NILITAKA KUJIUA
mtu akisumbuka kuweka taa kubwa ni mfano wa jaribu gumu katika maisha . |
- ''kuna wakati ilikua karibu kabisa nijiue kwa sababu ya mapito magumu niliyokuwa napitia'' ; alisema Jerry akiwa na miaka 19. kila sekunde 40 mtu mmoja hufanikiwa kujiua mahali fulani duniani na kila sekunde 3 huwa mtu anajaribu kujiua ila hafanikiwi. siku moja mtaani kwetu jamaa mmoja aliyezoea kugombana na mke wake wakati wa kutishia kujiua alijiua kweli. Tulimkuta amejitundika mtini kwa kanga ya mkewe. Sababu za watu kujiua 1.Aibu ya kukosa au kushindwa kufikia malengo 2.Kujiona hawafai, hawapendwi na ni wapweke 3.Kuachwa na mpenzi-mvulana au msichana, mme au Nmke 4.Kupata mkasa mkubwa wa deni au fedha,au madeni mazito 5.Kupata janga zito kifamilia, kazini na kukata tamaa. Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu cha Dar es salaam aliamua kujirusha toka ghorofa ya tisa akajiua kwa kufeli mitihani, mfanyabiashara mkubwa wa Surabaya Indonesia alikuwa ameamua kujiua kwa kujisababishia ajali. jioni akapita mahali polipokuwa na mkutano wa neno la MUNGU. mhubiri bila kujua kinachoendelea akasema naguswa moyoni kwamba kuna mtu hapa ameamua kutaka kujiua leo lakini BWANA YESU anampenda mtu huyo na hataki afe kwani mtu huyu anataka kujiua kwa kujisababishia ajali ya gari lake watu wakadhani amekufa kwa ajali ya kawaida. Hebu atoke mbele mbele tumwombee, jamaa akatoka akaombewa na akashuhudia kisa chake na watu wakamtukuza MUNGU. USIJIUE; Mlinzi wa gereza la filipi alitaka kujiua,MATENDO 16:27.lakini paulo akamuwahi akamzuia, Akampa tumaini. mlinzi yule akamuuliza ''yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? paulo akamwambia mwamini BWANA YESU nawe utaokoka pamoja na nyumba yako'' Akamwamini YESU akaokoka yeye na nyumba yake akapata furaha ya ajabu. BADALA YA KUJIUA Badala ya kujiua tambua kwamba liko tumaini kwa YESU, yeye anasema ''Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo {mambo], nami nitawapumzisha'' MATHAYO 11:28. Ninajua una mapito magumu sana, na maisha yako hayana ladha . umekata tamaa ya kuishi. Ndugu hawakupendi. kazi umefukuzwa, kodi unadaiwa. kusoma hukusoma.hakuna anayekujali ni kama vile una laana, unaishi kwa hofu ukibangaiza, unakula kwa ugumu ,unaishi mradi tu siku ipite. umechoka kuishi. Badala ya kukata tamaa na kutamani kujiua mpe YESU maisha yako. yeye ndio suruhisho la yote '' ukimkiri na kumuamini moyoni mwako utaokoka'' WARUMI 10:9-10. Nenda kanisa lolote la watu waliookoka lililo karibu nawe. wambie umeamua kumpokea BWANA YESU maishani mwako kuanzia sasa watakusaidia. kama una ushuhuda wowote wasiliana nami kwa mabula86@yahoo.com. MUNGU wangu na akubariki sana na ombi langu uishi maisha ya furaha kwani kujiua ni kujipeleka motoni kwani anaejiua ni sawa na muuaji hivyo dhambi ya kuua inaweza kumpeleka mtu motoni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni