JE INAWEZEKANA UWE MKRISTO BILA KWENDA KANISANI?
Ndugu nakukaribisha katika somo hili muhimu kwa maisha ya waenda mbinguni.Na kumbuka kuwa HUWEZI KUWA MKRISTO KAMA HUNA KRISTO MOYONI MWAKO. Hivyo hakikisha kwanza unakuwa na KRISTO maishani mwako ndipo utakuwa MKRISTO sahihi na sio mkristo jina.
Je mtu anaweza kuwa baharia bila kwenda baharini? Mkristo maana yake ni mfuasi wa YESU KRISTO. Tunasoma katika Biblia kuwa YESU alikuwa na desturi ya kwenda hekaluni na angali anapatikana mahali pa ibada hata leo. Wakristo ni watu wanaompenda MUNGU, na kwa hivyo wanawapenda watu wa MUNGU na nyumba ya MUNGU. Biblia haiwapendekezi Wakristo pekee, Hata ile hali ya kuwa Mkristo asiyekwenda kanisani haimfai mtu yeyote. Ni kama mtu anayeishi kwa kula tu mkate na maji hali anaweza kupata chakula kizuri kwa afya yake. Kama alivyosema mwana mpotevu. ''Nyumbani mwa Baba yangu kuna chakula kingi, wanakula mpaka wanakiacha''(Luka 15:17).
Katika kanisa utapokea mkate wa uzima ambao ni neno la MUNGU. Kumbuka ya kuwa vitabu fulani katika Biblia viliandikwa kama barua kwa makanisa na faida yake kamili inaweza tu kupatikana unaposhirikiana na wengine.. Ni afadhali kupata kilicho bora zaidi. Kumbuka mwanajeshi hufanya kazi kwenye jeshi nalo kaa la moto likitengwa na mengine litazima..
Hakuna ndoa ya mtu mmoja tu peke yake, Ndoa ni uhusiano na upendo. Ndoa inakuhusisha na jamaa wa pande zote mbili. Hakuna mtu anayeweza kuwa kristo wa peke yake tu. mtu hawezi kuzaliwa tu peke yake bila ya kuwa na wazazi na jamaa wa karibu.. Unapozaliwa mara ya pili yaani unapobatizwa ubatizo wa maji mengi na pia unapobatizwa ubatizo wa ROHO MTAKATIFU unafanyika sehemu ya jamii ya waaminio, Biblia katika Marko 16:16 inasema ''Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini atahukumiwa'' hivyo kubatizwa pia ni muhimu ili kuitimiza haki yote ya MUNGU. Jambo hili la kuamini na kubatizwa lina manufaa makubwa kwako, huu ni urithi wako na kama mtume Paulo anavyosema , MKRISTO NI WA AINA MOJA TU-MSHRIKA WA MWILI WA KRISTO.
Sisi ni washirika wa mwili wake katika ulimwengu huu. Kanisa liko duniani kwa sababu sisi sio roho tu bali pia ni watu wenye mwili na damu. BWANA aliliunda Kanisa hapa duniani kwa manufaa yetu na ametukirimia vipawa kutoka mbinguni ili tuweze kupata nguvu kutoka kwa wenzetu na kufurahia ushirika wa KIKRISTO na upendo. Maandiko yamejaa habari za ushirika na kutushauri kwamba tusiache kutumia nafasi nzuri za ushirikiano na kushauriana na kwamba tusiache kukusanyikana pamoja kumwabudu MUNGU wetu.
JINSI YA KUWA KRISTO MWENYE AFYA .
1: Kula chakula kizuri yaani NENO LA MUNGU.
2: Kunywa maji mengi yaani ROHO MTAKATIFU.
3: Fanya mazoezi yaani MTUMIKIE MUNGU NA KUTENDA KAZI KWA AJILI YAKE.
4: Pata hewa safi yaani HUSIKA KATIKA IBADA NA SIFA.
J5: iburudishe yaani KWENYE USHIRIKIANO NA WAKRISTO WENGINE.
MUNGU awabariki sana na kama hujamba BWANA YESU maisha yako wakati wa kufanya hivyo ni sasa maana hakuna uzima wa milele bila YESU KRISTO (Yohana 14:6) hivyo kwa sababu ndugu unataka uzima wa milele mpe YESU maisha yako na utakuwa huru mbali na uonevu wa shetani.
MUNGU akubariki tena
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.
Peter Michael blogger maisha ya ushindi blog |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni