MTOTO WA MCHUNGAJI APONYWA KATIKA MKUTANO WA MCH. JOSEPHAT GWAJIMA - MOSHI.
Mchungaji Kapange, wa mjini moshi baada ya kutoka kwenye mkutano wa Mch.Kiongozi josephat Gwajima, na kuona jinsi watu maelfu kwa maelfu wanavyo rudishwa kutoka katika vifungo vya shetani kwa kuitwa njoo na kuitiwa kwa Jina la Yesu, aliona ni vyema akajaribu kuyatumia maarifa na mamlaka hayo nyumbani kwake kwa mwane wa kike aitwaye Herrith .
Baada
ya kumuita kwa muda kidogo tu, mtoto akashtuka kwa nguvu sana, na
kuanza kumuhoji baba yake ambaye ndiye mchungaji aliyeyabeba maarifa
hayo kutoka mkutanoni, na kumuuliza hapa ni wapi baba?, mbona mimi skua
hapa...
ndipo
Mchungaji kapange alipo amua kukoleza moto na kumrudisha mtoto wake
vizuri na baada ya hapo akamuweka ufahamu wake sawa kwa kumuombea tena
kwa Jina la Yesu,na kumuwekea ulinzi wa Damu ya Yesu, ndipo mtoto
alipoanza kutoa ushuhuda wake kuwa alikuwa anaishi kuzimu, na dude
linaloaminika kuwa ni shetani aitwaye, mkuu wa kafara pia baba yake
akamuuliza kwa nini kila siku nilipokuwa nakuuliza kama unashida yoyote
hukuwa unasema? , mtoto akajibu kuwa alikuwa amefungwa na haoni na wala
hawezi kusema, na alipohojiwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima
wakati akitoa ushuhuda wake mbele ya mkutano alidai kuwa alikuwa
amechukuliwa na mtu anayeitwa KANUMBA...na uwanja mzima ukalipuka kwa
mshangao na haikuweza kujulikana kwa haraka ni kanumba yupi
aliyemchukua, ama mwigizaji au ni jina la mchawi wa mtaani kwao.
"Na ndio maana kama kuna wakuchukia Duniani, ambaye anatakiwa abezwe na watu wote ni mchawi anaye "m-host" shetani - -Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni