JE TWAWEZA KURITHI MAOVU NA LAANA ZA BABA ZETU WALIOPITA?
JE TWAWEZA KURITHI MAOVU NA LAANA ZA BABA ZETU WALIOPITA?
|
GASPER MADUMLA |
Ninakukaribisha mpendwa katika tafakari hii.
Ambayo inakuhusu wewe pia na mimi maana sisi sote tumetokana na wazazi
wetu wa kimwili,yaani tulizaliwa kwa jinsi ya mwili licha ile jinsi ya
kiroho,ambayo kwa hiyo sisi si mali ya shetani tena bali ni mali ya
Mungu Baba wa mbinguni,tena kwa hiyo sisi tunao ukombozi yaani msamaha
wa dhambi.
Ni ukweli kabisa kwamba twaweza kurithi MAOVU na LAANA kutoka kwa mababa zetu waliopita ENDAPO KAMA MILANGO YAO IKO WAZI.
Labda nikupe mfano mdogo;
Tazama yale makabila kumi na mawili ya wana wa Israeli,Yale makabila
yalikuwa na watu ( watoto wa Yakobo kumi na mbili ) ambao leo hii hatuko
nao kimwili lakini MALANGO yao yalikuwa wazi,na ndio maana kukuwepo na
muendeleo wa kabila hizo kumi na mbili, HIVYO WOTE WALIKUFA LAKINI
MALANGO YAO YAKO WAZI
Soma EZEKIELI 48 :30-35
Hapo
awali,Wazazi wetu wetu wea kwanza,walipotenda dhambi na kulaaniwa basi
ilikuwa ni moja kwa moja zile laana zilikuwa na uwezo wa kutufuta sisi
na kutuingiza katika hukumu ambayo tulikuwa hatujahusika kwa dhambi
yoyote ile tena wala hatujui baba zetu walichokifanya.
Haleluyaaa..
Tunasoma Warumi 5 : 19
“ Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa
katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi
wameingizwa katika hali ya wenye haki. ”
Pia,
Tunasoma MAOMBOLEZO 5 :7
“ Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao. ”
Wazazi hawa walipoasi mbele za Bwana Mungu,ile dhambi ya kuasi ilikuwa
na upenyo kuweza kuingia kizazi kimoja hadi kingine,endapo kama mlango
wa dhambi uko wazi.
Tazama Kaini alivyoambiwa na Bwana Mungu
“ ”
Ona sasa;
Kaini aliposhindwa KUISHINDA DHAMBI ILIYOKUWA INAMUOTEA MLANGONI akaja
akamua ndugu yake, nayo ile dhambi ya mauji na roho ya mauti haikuishia
hapo maana mlango ulikuwa wazi, ile dhambi na roho ya mauti ikasimama
mlangoni,na baada ya kizazi cha tano,ile dhambi inajirudia tena vile
vile.
Kumbuka ;
Kizazi cha kwanza cha Kaini kinaanzia kwa
mwanaye wa kwanza Henoko,kisha kizazi cha pili ni Iradi,kizazi cha tatu
ni Mehuyaeli,,kizazi cha nne ni Methushaeli,na kizazi cha tano ni
Lameki.
Tazama namna ya uovu wa baba zao ulivyopita kuanzia kwa babu yao Kaini mpaka kwa Lameki ,
Tunasoma ;
Mwanzo 4 : 23
“ Lameki akawaambia wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi
wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; Maana nimemwua mtu kwa kunitia
jeraha; Kijana kwa kunichubua; ”
Bwana Yesu asifiwe…,Oooh Haleluyaaa……
Tazama pia namna ya dhambi na uovu ulivyopita kizazi hadi kizazi
kikianzia kizazi Abramu ( Ibrahimu ) pale kulipotokea njaa kali ya
kwanza naye akashuka hata Misri
Tunasoma ;
Mwanzo 12 : 10-13
“ Basi kulikuwa njaa katika nchi ile; Abramu akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa nzito katika nchi.
Ikawa alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, Tazama, najua ya kuwa u mwanamke mzuri wa uso;
basi itakuwa, Wamisri watakapokuona watasema, Huyu ni mkewe; kisha wataniua mimi na wewe watakuacha hai.
Tafadhali useme, wewe u ndugu yangu, iwe heri kwangu kwa ajili yako, na nafsi yangu iishi kwa ajili yako. ”
Tazama sasa na kizazi cha pili cha ISAKA
Mwanzo 26 :7,
“ Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni ndugu
yangu huyu maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije
wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso. ”
Pia ;
Tazama dhambi ile ile ya kusema uongo iliyoanzia kwa IBRAHIMU,ikaenda kwa ISAKA na mwishoe kizazi cha tatu cha YAKOBO.
Hapa utaona Yakobo naye anamdanganya baba yake Isaka ili apate
mbaraka ambao ulikuwa unastahili aupate kaka yake Esau ( SOMA ; Mwanzo
27 :1-27 )
Na ndio maana dhambi hizi bado hata leo zinatutesa
sana,watu wengi wamekuwa hawavuki kimaendeleo si kwa sababu hawafanyi
kazi kwa bidii,bali maovu ya baba yao yanatafuna bidii zao.
Mfano ;
• Utakuta katika famili,watoto wote wanaishia elimu ya darasa la saba tu,au wengine kikomo chao ni elimu ya form four tu.
• Utakuta katika familia,babu kafa kwa ugonjwa wa kisukari,baba naye
kafa kwa kisukari,mtoto naye alishakufa kwa ugonjwa wa kisukari,Mjukuu
sasa ndio anaumwa ugonjwa huo huo wa kisukari,Na ukiuliza watakuambia “
AAH! HUU NDIO UGONJWA WETU NDUGU ! ”
• Au utakuta katika
familia,Tatizoi la kuoa au kuolewa ni sugu,yaani watoto wote hawaoelewi /
Kuoa wakijitahidi sana ni kuishi maisha ya UCHUMBA SUGU na kuzaa watoto
ndani uchumba sugu.
Ila leo ninakuambia hivi Yesu Kristo U hai kukuponya na hizo laana za mababa waliopita,
NA KWANZA KABISA ACHA TABIA YA KUSEMA ETI “ UGONJWA HUU NDIO UGONJWA WANGU,!
YAANI MWENYE HAYO MAGOJWA NI SHETANI PEKEE, UKISEMA NI UGONJWA WAKO
MAANA UNATENGENEZA UWE WAKO,NA UTAKUWA HIVYO MAANA NI WEWE MWENYEWE
UMEUUMBA KWA KINYWA CHAKO ”
Lakini napenda kukutangazia wewe
mpendwa kwamba ipo njia ya kutatua matatizo haya yote ya
magonjwa,laana,roho za mauti n.k yaani zootee. Njia ya kuzuia vyote
hivi ni YESU KRISTO,PEKEE. Nasema YESU KRISTO TUU ndio dactari wa yote
haya
Yeyote yule atakayempokea Yesu Kristo kuwa Bwana na
Mwokozi wa maisha yake,na kukaa ndani yake,kwanza kwa KUFANYIWA IBADA
MAALUM YA UKOMBOZI hakika mtu huyo hatakuwa tena chini ya laana zote
hizo.
Kumbuka ipo njia moja tu ya msamaha wa dhambi pindi utubupo nayo ni DAMU YA YESU KRISTO WA NAZARETI .
Tunasoma ;
Mathayo 26 : 28
“ kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. ”
Wito wangu kwako ;
Sio kila laana za kurithi kwamba zinatoka kwa kuongozwa sala ya toba pekee,
kwa njia hiyo laana nyingine hazitoki ngo’ hata kama umeokoka laikini
utajikuta laana zinakufuatilia,au utakuta maovu haya ya baba zetu
waliopita yanakufuatilia
hivyo baadae unashangaa na kusema “ Mbona mimi nimeokoka,lakini nashindwa kuaacha UZINZI ? ”
Bali laana hizi zinatoka pale tu utakapofanyiwa IBADA YA UKOMBOZI kwa damu ya Yesu Kristo tu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni