NINI HUONGOZA MAISHA YAKO?
Nilichunguza na kuona kuwa nia kubwa ya mafanikio ni ule msukumo na wivu! Mhubiri 4:4 (LB)
Mtu asiye na Lengo ni sawa na meli bila usukani, mtu aliyepotea ,mtu bure kabwela.
Maisha ya kila mtu yanaongozwa na kitu flani. Je, ni nguvu gani inayoongoza maisha yako? sasa hivi unaweza kuongozwa na tatizo ,msukumo flani, au tarehe yamwisho kwa kitu flani .Unaweza kuongozwa nakumbukumbu ya jambo flani linalo umiza ,hofu mbaya ,imani ya ndani. Hapa kuna mambo matano ambayo ni ya kawaida kwa wengi .
Watu wengi huongozwa na hatia: Watu hawa hutumia muda wa maisha yao yote wakiepuka lawama nakuficha aibu. Watu wanaoongozwa na hatia wanaongozwa sana na kumbukumbu wanaruhusu mambo yaliopita kutawala mambo yao ya usoni wanajiadhibu bila kujua kwa kuharibu mafanikio yao.Kaini alipotenda dhambi,hatia yake ilimtenga na Mungu. Kusudi la Mungu alifungwi na muda wako uliopita. Mungu ni mtaalamu wa kuwapa watu mwanzo mpya.
Watu wengi wanaongozwa na chuki na hasira:Watu hawa wanashikilia maumivu (machungu bila kuyaacha .Badala ya kutoka katika maumivu kwa kusamehe ,wanaendelea kuyakumbuka katika mawazo yao.Watu wengine wanaongozwa na chuki hutunza ndani uchungu wao na wengine huwalipukia watu wengine.Hali zote hizi si nzuri na wala hazisaidii maishani. Biblia inasema, Kuwa na hofu kiasi cha kufa kwa sababu ya uchungu ni upumbavu ,ni kitu cha kipumbavu kukifanya.
Watu wengi wanaongozwa na woga: Watu wanaoongozwa na woga mara nyingi hupitwa na nafasi kubwa kwa sababu wanaogopa kuchukua hatua.Woga ni kifungo ambacho mtu hujifunga mwenyewe na chaweza kukuzuia kuwa mtu yule ambaye Mungu anapenda uwe.Unatakiwa utoke humo kwa njia ya silaha ya imani na upendo. Biblia inasema, Upendo halisi huindoa hofu , kwa kuwa hofu hulemaza maisha ya hofu, hofu ya hukumu ni maisha ambayo hayajakamilika katika upendo.
Watu wengi wanaongozwa na mali:Tamaa ya kupata vitu linakuwa ndilo Lengo la maisha yao yote.Utajiri unaweza kupotezwa mara moja kwa sababu zisizozuilika,usalama halisi unaweza kupatikana katika kile ambacho huwezi kunyanganywa yaani uhusiano wako na Mungu.
Watu wengi wanaongozwa na kutaka sifa:Watu hawa hawa wanaruhusu matarajio ya wazazi ,waume,wake,watoto, waalimu,au marafiki zao kutawala maisha yao. Kuna nguvu zingine zinazoweza kutawala maisha yako lakini zote mwisho wake ni mfu,bila Malengo maisha ni mwendo usio na maana ,shughuli bila mwelekeo,na matukio bila sababu,bila malengo, maisha ni kitu duni,kisicho na umuhimu wowote.Biblia inasema, hakuna mtu anaweza kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.
FAIDA ZA KUISHI KWA MALENGO
Kuna faida kuu tano za kuishi maisha yenye kuongozwa na Malengo:
Kujua Lengo lako hukupa maana ya maisha yako:Tuliumbwa tuwe na maana.bila Mungu maisha hayana Lengo ,na bila Lengo maisha hayana maana.bila maana maisha hayana umuhimu wala thamani au matumaini. Kuwa na tumaini ni muhimu kwa maisha yako.unahitaji tumaini ili kukabili mambo ya maisha.
Kujua lengo hurahisisha maisha yako:Hii hukuwezesha kuelewa ni nini ufanye na ni nini usifanye,kuishi kwa kuongozwa na Malengo huwezesha kuishi maisha rahisi na yenye ratiba iliyopangwa kwa busara;Biblia inasema, Maisha ya kuigiza na ya kujionyesha ni maisha batili ;maisha ya uwazi na yaliyo rahisi ni maisha ya utoshelevu . Maisha yanayoongozwa na Malengo pia huleta amani moyoni:Wewe bwana unawapa amani kamili wale wanaotunza malengo yao kwa uthabiti na kuweka tumaini lao kwako.
Kujua lengo lako hukupa mwelekeo wa maisha yako: Hukuwezesha kukusanya pamoja juhudi na nguvu zako kufanya kilicho cha muhimu.Unakuwa na ufanisi kuchagua kilicho cha muhimu. Biblia inasema, Msiishi pasipo uangalifu ,bila kufikiri .hakikisheni Bwana wenu anapenda nini.nguvu ya kuwa na mwelekeo inaweza kuonekana kwenye nuru.Nuru hafifu ina nguvu kidogo.hakuna kitu chenye nguvu kama maisha yenye mwelekeo ,ukiyaishi kwa Malengo.
Kujua lengo hukuandaa kwa ajili ya maisha ya milele: Matumizi mazuri ya muda ni kujenga urithi wa milele.Haukuwekwa duniani ili ukumbukwe ,uliwekwa hapa duniani ili kujiandaa kwa ajili ya umilele. Mungu anasema, Mimi ndimi njia kweli na uzima.hakuna mtu awezaye kuja kwa baba isipokuwa kwa kwa njia ya mimi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni