WATU WALIOCHUKULIWA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA
MCHUNGAJI JOSEPHAT
GWAJIMA.
“Saa inakuja na sasa ipo, ambapo wafu wataisikia sauti ya mwana wa Adamu”
2Wafalme3:4-27,”Ndipo akamtwaa mwanae wa kwanza…….” hizi ni habari za mfalme wa israeli
ambae aliamua kwenda vitani kumpiga mfalme
wa Moabu, na alipoona kuwa vita inakuwa ngumu sana, akaamua kumtoa kafala
mwanaye wa kiume. Hii ilikuwa agano la kale lakini hata sasa bado kuna watu
ambao wakitaka ushindi huwa anatoa kafara ili apate ushindi, kafara hii inaweza
kutolewa na mkuu wa nchi au yeyote atakaye ushindi. Inaweza kuwa ili kupata
ushindi wa biashara, uongozi au mali.
1Wafalme 16:29-34, "Ahabu
mwana wa Omrai lianza kutawala juu ya Israeli………..34’ Katika siku zake Hieli
Mbetheli akajenga Yeriko, akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa
wake wa kwanza na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu
sawasawa na neno la BWANA alilonena kwa Yoshua mwana wa Nuni”
Biblia inasema, Ingawa tunaenenda kwa jinsi ya mwili lakini hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili, vita vyetu ni vya rohoni. Ndio maana hata tunapoimba sifa kwenye ulimwengu wa mwili ndivyio tunabomoa misingi ya kisheni katika ulimwengu wa roho, Ukiweza kuutawala ulimwengu wa roho unakuwa wumeutawala ulimwengu wa mwili bila kipingamizi.
Maombi: Naamuru
ngome ya magonjwa, balaa, mikosi na ngome zote za giza amabazo zimeletwa kwenye
maisha yako kwasababu ya kafala ziharibiwe katika Jina la Yesu. Na kama Yoshua
alivyotangaza kwa atakaye ujenga tena Yeriko name naalaaniwe pepo yeyote
atakaye jaribu kukufunga tena.
Huwezi kwenda kwenye utawala bila kuwekwa na mamlaka ya rohoni, ama mamalaka ya shetani au mamlaka ya kutoka kwa Mungu.
Hivyo kiongozi ambaye hajatoka kwa Mungu ni lazima atakuwa ametoka kwa shetani
kwasababu watoa kafara hizi wapo hata sasa.
NINI KINAWAFANYA WATU WANATOA KAFARA WAFANIKIWE.
Biblia iko wazi kabisa kuhusu watu wanaotoa watu kuwa
kafala, swali kwanini wanafanikiwa? Ni muhimu kujua kuwa chakula cha mashetani
ni damu, hivyo wachawi wanapotoa kafara ya watu wanamwaga damu ambayo kimsingi
inawapa uhai na nguvu kwa mashetani, na mtu huyo anayetoa kafara huwa ananuiza
damu hiyo kwa ajili ya kushindwa na kupata matatizo kwa mtu aliye mkusudia.
Damu ni uhai, Mwanzo 9:4,
Kafara inapotolewa damu humwagika na kwasababu damu ni uhai, Damu hiyo hunena
kwa jina lako na kwa ubaya ilikusudiwa kwayo. Ukisoma Mwanzo 4:10,
utagundua kuwa Habili alipouawa na ndugu yake Kaini, damu yake ilikuwa ikinenea
katika ulimwengu wa roho. Vivyohivyo, damu inaponena mashetani huja na
kuitimiza makusudi iliyonuiwa kwayo. Leo una matatizo kwasababu ya kafara iliyo
tolewa na adui yako. Uwezi kuwa huru bila kunyamazisha kafara zote na damu zote
zinazonena mabaya juu ya maisha yako.
Pale ambapo damu imemwagika ndipo madhabahu ya kifungo chako
na ndipo sauti ya kifungo chako inapotokea na inaweza kuwa sehemu yeyote ama
shambani, njia panda kuzimu ama mahali popote, ndio maana ajali inaweza kutokea
na mtu mmoja tu ndio akapoteza maisha kwasababu yeye ndio aliyekusudiwa.
Unapoinyamazisha damu leo,wanaweza kwenda kumwaga tena damu
nyingine kwa kutoa kafara na tatizo lako kuanza tena,cha msingi ni kubomoa
madhabahu hiyo na kumteka nyara kuhani wa madhabahu hiyo na kumyonga kwa Jina
la Yes,ukifanya hivo utakuwa umemkamata farasi na mpanda farasi na kuwatupa
baharini.Kuna wengine huwa hawamwagi damu bali hupeleka mashataka kwenye vikao
vyao vya kichawi.
Roho yako kulazwa
usingizi na Mashetani.
Kama unavyojua mtu ni roho inayokaa ndani ya nyumba iitwayo
mwili, hivyo Shetani anaweza kumwingia mtu na kuikaba roho yake, mtu wa namna
hii huanza kusikia kichwa kinamuuma na baadaye anapata kujikuta amekufa au
anaishi huku akiwa hawezi kufanya mipango yoyote kwasababu roho imelezwa ndani
au anaweza kuonekana amechanganyikiwa ; mtu kama huyo aweza kufunguliwa kwa
jina la Yesu.
3.Kuchukuliwa mzima mzima
Watu wa namna hii huitwa mzima mzima usiku,hapo yako ndiyo
huitwa na kama huna Yesu lazima utaitika kwasababu roho yako haina ulinzi wa Yesu,
Na unapoitwa unafungua mlango mwenyewe na kuifuata sauti na matokeo yake unapotea
na unakuwa hauonekani. Ndio utasikia matangazo kwenye kwenye vyombo vya habari
kuwa mtu Fulani amepotea kumbe kwasababu ya kuitwa.
Kwa njia hii shetani ametumia roho za watu. Shetani huamua kutumia
wanadamu kwasababu roho za pepo ni rahisi kuangamizwa kwa Jina la Yesu, Hivyo
huamua kutumia roho ya mwanadamu (superior).
Kutoa roho ndani ya
mwili wa mtu na kuweka pepo.
Kwa kawaida mtu wa jinsi hii roho yake hutolewa na huingizwa
ndani, na unapokuwa unaomba watu wa namna hii hawawezi kuangamia kwasababu Yesu
anawapenda wanadamu, watu wa namna hii ni wengi kwelikweli. Watu wengi unawaona
ni wagonjwa sana, wana matatizo sana ndani wanakuwa wamechukuliwa, watu wanamna
hii unaweza kuwaombea muda mrefu na pepo lisitoke, ukiona hivyo tambua kuwa mtu
huyo ambaye ni roho hayumo ndani hayumo ndani.
Watu hawa ndio ambao huombewa makanisani miaka mingi bila
kufunguliwa lakini kumbe siri hii kuwa roho imetekwa haijajulikana kwao. Katika
Jina la Yesu Kristo ninaamuru roho yako iwe huru. Na ufunguliwe kutoka katika
udhaifu wako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni