Wana wa Israeli waliangamizwa jangwani kwa sababu walilizoea Neno la
Mungu, ingawa kila siku walikuwa wakilisikia (1WAKORINTHO 10:1-5). Wana
wa Israeli walifikia mahali pa kudai wapewe mfalme mwanadamu badala ya
Mungu aliyekuwa amewachosha, kwasababu walilizoea Neno lake (1SAMWELI
8:4-7), kwa sababu hiyo, wpte hawakuingia Kaanani isipokuwa watu wawili
tu, Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni (KUMBUKUMBU LA
TORATI 1::35-38). Yuda Iskariote yeye naye yuko motoni leo kwasababu
alilizoea Neno la Yesu Kristo ingawa alikuwa naye kila siku. Watu
waliookoka siku nyingi au Watendakazi wengi huingia katika mtego wa
kulizoea Neno. Tukiisha kulizoea Neno , tujue hatuwezi kuingia Kanaani,
yaani mbinguni, bali mahali petu nin motoni. Bwana atusaidie tusilizoee
Neno la Mungu, katika jina la Yesu. (3). DALILI ZA KULIZOEA NENO LA MUNGU. Zipo dalili kadha ambazo tunaweza kuziona kirahisi, kwa watu
waliolizoea Neno la Mungu. Tukiziangalia, zitatusaidia kuwa na
tahadhari:-
Watu waliolizoea Neno la Mungu, huhesabu kwamba Neno linalotoka katika
Kinywa cha Mtumishi wa Mungu, ni neno lake huyu mwanadamu na wala
siyo Neno la Mungu. Watu ambao hawajalizoea Neno la Mungu, huhesabu
kwamba neno la ujumbe litokalo katika vinywa vya Watumishi wa Mungu, ni
Neno la Mungu mwenyewe (1 WATHESALONIKE 2:13).
Watu waliolizoea Neno la Mungu, wanakuwa hawana shauku tena ya
Kuhudhuria ibada zote. Watu hawa wanachagua kuhudhuria ibada
fulanifulani tu na hata wakihudhuria wanaweza wakawa wanazurura nje tu
bila kufuatilia Neno. Kwao kuwemo ndani ya nyumba ya Mungu siku zote
siyo muhimu tena (LUKA 2:49), tofauti na mwanzoni walipokuwa wachanga
kiroho, ambapo waliumia sana kukosa Neni la Mungu siku yoyote.
. Watu waliolizoea Neno hujiona wanajua Neno lote na kuona kwamba
maneno yanayofundishwa ni ya wachanga kiroho na siyo ya wale waliookoka
siku nyingi. Mtu akijiona anajua Neno, hajajua Neno lolote bado kama
impasavyo kujua (1 WAKORITHO 8;2), ila tu ni kwamba amelizoea.
Mtu aliyelizoea Neno, hata akiketi kulisikia Neno, anakuwa mzito
sana kubadilishwa na Neno hilo, na kulitendea kazi kwa sababu roho yake
ni ngumu, siyo roho iliyopondeka. Hufikiri ni mjanja kwa jinsi asivyo
litendea kazi Neno la Mungu kwa bidii kama wakati wa uchanga wake, kumbe
sasa ndiyo amekuwa mpumbavu (MATHAYO 7:24-27).
Bwana atusaidie, ili tusilizoee kamwe Neno la Mungu, na kama
tumekwisha kulizoea, tutubu na kumwomba Mungu atuumbie roho iliyopondeka
kama ile tuliyokuwa nayo mwanzo na kuzidi, katika jina la Yesu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni