Ijumaa, 1 Novemba 2013

USHUHUDA WA ADAM NA UPONYAJI ALIOPOKEA MKUTANONI ARUSHA

USHUHUDA WA ADAM NA UPONYAJI ALIOPOKEA MKUTANONI ARUSHA


Akielezea ushuhuda huo, mtu aliyemwokota, Frank Justin Lyamuya alikuwa na haya ya kusema kuwa majira ya asubuhi wakati akielekea kazini kwake na kufika maeneo ya kwa Lowasa hapa  Arusha na kumkuta kijana, Adamu Joshua ambaye alikuwa anagalagala pembeni ya barabara ya lami na akachukua jukumu la kuwauliza walinzi wa majengo yaliyokuwa jirani mwa barabara ambao walimwelezea kuwa kijana Adamu alikuja maeneo hayo muda wa saa kumi na mbili asubuhi. Walinzi walizidi kusimulia kuwa Adam alisimamisha pikipiki na akavua kofia ngumu ya pikipiki (helmet) kando ya barabara na kuanza kugalagala huku akisema kuwa “siendi kuzimu mimi na umemchukua dada yangu na mama yangu” alipofika.


Frank Lyamuya aliamua kwenda kituo cha polisi kilichopo jirani na kutoa taarifa za tukio hilo lakini cha kushangaza polisi wakasema kuwa mtu huyo ni mlevi hivyo hawawezi kumpokea. 
Mchungaji Josephat Gwajima akimuhoji  Adamu (Kulia) mara baada ya kufunguliwa na kukaa sawa

Ndipo Frank akaamua kuondoka naye na baadaye akashauriwa na mama Lishe waliokuwa karibu kuwa ampeleke kwenye uwanja wa relini ndipo wakampakia kwenye pickup canter na kumleta kwenye kiwanja cha relini kunakofanyika Mkutano Mkubwa wa Injili uliondaliwa na Ufufuo na Uzima. Walipofika kiwanjani hapo kabla ya mkutano kuanza walikutana na wachungaji wasaidizi Richard, Jimmy na Alpha ambao walimuombea hadi akafunguka na kuponywa kabisa saa chache kabla ya mkutano kuanza. 

Baada ya kufunguliwa na Yesu kristo ndipo akaanza kueleza kuwa yeye anaishi Mererani ingawa nyumbani kwao ni Ngaramtoni na yeye ni mchimbaji madini mdogo maarufu kama wanaapolo na anaishi watoto wake watatu amabao ni Joshua mwenye miaka 13, Neema mwenye Miaka 11 na sharoni mwenye Miaka 7.

Ambapo katika watoto hao watatu mtoto wake aitwaye Neema alipotea alhamisi iliyopita katika mazingira tata.

Akihojiwa na Mchungaji Gwajima mkutanoni jioni, Adamu alisema kuwa hakumbuki alitokaje Mererani na kwamba anajishangaa kujikuta pale na pia hajui wapi mtoto wake alipo. Ndipo Mchungaji Gwajima akamwombea awaone watu wanaomtesa na kuifanyia mabaya familia yake. 
Mchungaji Gwajima akamwombea hapo hapo akaanguka chini akitetemeka kuwa amemuona kaka yake. 
Adamu (aliyeshikwa mikono chini) akisaidiwa kusimama mara baada kuombewa na Mch.Kiongozi Josephat Gwajima (Kulia)

Adamu aliendelea kusema kuwa, hata mama yao alipokufa; dada yake akamwambia kaka yao kwanini umemuua mama na akamjibu nawe utamfuata mama yako ndipo baada ya mwaka mmoja na dada yake naye akafariki dunia. 
Kaka yake Adamu yupo Dar es Salaam akiwa na maduka makubwa ambayo kwasasa ndipo anatambua kuwa yanendeshwa kishirikina. Baada ya maombezi kwa sasa, Adamu ni mzima kabisa na amewekwa huru kwa jina la Yesu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni