JINSI YA KUSIKIA SAUTI YA MUNGU
WATU WA MUNGU WAKIMWABUDU MUNGU |
MUNGU ANAONGEA NA WATU KWA NJIA ZIFUATAZO; 1.kwa njia ya malaika; Alimtokea Dideoni Waamuzi 6:11-14 2, pia alimtokea Mariam Luka 1:26-37, pia alimtokea Petro gerezani Matendo 12:7-11. 2.Kwa sauti ya wazo; MUNGU alisema na Yahazieli kwenye kundi la watu 2Nyakati 20:12-17. 3.Kwa njia ya watumishi wake; Waebrania 1:1-2 {MUNGU ambaye zamani alisema na baba zetu katika manabii na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika MWANA ambaye amemweka kuwa mrithi wa yote tena kwa yeye aliufanya ulimwengu} pia MUNGU alimtuma Isaya kwa mfalme Hezekia 2Wafalme 20:12-17. 4.Kwa njia ya neno lake; alisema na Daniel kwa njia ya neno katika Danieli 9:1-4. 5.Kwa njia ya ndoto; alisema na Yusufu kuhusu ndoto ya Farao Mwanzo 41:15-32. 6. Kwa njia ya ishara; alisema na nabii Isaya kuhusu kuzaliwa kwa YESU katika Isaya 7:14. 7.Kwa njia ya maono; alisema ma Mtume Yohana katika Ufunuo 1:10. 8.Kwa njia ya mazingira; Katika kitabu cha Esta sura ya 2hadi sura ya 7
JEHOVAH NI MUNGU MPONYAJI |
MAMBO YA KUZINGATIA ILI USIKIE SAUTI YA MUNGU A.Kwanza kabla ya kuisikia sauti ya MUNGU lazima uwe na shauku ya kuisikiliza sauti ya MUNGU. B.Lazima uwe mwombaji/mwana maombi;mfano ili uongee na mtu lazima uanze kumsemesha mtu huyo na kwa MUNGU ni hivyo hivyo ila kwa MUNGU tunatumia njia ya maombi ndio maana amesema katika Yohana 14:14 kwamba tuombe chochote kwa jina la YESU yeye atajibu. C.Lazima utengeneze mazingira; Maana MUNGU ni utakatifu hivyo anatutaka tuwe watakatifu na tuwe tumefanyika watoto wake kupitia YESU KRISTO yaani Tumeokoka kwa kumaanisha maana MUNGU anajua yote hata siri zote za mioyoni mwetu. D.lazima uwe mtii wa kile anachokisema MUNGU.
YESU KRISTO NDIYE MWOKOZI PEKEE KWA WANADAMU WOTE |
Ubarikiwe sana ndugu popote ulipo na kama hujaokoka kumbuka kuwa wakati wa wokovu ni sasa hivyo tafuta kanisa la kiroho na waeleze watakusaidia kwani hakuna ajuaye kalenda ya maisha yake na BWANA YESU alikuja tuwe na uzima wa milele katika yeye kwani hakuna uzima wa milele kwingine kokote.MUNGU wa milele akubariki sana.
MUNGU AWE WA KWANZA KATIKA MAISHA YAKO YOTE |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni