafsiriwa’hell’ kwa kiingereza. kwa hiyo
Biblia ya kiswahili ilipoandikwa tafsiri toka kiingereza neno
liliandikwa’Kuzimu’ likiwa na maana’mahala pa kuzika wafu’ Leo watu
wametoa habari zinazotofautiana na Biblia inavyoelezea kuhusu neno
kuzimu. Biblia yetu ya kiswahili hapa Afrika Mashariki ni U.V ikiwa na
maana kuwa ni tafsiri tofauti -tofauti toka Biblia mbali mbali za
kiingereza ambazo ni K.J.V, R.S.V, R V n.k sasa hivi Biblia zilizopo kwa
kiswahili ni U.V na Biblia habari njema kiswahili cha kisasa kwa kifupi
(B.H.N) mifano michache ambayo katika Biblia hili neno’Kuzimu’
limetafsiriwa’kaburi’ linafanya wazo la watu wengi kutofaa kuhusu kuzimu
kuwa ni mahala pa ziwa la moto na kuteswa wabaya ni: -
“E e BWANA, …….. wasio haki wanyamaze kuzimu” (Zab. 31:17).
“Bali BWANA ataikomboa nafsi yangu, atanitoa mikononi mwa kuzimu –
Kaburi (Zab. 49:15) yaani nafsi ya Daudi au mwili atafufuliwa toka
kaburini, au kuzimu’.
Imani ya kuwa kuzimu ni sehemu ya kuadhibiwa wabaya mahala ambapo
hawawezi kuepuka haiwezi kupatana na hii; mtu mwenye haki anaweza kwenda
kuzimu (Kaburini) na kutoka tena. Hosea 13:14 anathibitisha hivi:
“Nitawakomboa (watu wa Mungu) na nguvu za kaburi (kuzimu); nitawaokoa na
mauti” mstari huu umenukuliwa katika 1 Kor. 15: 55 unahusu ufufuo
Kristo akirudi. vivyo hivyo katika maono ya ufufuo wa pili (ona somo la
5. 5) “mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwemo ndani yake” (Uf.
20:13). Tazama mfano kati ya mauti yaani, Kaburi, na kuzimu (pia ona
zaburi 6:5).Maneno ya hana katika 1 Sam. 2:6 yapo wazi kabisa: “BWANA
huua naye hufanya kuwa hai (Kwa njia ya ufufuo): hushusha hata kuzimuni
(kaburini), tena huleta juu”.Kwa kuwa’kuzimu’ ni kaburi itegemewe kwamba
wenye haki wataokolewa kutoka hilo kwa njia ya kufufuliwa kwao kupata
uzima wa milele. Hivi inawezekana kabisa kuingia’Kuzimu’ au kaburini, na
baadae kuliacha kwa njia ya ufufuo. Mfano mkubwa ni huo wa Yesu, ambaye
roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukupata kuoza’ (mdo.
2:31).wa sababu alifufuliwa. Angalia usambamba kati ya’roho’ ya Kristo
na’mwili’ wake. kama mwili wake “haukuachwa kuzimu” ni kudokezwa kuwa
alikuwako huko kwa kipindi, yaani, siku tatu ambazo mwili wake ulikuwamo
kaburini. Kama Kristo alikwenda’kuzimu’ uwe ushahidi wa kutosha kwamba
sio sehemu wanako kwenda wabaya.
Watu wote wabaya na wazuri wanakwenda’Kuzimu’ yaani kaburini. Hivyo
Yesu “Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya” (Isa. 53:9) kwa kufuatana na
mstari huu, ipo mifano mingine mingi ya watu wenye haki kwenda kuzimu,
yaani kaburini. Yakobo alisema ya kwamba “nitamshukia mwanangu,
nikisikitika, hata kuzimu (kaburini) …. Akamlilia” Yusufu (Mwa. 37:35).
Ni moja ya mambo ya awali ya Mungu ya kuwa adhabu kwa ajili ya dhambi
ni mauti (Rum 6:23;8:13;Yakobo 1:15). Hapa kwanza tumeonyesha mauti ni
hali ya kutokuwa na fahamu kabisa. Dhambi husababisha kuangamia kabisa,
sio kuteswa milele (math. 21:41;22:7; Marko. 12:9; Yakobo 4:12), hakika
kama watu walivyoangamia kwa gharika (Luk. 17: 27, 29), Kama waisraeli
walivyokufa jangwani (1 Kor. 10:10). katika sehemu zote hizi watenda
dhambi walikufa kuliko waliteswa milele. Basi haiwezekani kwamba wabaya
wanaadhibiwa wakiwa na fahamu kwa mateso na kuona.
Vile vile tumeona kuwa Mungu hahesabu dhambi – au kutuweka katika
taarifa ikiwa hatujui neno lake (Rum 5:13). Walio katika nafasi hii
watasalia wakiwa wafu. Walio kwisha jua matwaka ya Mungu watafufuliwa na
kuhukumiwa Kristo akirudi. Ikiwa wabaya adhabu wanayopata itakuwa ni
kifo, kwa sababu hii ni hukumu kwa ajili ya dhambi. Kwa sababu hii baada
ya kuja mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, wataadhibiwa na kisha kufa
tena, kubaki katika kifo milele. Hii itakuwa ni’Mauti ya pili’
iliyosemwa katika ufu. 2:11; 20:6. Watu hawa walikuwa wamekufa mara ya
kwanza, kifo cha kutokuwa na ufahamu kabisa. Watafufuliwa na kuhukumiwa
Kristo akirudi, na kisha kuadhibiwa na mauti ya pili, ambayo, kama mauti
yao ya kwanza, hawatakuwa na ufahamu kabisa. Hii itadumu milele.
Ni katika maana hii ya kuwa adhabu kwa ajili ya dhambi ni ya’milele’,
katika hiyo haitakuwa na mwisho mauti yao. Kubaki wafu milele ni adhabu
isiyo na mwisho. Mfano wa Biblia kutumia aina hii ya maelezo
yanapatikana katika K/Torati 11:4. Huu unaeleza Mungu akiwaangamiza mara
moja Jeshi la Farao katika Bahari ya shamu milele, maangamizi
yanayoendelea ni kama hasa jeshi hili halikurudia tena kuwasumbua
Israeli, “alivyowafunikiza na maji ya Bahari ya Shamu ……..
alivyowaangamiza BWANA hata hivi leo”.
Hata katika nyakati za awali za Agano la Kale waamini walielewa
kwamba kutakuwa na ufufuo siku ya mwisho, ambapo waovu wanaowajibika
watarudi kaburini. Ayu. 21:30,32 yupo wazi sana: “Kwamba mwovu …… na
kuongozwa nje (Yaani kufufuliwa) katika siku ya Adhabu ….. pamoja na
hayo atachukuliwa (kwenda) kaburini”. Moja ya mifano ya mahubiri kuhusu
kurudi kwa Kristo na hukumu inazungumzia wabaya’Kuchinjwa’ mbele yake
(Luk. 19: 27). Mfano huu ni shida kufaa katika wazo la wabaya wanaishi
milele katika hali ya kuwa na fahamu daima wakipokea mateso. Kwa
vyovyote hii itakuwa ni adhabu isiyo na maana – mateso ya milele kwa
matendo ya miaka 70. Mungu haoni raha kuwaadhibu watu wabaya; basi
inategemewa kuwa hatawapa adhabu isiyo na mwisho. (Ezek. 18:23, 32;
33:11; 2 Pet. 3:9).
Ufalme wa Kikristo ulioiacha imani mara nyingi unajumuisha’kuzimu’ na
wazo la moto na mateso. wazo hili hutofautiana vikali na mafunzo ya
Biblia kuhusu kuzimu (kaburi). “Kama kondooo wamewekwa kwenda kuzimu
(kaburini); na mauti itawachunga” (Zab. 49:14) inadokeza ya kuwa kaburi
ni mahala pa usahaulifu kwenye utulivu. Mbali ya roho ya Kristo, au
mwili kuwa kuzimu kwa siku tatu, haukuachwa uoze (Mdo. 2:31)
isingewezekana kama kuzimu ni mahala pa moto.
Ezek. 32: 26- 30 inatoa picha ya mashujaa wa vita wa mataifa
yaliyowazunguka, wanalala kwa amani katika makaburi yao: “Mashujaa wao
….. walioanguka (katika vita) walioshuka kuzimu pamoja na silaha zao za
vita: ambazo wameweka panga chini ya vichwa vyao ….. wamelala ….. pamoja
nao washukao shimoni”Hapa tunatajiwa desturi za mashujaa kuzikwa na
silaha zao na kukilaza kichwa cha maiti juu ya upanga wake. Lakini haya
ni kueleza’Kuzimu’ – kaburi. Hawa watu mashujaa bado wanalala kuzimu
(yaani, kaburini) ni shida kusaidia wazo la kuwa kuzimu ni sehemu ya
moto.
Vitu vya mwili (kwa mfano, mapanga) kwenda sehemu moja “kuzimu” kama
watu, ikionyesha kwamba kuzimu sio uwanja wa mateso ya kiroho. Hivyo
Petro alimwambia mtu mwovu, “Fedha yako na ipotele mbali pamoja nawe
(mdo. 8:20) Taarifa ya yaliyompata Yona yanapinga hili. Akiisha mezwa
hai na samaki mkubwa, “Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, katika tumbo la
yule samaki akisema, Nalimlilia Bwana …. Katika tumbo la kuzimu
naliomba” (Yona. 2:1,2).’Tumbo la kuzimu’ hili ni sambamba na hilo la
nyangumi. Tumbo la nyangumi kweli palikuwa ni’mahala pa uficho’ ambayo
ndiyo maana ya neno msingi’Kuzimu’ lililotafsiriwa’kaburi’ Ni wazi
haikuwa ni sehemu ya moto, Yona alitoka nje ya “tumbo la kuzimu” hapo
nyangumi alipomtapika. Jambo hili lililenga mbele kwenye ufufuo wa
Kristo toka’kuzimu’ (kaburini) – ona Mathayo 12:40.
Nadhani maelezo haya kwa leo yanatosha. Baadaye nitawaletea zaidi kuhusu mada hii kwani mjadala unaendelea.
Mpendwa Lwembe
Najua kwa sehemu haya ninayoandika unayafahamu ninaandika nikikumbuka
wengine hawana ufahamu nao waupate ili tufaidiane kwa yale tunayoamini
ktk imani yetu.
Jehanamu ni neno la kiarabu/Kiswahili
Waebrania wanaita gehenna
Gehenna ni bonde nje kidogo ya Yerusalem,
hilo eneo walikuwa watupa takataka tuseme dampo,sasa moto hapo ulikuwa
hauzimiki,Yesu alilitumia jina gehenna kama mfano kuwa waovu ambao
wameuasi Mungu wataupwa kwenye moto usiozimika milele(ZIWA LA MOTO) kwa
mfano wa huo moto wa dampo la gehenna.
kwa sehemu nafahamu kuna kitu kinaitwa sheol na hedes,
hedes ni sehemu walikufungiwa wale malaika walioasi ,lusifa yuko huko
angani sijui mbingu ya ngapi(mkuu wa anga) yeye bado hajafungwa ndio
maana kuna OLE kwa walio duniani maana Lusifa anajua kuwa ana siku
chache kabla ya kifungo ufunuo 20:1-3.naye ataafungiwa kuzimu miaka
elfu.
Sheol ni pahala ktk ulimwengu wa wafu walikokaa wateule/watakatifu kabla
ya ukombozi wa Bwana yetu yesu kristo,ambayo ndio ile paradiso ya sasa
wateule/watakatifu wakisubiri ule utawala wa miaka elfu wa Bwana Yesu.
kabla watu upande mmoja wa sheol kuamishwa na kupelekwa mbingu ya tatu(paradise) pale Bwana Yesu alipopaa na kuteka mateka,
sheol ni kifungo kwa wafu wote waliolala watakaokolewa na watakao
angamizwa upande mwingine, mf (Lazaro na tajiri)siku ya hukumu
.
kuzimu hakuna moto,ni eneo la kusubiri hukumu.
Jehenamu(ziwa la moto) ni Mauti ya pili kwao walioasi/wasio haki,Lucifa na wajumbe wake baada ya hukumu ya wafu
Jehenamu ni eneo halisi ktk ulimwengu wa roho
Kuzimu ni eneo halisi ktk ulimwengu wa roho
Inawezeka nachanganya majina maana kuna greek/Hebrew hapo,Wapendwa
mnaweza kunisaidia kuweka sawa lugha ya majina kuna majina kama 5
yanayozungumzia neno kuzimu na maana zake.
Nikipata nafasi nitapitia maandiko nitakuja na usahihi Bwana akipenda
Barikiwa
Ndugu Lwembe na Milinga, kwa ufahamu wangu kuzimu ni sehemu
tofauti na jehanamu.Kwa kawaida mtu anapomaliza muda wake wa utumishi
hapa duniani(kufariki) kuna sehemu mbili za kwenda. Sehemu ya kwanza ni
peponi au paradiso huko wanapopumzika watakatifu na sehemu ya pili ni
kuzimu huko wanapopumzika waovu wote lakini tofauti na sehemu ya kwanza
yaani peponi au paradiso huko kuzimu hakuna kupumzika ni mateso
yanaendelea moto upo na roho zinaendelea kuumia vibaya. Baada ya hukumu
yaani mauti ya pili mauti na kuzimu zitatupwa katika ziwa la moto hii
ndiyo jehanamu na mateso ya humo ni makali zaidi kuliko kuzimu.
Ufunuo 20:10 “Na yule ibilisi mwenye kuwadanganya,akatupwa katika ziwa
la moto na kiberiti,alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo.Nao
watateswa mchana na usiku hata milele na milele”
Nimewahi kuona mafundisho fulani kwenye kipeperushi ambayo yalisema moto
upo lakini unaunguza mara moja tu na kuzimika. Nilisikitika sana
nilitamani hata tuonane uso kwa uso na mwandishi ili tuliangalie neno
kwa pamoja.
Wapo pia wanaofundisha kuwa Mungu kwa huruma yake aliyo nayo hawezi
kuwaandalia wanadamu moto uwakao kila siku na kuwatesa. Hili nalo pamoja
na mengine mengi na mengine bado yanakuja ni mafundisho ya
shetani.Lengo lake likiwa ni upotoshaji wa neno la Mungu.
Hata hapo juu ndugu Milinga kuna mambo umeyataja kwangu mimi nimeyaona kama ni mkanganyiko.
Kama watu wote wanaenda kuzimu ina maana hata Musa na Eliya
walivyoonekana wakisema na Bwana Yesu walitoka kuzimu?Mathayo 17:3
,Marko 9:4
Ndugu Milinga kuzimu siyo kaburi kama hili inamowekwa miili hii ya
duniani.Kaburi hili la kwaida la kuzikia wafu hapa duniani linaonekana
kwa macho yaani liko katika ulimwengu wa mwili lakini kuzimu haionekani
kwa macho ya nyama maana iko katika ulimwengu wa roho.Kwa taarifa yako
huko ndiko aliko shetani pamoja na majeshi yake(mapepo na roho zote
chafu).
Hapa nanukuu baadhi ya maneno yako “Kwa vyovyote hii itakuwa ni adhabu
isiyo na maana – mateso ya milele kwa matendo ya miaka 70. Mungu haoni
raha kuwaadhibu watu wabaya; basi inategemewa kuwa hatawapa adhabu isiyo
na mwisho. (Ezek. 18:23, 32; 33:11; 2 Pet. 3:9).”
Hii si kweli kabisa! ni kweli kabisa Mungu hafuraii kufa kwa muovu au
mateso yake ndiyo maana kasema mwenyewe tuchague uzima,tuchague kuishi
na ametoa utaratibu utupasao.Kumbukumbu la Torati 30:19-20
Mungu amefanya jitihada nyingi sana kumuokoa mwanadamu hadi akaitoa
nafsi yake ife kwa ajili ya wenye dhambi sasa kama mwenye dhambi hataki
kutubu na kuacha dhambi Mungu afanyeje?kumbuka dhambi ni uasi na ni
mauti unapotenda dhambi huitwi tena mwana wa Mungu ila unakuwa mwana wa
ibilisi hivyo usipotubu utaungana nae ibilisi kwenye ile adhabu
inayomsubiri.
Nanukuu tena maneno yako:
“Watu hawa walikuwa wamekufa mara ya kwanza, kifo cha kutokuwa na
ufahamu kabisa. Watafufuliwa na kuhukumiwa Kristo akirudi, na kisha
kuadhibiwa na mauti ya pili, ambayo, kama mauti yao ya kwanza,
hawatakuwa na ufahamu kabisa. Hii itadumu milele.”
Ndugu Milinga unamaanisha nini unaposema kifo cha kutokuwa na ufahamu kabisa? Je roho inakufa?
Maisha yajayo tunayoyatarajia kwa imani ni maisha ya milele.Hii ina
maana kwamba watakaokwenda mbinguni wataishi milele na hata wale
watakaokuwa jehanamu maisha yao humo ni ya milele na fahamu na hisia
zote wanakuwa nazo kama kawaida. Sasa napata shida kukuelewa unaposema
kwamba mtu aadhibiwe milele kwa dhambi aliyotenda kwa muda miaka 70 tu.
Hapa inaonyesha kuwa unajaribu kucompromise na Mungu kwamba si haki.
Hukumu za Mungu ni za haki
Zaburi 98:9, Zaburi 119:137
Kuna kuchanganyikiwa kwingi kuhusu swali hili. Mwelekeo watoka
kwa mafunzo ya mitume kumi na wawili ambao wasema, “alishuka kuzumuni.”
Kuna maandiko machache ambayo kulingana na vile yametafsiriwa yanaelezea
juu ya Yesu kuenda kuzimuni. Kwa kulichanganua swala hili, ni muimu
kwanza kuelewa chenye Bibilia inafunza kuusu ulumwengu wa wafu.
Katika bibilia ya Kiibrania neno ambalo limetumika kuelezea ulimwengu
wa wafu ni sheol. Linamaanisha “mahali pa wafu” au “mahali pa
roho/mioyo iliyotuacha” Neno la kigiriki katika Agano Jipiya limetumika
kusimamia ni “kuzumuni” ambalo pia lamaanisha “mahali pa wafu” maandiko
mengine katika Agano Jipiya yanaonyesha kuwa “kuzumu” ni mahali pa muda,
ambapo roho zinawekwa zinapongoja ufufuo na hukumu ya mwisho. Ufunuo
20:11-15 unatupa tofauti halisi kati ya maneno hayo mawili kifungoni
(sheol) na kuzumuni (hades). Jehanamu (ziwa la moto) ni mahali pa kudumu
na hukumu ya mwisho kwa wanaoangamia. Kuzimuni ni mahali pa muda. Kwa
hivyo, la! hasha Yesu hakuenda kuzumuni kwa sababu kuzumuni ni ulimwengu
ujao ndio neno hilo litakapokuwa likitumika baada ya kiti cheupe cha
hukumu (Ufunuo 20:11-15).
Kuzumu ni ulimwengu umegawa mara mbili (Mathayo 11:23, 16:18;
Luka10:15, 16:23; Matendo ya Mitume 2:27-31), mahali pa watakaokolewa na
wanao angamia. Mahali pa watakaokolewa paliitwa “paradiso” na ni “kifua
cha Abrahamu”. Mahali pa watakaokolewa na watakaoangamia
pametenganishwa na “shimo kubwa” (Luka 16:26). Wakati Yesu alipaa
mbunguni, aliwachukua wa hudumu wa paradiso waliokuwa waumini pamoja
naye kwenda mbunguni (Waefeso 4:8-10). Mahali pa kuzumuni
hapakubadilishwa. Wafu wote wasioamini walienda huko wakingoja hukumu
yao ya mwhisho ambayo inakuja. Je Yesu alienda kifungoni mahali roho
zilikuwa zikingoja hukumu?. Ndio kulingana na (Waefeso 4:8-10 na 1Petero
3:18-20).
Baadhi ya wasiwasi imechibuka kutoka kwa maandiko kama Zaburi
16:10-11 vile imetafsiriwa kwa Bibilia ya Mfalme Yakobo (King James
version), “Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu
wako aone uharibifu. Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko
furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele”.
“Kuzumu” is tafsiri sahihi ya aya hizi. Tafsiri kamili itakuwa
“kaburini”, Yesu alimwambia mwizi aliyekuwa kando yake msalabani “Leo
hivi utakuwa pamoja name peponi”. Mwili wa Yesu ulikuwa kaburini lakini
roho yake ikaenda paradiso. Ndipo akatoa watakatifu wote waliokufa toka
paradiso na kuwapeleka mbinguni. Naamu Bibilia zingine zaweza tafsiri au
waliotafsiri huenda walikosea mahali vile neno la kigiriki la “mahali
pa kuzumuni”, na “kifungoni”
Wengine wako na mtazamo kwamba Yesu alienda “kifungoni” ama “sehemu
ya matezo” ya kuzumuni ili atezwe zaidi kwa ajili ya dhambi zetu. Hili
wazo kamwe si la kibibilia. Ni kifo cha Yesu msalabani na kutezwa kwake
tulipata wokovu. Ni kupitia kwa damu yake iliomwagika ambayo kwayo
tulitakazika kutoka kwa dhambi zetu (1Yohana 1:7-9). Vile alivyo angikwa
msalabani, aliubeba mzigo wa dhambi wa mwanadamu juu ya mabega yake.
Alifanyika mwenye dhambi kwa ajili yetu; “Yeye asiyejua dhambi alimfanya
kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika
Yeye” (2Wakorintho5:21). Kuwepo kwa tuhuma ya dhambi kunatufanya tuelewe
jinsi Yesu alitezeka katika shamba la Gethesemane na kikombe cha dhambi
ambacho kulimwagwa juu yake msalabani.
Wakati Yesu alilia msalabani, “Mungu wangu, Mungu wangu mbona
umeniacha?” (Mathayo 27:46), ni wakati huo alitenganishwa na Baba kwa
sababu ya dhambi zetu zilizotunikwa kwake. Wakati alikata roho, “Ee
Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu” (Luka 23:46). Matezo yake kwa
ajili yetu yalimazika. Roho yake ilienda paradiso/peponi. Yesu hakuenda
kuzumuni/kifungoni. Matezo ya Yesu yaliisha wakati alikufa. mshahara wa
dhambi ulilibwa. Hapo ndipo alingoja kufufuliwa kwa mwili wake na
urejesho wa utukufu wake katika kupaa kwake mbinguni. Je Yesu alienda
kuzumuni? La hasha. Je Yesu alienda sehemu ya kifungoni? Naamu/ndio.
Naomba kuweka sawa Hayo maandiko ya pili sio ya kwangu nimecopy
tu toka sehemu .ili niwashirikishe kujibu swali la Mtumishi Lwembe
Mbarikiwe
Wapendwa,
Kwenye meza hii ya duara naona watu wameamua kweli kweli kuja na mawazo mbalimbali.
Wakati mjadala ukiendelea natamani watu waelewe kutofautisha ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili.
Kuna maneno watu bado wanayachanganya sana. Neno KUZIMU, KABURI,
JEHANAM, MAUTI, KIFO, PARADISO, PEPONI, MBINGUNI, AHERA, SHIMO LA
UHARIBIFU, nk kila mtu afanye zoezi la kuyatazama maana zake kwenye
kamusi ya Kiswahili Sanifu ndipo ajaribu kuyaleta katika maandiko na
katika somo hili.
Kuna watu bado vichwani mwao wakisoma neno, “KUZIMU” akili yao na
mapokeo yao huwapeleka katika “imaginable world” . Ukweli ni kwamba
mapokeo ndiyo yametufundisha hivyo. Lakini KUZIMU lina maana ya KABURI,
SHIMO, AHERA, ENEO LA MATESO, SHIMO LA UHARIBIFU, nk. Haya yote
yalitokana na jinsi wayahudi walivyokuwa wanafundisha enzi hizo na
kanisa la sasa limeyapokea hivyo kwa kuanza kudhania kuwa yana maana ya
kiroho au ulimwengu wa roho. Ukweli ni kwamba wayahudi walijenga ,
“Imaginable world” kwa kila mtu aliyefariki dunia. Wengi walijaribu
kudhania kuwa mtu akifa anaenda eneo la mateso kwa sababu ya kule
kufunika kwa udongo kaburini au kufunikwa kwa mwamba wa jiwe. Mapokeo
haya ndiyo yameendelea kujaa makanisani kwamba mtu akifa ameenda kwenye
mateso. Lakini ukiyachambua maandiko utagundua kwamba siyo sahihi.
Neno , “MAUTI” nalo limeendelea kuwakoroga watu hadi kudhani kuwa
MAUTI ni kama dude fulani au jitu fulani liko mahali fulani na
huwakamata watu na kuwaua. Waislam humwita malaika wa Mauti au “Israeli”
mtoa roho. Hata ukisikiliza mahubiri ya kiislam utagundua kuwa
wanamweleza mtu kuwa roho yake inachomolewa mwilini na kupelekwa mahali
pa mateso “KUZIMU”. Hata wanasema , ADHABU YA KABURI AU MAUTI AIJUA
MAITI”. Yaani maiti awapo kaburini anateswa sana. Yaani anatandikwa
viboko, anageuzwa analia na kusaga meno akiwa kaburini. Hii yote ni
mitazamo ya mapokeo tu.
Mapokeo yanatuonesha kwamba, Waislam na Wakristo wanaamini kwamba mtu
anapofariki kuna kitu kinaitwa “ROHO” huchomoka haraka toka mwilini,
waislam wanasema , “ROHO” huchomoka kwa kupitia kichwani kwa mfano wa
mtu anayechuna ngozi mnyama. Kitu kiitwacho “ROHO” huchomoka mara moja
na kupaa angani, Wakristo wao wanasema “ROHO” hiyo kama ni mwenye haki
inatoka ndani ya mwili unaokufa na kwenda PARADISO au KUZIMU kama
alikuwa siyo mcha Mungu. Mimi naona mitazamo yote hii ni mapokeo tu.
Kama tungejifunza kwa utulivu, tena kwa kutafakari na kujifunza kwa
kina maana na tofauti ya ROHO, NAFSI, MWILI, DAMU, na UHAI wa mwanadam
kwa mtazamo wa SAYANSI na BIBLIA sawia, huenda tungebadilisha mitazamo
na misimamo migumu. Hebu naomba ujielimishe tena juu ya:
MWILI NI NINI? UHAI NI NINI? DAMU NI NINI? PUMZI YA UHAI NI NINI?
ROHO NI NIN? NAFSI NI NINI? MTU NI NINI? MWANADAM INA MAANA IPI?
Naomba wapendwa tujaribu kutafiti maana ya maneno hayo niliyoyataja kwa HERUFI kubwa na kisha tuendelee na mjadala huu.
Millinga
Mpendwa saburi inatakiwa hapo,mafundisho ni mengi mengine ni mapokeo nk
Tunajifunza darasa lina wanafunzi wa viwango mbalimbali,ni vizuri
wapendwa waandike wanayoyafahamu, Swali alilouliza Lwembe ni changamoto
kwa wapendwa wengi,kama ni mapokeo hapa watajifunza kweli itakayo
waweka huru. Basi sisi hapa SG tunao hiyo nafasi ya kutafakari maandiko
kufundisha kweli,ndio maana tupo hapa kujifunza/kufundisha sawasawa na
agizo Math 28:20
Nakubaliana na wewe biblia ya Kiswahili kuna sehemu kaburi wameandika kama kuzimu.
Fahamu Kuzimu hipo hakika sio mapokeo,uliza huko kigoma watakwambia,mimi nimeoa huko.
Maandiko yanaposema bahari itatoa wafu unadhani ni bahari ya kimwili!
hiyo ni moja aina ya kuzimu pahala pa wafu,huko hauwezi kwenda mpaka
uingie ktk ulimwengu wa roho,na watu wanakwenda huko na kurudi,
malango ya kuzimu haitalishinda kanisa, malango kuna nguvu huko za giza amabazo haziwezi kulishinda kanisa.
Roho kuacha mwili sio mapokeo.roho inapotenganaa mwili ndio unaitwa mauti.
Huu mwili ni vazi tu .
Sio lazima uamini,lakini ulimwengu wa roho ni halisi
Barikiwa
Wapendwa
Jana nilisema nikipata nafasi nitapitia yale niliyojifunza huko
nyuma,maandiko yangu ya leo hayana tofauti kubwa na jana nimejaribu
kuongeza maandiko(neno) mbarikiwe
1:HADES kuzimu himaya ya shetani
Kuna sehemu nimekuta wameandika hivi-
*Pande za chini sana hapa ina maana ya neno la Kiyunani Hades au kwa Kiyahudi Sheol, yaani, Kuzimu
Math11: 23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu(pande za chini sana)
.
2:TARTARUS kuna maelezo mengi kidogo…
makao ya malaika walioasi,pahala Yesu alishuka(Math12;40),kwa roho
kutangaza ufalme wa Mbinguni,Pande za chini ya nchi ktk ulimwengu
waroho.ufunuo9:11 wengine wanaiita 911 ile namba ya dharura ya US, kwa
habari ya mfalme wa malaika wa kuzimu abadoni/ Apolioni.
2petro2: 4
Kwa maana kama Mungu hakuwasamehe malaika walipotenda dhambi, bali aliwatupa kuzimu
, katika vifungo vya giza wakae humo mpaka ije hukumu,
Wengine wanatumia 1Pet19-20Yesu aliwaendea wana wa Mungu waliofungwa ambao waliowatamani wana wa binadamu na kuwaoa Mw6:1-7
1Pet3:19-20 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni,
akawahubiri; watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa
ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani
yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.
Hao wana wa Mungu kuna wapendwa wengine wanasema ni wana Seth wakaoa mabinti wa kizazi cha uovu cha kaini
wengine wanasema ni malaika walioanguka kwa kutamani wana wa binadamu
wakiutumia Yuda1:6 malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini
wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele
chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
3:SHEOL waovu wanakaa kwao,watakatifu kwao(kable ya ufufuko wa YESU)
4:SHIMO LISILO NA MWISHO; Lk3;31 ni sehemu ilitenga kuzimu na
Paradiso,mahala pa mateso walio kwenda wanaona,sikia,tambua(wakati wa
agano la kale watu wote walikwenda kuzimu,ila shimo hilo
liliwatenganisha wenye dhambi na wasio dhambi
5:.GEHENNA (Jehenamu) mfano wa ziwa la moto
Lakini kuna haya maandiko
Kumbukumbu32:22 Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu, Unateketea hata
chini ya kuzimu, Unakula dunia pamoja na mazao yake, Unaunguza misingi
ya milima.
Wapendwa wengine wanaamini kama kuzimu ni mahala pa mateso,sijui kama ni sawa au la,
Mimi naamini kuzimu hakuna moto,wengine wanaamini kuna moto na mateso
Barikiwa
Kaka John, Ubarikiwe sana kwa ufafanuzi wa maandiko. Nimebarikiwa.
Somo la mambo ya KUZIMU linakuwa na mjadala mrefu sana na mara nyingi
mjadala usiofika mwisho baina ya wanatelojia na wanazuoni wa maandiko
ya Biblia.
Kama watu wanaamini “KUZIMU” ni ulimwengu wa roho inakuwaje hawa
wanaojiita watafiti wa jiolojia waseme eti walichimba shimo refu sana
kwenda ardhini na kusikia vilio na sauti za watu? Haiwezekani watu
waseme eti KUZIMU ni mahala pasipoonekana kwa macho ya binadam bali ya
rohoni hala watu wengine waibuke na kusema wamechimba ardhini ghafla
wanasikia vilio vya watu walioko KUZIMU. Ina maana kama wangeendelea
kuchimba wangejikuta wanakwenda KUZIMU yaani wangejikuta wanatumbukia
“KUZIMUNI” AU SIYO?
Swala la kusema KUZIMU ni chini ya ardhi hii ambayo ni sayari katika
“universe order” naona kama ni mitazamo HASI (Negative imaginations
towards the truth). Sayari zote zina maumbile yenye muundo wa duara au
kama tufe au tuseme kama yai. Sayari ya Jupter, Mars, Pluto, nk zote kwa
maana nyinge zina KUZIMU ndani yake kama maana inayotafsiriwa ndiyo
hiyo kwamba KUZIMU ni ulimwengu wa roho ulioko chini sana ya SAYARI HII,
“DUNIA”.
Kuna watu pamoja na kwamba wamefundishwa muundo wa sayari na jinsi
Mungu alivyozipanga wanashindwa kuyasoma maandiko na kuyatafsiri kwa
kuzingatia ukweli huo wa muundo wa sayari (Solar Systems). Dunia hii ni
sayari ndogo sana ambayo ndani ya tumbo lake ( stomach of this earth)
hakuna kitu chochote kilichomo zaidi ya mawe, miamba, maji, volkano, na
madongo ya kawaida. Unapokuwa mwalimu wa NENO ukasahau ukweli huu
unakuwa hujaitendea haki ELIMU YAKO HIYO. YA JIOGRAFIA NDOGO TU DARASA
LA 7.
Wapendwa wengi huchanganya mambo. Ukiwasikiliza watakwambia kuhusu
“ULIMWENGU WA ROHO” , ULIMWENGU WA GIZA, KUZIMU, nk. Ukiwauliza wanyoshe
kidole kuonesha huo “ULIMWENGU WA ROHO” ulipo; baadhi wataelekeza
kidole chao angani, wengine watanyamaza kwanza. Kama KUZIMU ni eneo
lililoko katika ulimwengu wa ROHO inajaje tena watu waseme KUZIMU ni
chini ya tumbo la dunia hii tunayokanyaga kila siku?
Mimi naelewa kwamba “ULIMWENGU WA ROHO” huwezi kuuona kwa kutumia
darubini wala macho ya binadam na wala hauwezi kugusika kwa mikono ya
binadamu au ukasafiri kwa magaari ya dunia hii au ndege za Airforce One
na ukasema eti unaenda kuwatembelea walioko “ULIMWENGU WA ROHO”.
Naomba niwaeleze kwamba “ULIMWENGU WA ROHO” ni mahali ambapo binadamu
hawezi kwenda akiwa katika hali ya mwili huu wa damu na nyama. Tafsiri
hii inakwenda hata kwenye swala la KUZIMU. Kama KUZIMU ni ulimwengu wa
roho basi hakuna awezaye kwenda huko hadi abadilishwe kutoka katika
ubinadamu na kwenda katika hali ya ROHO.
Aidha, “ULIMWENGU WA ROHO” hauko katika mfumo wa dunia hii na sayari
zake. yaani, “Spiritual World is the intangible world existing outside
the tangible solar system galaxy”.
Kama tutaelewana kwamba KUZIMU ina maana mbili: 1. KUZIMU = ULIMWENGU
WA ROHO, 2: KUZIMU = SHIMO REFU, AU KABURI LA KAWAIDA, Hapo inaweza
ikaleta mantiki. Lakini kisemantikia itakuwa siyo sahihi kusema KUZIMU
ni eneo wanakoishi watu. Kuna maandiko yasemayo hivyo, nakuomba
uyafafanue kwa uangalifu sana bila kuacha maana ya kimofolojia na
kisemantikia.
Ndugu zangu,
Ninafaidika sana na michango yenu, tena ni fursa kubwa ya kuyajua mambo
haya kwetu sote maana hayo ni makazi! Haitoshi tu kuwa na kiu ya kwenda
mbinguni, bali kuyajua makazi yote itatupa ujasiri wa kuihubiri Injili
katika kiwango cha wahusika kamili, maana ni kweli kuwa Injili
inatuhusu! Basi, kadiri tunavyoliendea jambo hili tutegemee Mungu
kutuongoza katika hilo ili furaha yetu iwe kamili!
Robert, Milinga, Haule na wote, Bwana awatie nguvu kwa kazi
mnayoifanya, maana wanafunzi mnao, tena tuko wengi sana! Kila
niliyejaribu kumuuliza, hakuna mwenye uhakika wa jambo hilo! Inashangaza
lakini huo ndio ukweli. Labda kila mtu roho inakuwa nyeusi kuliongelea
jambo hili au huona ni bora kuzungumzia barabara za dhahabu kuliko moto
au dhiki na hivyo kubaki katika msukumo wenye kuyaepuka mazungumzo yenye
mwelekeo huo!
Mbarikwe nyote, nasi twaendelea kujifunza!!
Mungu tu atusaidie! Wakati wa Lazaro na Tajiri, kule kuzimu,
tajiri alimuomba Ibrahimu atume mtu kutoka kwa wafu ili aje kwa waliio
hai aeleze ubaya wa mateso ya huko kuzimu. Lakini Ibrahimu alisema kuwa
Kama watu hawawezi kuwaamini manabii waliopo huku duniani, hata akija
mtu kutoka kwa wafu, hawawezi kushawishika kwamba kule kuna mateso!
Yahitajika mtu kuikubali Neema ya Wokovu inayohubiriwa katika uhuru
na utashi wa maamuzi. Hizi picha, sijui sauti za kuzimu n.k, kwa mtu
anayepotea bado hawezi kuona kama ni kitu cha mkumshawishi amwamini
Yesu. Nafikiri ndiyo maana hata mitume wenyewe hawakuweka msisitizo wa
mahuburi kwa kuelezea ubaya wa kuzimu bali Uzuri wa Yesu na umuhimu wa
mtu kuwa na ushirika na Mungu!
Kama hapa, ambavyo naona kuna mada imejitokeza juu ya Kuzimu na
Jehanamu. Mi nashauri kuwa inaweza isiwe na msaada sana kufahamu tofauti
ya Kuzimu na Jehanamu, bali la muhimu ni kule kujua kuwa sehemu ambayo
watakwenda wasiomwamini Yesu siyo Nzuri. Iwe Jehenamu, Kuzimu au jina
lolote lile. Ingawa kama alivyosema ndugu Ck Lwembe, jambo hili linaweza
kuongeza ufahamu na ujuzi katika kuihubiri Injili ya kweli!
Mungu atubariki wapendwa tunapoendelea kubadilishana ujuzi wa mambo haya!
Ndugu Millinga ,
Na wote ndugu zangu ktk Bwana , taifa teule miliki yake Bwana.
Kwa kweli sisi wengine tumeokolewa ktk moto(yuda1.23) kwa hiyo hatuwezi
kupenda sawa,,tunajua tunachandika ,tukiona injili nyepesi au wapendwa
wanacheza na wokovu hasira ya Mungu inatuijilia, tunatamani tuchukue
bakora tuwaswage kama mbuzi waingie zizini(ufalme wa Yesu),maana huko
nje wapo mbwa,wachawi na waabudu sanamu.,biblia inavyoandika hivyo
unaona mbwa/wachawi/waabudu sanamu ni kitu kidogo Bwana Yesu anasema
nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika
makanisa.ili tuzifue nguo zetu tuwe na amri ya kuendea mti wa uzima.
Dadi MIllinga ulimwengu wa roho ni halisi(uwe wa Mbinguni au
giza)nyumba tunazo kaa inaweza kuwa ktk ulimwengu wa mwili na pia
ulimwengu wa roho wakati huo huo sasa inategemea ni ulimwengu wa roho
upi Mbinguni au giza,,Mti mfano mwembe unaona ktk ulimwengu wa mwili
ni mti wa matunda lakini ni kitu kingine ktk ulimwengu wa roho,unaweza
panda daladala lakini sio daladala,uliza wachezaji mpira wote
wakivunjika mifupa wowote mwilini kwa nini wanaenda kigoma.
Nikisema haya sio kwamba mimi niliwahi kuwa mchawi la hasha,nimeona
hayo kwa macho yangu na si kuadithiwa wakati nilipokuwa mtu wa ulimwengu
huu,na hata sasa kwenye huu wokovu wangu ninaweza kuwa nasoma biblia
au nipo kwenye laptop ninasoma ghafla ninaweza ona labda kwa mfano tandu
mrefu kama futi moja,nikaingia ktk maombi siku haipiti tukio linatukia
na wala sijiulizi nakamata bakora namaliza na kuchoma moto,ukweli kazi
nilishamaliza ktk ulimwengu war oho pale Roho Mtakatifu
aliponionyesha,sasa inaweza kuwa Yule mdudu tandu ni wa kawaida au wa
giza.
Sasa wakati ukifanya jambo lingine ghafla unawaza ajali,lazima uiingie
ktk maombi nukiacha watu wanapata ajlali,kwahiyo tunaishi kwenye
ulimwengu wa mwili lakini mara unaingizwa katk ulimwengu wa roho,sasa
inategemea tu wewe unatii ishara za Roho Mtakatifu au unazipotezea.
Millinga Ulimwengu wa roho ni halisi.bahati mbaya wakovu wengi hawana uelewa wa ulimwengu wa giza au hawataki.
Nikubaliane na John Paul hii thread na yote yanayojili hapa hayampi
Bwana Mungu utukufu wowote,hayana mashiko,Pia wengine imani yao
haijafikia kiwango hicho ni hadithi tu kwao,Kumbe yatupasa kutafakari
yalio juu Mbinguni,yenye sifa na yakupendeza kusikia yanayo mpa Bwana
Yesu utukufu.
Shika ulicho nacho asije mtu akakunyang’ana taji yako ling’ang’anie
Wapendwa,
Kuzimu, Jehanamu, Mbinguni, Mauti, Roho Mtakatifu nk, mambo yote haya
yamo katika Biblia, kwa hiyo ni Neno la Mungu! Kwa hiyo sioni uhalali wa
kuambiwa kuwa kujadili lolote kati ya hayo hayampi utukufu Mungu au
hayana Mashiko!
Ninavyo fahamu mimi ni kwamba mtoto yeyote asiye zijua kazi za
babaye, hawezi kupewa mamlaka. Jehanamu na kuzimu ni kazi za Mungu, nazo
zinamtukuza yeye; kwa hiyo unaposema hazimtukuzi, inakuwa vigumu kidogo
kukuelewa, kwamba nawe huyajui hayo na hutaki kujifunza, au ni mtu
uliyejitosheleza, au unaogopa kuwa watu watajua kuwa huyajui hayo na
hivyo heshima yako kushuka au … !
Hili la watafiti ni jambo lililotokea. Nayo maelezo yake ndio kama
yalivyo, licha ya upagani wao, lakini conclusion waliyofikia katika
mkasa huo imemuhusisha Mungu, yaani kazi mojawapo ya mkono wake. Kwa
hiyo mtu mwenye shauku ya kulijua jambo hilo katika uhusiano na Mungu,
mimi naamini atamtafuta mwana wa Ufalme ili amjuze zaidi kuhusu tukio
hilo kulingana na kazi ya Baba yake, nayo majibu ya wana wa Ufalme ndio
kama unavyoyaona hapa yakilijibu swali nililoliuliza kutokana na mada
iliyopo!!
Basi, mwana mwenye kuyajua mambo hayo katika ukamilifu, naamini humpa
utukufu zaidi Baba yake kuliko mwana asiyejua ambaye ni rahisi
kujichanganya na kuondolewa katika njia ya kweli!!
Zitukuzwe kazi za Bwana wetu, maana hizo humtukuza yeye!
Shalom! jamani naomba kuuliza ivi shetani yuko duniani tu au
ulimwengu mzima?? kama yupo duniani inamaana nikiwa sayari nyingine
nimepona ,majaribu na hali ya kipepo? na neno linaposema shetani
alishushwa chini ina maana chini ya ninini??
barikiweni, naendelea kujifunza hapa
Mpendwa John Haule,
Nashukuru kwa kutushirikisha uzoefu wako enzi hizo ulipokuwa kuzimuni
yaani kwa shetani. Hongera kwa kuendelea mbele na nakuombe mwisho
mwema.
Mimi sijasema kwamba “ULIMWENGU WA ROHO” siyo HALISI. Labda
hukunielewa vyema. Soma tena maelezo yangu kwa makini. Ikiwezekana soma
mstari kwa mstari (read between lines).
Mimi nakubaliana na wewe mia kwa mia. Ulimwengu wa roho ni halisi
wala siyo porojo za watunga zaburi za bongo(Bongo Flavor). Ulimwengu wa
roho upo.
Mimi ninachojaribu kuwaeleza wapendwa ni kwamba waondokane na kasumba
ya kufikiri yasiyofikirika katika ulimwengu usiofikirika wala
kumithilika (Thinking of non-existing creatures in the imaginable
tangible or intangible world).
Tuondokane na kusonta kidole kwa kusema, “……mbinguni ni kuleeeeeee……”
au “…….. kuzimu ni paleeee, eti ukichimba futi kiasi fulani tu unafika
kuzimu, kwani kuzimu si ni kule baharini tu, au makaburini…….”. Hayo ni
baadhi ya maneno utakayosikia mtaani.
Kuna kipindi (nafikiri had leo hii) Waislam waliamini kwamba MWEZINI
ni mahali alnapokaa Mungu. Ndiyo maana alama ya mwezi wanaitumia sana.
Waliamini kwamba Mwezi ni mahali patakatifu sana alipo Mungu wao.
Ilipofika wanaanga wa Kimarekani na Urusi kukanyaga mwezini wakamaka
wakisema, “……Astaghafullah….” yaani hawa makafiri wamekanyaga nyumbani
kwa mwenyezi Mungu? Wanaukanyaga mwezi.
Mimi najaribu kuwarekebisha wapendwa wa Bwana wanaodhani kwamba huko
chini ya ardhi ndiko yaliko makao makuu ya shetani kwa sababu tu
Maandiko yanasema hivyo. Biblia hata ikisema kwamba Ibilisi ametupwa
chini au kuzimuni watu wasikimbilie kuelewa kwamba ni chini hapa juu ya
ardhi yetu. Maana ya chini yaweza kumaanisha tofauti na hiyo. Ibilisi
kutupwa kifungoni au kuzimu ni misamiati tu yenye kuonesha adhabu
aliyopewa lakini haina maana kwamba ukichimba ardhini utamwona. IBILISI
Kutupwa chini au KUZIMUNI inamaanisha kushushwa cheo na kulaani na Mungu
kwa kunyang’anywa mamlaka aliyokuwa nayo.
Kwa watu walioajiriwa wanaelewa kwamba mtu aweza kushushwa cheo kama
alikuwa juu akawa chini (sema kuzimu ukipenda) na mtu aweza kupandishwa
juu kwa cheo. Ibilisi naye alishushwa chini kwa maana ya cheo alichokuwa
anacho mbinguni na maandiko yasemapo ameshushwa chini haina maana
kwamba ni chini hapa kwenye ardhi ya dunia hii bali ni katika Ulimwengu
wa roho kabisa na wala siyo duniani. Biblia inaposema ametupwa duniani
na ana hasira nyingi na ole wa dunia kwa kuwa Ibilisi ametupwa chini ina
maanisha hasira zake za kunyang’anywa cheo chake anazielekeza kwa
viumbe wote wa Mungu kokote waliko ili awakoshe raha na fursa ya kuishi
na Mungu.
Neno KUZIMU limetumika kama neno linalowakilisha adhabu aliyopewa.
Hivi hujaona baadhi ya Mawaziri wa Kikwete walioshushwa chini (waweza
kusema kuzimu ukipenda) walivyokasirika sana hata wakawaendea wapiga
kura wao na kuanza kujiosha na kujikosha wao kama vile hawana makosa.
Unamkumbuka aliyekuwa waziri Mkuu Edward Lowasa alivyopokelewa kwao kwa
bashasha na nderemo na akaanza kujiosha ile kashifa ya Richmond?
Unamkumbuka Endrew Chenge wa Bariadi aliposhushwa chini kiutawala
alivyokasirika? Unakumbuka hata sasa alivyo na hasira kwa wapinzani
wake? Huku ndiko kushushwa chini hata kuzimu.
Kwa jinsi hiyo basi naomba nitofautiane na wale wote wenye dhana
potofu kwamba KUZIMU iko chini ya ardhi ya sayari hii tunayokanyaga na
niwaombe wakubaliane na mimi kwamba “KUZIMU” ni neno linalotumiwa
kumaanisha adhabu anayopewa mtu au sehemu inayopatikana katika ulimwengu
wa roho (invisible and spiritual world) wanakokaa watu walioshushwa
vyeo vyao vya kiroho (yaani kutengwa na Mungu milele) na hapo ndipo
alipo Ibilisi na malaika zake wote walioshushwa chini kivyeo. Lakini
usiondoke hapa ukielewa kwamba kushushwa huku ni katika kudondoka toka
mbinguni (anga tunaloliona juu) na kudondokea chini hapa tunapoishi na
kujenga majumba.
Mjadala unaendelea, wote tunajifunza Neno. Mtalaam wa Neno ni Mungu tu.
Si kweli maelezo yako nimesoma vizuri lakin hakuna uhalisia
wowote , hujatoa maelezo ya kutosha kama picha na sauti ni vitu ambavyo
tuna viona na kusikia katika movies za kutisha hizo picha na sauti za
kufikirika tu…
Oh Haleluya, Hakika Mungu hana upendeleo, maana alitaka hata hao
wasiomwamini Mungu (ambao ni wanasayansi) wajue kuwa kuzimu na mashetani
yake yake wapo,na Mungu naye yupo. Ili ujue kuchagua utakaye mtumikia.
Usipoamini kuwa Mungu yupo kuzimu inakusubiri, ukimwamini Mungu na
kutenda mema Mbingu ni yako.
Kataa kubali Mungu yupo, na Shetani naye yupo,Uamuzi ni wako wewe upingae
eeee MUNGU wangu nabadilika sitaji kushurutishwa tenaaaaaaa
Haya ndiyo mafundisho potofu ya wachungaji walio wengi, eti mtu
anapokufa, anakuwa anaendelea na maisha sehemu fulanni-kuzimu.
Upotoshaji mkuu kiasi gani!!! Biblia haifundishi hivyo.
Umebaki muda mfupi, watawafundisheni kuwa, walioko kuzimu, wameshajenga
nyumba za ghorofa, wanafanya ujasiliamali nk. Wanacheza sana na akili za
watu tu!!
Msiposoma neno la Mungu vizuri wapendwa, hatima yenu ni tete, labda Mungu afanye muujiza tu!! Tuombeane sote
wapendwa fahamuni kwamba biblia sio gazeti,hivi Mungu mnadhania
nimwanadamu?maeneno yake hayapiti kamwe,kama huamini kama wafu wakifa
hawana mahala pakuhifadhiwa,isingewezekana Musa na Eliya kumtokea
Yesu,isingewezekana mashahidi 2 waufunuo watakuja,hivyo tunamfanya yesu
kuwamwongo kama hana watakatifu sehemu flani.pia kifocha musa utaona
shetani anangangania roho ya musa,apeleke wapi kama hakuna mahala
waendako wafu?achiliambali mf.wa tajiri na lazaro,ikowazi kuwa mungu
huwatumia watakatifu wake ktk mambo yake kamatulivyoona,sasa ona kuwa
mtuafapo hawina mwilihuu wanyama nahilindolinalo sumbua mawazo
yetu.mwone Sauli na yule mchawi wa endor kama wafuhawana mahali na
kumbukumbu kwa nini samwel atokee na aliishakufa?hivyo Roho ndugu haifi
walakupotea bali mwili hurudia mavumbi.walio wa rohoni wanajua lakini
wengine litabakia fumbo tu, Mungu akamfanya mtu kwa mf.wake sasa utaona
mungu niroho,hivyo twafanana naye kwa jinsi ya roho,sasa utaona namna
gani mtu hapotei ila hudumu kungoja hukumu,nakinachohukumiwa ni roho.
Je, Kuzimu ndiko Jehanamu?
Aliye na uelewa mzuri anisaidie ili niweze kulielewa vizuri tukio hili!
Somo hili la kuzimu bado ni miongoni mwa mada ninazoziita zenye mitazamo mingi baina ya wapendwa na wanazuoni wa Biblia. Fuatana nami hapa uone maana ya kuzimu na ulinganishe na huo utafiti ambao bado hata mimi sijauamini.
KUZIMU NI NINI AU TOFAUTI YA KUZIMU NA JEHANAMU NI IPI?
Wazo la kuzimu kwa watu wengi ni mahala pa adhabu kwa’roho zisizopatwa na kifo’ za wabaya moja kwa moja baada ya kufa, au mahala pa kuteswa wale ambao watakataliwa. Ni tendo letu la kusadikisha kwamba Biblia inafundisha kuwa kuzimu ni kaburi, mahali watu wote wanakwenda wakifa.
Ni neno lisilotumika sana katika misemo ya watu, awali katika Kiebrania neno’Sheol’ limetafsiriwa’hell’ kwa kiingereza. kwa hiyo Biblia ya kiswahili ilipoandikwa tafsiri toka kiingereza neno liliandikwa’Kuzimu’ likiwa na maana’mahala pa kuzika wafu’ Leo watu wametoa habari zinazotofautiana na Biblia inavyoelezea kuhusu neno kuzimu. Biblia yetu ya kiswahili hapa Afrika Mashariki ni U.V ikiwa na maana kuwa ni tafsiri tofauti -tofauti toka Biblia mbali mbali za kiingereza ambazo ni K.J.V, R.S.V, R V n.k sasa hivi Biblia zilizopo kwa kiswahili ni U.V na Biblia habari njema kiswahili cha kisasa kwa kifupi (B.H.N) mifano michache ambayo katika Biblia hili neno’Kuzimu’ limetafsiriwa’kaburi’ linafanya wazo la watu wengi kutofaa kuhusu kuzimu kuwa ni mahala pa ziwa la moto na kuteswa wabaya ni: -
“E e BWANA, …….. wasio haki wanyamaze kuzimu” (Zab. 31:17).
“Bali BWANA ataikomboa nafsi yangu, atanitoa mikononi mwa kuzimu – Kaburi (Zab. 49:15) yaani nafsi ya Daudi au mwili atafufuliwa toka kaburini, au kuzimu’.
Imani ya kuwa kuzimu ni sehemu ya kuadhibiwa wabaya mahala ambapo hawawezi kuepuka haiwezi kupatana na hii; mtu mwenye haki anaweza kwenda kuzimu (Kaburini) na kutoka tena. Hosea 13:14 anathibitisha hivi: “Nitawakomboa (watu wa Mungu) na nguvu za kaburi (kuzimu); nitawaokoa na mauti” mstari huu umenukuliwa katika 1 Kor. 15: 55 unahusu ufufuo Kristo akirudi. vivyo hivyo katika maono ya ufufuo wa pili (ona somo la 5. 5) “mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwemo ndani yake” (Uf. 20:13). Tazama mfano kati ya mauti yaani, Kaburi, na kuzimu (pia ona zaburi 6:5).Maneno ya hana katika 1 Sam. 2:6 yapo wazi kabisa: “BWANA huua naye hufanya kuwa hai (Kwa njia ya ufufuo): hushusha hata kuzimuni (kaburini), tena huleta juu”.Kwa kuwa’kuzimu’ ni kaburi itegemewe kwamba wenye haki wataokolewa kutoka hilo kwa njia ya kufufuliwa kwao kupata uzima wa milele. Hivi inawezekana kabisa kuingia’Kuzimu’ au kaburini, na baadae kuliacha kwa njia ya ufufuo. Mfano mkubwa ni huo wa Yesu, ambaye roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukupata kuoza’ (mdo. 2:31).wa sababu alifufuliwa. Angalia usambamba kati ya’roho’ ya Kristo na’mwili’ wake. kama mwili wake “haukuachwa kuzimu” ni kudokezwa kuwa alikuwako huko kwa kipindi, yaani, siku tatu ambazo mwili wake ulikuwamo kaburini. Kama Kristo alikwenda’kuzimu’ uwe ushahidi wa kutosha kwamba sio sehemu wanako kwenda wabaya.
Watu wote wabaya na wazuri wanakwenda’Kuzimu’ yaani kaburini. Hivyo Yesu “Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya” (Isa. 53:9) kwa kufuatana na mstari huu, ipo mifano mingine mingi ya watu wenye haki kwenda kuzimu, yaani kaburini. Yakobo alisema ya kwamba “nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu (kaburini) …. Akamlilia” Yusufu (Mwa. 37:35).
Ni moja ya mambo ya awali ya Mungu ya kuwa adhabu kwa ajili ya dhambi ni mauti (Rum 6:23;8:13;Yakobo 1:15). Hapa kwanza tumeonyesha mauti ni hali ya kutokuwa na fahamu kabisa. Dhambi husababisha kuangamia kabisa, sio kuteswa milele (math. 21:41;22:7; Marko. 12:9; Yakobo 4:12), hakika kama watu walivyoangamia kwa gharika (Luk. 17: 27, 29), Kama waisraeli walivyokufa jangwani (1 Kor. 10:10). katika sehemu zote hizi watenda dhambi walikufa kuliko waliteswa milele. Basi haiwezekani kwamba wabaya wanaadhibiwa wakiwa na fahamu kwa mateso na kuona.
Vile vile tumeona kuwa Mungu hahesabu dhambi – au kutuweka katika taarifa ikiwa hatujui neno lake (Rum 5:13). Walio katika nafasi hii watasalia wakiwa wafu. Walio kwisha jua matwaka ya Mungu watafufuliwa na kuhukumiwa Kristo akirudi. Ikiwa wabaya adhabu wanayopata itakuwa ni kifo, kwa sababu hii ni hukumu kwa ajili ya dhambi. Kwa sababu hii baada ya kuja mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, wataadhibiwa na kisha kufa tena, kubaki katika kifo milele. Hii itakuwa ni’Mauti ya pili’ iliyosemwa katika ufu. 2:11; 20:6. Watu hawa walikuwa wamekufa mara ya kwanza, kifo cha kutokuwa na ufahamu kabisa. Watafufuliwa na kuhukumiwa Kristo akirudi, na kisha kuadhibiwa na mauti ya pili, ambayo, kama mauti yao ya kwanza, hawatakuwa na ufahamu kabisa. Hii itadumu milele.
Ni katika maana hii ya kuwa adhabu kwa ajili ya dhambi ni ya’milele’, katika hiyo haitakuwa na mwisho mauti yao. Kubaki wafu milele ni adhabu isiyo na mwisho. Mfano wa Biblia kutumia aina hii ya maelezo yanapatikana katika K/Torati 11:4. Huu unaeleza Mungu akiwaangamiza mara moja Jeshi la Farao katika Bahari ya shamu milele, maangamizi yanayoendelea ni kama hasa jeshi hili halikurudia tena kuwasumbua Israeli, “alivyowafunikiza na maji ya Bahari ya Shamu …….. alivyowaangamiza BWANA hata hivi leo”.
Hata katika nyakati za awali za Agano la Kale waamini walielewa kwamba kutakuwa na ufufuo siku ya mwisho, ambapo waovu wanaowajibika watarudi kaburini. Ayu. 21:30,32 yupo wazi sana: “Kwamba mwovu …… na kuongozwa nje (Yaani kufufuliwa) katika siku ya Adhabu ….. pamoja na hayo atachukuliwa (kwenda) kaburini”. Moja ya mifano ya mahubiri kuhusu kurudi kwa Kristo na hukumu inazungumzia wabaya’Kuchinjwa’ mbele yake (Luk. 19: 27). Mfano huu ni shida kufaa katika wazo la wabaya wanaishi milele katika hali ya kuwa na fahamu daima wakipokea mateso. Kwa vyovyote hii itakuwa ni adhabu isiyo na maana – mateso ya milele kwa matendo ya miaka 70. Mungu haoni raha kuwaadhibu watu wabaya; basi inategemewa kuwa hatawapa adhabu isiyo na mwisho. (Ezek. 18:23, 32; 33:11; 2 Pet. 3:9).
Ufalme wa Kikristo ulioiacha imani mara nyingi unajumuisha’kuzimu’ na wazo la moto na mateso. wazo hili hutofautiana vikali na mafunzo ya Biblia kuhusu kuzimu (kaburi). “Kama kondooo wamewekwa kwenda kuzimu (kaburini); na mauti itawachunga” (Zab. 49:14) inadokeza ya kuwa kaburi ni mahala pa usahaulifu kwenye utulivu. Mbali ya roho ya Kristo, au mwili kuwa kuzimu kwa siku tatu, haukuachwa uoze (Mdo. 2:31) isingewezekana kama kuzimu ni mahala pa moto.
Ezek. 32: 26- 30 inatoa picha ya mashujaa wa vita wa mataifa yaliyowazunguka, wanalala kwa amani katika makaburi yao: “Mashujaa wao ….. walioanguka (katika vita) walioshuka kuzimu pamoja na silaha zao za vita: ambazo wameweka panga chini ya vichwa vyao ….. wamelala ….. pamoja nao washukao shimoni”Hapa tunatajiwa desturi za mashujaa kuzikwa na silaha zao na kukilaza kichwa cha maiti juu ya upanga wake. Lakini haya ni kueleza’Kuzimu’ – kaburi. Hawa watu mashujaa bado wanalala kuzimu (yaani, kaburini) ni shida kusaidia wazo la kuwa kuzimu ni sehemu ya moto.
Vitu vya mwili (kwa mfano, mapanga) kwenda sehemu moja “kuzimu” kama watu, ikionyesha kwamba kuzimu sio uwanja wa mateso ya kiroho. Hivyo Petro alimwambia mtu mwovu, “Fedha yako na ipotele mbali pamoja nawe (mdo. 8:20) Taarifa ya yaliyompata Yona yanapinga hili. Akiisha mezwa hai na samaki mkubwa, “Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki akisema, Nalimlilia Bwana …. Katika tumbo la kuzimu naliomba” (Yona. 2:1,2).’Tumbo la kuzimu’ hili ni sambamba na hilo la nyangumi. Tumbo la nyangumi kweli palikuwa ni’mahala pa uficho’ ambayo ndiyo maana ya neno msingi’Kuzimu’ lililotafsiriwa’kaburi’ Ni wazi haikuwa ni sehemu ya moto, Yona alitoka nje ya “tumbo la kuzimu” hapo nyangumi alipomtapika. Jambo hili lililenga mbele kwenye ufufuo wa Kristo toka’kuzimu’ (kaburini) – ona Mathayo 12:40.
Nadhani maelezo haya kwa leo yanatosha. Baadaye nitawaletea zaidi kuhusu mada hii kwani mjadala unaendelea.
Najua kwa sehemu haya ninayoandika unayafahamu ninaandika nikikumbuka wengine hawana ufahamu nao waupate ili tufaidiane kwa yale tunayoamini ktk imani yetu.
Jehanamu ni neno la kiarabu/Kiswahili
Waebrania wanaita gehenna
Gehenna ni bonde nje kidogo ya Yerusalem,
hilo eneo walikuwa watupa takataka tuseme dampo,sasa moto hapo ulikuwa hauzimiki,Yesu alilitumia jina gehenna kama mfano kuwa waovu ambao wameuasi Mungu wataupwa kwenye moto usiozimika milele(ZIWA LA MOTO) kwa mfano wa huo moto wa dampo la gehenna.
kwa sehemu nafahamu kuna kitu kinaitwa sheol na hedes,
hedes ni sehemu walikufungiwa wale malaika walioasi ,lusifa yuko huko angani sijui mbingu ya ngapi(mkuu wa anga) yeye bado hajafungwa ndio maana kuna OLE kwa walio duniani maana Lusifa anajua kuwa ana siku chache kabla ya kifungo ufunuo 20:1-3.naye ataafungiwa kuzimu miaka elfu.
Sheol ni pahala ktk ulimwengu wa wafu walikokaa wateule/watakatifu kabla ya ukombozi wa Bwana yetu yesu kristo,ambayo ndio ile paradiso ya sasa wateule/watakatifu wakisubiri ule utawala wa miaka elfu wa Bwana Yesu.
kabla watu upande mmoja wa sheol kuamishwa na kupelekwa mbingu ya tatu(paradise) pale Bwana Yesu alipopaa na kuteka mateka,
sheol ni kifungo kwa wafu wote waliolala watakaokolewa na watakao angamizwa upande mwingine, mf (Lazaro na tajiri)siku ya hukumu
.
kuzimu hakuna moto,ni eneo la kusubiri hukumu.
Jehenamu(ziwa la moto) ni Mauti ya pili kwao walioasi/wasio haki,Lucifa na wajumbe wake baada ya hukumu ya wafu
Jehenamu ni eneo halisi ktk ulimwengu wa roho
Kuzimu ni eneo halisi ktk ulimwengu wa roho
Inawezeka nachanganya majina maana kuna greek/Hebrew hapo,Wapendwa mnaweza kunisaidia kuweka sawa lugha ya majina kuna majina kama 5 yanayozungumzia neno kuzimu na maana zake.
Nikipata nafasi nitapitia maandiko nitakuja na usahihi Bwana akipenda
Barikiwa
Ufunuo 20:10 “Na yule ibilisi mwenye kuwadanganya,akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti,alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo.Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele”
Nimewahi kuona mafundisho fulani kwenye kipeperushi ambayo yalisema moto upo lakini unaunguza mara moja tu na kuzimika. Nilisikitika sana nilitamani hata tuonane uso kwa uso na mwandishi ili tuliangalie neno kwa pamoja.
Wapo pia wanaofundisha kuwa Mungu kwa huruma yake aliyo nayo hawezi kuwaandalia wanadamu moto uwakao kila siku na kuwatesa. Hili nalo pamoja na mengine mengi na mengine bado yanakuja ni mafundisho ya shetani.Lengo lake likiwa ni upotoshaji wa neno la Mungu.
Hata hapo juu ndugu Milinga kuna mambo umeyataja kwangu mimi nimeyaona kama ni mkanganyiko.
Kama watu wote wanaenda kuzimu ina maana hata Musa na Eliya walivyoonekana wakisema na Bwana Yesu walitoka kuzimu?Mathayo 17:3 ,Marko 9:4
Ndugu Milinga kuzimu siyo kaburi kama hili inamowekwa miili hii ya duniani.Kaburi hili la kwaida la kuzikia wafu hapa duniani linaonekana kwa macho yaani liko katika ulimwengu wa mwili lakini kuzimu haionekani kwa macho ya nyama maana iko katika ulimwengu wa roho.Kwa taarifa yako huko ndiko aliko shetani pamoja na majeshi yake(mapepo na roho zote chafu).
Hapa nanukuu baadhi ya maneno yako “Kwa vyovyote hii itakuwa ni adhabu isiyo na maana – mateso ya milele kwa matendo ya miaka 70. Mungu haoni raha kuwaadhibu watu wabaya; basi inategemewa kuwa hatawapa adhabu isiyo na mwisho. (Ezek. 18:23, 32; 33:11; 2 Pet. 3:9).”
Hii si kweli kabisa! ni kweli kabisa Mungu hafuraii kufa kwa muovu au mateso yake ndiyo maana kasema mwenyewe tuchague uzima,tuchague kuishi na ametoa utaratibu utupasao.Kumbukumbu la Torati 30:19-20
Mungu amefanya jitihada nyingi sana kumuokoa mwanadamu hadi akaitoa nafsi yake ife kwa ajili ya wenye dhambi sasa kama mwenye dhambi hataki kutubu na kuacha dhambi Mungu afanyeje?kumbuka dhambi ni uasi na ni mauti unapotenda dhambi huitwi tena mwana wa Mungu ila unakuwa mwana wa ibilisi hivyo usipotubu utaungana nae ibilisi kwenye ile adhabu inayomsubiri.
Nanukuu tena maneno yako:
“Watu hawa walikuwa wamekufa mara ya kwanza, kifo cha kutokuwa na ufahamu kabisa. Watafufuliwa na kuhukumiwa Kristo akirudi, na kisha kuadhibiwa na mauti ya pili, ambayo, kama mauti yao ya kwanza, hawatakuwa na ufahamu kabisa. Hii itadumu milele.”
Ndugu Milinga unamaanisha nini unaposema kifo cha kutokuwa na ufahamu kabisa? Je roho inakufa?
Maisha yajayo tunayoyatarajia kwa imani ni maisha ya milele.Hii ina maana kwamba watakaokwenda mbinguni wataishi milele na hata wale watakaokuwa jehanamu maisha yao humo ni ya milele na fahamu na hisia zote wanakuwa nazo kama kawaida. Sasa napata shida kukuelewa unaposema kwamba mtu aadhibiwe milele kwa dhambi aliyotenda kwa muda miaka 70 tu. Hapa inaonyesha kuwa unajaribu kucompromise na Mungu kwamba si haki. Hukumu za Mungu ni za haki
Zaburi 98:9, Zaburi 119:137
Katika bibilia ya Kiibrania neno ambalo limetumika kuelezea ulimwengu wa wafu ni sheol. Linamaanisha “mahali pa wafu” au “mahali pa roho/mioyo iliyotuacha” Neno la kigiriki katika Agano Jipiya limetumika kusimamia ni “kuzumuni” ambalo pia lamaanisha “mahali pa wafu” maandiko mengine katika Agano Jipiya yanaonyesha kuwa “kuzumu” ni mahali pa muda, ambapo roho zinawekwa zinapongoja ufufuo na hukumu ya mwisho. Ufunuo 20:11-15 unatupa tofauti halisi kati ya maneno hayo mawili kifungoni (sheol) na kuzumuni (hades). Jehanamu (ziwa la moto) ni mahali pa kudumu na hukumu ya mwisho kwa wanaoangamia. Kuzimuni ni mahali pa muda. Kwa hivyo, la! hasha Yesu hakuenda kuzumuni kwa sababu kuzumuni ni ulimwengu ujao ndio neno hilo litakapokuwa likitumika baada ya kiti cheupe cha hukumu (Ufunuo 20:11-15).
Kuzumu ni ulimwengu umegawa mara mbili (Mathayo 11:23, 16:18; Luka10:15, 16:23; Matendo ya Mitume 2:27-31), mahali pa watakaokolewa na wanao angamia. Mahali pa watakaokolewa paliitwa “paradiso” na ni “kifua cha Abrahamu”. Mahali pa watakaokolewa na watakaoangamia pametenganishwa na “shimo kubwa” (Luka 16:26). Wakati Yesu alipaa mbunguni, aliwachukua wa hudumu wa paradiso waliokuwa waumini pamoja naye kwenda mbunguni (Waefeso 4:8-10). Mahali pa kuzumuni hapakubadilishwa. Wafu wote wasioamini walienda huko wakingoja hukumu yao ya mwhisho ambayo inakuja. Je Yesu alienda kifungoni mahali roho zilikuwa zikingoja hukumu?. Ndio kulingana na (Waefeso 4:8-10 na 1Petero 3:18-20).
Baadhi ya wasiwasi imechibuka kutoka kwa maandiko kama Zaburi 16:10-11 vile imetafsiriwa kwa Bibilia ya Mfalme Yakobo (King James version), “Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu. Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele”. “Kuzumu” is tafsiri sahihi ya aya hizi. Tafsiri kamili itakuwa “kaburini”, Yesu alimwambia mwizi aliyekuwa kando yake msalabani “Leo hivi utakuwa pamoja name peponi”. Mwili wa Yesu ulikuwa kaburini lakini roho yake ikaenda paradiso. Ndipo akatoa watakatifu wote waliokufa toka paradiso na kuwapeleka mbinguni. Naamu Bibilia zingine zaweza tafsiri au waliotafsiri huenda walikosea mahali vile neno la kigiriki la “mahali pa kuzumuni”, na “kifungoni”
Wengine wako na mtazamo kwamba Yesu alienda “kifungoni” ama “sehemu ya matezo” ya kuzumuni ili atezwe zaidi kwa ajili ya dhambi zetu. Hili wazo kamwe si la kibibilia. Ni kifo cha Yesu msalabani na kutezwa kwake tulipata wokovu. Ni kupitia kwa damu yake iliomwagika ambayo kwayo tulitakazika kutoka kwa dhambi zetu (1Yohana 1:7-9). Vile alivyo angikwa msalabani, aliubeba mzigo wa dhambi wa mwanadamu juu ya mabega yake. Alifanyika mwenye dhambi kwa ajili yetu; “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye” (2Wakorintho5:21). Kuwepo kwa tuhuma ya dhambi kunatufanya tuelewe jinsi Yesu alitezeka katika shamba la Gethesemane na kikombe cha dhambi ambacho kulimwagwa juu yake msalabani.
Wakati Yesu alilia msalabani, “Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?” (Mathayo 27:46), ni wakati huo alitenganishwa na Baba kwa sababu ya dhambi zetu zilizotunikwa kwake. Wakati alikata roho, “Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu” (Luka 23:46). Matezo yake kwa ajili yetu yalimazika. Roho yake ilienda paradiso/peponi. Yesu hakuenda kuzumuni/kifungoni. Matezo ya Yesu yaliisha wakati alikufa. mshahara wa dhambi ulilibwa. Hapo ndipo alingoja kufufuliwa kwa mwili wake na urejesho wa utukufu wake katika kupaa kwake mbinguni. Je Yesu alienda kuzumuni? La hasha. Je Yesu alienda sehemu ya kifungoni? Naamu/ndio.
Mbarikiwe
Kwenye meza hii ya duara naona watu wameamua kweli kweli kuja na mawazo mbalimbali.
Wakati mjadala ukiendelea natamani watu waelewe kutofautisha ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili.
Kuna maneno watu bado wanayachanganya sana. Neno KUZIMU, KABURI, JEHANAM, MAUTI, KIFO, PARADISO, PEPONI, MBINGUNI, AHERA, SHIMO LA UHARIBIFU, nk kila mtu afanye zoezi la kuyatazama maana zake kwenye kamusi ya Kiswahili Sanifu ndipo ajaribu kuyaleta katika maandiko na katika somo hili.
Kuna watu bado vichwani mwao wakisoma neno, “KUZIMU” akili yao na mapokeo yao huwapeleka katika “imaginable world” . Ukweli ni kwamba mapokeo ndiyo yametufundisha hivyo. Lakini KUZIMU lina maana ya KABURI, SHIMO, AHERA, ENEO LA MATESO, SHIMO LA UHARIBIFU, nk. Haya yote yalitokana na jinsi wayahudi walivyokuwa wanafundisha enzi hizo na kanisa la sasa limeyapokea hivyo kwa kuanza kudhania kuwa yana maana ya kiroho au ulimwengu wa roho. Ukweli ni kwamba wayahudi walijenga , “Imaginable world” kwa kila mtu aliyefariki dunia. Wengi walijaribu kudhania kuwa mtu akifa anaenda eneo la mateso kwa sababu ya kule kufunika kwa udongo kaburini au kufunikwa kwa mwamba wa jiwe. Mapokeo haya ndiyo yameendelea kujaa makanisani kwamba mtu akifa ameenda kwenye mateso. Lakini ukiyachambua maandiko utagundua kwamba siyo sahihi.
Neno , “MAUTI” nalo limeendelea kuwakoroga watu hadi kudhani kuwa MAUTI ni kama dude fulani au jitu fulani liko mahali fulani na huwakamata watu na kuwaua. Waislam humwita malaika wa Mauti au “Israeli” mtoa roho. Hata ukisikiliza mahubiri ya kiislam utagundua kuwa wanamweleza mtu kuwa roho yake inachomolewa mwilini na kupelekwa mahali pa mateso “KUZIMU”. Hata wanasema , ADHABU YA KABURI AU MAUTI AIJUA MAITI”. Yaani maiti awapo kaburini anateswa sana. Yaani anatandikwa viboko, anageuzwa analia na kusaga meno akiwa kaburini. Hii yote ni mitazamo ya mapokeo tu.
Mapokeo yanatuonesha kwamba, Waislam na Wakristo wanaamini kwamba mtu anapofariki kuna kitu kinaitwa “ROHO” huchomoka haraka toka mwilini, waislam wanasema , “ROHO” huchomoka kwa kupitia kichwani kwa mfano wa mtu anayechuna ngozi mnyama. Kitu kiitwacho “ROHO” huchomoka mara moja na kupaa angani, Wakristo wao wanasema “ROHO” hiyo kama ni mwenye haki inatoka ndani ya mwili unaokufa na kwenda PARADISO au KUZIMU kama alikuwa siyo mcha Mungu. Mimi naona mitazamo yote hii ni mapokeo tu.
Kama tungejifunza kwa utulivu, tena kwa kutafakari na kujifunza kwa kina maana na tofauti ya ROHO, NAFSI, MWILI, DAMU, na UHAI wa mwanadam kwa mtazamo wa SAYANSI na BIBLIA sawia, huenda tungebadilisha mitazamo na misimamo migumu. Hebu naomba ujielimishe tena juu ya:
MWILI NI NINI? UHAI NI NINI? DAMU NI NINI? PUMZI YA UHAI NI NINI?
ROHO NI NIN? NAFSI NI NINI? MTU NI NINI? MWANADAM INA MAANA IPI?
Naomba wapendwa tujaribu kutafiti maana ya maneno hayo niliyoyataja kwa HERUFI kubwa na kisha tuendelee na mjadala huu.
Mpendwa saburi inatakiwa hapo,mafundisho ni mengi mengine ni mapokeo nk
Tunajifunza darasa lina wanafunzi wa viwango mbalimbali,ni vizuri wapendwa waandike wanayoyafahamu, Swali alilouliza Lwembe ni changamoto kwa wapendwa wengi,kama ni mapokeo hapa watajifunza kweli itakayo waweka huru. Basi sisi hapa SG tunao hiyo nafasi ya kutafakari maandiko kufundisha kweli,ndio maana tupo hapa kujifunza/kufundisha sawasawa na agizo Math 28:20
Nakubaliana na wewe biblia ya Kiswahili kuna sehemu kaburi wameandika kama kuzimu.
Fahamu Kuzimu hipo hakika sio mapokeo,uliza huko kigoma watakwambia,mimi nimeoa huko.
Maandiko yanaposema bahari itatoa wafu unadhani ni bahari ya kimwili! hiyo ni moja aina ya kuzimu pahala pa wafu,huko hauwezi kwenda mpaka uingie ktk ulimwengu wa roho,na watu wanakwenda huko na kurudi,
malango ya kuzimu haitalishinda kanisa, malango kuna nguvu huko za giza amabazo haziwezi kulishinda kanisa.
Roho kuacha mwili sio mapokeo.roho inapotenganaa mwili ndio unaitwa mauti.
Huu mwili ni vazi tu .
Sio lazima uamini,lakini ulimwengu wa roho ni halisi
Barikiwa
Jana nilisema nikipata nafasi nitapitia yale niliyojifunza huko nyuma,maandiko yangu ya leo hayana tofauti kubwa na jana nimejaribu kuongeza maandiko(neno) mbarikiwe
1:HADES kuzimu himaya ya shetani
Kuna sehemu nimekuta wameandika hivi-
*Pande za chini sana hapa ina maana ya neno la Kiyunani Hades au kwa Kiyahudi Sheol, yaani, Kuzimu
Math11: 23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu(pande za chini sana)
.
2:TARTARUS kuna maelezo mengi kidogo…
makao ya malaika walioasi,pahala Yesu alishuka(Math12;40),kwa roho kutangaza ufalme wa Mbinguni,Pande za chini ya nchi ktk ulimwengu waroho.ufunuo9:11 wengine wanaiita 911 ile namba ya dharura ya US, kwa habari ya mfalme wa malaika wa kuzimu abadoni/ Apolioni.
2petro2: 4
Kwa maana kama Mungu hakuwasamehe malaika walipotenda dhambi, bali aliwatupa kuzimu
, katika vifungo vya giza wakae humo mpaka ije hukumu,
Wengine wanatumia 1Pet19-20Yesu aliwaendea wana wa Mungu waliofungwa ambao waliowatamani wana wa binadamu na kuwaoa Mw6:1-7
1Pet3:19-20 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.
Hao wana wa Mungu kuna wapendwa wengine wanasema ni wana Seth wakaoa mabinti wa kizazi cha uovu cha kaini
wengine wanasema ni malaika walioanguka kwa kutamani wana wa binadamu wakiutumia Yuda1:6 malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
3:SHEOL waovu wanakaa kwao,watakatifu kwao(kable ya ufufuko wa YESU)
4:SHIMO LISILO NA MWISHO; Lk3;31 ni sehemu ilitenga kuzimu na Paradiso,mahala pa mateso walio kwenda wanaona,sikia,tambua(wakati wa agano la kale watu wote walikwenda kuzimu,ila shimo hilo liliwatenganisha wenye dhambi na wasio dhambi
5:.GEHENNA (Jehenamu) mfano wa ziwa la moto
Lakini kuna haya maandiko
Kumbukumbu32:22 Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu, Unateketea hata chini ya kuzimu, Unakula dunia pamoja na mazao yake, Unaunguza misingi ya milima.
Wapendwa wengine wanaamini kama kuzimu ni mahala pa mateso,sijui kama ni sawa au la,
Mimi naamini kuzimu hakuna moto,wengine wanaamini kuna moto na mateso
Barikiwa
Somo la mambo ya KUZIMU linakuwa na mjadala mrefu sana na mara nyingi mjadala usiofika mwisho baina ya wanatelojia na wanazuoni wa maandiko ya Biblia.
Kama watu wanaamini “KUZIMU” ni ulimwengu wa roho inakuwaje hawa wanaojiita watafiti wa jiolojia waseme eti walichimba shimo refu sana kwenda ardhini na kusikia vilio na sauti za watu? Haiwezekani watu waseme eti KUZIMU ni mahala pasipoonekana kwa macho ya binadam bali ya rohoni hala watu wengine waibuke na kusema wamechimba ardhini ghafla wanasikia vilio vya watu walioko KUZIMU. Ina maana kama wangeendelea kuchimba wangejikuta wanakwenda KUZIMU yaani wangejikuta wanatumbukia “KUZIMUNI” AU SIYO?
Swala la kusema KUZIMU ni chini ya ardhi hii ambayo ni sayari katika “universe order” naona kama ni mitazamo HASI (Negative imaginations towards the truth). Sayari zote zina maumbile yenye muundo wa duara au kama tufe au tuseme kama yai. Sayari ya Jupter, Mars, Pluto, nk zote kwa maana nyinge zina KUZIMU ndani yake kama maana inayotafsiriwa ndiyo hiyo kwamba KUZIMU ni ulimwengu wa roho ulioko chini sana ya SAYARI HII, “DUNIA”.
Kuna watu pamoja na kwamba wamefundishwa muundo wa sayari na jinsi Mungu alivyozipanga wanashindwa kuyasoma maandiko na kuyatafsiri kwa kuzingatia ukweli huo wa muundo wa sayari (Solar Systems). Dunia hii ni sayari ndogo sana ambayo ndani ya tumbo lake ( stomach of this earth) hakuna kitu chochote kilichomo zaidi ya mawe, miamba, maji, volkano, na madongo ya kawaida. Unapokuwa mwalimu wa NENO ukasahau ukweli huu unakuwa hujaitendea haki ELIMU YAKO HIYO. YA JIOGRAFIA NDOGO TU DARASA LA 7.
Wapendwa wengi huchanganya mambo. Ukiwasikiliza watakwambia kuhusu “ULIMWENGU WA ROHO” , ULIMWENGU WA GIZA, KUZIMU, nk. Ukiwauliza wanyoshe kidole kuonesha huo “ULIMWENGU WA ROHO” ulipo; baadhi wataelekeza kidole chao angani, wengine watanyamaza kwanza. Kama KUZIMU ni eneo lililoko katika ulimwengu wa ROHO inajaje tena watu waseme KUZIMU ni chini ya tumbo la dunia hii tunayokanyaga kila siku?
Mimi naelewa kwamba “ULIMWENGU WA ROHO” huwezi kuuona kwa kutumia darubini wala macho ya binadam na wala hauwezi kugusika kwa mikono ya binadamu au ukasafiri kwa magaari ya dunia hii au ndege za Airforce One na ukasema eti unaenda kuwatembelea walioko “ULIMWENGU WA ROHO”.
Naomba niwaeleze kwamba “ULIMWENGU WA ROHO” ni mahali ambapo binadamu hawezi kwenda akiwa katika hali ya mwili huu wa damu na nyama. Tafsiri hii inakwenda hata kwenye swala la KUZIMU. Kama KUZIMU ni ulimwengu wa roho basi hakuna awezaye kwenda huko hadi abadilishwe kutoka katika ubinadamu na kwenda katika hali ya ROHO.
Aidha, “ULIMWENGU WA ROHO” hauko katika mfumo wa dunia hii na sayari zake. yaani, “Spiritual World is the intangible world existing outside the tangible solar system galaxy”.
Kama tutaelewana kwamba KUZIMU ina maana mbili: 1. KUZIMU = ULIMWENGU WA ROHO, 2: KUZIMU = SHIMO REFU, AU KABURI LA KAWAIDA, Hapo inaweza ikaleta mantiki. Lakini kisemantikia itakuwa siyo sahihi kusema KUZIMU ni eneo wanakoishi watu. Kuna maandiko yasemayo hivyo, nakuomba uyafafanue kwa uangalifu sana bila kuacha maana ya kimofolojia na kisemantikia.
Ninafaidika sana na michango yenu, tena ni fursa kubwa ya kuyajua mambo haya kwetu sote maana hayo ni makazi! Haitoshi tu kuwa na kiu ya kwenda mbinguni, bali kuyajua makazi yote itatupa ujasiri wa kuihubiri Injili katika kiwango cha wahusika kamili, maana ni kweli kuwa Injili inatuhusu! Basi, kadiri tunavyoliendea jambo hili tutegemee Mungu kutuongoza katika hilo ili furaha yetu iwe kamili!
Robert, Milinga, Haule na wote, Bwana awatie nguvu kwa kazi mnayoifanya, maana wanafunzi mnao, tena tuko wengi sana! Kila niliyejaribu kumuuliza, hakuna mwenye uhakika wa jambo hilo! Inashangaza lakini huo ndio ukweli. Labda kila mtu roho inakuwa nyeusi kuliongelea jambo hili au huona ni bora kuzungumzia barabara za dhahabu kuliko moto au dhiki na hivyo kubaki katika msukumo wenye kuyaepuka mazungumzo yenye mwelekeo huo!
Mbarikwe nyote, nasi twaendelea kujifunza!!
Yahitajika mtu kuikubali Neema ya Wokovu inayohubiriwa katika uhuru na utashi wa maamuzi. Hizi picha, sijui sauti za kuzimu n.k, kwa mtu anayepotea bado hawezi kuona kama ni kitu cha mkumshawishi amwamini Yesu. Nafikiri ndiyo maana hata mitume wenyewe hawakuweka msisitizo wa mahuburi kwa kuelezea ubaya wa kuzimu bali Uzuri wa Yesu na umuhimu wa mtu kuwa na ushirika na Mungu!
Kama hapa, ambavyo naona kuna mada imejitokeza juu ya Kuzimu na Jehanamu. Mi nashauri kuwa inaweza isiwe na msaada sana kufahamu tofauti ya Kuzimu na Jehanamu, bali la muhimu ni kule kujua kuwa sehemu ambayo watakwenda wasiomwamini Yesu siyo Nzuri. Iwe Jehenamu, Kuzimu au jina lolote lile. Ingawa kama alivyosema ndugu Ck Lwembe, jambo hili linaweza kuongeza ufahamu na ujuzi katika kuihubiri Injili ya kweli!
Mungu atubariki wapendwa tunapoendelea kubadilishana ujuzi wa mambo haya!
Na wote ndugu zangu ktk Bwana , taifa teule miliki yake Bwana.
Kwa kweli sisi wengine tumeokolewa ktk moto(yuda1.23) kwa hiyo hatuwezi kupenda sawa,,tunajua tunachandika ,tukiona injili nyepesi au wapendwa wanacheza na wokovu hasira ya Mungu inatuijilia, tunatamani tuchukue bakora tuwaswage kama mbuzi waingie zizini(ufalme wa Yesu),maana huko nje wapo mbwa,wachawi na waabudu sanamu.,biblia inavyoandika hivyo unaona mbwa/wachawi/waabudu sanamu ni kitu kidogo Bwana Yesu anasema nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa.ili tuzifue nguo zetu tuwe na amri ya kuendea mti wa uzima.
Dadi MIllinga ulimwengu wa roho ni halisi(uwe wa Mbinguni au giza)nyumba tunazo kaa inaweza kuwa ktk ulimwengu wa mwili na pia ulimwengu wa roho wakati huo huo sasa inategemea ni ulimwengu wa roho upi Mbinguni au giza,,Mti mfano mwembe unaona ktk ulimwengu wa mwili ni mti wa matunda lakini ni kitu kingine ktk ulimwengu wa roho,unaweza panda daladala lakini sio daladala,uliza wachezaji mpira wote wakivunjika mifupa wowote mwilini kwa nini wanaenda kigoma.
Nikisema haya sio kwamba mimi niliwahi kuwa mchawi la hasha,nimeona hayo kwa macho yangu na si kuadithiwa wakati nilipokuwa mtu wa ulimwengu huu,na hata sasa kwenye huu wokovu wangu ninaweza kuwa nasoma biblia au nipo kwenye laptop ninasoma ghafla ninaweza ona labda kwa mfano tandu mrefu kama futi moja,nikaingia ktk maombi siku haipiti tukio linatukia na wala sijiulizi nakamata bakora namaliza na kuchoma moto,ukweli kazi nilishamaliza ktk ulimwengu war oho pale Roho Mtakatifu aliponionyesha,sasa inaweza kuwa Yule mdudu tandu ni wa kawaida au wa giza.
Sasa wakati ukifanya jambo lingine ghafla unawaza ajali,lazima uiingie ktk maombi nukiacha watu wanapata ajlali,kwahiyo tunaishi kwenye ulimwengu wa mwili lakini mara unaingizwa katk ulimwengu wa roho,sasa inategemea tu wewe unatii ishara za Roho Mtakatifu au unazipotezea.
Millinga Ulimwengu wa roho ni halisi.bahati mbaya wakovu wengi hawana uelewa wa ulimwengu wa giza au hawataki.
Nikubaliane na John Paul hii thread na yote yanayojili hapa hayampi Bwana Mungu utukufu wowote,hayana mashiko,Pia wengine imani yao haijafikia kiwango hicho ni hadithi tu kwao,Kumbe yatupasa kutafakari yalio juu Mbinguni,yenye sifa na yakupendeza kusikia yanayo mpa Bwana Yesu utukufu.
Shika ulicho nacho asije mtu akakunyang’ana taji yako ling’ang’anie
Kuzimu, Jehanamu, Mbinguni, Mauti, Roho Mtakatifu nk, mambo yote haya yamo katika Biblia, kwa hiyo ni Neno la Mungu! Kwa hiyo sioni uhalali wa kuambiwa kuwa kujadili lolote kati ya hayo hayampi utukufu Mungu au hayana Mashiko!
Ninavyo fahamu mimi ni kwamba mtoto yeyote asiye zijua kazi za babaye, hawezi kupewa mamlaka. Jehanamu na kuzimu ni kazi za Mungu, nazo zinamtukuza yeye; kwa hiyo unaposema hazimtukuzi, inakuwa vigumu kidogo kukuelewa, kwamba nawe huyajui hayo na hutaki kujifunza, au ni mtu uliyejitosheleza, au unaogopa kuwa watu watajua kuwa huyajui hayo na hivyo heshima yako kushuka au … !
Hili la watafiti ni jambo lililotokea. Nayo maelezo yake ndio kama yalivyo, licha ya upagani wao, lakini conclusion waliyofikia katika mkasa huo imemuhusisha Mungu, yaani kazi mojawapo ya mkono wake. Kwa hiyo mtu mwenye shauku ya kulijua jambo hilo katika uhusiano na Mungu, mimi naamini atamtafuta mwana wa Ufalme ili amjuze zaidi kuhusu tukio hilo kulingana na kazi ya Baba yake, nayo majibu ya wana wa Ufalme ndio kama unavyoyaona hapa yakilijibu swali nililoliuliza kutokana na mada iliyopo!!
Basi, mwana mwenye kuyajua mambo hayo katika ukamilifu, naamini humpa utukufu zaidi Baba yake kuliko mwana asiyejua ambaye ni rahisi kujichanganya na kuondolewa katika njia ya kweli!!
Zitukuzwe kazi za Bwana wetu, maana hizo humtukuza yeye!
barikiweni, naendelea kujifunza hapa
Nashukuru kwa kutushirikisha uzoefu wako enzi hizo ulipokuwa kuzimuni yaani kwa shetani. Hongera kwa kuendelea mbele na nakuombe mwisho mwema.
Mimi sijasema kwamba “ULIMWENGU WA ROHO” siyo HALISI. Labda hukunielewa vyema. Soma tena maelezo yangu kwa makini. Ikiwezekana soma mstari kwa mstari (read between lines).
Mimi nakubaliana na wewe mia kwa mia. Ulimwengu wa roho ni halisi wala siyo porojo za watunga zaburi za bongo(Bongo Flavor). Ulimwengu wa roho upo.
Mimi ninachojaribu kuwaeleza wapendwa ni kwamba waondokane na kasumba ya kufikiri yasiyofikirika katika ulimwengu usiofikirika wala kumithilika (Thinking of non-existing creatures in the imaginable tangible or intangible world).
Tuondokane na kusonta kidole kwa kusema, “……mbinguni ni kuleeeeeee……” au “…….. kuzimu ni paleeee, eti ukichimba futi kiasi fulani tu unafika kuzimu, kwani kuzimu si ni kule baharini tu, au makaburini…….”. Hayo ni baadhi ya maneno utakayosikia mtaani.
Kuna kipindi (nafikiri had leo hii) Waislam waliamini kwamba MWEZINI ni mahali alnapokaa Mungu. Ndiyo maana alama ya mwezi wanaitumia sana. Waliamini kwamba Mwezi ni mahali patakatifu sana alipo Mungu wao. Ilipofika wanaanga wa Kimarekani na Urusi kukanyaga mwezini wakamaka wakisema, “……Astaghafullah….” yaani hawa makafiri wamekanyaga nyumbani kwa mwenyezi Mungu? Wanaukanyaga mwezi.
Mimi najaribu kuwarekebisha wapendwa wa Bwana wanaodhani kwamba huko chini ya ardhi ndiko yaliko makao makuu ya shetani kwa sababu tu Maandiko yanasema hivyo. Biblia hata ikisema kwamba Ibilisi ametupwa chini au kuzimuni watu wasikimbilie kuelewa kwamba ni chini hapa juu ya ardhi yetu. Maana ya chini yaweza kumaanisha tofauti na hiyo. Ibilisi kutupwa kifungoni au kuzimu ni misamiati tu yenye kuonesha adhabu aliyopewa lakini haina maana kwamba ukichimba ardhini utamwona. IBILISI Kutupwa chini au KUZIMUNI inamaanisha kushushwa cheo na kulaani na Mungu kwa kunyang’anywa mamlaka aliyokuwa nayo.
Kwa watu walioajiriwa wanaelewa kwamba mtu aweza kushushwa cheo kama alikuwa juu akawa chini (sema kuzimu ukipenda) na mtu aweza kupandishwa juu kwa cheo. Ibilisi naye alishushwa chini kwa maana ya cheo alichokuwa anacho mbinguni na maandiko yasemapo ameshushwa chini haina maana kwamba ni chini hapa kwenye ardhi ya dunia hii bali ni katika Ulimwengu wa roho kabisa na wala siyo duniani. Biblia inaposema ametupwa duniani na ana hasira nyingi na ole wa dunia kwa kuwa Ibilisi ametupwa chini ina maanisha hasira zake za kunyang’anywa cheo chake anazielekeza kwa viumbe wote wa Mungu kokote waliko ili awakoshe raha na fursa ya kuishi na Mungu.
Neno KUZIMU limetumika kama neno linalowakilisha adhabu aliyopewa. Hivi hujaona baadhi ya Mawaziri wa Kikwete walioshushwa chini (waweza kusema kuzimu ukipenda) walivyokasirika sana hata wakawaendea wapiga kura wao na kuanza kujiosha na kujikosha wao kama vile hawana makosa. Unamkumbuka aliyekuwa waziri Mkuu Edward Lowasa alivyopokelewa kwao kwa bashasha na nderemo na akaanza kujiosha ile kashifa ya Richmond? Unamkumbuka Endrew Chenge wa Bariadi aliposhushwa chini kiutawala alivyokasirika? Unakumbuka hata sasa alivyo na hasira kwa wapinzani wake? Huku ndiko kushushwa chini hata kuzimu.
Kwa jinsi hiyo basi naomba nitofautiane na wale wote wenye dhana potofu kwamba KUZIMU iko chini ya ardhi ya sayari hii tunayokanyaga na niwaombe wakubaliane na mimi kwamba “KUZIMU” ni neno linalotumiwa kumaanisha adhabu anayopewa mtu au sehemu inayopatikana katika ulimwengu wa roho (invisible and spiritual world) wanakokaa watu walioshushwa vyeo vyao vya kiroho (yaani kutengwa na Mungu milele) na hapo ndipo alipo Ibilisi na malaika zake wote walioshushwa chini kivyeo. Lakini usiondoke hapa ukielewa kwamba kushushwa huku ni katika kudondoka toka mbinguni (anga tunaloliona juu) na kudondokea chini hapa tunapoishi na kujenga majumba.
Mjadala unaendelea, wote tunajifunza Neno. Mtalaam wa Neno ni Mungu tu.
Kataa kubali Mungu yupo, na Shetani naye yupo,Uamuzi ni wako wewe upingae
Umebaki muda mfupi, watawafundisheni kuwa, walioko kuzimu, wameshajenga nyumba za ghorofa, wanafanya ujasiliamali nk. Wanacheza sana na akili za watu tu!!
Msiposoma neno la Mungu vizuri wapendwa, hatima yenu ni tete, labda Mungu afanye muujiza tu!! Tuombeane sote