"NIPO DUNIANI KWA KUSUDI GANI???"
Je, niko duniani kwa kusudi gani? mwisho wa safari hii utajua kusudi la Mungu kwa maisha yako. Kwa kuwa na mtazamo huu utapunguza taabu zako ,na kurahisisha maamuzi ,pamoja na kuongeza utoshelevu wako,na cha muhimu zaidi ni kukuandaa katika umilele.
‘Wawili ni bora kuliko mmoja, kwa sababu kwa pamoja mwaweza kufanya kazi bora. Kama mmoja ataanguka chini ,mwenzake atamwinua……Wawili wanaweza kushinda mashambulizi yanayoweza kumshinda mtu akiwa peke yake.
Kamba iliyosokotwa kwa nyuzi tatu ni vigumu kuikata’Mhubiri 4:9
NIKO DUNIANI KWA KUSUDI GANI?
Maisha yanayotegemea vitu ni maisha mfu, kama kisiki; maisha yanayotegemea Mungu ni mti unaostawi sana. Mithali 11:28
Wamebarikiwa wanaomtumaini BWANA ……..
Ni kama miti iliyopandwa kandokando ya mto,
Yenye mizizi ifikayo chini kwenye maji.Miti kama hiyo
Haisumbuliwi na joto wala miezi ya ukame.Majani yake
Hhukaa mabichi na hudumu kuzaa matunda mazuri.Yeremia 17:7-8
YOTE HUANZA NA MUNGU
Kwa kila jambo,katika kila kitu, kilicho juu na kilicho chini kinachoonekana na kisichoonekana…..kila kitu kilianza katika yeye na hupata kusudi katika yeye.
Wakolosai 1:16
Bila kukubali kuwa kuna Mungu, swali kuhusu kusudi la maisha halina maana.
Kusudi la maisha yako liko juu zaidi ya utoshelevu wako binafsi, amani yako,au hata furaha yako.Kama unataka kujua kwanini uliwekwa hapa duniani, lazima uanze na Mungu. Kutafuta maana ya maisha kumewatatiza wengi kwa maelfu ya miaka. Hivi ni kwa sababu tunaanza na mwanzo mbaya –sisi wenyewe. Biblia inasema, Mungu ndie huongoza maisha ya viumbe vyake; maisha ya kila mtu yako katika uweza wake. Huwezi kuvuka kwenye kusudi la maisha yako kwa kuanza kujitazama mwenyewe. Ni lazima uanze na Mungu, muumba wako.Unaishi kwa sababu tu Mungu anapenda uishi.Wewe uliumbwa na Mungu na kwa ajili ya Mungu na mpaka ufahamu hivyo,maisha hayatakuwa na maana yoyote.Ni katika Mungu peke yake ndio tunaweza kuvumbua asili yetu,utambulisho wetu,umuhimu wetu, kusudi letu, umaana wetu, na mwisho wa maisha yetu kwa ujumla. Njia nyingine yeyote hugonga ukuta.
Uliumbwa kwa ajili ya Mungu, na sio kinyume, na maana ya maisha ni kumruhusu Mungu, akutumie kwa malengo yake, na sio wewe umtumie Mungu kwa Malengo yako. Biblia husema kuendekeza nafsi yako katika mambo haya, huleta mauti, lakini kumtazama Mungu hutuongoza mahali pa uwazi na maisha huru.Angalia ndoto zako, changanua mambo unayothamini (values). Weka Malengo, tambua kipawa chako Uwe na malengo ya juu, shughulikia hayo, jiweke wakfu, Amini unaweza kutimiza Malengo yako.Wahusishe wengine na usikate tama.Kwa hakika, melezo hayo huleta mafanikio makubwa kila mara.Mara nyingi unafanikiwa kufikia Lengo lako unapoweka moyo wako hapo.
Ili kugundua kusudi la maisha yako lazima ugeukie Neno la Mungu, sio hekima ya ulimwengu .Unapaswa kujenga maisha yako kwenye msingi wa kweli wa umilele .Sio katika saikolojia hamasa ya mafanikio au hadithi za kuhamasisha Biblia inasema “katika Kristo tunatambua sisi ni nani na tunaishi kwaajili gani. Mwanzoni tulipokua hatujasikia habari za Kristo na kutupa matumaini, yeye aliweka jicho lake kwetu ,alikuwa na mpango juu yetu wa maisha ya Utukufu, ambayo ni sehemu ya mpango uliokamilika unaotekeleza katika kila kitu na kila mtu.Bila Mungu maisha hayana maana.
KUFIKIRI JUU YA MAISHA YANGU
Jambo la kutafakari: Sio kuhusu mimi
Kila kitu kilianza katika yeye na hupata kusudi lake katika yeye.
Wakolosai 1:16
Swali la kujiuliza: Pamoja na matangazo yote yanayonizunguka ,je,nawezaje kujikumbusha kwa maisha hakika ni kuishi kwa ajili ya Mungu.?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni