Jumatatu, 4 Novemba 2013

JIFUNZE KUHUSU KUFUNGA NA KUOMBA

JIFUNZE KUHUSU KUFUNGA NA KUOMBA


Isaya 58:1-14 ''
Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao. Walakini wanitafuta kila siku; hupenda kujua njia zangu; kama vile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao, hutaka kwangu amri za haki; hufurahi kumkaribia MUNGU. Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya KUFUNGA kwenu MNATAFUTA ANASA ZENU WENYEWE, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu. Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu. Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA?  Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.Ndipo utaita, na BWANA ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;
 na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri. Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui. Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia.
 Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe; ndipo utakapojifurahisha katika BWANA; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha BWANA kimenena hayo''
Yafuatayo ni mafundisho kuhusu kufunga na kuomba na yote hayo yanatokana na hiyo Isaya 58:1-14''
 -Tusifunge kwa ajili ya kutafuta furaha yetu bali tufunge kwa ajili ya kazi ya MUNGU.
-Ni watu wachache wanaoweza kufunga kwa ajili kuomba kwa ajili ya mikutano ya injili na kuombea watumishi wa MUNGU.
Mathayo 6:33 ''Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.'' Hapo ndipo watu wengi tunakosea, maombi yetu hayajibiwi kwa sababu ya kutaka mambo yetu tu ,
-unafunga kwa sababu unamtaka MUNGU na nguvu zake na mapenzi ya MUNGU
-Wengine wanafunga ili waonekane wa kiroho zaidi.
-Watu wengi hawawezi kufunga kwa ajili ya wengine.

=Funga ambayo MUNGU anaitaka ni ile ya kuutafuta ufalme wake ,

KATIKA KUFUNGA MUNGU ANATAKA YAFUATAYO.

1:  Kufungua vifungo vya uovu kwako.
-Au kwa wengine au hata kwa kanisa  baadhi ya vifungo ambavyo mtu anaweza kufunga ili kuvifungua kwake au kwa wengine ni pamoja , ulevi, uasherati, uzinzi, uchawi n.k
2:  Kuzilegeza kamba za nira.
-Kama ng’ombe  ili achomoke kwenye kwenye nira ili awe huru bila kufungwa na nira, watu wengi wamefungwa na nira mfano nira za rushwa na uzinzi, uchawi na uongo, usengenyaji na dini.
3:  Kuwaacha huru walionewa.
-Kuna watu wameonewa na shetani hivyo kwa maombi ya kufunga ni lazima tuwaache huru mfano mazezeta kuonewa na watu.
4:  Kuvunja kila nira ambayo imekufanya au imekufunga au imemfunga mwingine unayemfahamu.

 =pamoja na kufunga na kufanya yote hayo  lazima ufanye na haya.

(a) Kuwagawia watu wenye uhitaji na kuwa mtoaji kwa ujumla.

(b) Kuwasaidia maskini.
(c) Umuonapo mtu yuko uchi mvike nguo.
(d) Usijifiche na wenye damu moja na wewe.

Baada ya hapo nuru yako  itapambazuka. Yaani vyote unavyovitaka vitakuja vyenyewe  lakini haya yote hukiyatafuta wala kuyaomba ila ni kwasababu ulitafuta kwanza ufalme wa MUNGU.
MUNGU awabariki sana.
Ni mimi ndugu yako  Peter Michael Mabula
                  Maisha ya ushindi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni