Ijumaa, 1 Novemba 2013

MAMBO YAKUPASAYO KUYAFANYA ILI KUFIKIA TARAJIO LAKO

MAMBO YAKUPASAYO KUYAFANYA ILI KUFIKIA TARAJIO LAKO

TARAJIO LAKO LINAWEZA KUWA GARI

YESU ni jawabu la mambo yote


Matarajio ni mategemeo ambayo unayo katika maisha yako. Na ili ufikie matarajio yako kama mtoto wa MUNGU lazima uzingatie haya                                                                                                                 [1] IMANI; Lazima uwe na imani kwani bila imani huwezi kumpendeza MUNGU Webrania 11:6.   [2]UJASIRI WA KUENENDA ILI KUIFIKIA HATIMA YAKO;Kipingamizi ni kitu chochote ambacho kiko tofauti na wewe hivyo lazima uwe jasiri ili kuonyesha kwamba unamwamini MUNGU na yeye atakushindia hadi ufikie baraka yako au talajio lako pia kumbuka matendo yana nguvu sana kuliko maneno na Ibrahimu alimwamini MUNGU na akahesabiwa kuwa na haki Warumi 4:1-6.                                       [3] FAHAMU AHADI YA MUNGU NI HAKIKA;shetani anatukatisha tamaa kwa sababu hatulifahamu neno la MUNGUna inafika kipindi hadi unasema hivi ni kweli MUNGU amesema na mimi? kwa mashaka hayo huwezi kufikia talajio lako ambalo MUNGU amesema na wewe kwamba itakuwa hivyo. Lakini kumbuka kuwa ahadi ya MUNGU ni ndiyo na hakika ili MUNGU atukuzwe kwa sisi kufikia matarajio yetu .2 Korintho 1:20.                                                                                                                         [4]UNAPASWA UWE NA TUMAINI; 2 Korintho 3:4-6 kwani utoshelevu wetu watoka kwa MUNGU.Uwe na tumaini kwamba lazima utafikia pale MUNGU anataka ufike pia kumbuka hutafanikiwa kwa sababu una juhudi katika jambo hilo bali unamtumainia MUNGU anayeweza yote.Warumi 15:13
ishi kwa ajili ya KRISTO
Ndugu kumbuka kuwa hata kama kutakuwa na vikwazo gani lakini tambua kwamba kusudi la MUNGU kwako halina mabadiriko. pia kama huna vikwazo basi huna unapokwenda lakini MUNGU lazima atakufikisha kwenye talajio lako. Warumi 8:24-25 Biblia inasema KWA MAANA TULIOKOLEWA KWA TARAJA; LAKINI KITU KILICHOTALAJIWAKIKIONEKANA, HAKUNA TARAJA TENAKWA MAANA NANI ANAKITARAJIA AKIONACHO? BALI TUKITARAJIA TUSICHOKIONA TWAKINGOJA KWA SABURI. Ubarikiwe sana na kama hujampa BWANA YESU maisha yako muda wa kufanya hivyo ni sasa hivyo tafuta kanisa la kiroho karibu na wewe waeleze watakusaidia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni