Ijumaa, 1 Novemba 2013

Mungu Asipokujibu Maombi Yako Muulize Ni Kwa Nini Hajakujibu

Mungu Asipokujibu Maombi Yako Muulize Ni Kwa Nini Hajakujibu

Mwl. Christopher Mwakasege

Habakuki 1: 1 – 4 … Ee BWANA, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa. Mbona wanionyesha uovu, na kunitazamisha ukaidi? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea. Kwa sababu hiyo sheria imelegea, wala hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa sababu hiyo hukumu ikipatikana imepotoka.

Nilie hata lini wewe hutaki kusikia
Habakuki inatueleza habari za mtu ambaye aliomba na Mungu akanyamaza lakini hakuacha kuomba
  • Alipokuwa anamuoma Mungu ondoa UOVU/ UDHALIMU/ MASHINDANO ailitegemea asubuhi asivione lakini kulipokucha akaviona bado vipo, kwa muda mrefu havijaondoka!
  • Akarudi kwa Mungu kuuliza kwa nini hajiondoka
V.4 sheria imelegea/ wala hukumu haipatikani! Kesi zinahairishwa, na hukumu ikipatikana imepotoka.
  • Habakuki hakunyamaza ila Mungu alinyamaza na Habakuki akauliza kwa nini hukujibu maombi (Habakuki 2: 1)
  • Kutokujibiwa maombi kuna zaa malalamiko usipojifunza kurudi kwa Mungu na kuuliza – badala ya kurudi kwa Mungu kuuliza kwa nini sikujibiwa!
  • Ndio maana wakati mwingine unaingia katika maombi na unaanza kulalamika, wewe unadhani unaomba lakini kumbe unalalamika kwa sababu ya maombi unayoomba muda mrefu bila majibu.
Mathayo 17: 19 … MBONA SISI HATUKUWEZA KUMTOA…
Wanafunzi wamejaribu kukemea pepo wakashindwa lakini Yesu akamkemea akatoka; unaona kabisa wakipewa malaka ya kukanyaga nyoka na ng’e na kukemea pepo; sasa hawa wamefuata maagizo.
  • Wanafunzi wakarudi kwa Yesu kuuliza kwa nini sisi hatukuweza japo tulishapewa mamlaka, amri na maagizo juu ya pepo wachafu. Wangeweza wakanyamaza!
  • Ukishindwa kukemea pepo nenda faragha umuulize Bwana Yesu kwa nini pepo hakutoka; maana jibu atakalokupa linaweza kuwa msaada kwako na kwa wengine.
  • Yesu akawajibu kwa sababu ya upungufu wa imani! Ni kweli ukiwa na imani kama chembe ya haradani unaweza kuhamisha milima; lakini tena akaongeza hii hata kama una imani haitoki, mpaka KUFUNGA NA KUOMBA.

(2Samweli 12: 15 – 20) Daudi kampa mimba mke wa askari, Mungu katuma mtumishi kumueleza Daudi na adhabu kuwa mtoto atafariki. Daudi alikuwa amepakwa mafuta lakini  akaomba na kufunga kwa siku 7, lakini mtoto akafa; baada ya mtoto kufa akaoga akavaa nguo zake akala akaenda hekaluni. Lakini haukuona Daudi akimuuliza Mungu kwa nini mtoto hakupona?
  • Usije ukafunga na kuomba kwa muda mrefu ukaona haujibiwi ukakata tama.
  • Swali ni kwa nini Mungu alinyamaza na hakumjibu Daudi. Watu watasema ni kwa sababu mtoto alizaliwa nje ya ndoa! Je ni watoto wangapi wamezaliwa nje ya ndoa lakini hawajafa lakini wa Daudi afe? Ni wanawake wangapi wamezaa nje na watoto wao wanakua lakin mtoto wa Daudi ndio afe?
  •  
  • (Zaburi 51: 5) … mimi naliumbwa katika hali ya uovu, mama yangu alinichukua mimba hatiani/dhambini
  • Watoto waliochukuliwa mimba dhambini, ile dhambi ni juu ya wazazi. Lakini mambo ya kuishi au kufa ni juu ya Mungu, kwamba ile tu unaishi ni kwa ajili ya Bwana. Kwa nini mtoto wa Daudi afe?
  • Jizoeze kumuuliza Mungu kwa nini sijajibiwa!
Bwana Yesu pia anaombi moja ambalo lilikataliwa …ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke…
  • Cha muhimu hapo sio kutojuibiwa ili kufahamu kwa nini Mungu hakukujibu maombi yako
  • Paulo aliachwa na Mjumbe wa shetani na alimuomba Mungu mara 3 na akajibiwa kwa neema yangu yakutosha na mahusiano yake na Mungu hayakudhurika

Hii ni Semina ya Mwl.Mwakasege nchini Uingereza iliyoandaliwa na CITE

Mtumishi wa Mungu kama haendi mbele za Mungu nakuulilza kwa nini alipokuombea hayo maombi hayajajibiwa itasababisha uhusiano wako na Mungu uwe duni na ukuaji kwako udumae.Ndio maana mahusiano mengine na Mungu yanakwama
Mmoja anaombewa na kupona na mwingine haponi, Mungu ni huyo huyo, madhabahu ni hiyo hiyo na biblia ni ile ile. Niliionja ile furaha ya mmoja kupona na pia nikaonja ila huzuni ya mwingine kutokupona, sasa utapata picha mchanganyiko wa chumvi na sukari! Inasumbua sana na usiporudi kwa Mungu  kuuliza na Mungu asipokusemesha unapata shida sana na kukwama, ni muhimu Mungu akusemeshe kwa nini hajakujibu ili mahusiano yako na Mungu yawe mazuri

Baba yangu alifariki mwaka jana, Bwana alinisemesha 2010 nikaomba aahirishe akakataa! Mungu alimuonyesha mpaka mahali pa kumzika. Tukagawa vitu akiwa hai, akasaini na baada ya hapo, nilikuwa naomba tu,  mwezi wa 8 tar 24 akafa! Tukiwa hosipitali tunaenda kushughulikia death certificate, wakati tunatoka saa 6 usika mama mmoja akaja kwetu akasema POLE SANA NIMESIKIA KITU AMBACHO KIMETOKEA. 

Lakini mtoto wangu kesho asubuhi anafanyiwa operation naoma umuombee, asubuhi saa 11 Roho Mtakatifu akanikumbuka, na nikaomba tukiwa kwenye msiba. Sasa Mungu asingekuwa ameniambia kwa nini baba ameondoka, unafikiri ingekuwa rahisi kumuombea Yule mtu wakati unaona kabisa kwa maombi yako hayajajibiwa!
Ni kitu ambacho kingeweza kutuletea mkwaruzo na Mungu rohoni. Wengine wameacha wokovu wengine wameenda kwa waganga kwasababu walipoombewa hawakujibiwa! Ukishaona namna hiyo uhusiano wako na Mungu haujakaa sawa. Ukiona Mungu hajajibu maswali yako na mahitaji yako, huhitaji kulalamika ila unahitaji kurudi kwake na kuuliza kwa nini!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni