Ijumaa, 1 Novemba 2013

MTOTO AFUFUKA KANISANI UFUFUO NA UZIMA - ARUSHA

MTOTO AFUFUKA KANISANI UFUFUO NA UZIMA - ARUSHA


Ni jumapili tulivu katika viwanja vya kanisa jipya la Ufufuo na Uzima jijini Arusha; ambapo Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Tanzania, Mch. Josephat Gwajima ameendelea na ziara yake mkoani humo kwa kuwafundisha viongozi wapya wa masomo ya kumtumikia Mungu maarufu kama Potential shepherd. Mwisho wa Ibada ya Asubuhi ambayo ilitawaliwa na mafundisho zaidi ilifungua pazia kwa ibada ya jioni ambayo ilikuwa ni fursa  kwa wale ambao hawakuweza kuwepo asubuhi nao kushiriki.

Mtoto aliyefufuka (katikati) akiwa ameshikwa na Mch. Gwajima (kulia) na Mch. Costa (kushoto)

Majira ya saa kumi kamili, sifa zilivuma na baadaye kufuatiwa na ukaribisho wa Mch. Gwajima kutoa neno la Uzima. majira ya saa kumi na mbili kasoro; akaingia mama mmoja katikati ya ibada akiwa amembeba mwanaye ambaye kwa muonekano wa awali alikuwa amelegea mwili wote yaani amekufa.

Mchungaji Gwajima akielezea ushuhuda huu mkubwa na mama wa mtoto (kulia mwenye kitenge)

Mama huyo ambaye alikuwepo katika mafundisho ya asubuhi na kujiunga na mafundisho hayo ya potential shepherd; aliendelea kusema kuwa baada ya kuona mwanaye hapumui wala mapigo ya moyo hayasikiki hakuona msaada wa haraka zaidi ya kumkimbiza kanisani hapo Ufufuo na Uzima. 


Aliingia kanisani wakati Mch. Josephat Gwajima akiwa anahubiri hivyo kupokelewa na Mchungaji Msaidizi aitwaye Yeconia Bihagaze ambaye alimuombea mtoto huyo palepale na muda mfupi uliofuata mtoto alifufuka kutoka kwa wafu. Mungu ameendelea kudhihirisha neno la Mchungaji Josephat Gwajima ndani ya jiji la Arusha hali inayosababisha maelfu ya watu kuingia na kutoka katika viwanja hivyo kwaajili ya maombezi.

Maelfu walioshuhudia wakati mama huyo akimleta mwanye na baadaye kufufuka.

MUNGU KWETU NI MUNGU WA KUOKOA NA NJIA ZA KUTOKA MAUTINI ZINA YEYE!!!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni