Ijumaa, 1 Novemba 2013

WATOTO WAZIMIA BAADA YA KUMUONA MAMA YAO ALIYEKUFA MIAKA MINGI KUFUFUKA TOKA KWA WAFU

WATOTO WAZIMIA BAADA YA KUMUONA MAMA YAO ALIYEKUFA MIAKA MINGI KUFUFUKA TOKA KWA WAFU

Ni siku ya nne ya mkutano mkubwa wa ufufuo na uzima na Mchungaji Josephat Gwajima jijini arusha, ambapo miujiza mingi imeendelea kutendeka.

Leo Mch. Kiongozi Josephat Gwajima amefundisha kuhusu "ULIMWENGU WA ROHO" na kufundisha aina za misukule na jinsi wanavyochukuliwa somo ambalo lilifungua watu wengi ambao walikuwa msukuleni.

Umati uliokuwepo mkutanoni siku ya nne...


Watu wengi walirudishwa kutoka msukuleni na kufanya watu kushangazwa sana na matendo makuu ya Mungu, kiasi kufanya hata baada ya kuruhusiwa kuondoka wao wakaamua kubaki ili tu waone maajabbu ya Mungu...



Ni makutano makubwa sana katika viwanja vya relini jijini Ariusha; Mungu amedhihirisha uweza wake kwa namna isiyokuwa ya kawaida.

Dada aliyekuwa amechukuliwa msukule akitoa ushuhuda baada ya Kurudishwa.

Siku ya nne kumetokea jambo la ajabu pale wanawake wawili walipoanguka karibu na eneo la mkutano kutoka hewani. Na kuleta taharuki miongoni mwa watu waliokuwepo mkutanoni. picha zifuatazo zinaonyesha tukio zima.

Mmoja wa mwanamke aliyeanguka kutoka hewani muda mfupi baada ya maombi ya Mchungaji Gwajima


   Kulia ni bibi aliyefufuka wakati mkutano ukiendelea na kuzua tafrani ya wanawe kuzimia, na kushoto ni mwanamke mmoja mchawi aliyedondokea katika viwanja vya mkutano wa injili unaoendelea hapa Arusha
  
Mtoto azimia mara baada ya kumwona mamaye aliyekufa miaka mingi.

Watoto wa mwanamke aliyekufa miaka mingi baada ya kuzinduka..tena...



Maelfu ya watu wakiwahawataki kiondoka mara baada ya kushuhudia mambo makuu ya Yesu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni