ALICHUKULIWA MSUKULE NA KUWEKWA NYUMA YA MLANGO
NEEMA AUGUSTINE MLINGI: |
Siku ya Sita Mchungaji Josephat Gwajima alifundisha kuhusu aina za Misukule, hapo aliainisha aina za Misukule kama ifuatavyo:-
- Ainaya kwanza; Ni yule ambaye anaonekana amekufa na kuzikwa kabisa, lakini kumbe anakuwa ametolewa nje ya mwili wake na kubadili macho ya watu wahisi ni yeye.
- · Aina ya pili; Ni yule mtu ambaye wachawi wanamwita usiku akiwa amelala na kujikuta ameondoka nyumbani na kutokomea. Wengi wao ni wale wanaotajwa kupotea katika vyombo vya habari.
- · Aina ya tatu; Huyu ni mtu ambaye alikufa kichawi na baadaye mwili wake kuja kufukuliwa na kwenda kufanyishwa kazi za kichawi huko msukuleni.
- · Aina ya nne; Hii ni aina ambayo watu wengi wamechukuliwa kwa namna hii; yaani wapo wanaishi lakini kumbe ndani walishachukuliwa zamani. Na watu hawa utawakuta wanasumbuliwa na matatizo ya ajabu bila ufumbuzi kamili.
USHUHUDA WA NEEMA AUGUSTINE MLINGI:
Neema akifunguliwa baada ya kurudishwa |
nneema
anaishi jijini Arusha sehemu inaitwa Ngulelo ambapo anaishi na mama
yake. Neema ni mtoto pekee wa mama yake (amezaliwa peke yake)
Baada
ya kuhojiwa na Mwandishi wetu, Neema alisema kuwa anakumbuka
alichukuliwa msukule na kuwekwa nyuma ya mlango wa nyumba ya shangazi
yake kabisa.
Alipokuwa
nyuma ya mlango Neema alikuwa anaishi na nyoka kwa mida wa miaka mingi.
akiwa nyuma ya mlango aliishi maisha ya mateso sana kiasi kwamba
hatamani tena kurudi.
Anamshukuru Yesu kwa kumtoa huko kwani sasa yupo huru kabisa..
Neema katika mahojiano na mwandishi (alieleza kisa chote.) chanzo:ufufuo na uzima |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni