MAPEPO HAYAWEZI KUSTAHIMILI KUSIKIA NENO LA MUNGU
Mapepo hayawezi
kustahimili kusikia Neno la Mungu.
Wakati fulani nilirudi nyumbani kutokea kanisani na nikawa nasoma
Maandiko. Niliinua macho na kuyaona mapepo kadhaa. Nikaanza kumwomba Mungu
anisaidie. Sikuwa nina hofu lakini nilikuwa tu sijisikii amani kuyaona. Wakati
nikiwa namwomba Mungu anisaidie, nilisikia sauti moyoni mwangu ikisema, “Soma
Maandiko.”
Nikauliza: “Nini?” Sauti ile ikarudia tena: “Soma Maandiko.”
Nilitii na nikaanza kusoma Maandiko. Lakini baada ya muda kidogo, Mungu
akaniambia: “Soma kwa sauti.” Nikawa
kama nimechanganyikiwa kidogo, lakini Mungu akarudia tena: “Soma Maandiko kwa sauti.” Nilipoanza kusoma Maandiko
kwa sauti niliona kuwa mapepo yale yanafunika masikio yao kwa mikono yao yenye
makucha na kuanza kuhangaika kwa mateso makubwa. Hivi ndivyo nilivyojifunza
kuwa mapepo hayawezi kustahimili kusikia Neno la Mungu. Neno la Mungu
likitumika kwa imani na kweli, ni silaha kubwa dhidi ya nguvu za giza.
Tangu hapo, nimejenga tabia ya kusoma Neno la Mungu kwa sauti. Pia
nimepakua kutoka kwenye intaneti Agano Jipya la sauti (lililo katika fomati ya
MP3). Nikiwa nyumbani, karibu muda wote huwa nimefungulia Biblia hiyo. Huwa
naisikiliza nikiwa nakula, napika, najipamba, nk. Mara kadhaa Mungu amekuwa
akielekeza umakini wangu kwenye mistari ya muhimu sana na kunieleza maana yake
wakati nikiwa nakula au najiandaa kwenda kazini. Mwenzangu mmoja aliniuliza ni
rekodi ya aina gani hii ambayo huwa naisikiliza karibu saa 24 kila siku.
Nilimweleza na kumshirikisha sababu zangu za kufanya hivyo, lakini najua kuwa
hakunielewa kikamilifu.
Vilevile nilipakua Agano Jipya kwa ajili ya kompyuta yangu ya mfukoni.
Kila ninapopata nafasi, huwa najaribu kusikiliza Maandiko niwapo kazini. Mara
nyingi ninapopatwa na mashambulizi ya adui nikiwa kazini, huwa naamua
kusikiliza Biblia hiyo kama njia yangu mojawapo ya kunisaidi kushinda vita.
Pia nilijifuza kwamba mapepo huteswa sana hasa na Kitabu cha Ufunuo, na
hususani sura ya 17, 18, 19, pale ambapo Maandiko yanazungumzia kuhusu hatima
yao ya mwisho. Hayawezi kabisa kusikiliza mistari kuhusu Babeli ulioanguka na
mistari kuhusu ibilisi na manabii wake wa uongo kutupwa kwenye ziwa la moto.
Kuna mara kadhaa ambapo niliyatishia mapepo kuyasomea Kitabu cha Ufunuo
kama hayakuacha kunisumbua au kuondoka. Ni wazi kuwa sikuyatishia tu, bali
nilisoma sehemu hizo. Mbinu hii hata hivyo si kwamba ndiyo jibu la kila kitu.
Haikuhakikishii ushindi kwenye kila shambulizi, lakini ni mbinu nzuri ya msaada
upande wetu. Mungu mara zote hunisaidia kupata mstari ambao unaweza
kunyamazisha kabisa sauti ya adui. Nimeshajifunza kuwa si kila mstari
utanyamazisha manyanyaso ya adui bali ni ile mistari ambayo inahusiana moja kwa
moja na tatizo lililopo. Ni kama ilivyo kuinua upanga hewani na kupiga kushoto wakati
adui yuko kulia. Hiyo haisaidii kumshinda adui. Ni pale tu unapoelekeza mapigo
yako kwenye lengo ndipo utashinda mapambano. Hali ni ileile hata kwenye mistari
ya Biblia na uongo na unyanyasaji wa adui. Ndiyo maana NI LAZIMA kujifunza Maandiko kwa bidii na kuweka
mistari kwenye kumbukumbu kichwani.
Katika majaribu ya Yesu ya siku 40 kule jangwani – pale shetani
alipomjaribu – je, Yesu alifanya nini? Alimjibu shetani kwa kutumia mistari
sahihi kutoka kwenye Neno la Mungu. Alishindana na shetani kwa kutumia upanga
wa Roho Mtakatifu, ambao ni Neno la Mungu. Shetani anamnukulia Yesu Neno lakini
si kikamilifu; anataja nusu ukweli. Ukweli nusu mara zote huwa ni uongo uliokusudiwa kudanganya wanadamu na
kupoteza makusudi ya Mungu kwa ajili ya wanadamu. Yesu alimnukulia shetani
Kweli yote kwa 100% ... na shetani hakuwa na kitu chochote cha
kushindana na mbinu ya mapambano ya Yesu. Shetani alishindwa kwa 100% kwenye
vita hivyo. Mungu hakuruhusu jambo hili liandikwe kwenye Biblia kwa bahati tu
ili kujaza nafasi. Shindana na
mashambulizi ya mapepo kwa kutumia kwa usahihi Neno la Mungu.
Lijue Neno ... Liamini Neno ... Fahamu lini pa kulitumia kwa usahihi
(usinukuu tu Neno nje ya uhalisia wa hali yako; mapepo watakucheka!); kisha
tamka Neno la Mungu kwa sauti, imba nyimbo zinazotokana na Maandiko; omba Neno
wakati wa maombi yako na kuyaambia mapepo yanayokuzunguka, (japo huenda hutakaa
uyaone) – sikiliza Neno la Mungu linapoongelewa dhidi ya matatizo
yanayokukabili, lakini kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu.
Mambo yote
yanaweza kushindwa lakini haiwezekani kwa Neno la Mungu kushindwa maana Roho
Mtakatifu ndiye anayelifanya litende kazi. Mungu hawezi kusema uongo; hivyo
Neno la Mungu nalo haliwezi kuongopa. Wanadamu hapa duniani wanaweza
wasilielewe Neno la Mungu, hivyo wakalitumia kimakosa katika hali zao, lakini
hilo haliwezi kutokea kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Hilo kila mara hutokea kwa
sababu ya nguvu za kipepo na mawazo ya kimwili ya wanadamu ambao hawana ufunuo
kamili wa Neno la Mungu, au huenda wamelipindisha bila wao kujua, na kulifanya
liseme kitu ambacho Mungu hajasema. Kama Mungu alivyoandika: "Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita
kamwe.” (Tazama: Mt.
24:35; Mk 13:31; Lk 21:33). Mtu anapopokea ufunuo kamili kwamba Yesu
Kristo ndiye Neno, haishangazi basi
kwamba halitapita kamwe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni