NATAKA NIPATE KUONA* sehemu ya mwisho* Marko 10:51
Na mtumishi Gasper Madumla |
Bwana Yesu asifiwe...
Jina la Bwana lisifiwe sana...
Haleluya...
"Yesu akamjibu,akamwambia,Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia,Mwalimu wangu,NATAKA NIPATE KUONA" Marko 10:51
Ni maombi yangu kwako wewe mpendwa usomaye ujumbe huu,kwamba Mungu wa mbinguni,Baba yetu,Jehova akusaidie upate kuona kiroho.
Hakuna jambo la msingi kama kuona kiroho,
Mambo mengine yote hata kama utayakosa likini ni afadhali usikose kuona.
Lakini kuona kiroho hutegemea ile namna ya kuja kwako. Kweli ninakubali ya kwamba kuna watu ambao wamepewa neema hiyo ya kuona mambo katika ulimwengu wa roho.
Lakini watu wa namna hiyo ni wachache mno,
Wengine waliobakia ni vipofu.
Sasa hatari ni hii;
Kuwa kipofu,lakini hujitambui kama wewe U kipofu.
Tumeona na kujifunza mengi kupitia Bartimayo aliyekuwa kipofu,
Na hata katika andiko hilo hapo juu,tazama kwanza yeye mwenyewe alijitambua kwamba ni mtu kipofu asiyeona.
Kisha akachukua HATUA ya kutaka kupata kuona.
Na hizo hatua madhubuti alizozichukua Bartimayo ndio hizo tunazojifunza siku ya leo,ili sisi nasi tupate KUONA.
Wale wote waliokuwa na Bwana Yesu akitokea Yeriko hawakupata kuona kwa sababu ndani yao walijiona ni watu wenye uwezo wa kuona
Na kumbe wao pia walikuwa vipofu.
Tazama;
Bartimayo alipogundua siri hiyo ya kwamba inambidi aone,ndipo alipompazia Bwana sauti kuu,ingawa alikemewa anyamaze lakini yeye ALIKAZA kuliitia Jina la Bwana,
Naye akaokoka na ule msiba.
Jambo moja la msingi tunalojifunza kupitia mfano huo wa Bartimayo (Marko 10 : 51)
Ni hili;
* kuwa na shauku ya kutaka kuona mambo ya kiroho,macho ya mioyo yetu yatiwe nuru.
Utakapo KAZA kuliitia Jina la Bwana kwa habari ya kuona,basi ujue utapewa kuona tu.
Lakini ni lazima UKAZE kutaka kuona
* Kukaza maana yake ni kungangana kuliitia Jina la Bwana pasipo kujali mazingira yanasemaje.
Maombi mengi tuyaombayo sisi wakristo hayafanikiwi kwa sababu hatuoni nini tunachokiombea. Yaani ni kama vile kuitafuta shilingi gizani pasipo taa.
Hivyo hujikuta tukiomba sana pasipo kujua tunaomba nini maana tu vipofu.
Ni maombi yangu kwako,kwanza utamani sana kumuomba Bwana wa Utukufu akupe kuona kwanza kabla ya kuomba kitu chochote kile.
Ni sawa yamkini una shida nyingi,lakini hata kama shida hizo zi nyingi namna gani,bali wewe KAZA kumuomba Bwana akupe macho ya rohoni upate kuona.
Bartimayo alikuwa ni mtu mwenye shida kubwa,tena ni muhitaji,mtu omba omba.
Lakini hakuona vyema kwamba awe tajiri akiwa bado ni kipofu pale alipoambiwa na Bwana wataka nikufanyie nini?
Yeye alichokiona kuwa ni chema ni kutaka kupata kuona tu,hivyo vingine ni vya ziada.
Maana ukweli ang'eliweza kumuomba Bwana awe tajiri,lakini utajiri ukiwa kipofu ni sawa na kuwa na gari pasipo kujua njia uiendayo.
Imefika wakati sasa tubadili mkao wetu wa maombi mbele za Bwana.
Yatosha kuomba kuoa,
Yatosha kuomba kuolewa,
Yatosha kuomba kujenga,
Yatosha kuomba kupata kazi,
Yatosha kuomba kupata gari.
Bali yafaa kuomba kuona kiroho tu.
Ndiko kwenye manufaa zaidi, kuliko maombi ya namna yoyote ile.
Wachungaji wote na watumishi wote wa Mungu nasi tu vipofu bado,
Hatutakiwi kujihesabia haki na kujiona tu macho kiroho.
Bali nasi tuzidi sana kuomba kupata kuona
Ambapo kutasaidia sana katika huduma zetu za kiroho. Maana huwezi kufanya huduma yenye mafanikio ukiwa kipofu.
Bwana asema twende mbele zake tukiwa na hoja ya msingi yenye nguvu., kutaka kupata kuona ni hoja moja ya msingi na yenye nguvu.
*Hatuwezi kuona tukiwa ni wa dhambi.
*Sharti tusafishwe kwa damu ya mwanakondoo kwanza.
Mfano:
Uingiapo ndani ya chombo kama pipa ya glass,huwezi kuona nje ikiwa sehemu za hilo pipa la glass likiwa ni chafu.
Kwamba wewe mwenyewe huwezi kuona nje na wala wa nje hawezi kukuona wewe uliyendani.
Alikadhalika kwa Mungu ni vivyo hivyo.
Wewe ukiwa ni mchafu wa dhambi,huwezi kumuona Mungu,wala Mungu hakusikii uombapo.
Wito wangu kwako ni kuchukua hatua , kama zile za Bartimayo za kwenda mbele za Bwana kwa kuomba rehema zake/ kuomba toba ya ukweli.
Kisha kuomba jambo moja tu la kutaka kupata kuona kiroho.
MWISHO.
*kwa maombezi na kusalimiana;
0655 111149.
0783 327375.
* Nakutakia mafanikio mema ya kukua kiroho kwa kuona katika ulimwengu wa roho.
UBARIKIWE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni