Ushuhuda wa Adelaida Juu ya Mbingu na Kuzimu
Mwanamke mmoja kutoka Bolivia aitwaye Adelaida De
Carrillo alipelekwa Mbinguni na Kuzimu na Yesu Kristo. Kule alionyeshwa ni
Utakatifu gani anaotakiwa mtu kuwa nao ili aweze kuingia kwenye UFALME WA
MUNGU, na pia ni dhambi gani (ambazo wengi wetu tunadhani kuwa ni ndogo),
zinaweza kumfanya mtu aingie Jehanamu.
Tuko kwenye safari ya maisha ya kimwili hapa duniani
tukielekea kwenye maisha ya kiroho kwenye ulimwengu ule ujao. Huo ni ulimwengu
halisi ambao una maisha halisi, utawala halisi na kanuni halisi za kuingia
huko.
Wakati ulimwengu tuaoishi leo una serikali nyigi na
watawala wengi, ulimwengu ule ujao utakuwa na serikali moja tu inayoongozwa na
Yesu Krito. Wakazi wa uliwengu huo ni watakatifu WOTE!!!
Huo ni ulimwengu unaoongozwa na Mungu mwenyewe kwa upendo
na amani. Kule hakuna magonjwa, vita, njaa, na dhambi zingine zote. Tiketi ya
kuingia kule ni moja tu: nayo ni kumwamini Yesu Kristo kama
Mwokozi aliyekufa na kufufuka kwa ajili yetu. Kisha tunaishi hapa duniani kwa kutii
maagizo yake.
Hata hivyo, wale wote ambao hawatakuwa wamestahili
kuingia kwenye ulimwengu huo (kutokana na wao kuishi maisha ya dhambi na uasi
dhidi ya sheria za Mungu hapa duniani), watatupwa nje ya mbingu kweny giza na moto, yaani
kwenye jehanamu ya milele.
Katika ushuhuda huu, tunaona kile ambacho Bwana Yesu
anatuagiza ili tuweze kustahili kuingia kwenye ufalme ule ujao na kuishi na
Mungu MILELE!!!
Adelaida De Carrillo anasema:
HATUA YA 1: Ilianzia Kanisani kwenye wakati wa Huduma
Katika Ezekieli 36:25-26,
Biblia inasema:
“Nami nitawanyunyizia maji safi,
nanyi mtakuwa safi;
nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia
roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu,
nami nitawapa moyo wa nyama.”
Ushuhuda wangu uko namna hii: Siku moja ya Jumapili,
kwenye saa 3 hivi, Kanisa letu lilikuwa na kipindi cha Huduma. Mungu alikuwa
akimimina baraka zake juu yetu. Mchungaji wangu aliniambia, “Adelaida, Bwana ananiambia nikupake
mafuta.”
Aliweka mafuta mengi kwenye viganja vya mikono yake na
akaanza kunipaka mwilini. Alinipaka masikioni, miguuni, tumboni na kwenye mwili
wangu wote. Alipoweka mikono yake kwenye uso wangu, niliona mwanga mkubwa ukija
kutokea juu, ukinielekea mimi. Kuanzia hapo nilipoteza fahamu na sikujua
kilichokuwa kinaendelea kwangu.
HATUA YA 2: Safari Yangu Kwenda Mbinguni
Malaika walikuja na kunichukua tukaenda juu pamoja nao.
Walianza kupambana na mashetani maana njia yetu ilikuwa imewekewa vizuizi.
Kulikuwa na blangeti jeusi kwenye mawingu, likiwa limejaa mapepo yaliyojaribu
kutuzuia kupita. Baadaye niliona mwanga mweupe kutoka Mbinguni na malaika mzuri
sana akiwa na upanga wenye nuru mkononi mwake.
Aliinua upanga wake na kuanza kupigana na mapepo yale ili sisi tupite.
Malaika yule alionekana kama Mwana wa Mfalme. Alikuwa na bamba la dhahabu
kifuani mwake na nguo nzuri sana. Nywele zake zilikuwa za rangi ya dhahabu, na
uso wake ulikuwa kama miali ya mwanga. Alikuwa mzuri sana!
HATUA YA 3: Kuoshwa na Kubadilishwa Moyo Wangu
Malaika walikuja na kunichukua tukaenda juu pamoja nao.
Walianza kupambana na mashetani maana njia yetu ilikuwa imewekewa vizuizi.
Kulikuwa na blangeti jeusi kwenye mawingu, likiwa limejaa mapepo yaliyojaribu
kutuzuia kupita. Baadaye niliona mwanga mweupe kutoka Mbinguni na malaika mzuri
sana akiwa na upanga wenye nuru mkononi mwake.
Aliinua upanga wake na kuanza kupigana na mapepo yale ili sisi tupite.
Malaika yule alionekana kama Mwana wa Mfalme. Alikuwa na bamba la dhahabu
kifuani mwake na nguo nzuri sana. Nywele zake zilikuwa za rangi ya dhahabu, na
uso wake ulikuwa kama miali ya mwanga. Alikuwa mzuri sana!
Ghafla, nilisikia sauti ndani yangu, ikisema, “Nataka
ufahamu kuwa nilikupa magoti hayo ili uwe mwanamke wa maombi, na si kwa ajili
ya kuzungukazunguka ukifanya mambo yasiyonipendeza Mimi. Magoti haya ulipewa
ili kufanya maombezi kwa ajili ya Kanisa. Ulitakiwa kulijua hilo.”
Kwa ujumla mimi nilikuwa si mwanamke wa maombi sana.
Maombi yangu yalikuwa na kawaida ya kuwa mafupi sana. Lakini Bwana alitaka niwe
mwombaji zaidi.
Malaika aliendelea kuosha miguu yangu, huku akiiparua, na
mimi nilikuwa namlilia Mungu anihurumie kutokana na maumivu yale. Bwana
akasema: “Miguu hii ulipewa ili uwe unazunguka kwenda kuhubiri Injili yangu,
kueneza Neno langu na si kuzungukazunguka kwa majirani zako kupeleka umbeya, na
kufanya mambo ambayo hayanipendezi Mimi. Na kwa sababu hii,” Bwana akasema, “ninasafisha
miguu yako.”
Jambo hili liliendelea na lilifanyika kwa maumivu makali
sana. Bwana akasema, “Hii ni muhimu sana ili uweze kuelewa mipango
niliyo nayo kwa ajili yako.”
Baadaye, nilipelekwa kwenye sehemu nyingine ambako
malaika wngine watatu walikuwa wananingojea. Sehemu hii ilikuwa tofauti.
Niliona vitu kama mashine. Malaika wale walianza mchakato mwingine wa kusafisha
macho yangu kwa kutumia aina fulani ya mafuta. Nilihisi kama vile macho
yameng’olewa kutoka kwenye matundu yake. Nikasema: “Tafadhali mnihurumie.
Naomba msaada. Kwa nini mnanifanyia hivi?” Ilikuwa kama vile wanakwangua
macho yangu. Kitu kama samaki kilitolewa kutoka kwenye macho yangu.
Bwana akasema, “Binti yangu, nafanya hivi kwa ajili yako kwa
sababu nataka ubadilike. Mambo uliyokuwa ukifanya duniani hayakuwa
yakinipendeza. Sikuwa nafurahi ukiwa duniani ulipokuwa ukitazama mambo ambayo
hayakunipendeza Mimi. Ulikuwa ukitazama TV” [Soap Operas]
... “Hayo hayajengi maisha yako.”
... “Sifurahii pale wanangu wanapoangalia vitu kama
hivyo; vitu ambavyo havinipi utukufu.”
Nikasema, “Bwana, nisamehe. Naomba rehema zako.” Na Bwana akasema, “Katikati ya usiku kwenye saa
sita, mara zote huwa uko macho ukiangalia sinema ambazo hazikujengi wewe; na
nyingi ya sinema hizo zimejazwa mambo mengi yanayohusu mapenzi. Sikukupa macho
hayo kwa ajili ya mambo kama hayo. Nilikupa hayo macho ili utazame mambo yale
tu yanayonipa Mimi utukufu. Na kwa sababu hii ndiyo maana ninasafisha macho
yako.”
Malaika waliendelea kusafisha macho yangu huku mimi
nikiendelea kuomba kuhurumiwa. Baadaye macho yangu yalipakwa mafuta, na kuanzia
hapo nikawa na mtazamo tofauti; macho yangu yalibadilishwa kabisa. Bwana
akasema, “Usitamani waume wa watu wengine tena!” Mimi
nilikuwa na kawaida ya kuvutiwa sana na wanaume wengine, na Bwana alisema kuwa
mambo hayo hayampendezi.
Nitakueleza mimi nilikuwa mtu wa namna gani. Nilikuwa
Mkristo duni wa kilokole ambaye alikuwa hatendi mambo sawasawa na Biblia
inavyoagiza. Kila nilichofanya kilikuwa ni kutokana na matamanio yangu na njia
zangu binafsi, kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu. Nakueleza haya ili uweze
kurekebisha njia zako; ili roho ziweze kuokolewa. Nakueleza kuwa tamaa NI
dhambi; kuangalia michezo ya kwenye TV [Soap Operas], sinema za kidunia – mambo
yote haya hayampendezi Mungu.
Malaika waliendelea na mchakato wa usafishaji. Walikuwa
na kijifimbo kidogo cha kioo ambacho walikiingiza moja kwa moja masikioni
mwangu. Walipoanza kukwangua masikio yangu, nilihisi maumivu makali sana. Moyo
wangu ulihisi maumivu haya yote. Mara maji meusi yalianza kutoka kwenye masikio
yangu, na baadaye maji ya rangi ya kijivu. Niliendelea kulia.
Bwana akasema, “Binti yangu, ninasafisha masikio yako kwa
sababu ulipenda sana kusikiliza mambo ambayo hayanipendezi Mimi. Ulipenda
kusikiliza umbeya. Uliyatoa kabisa masikio yako kusikiliza mambo
yasiyonipendeza Mimi. Baadhi ya watu wanakuja kwako kuleta umbeya na wewe
ulipenda kuwasikiliza hata kama walileta umbeya dhidi ya Mchungaji wako
mwenyewe. Ulipenda kuwasikiliza hao. Badala ya kumtetea Mchungaji wako na
kumsahihisha mbeya huyo ili arekebishe njia zake, ulikuwa kama wao, ukifanya
umbeya pamoja nao. Usisikilize umbeya tena. Mtu akija kwako na umbeya wa aina
yoyote, waombe radhi, kisha ondoka mara moja bila kushiriki. Usisikilize tena
mambo yasiyokujenga!”
Nikasema: “Bwana, nisamehe!” Nilijua kuwa nilikuwa
nina hatia. Hakuna jambo lililofichika mbele za Mungu. Hakuna anayeweza
kujificha mbele zake. Kila tunachofanya na kusema hapa duniani kimewekwa
kumbukumbu Mbinguni. Kutokana na maumivu yote yale masikioni mwangu, nikasema: “Bwana,
nisamehe. Naomba rehema zako.” Hatimaye
masikio yangu yalipakwa mafuta na malaika.
Bwana akaniambia: “Kuanzia leo na kuendelea, utasikiliza tu
mambo ambayo nimekuruhusu kusikiliza. Utafanya mambo yale tu ambayo nimekutaka
ufanye; hautakuwa Adelaida wa zamani tena. Hivi sasa wewe ni mtu mpya na ni
lazima uwe ni mwanamke yule ambaye ninataka uwe.”
Baada ya hapo nilipelekwa kwenye idara nyingine ambako
malaika walianza kusafisha kinywa changu. Ulimi wangu ulitolewa kabisa kinywani
na kuwekwa kwenye aina fulani ya sinia. Malaika alianza kusafisha ulimi wangu,
na hapa tena nilihisi maumivu makali sana. Bwana akasema: “Nataka
kukusafisha. Nataka kukusafisha.”
Malaika walivyokuwa wanakwangua ulimi wangu, maji meusi
yalikuwa yanatoka humo, na baadaye yalitoka maji meupe. Mwishowe malaika walitumia
maji matamu sana kuoshea ulimi wangu. Yalikuwa matamu mno. Hakuna kitu duniani
kinachoweza kulinganishwa na utamu wa maji yale. Kisha ulimi wangu ulipakwa
mafuta. Kinywa changu nacho kilipitia mchakato huohuo. Maji meusi yalitoka
kwenye kinywa changu.
Bwana akasema, “Binti yangu, ninafanya hivi kwa ajili yako
ili usifanye umbeya tena; ili uache kufanya mambo yasiyonipendeza; maana ulimi
wako ulishiriki katika mambo mengi sana ambayo hayanipi utukufu Mimi. Ulisema
uongo mwingi sana. Acha kusema uongo! Kusema uongo hakutoki kwangu. Waongo
hawanipendezi Mimi. Waongo wote hawataniona Mimi. Hakuna mwongo atakayeingia
kwenye Ufalme wa Mbinguni.”
Nikasema: “Bwana, nihurumie. Najua kuwa nilifanya
mambo hayo yote. Nilisema uongo mara nyingi, lakini tafadhali nisamehe.”
Nilisema yote haya kwa sababu ya maumivu niliyokuwa nayahisi.
Bwana akasema: “Ninafanya hivi kwa sababu ninakupenda.
Ukiendelea na hali uliyokuwa nayo, nitakupoteza. Kama nisingefanya yote haya,
usingebadilika kamwe. Ni lazima niokoe moyo wako na hii ndiyo sababu ya kufanya
yote haya. Nakupenda, na kwa sababu nakupenda, sitaki kukupoteza.”
Bwana akasema tena: “Kama ulivyo wewe, wengi
kati ya watu wangu wako namna hiyohiyo.Wanasema uongo, wanaishi maisha ya aina
mbilimbili, na wanaonekana wako safi mbele ya watu wengine. Unapomwinulia mumeo
sauti ulimi wako unakuwa unatumiwa pia.” Kinywa changu
kilitakaswa kabisa. Halafu Bwana akaniambia nimeze maji hayo. Nami nikafanya
hivyo.
Ulimi wangu na kinywa changu vilipakwa mafuta ya thamani
sana ya mbinguni. Mafuta hayo yalikuwa maalum sana, yakiwa na harufu ya thamani
sana. Hayawezi kulinganishwa na mafuta yoyote ya hapa duniani. Ulimi wangu
ulirudishwa tena kinywani mwangu. Malaika mmoja alikuja na kuweka hatamu kwenye
koo langu. Na Bwana akaniambia: “Hii ni sawa na vile farasi anavyowekewa
hatamu.”
Nikwambie tu kwamba, hii ndiyo njia pekee tunayoweza
kubadilishwa. Acha kuongea maneno machafu na kushiriki katika mambo ambayo
hayatujengi. Mambo haya hayampendezi Mungu kamwe.
Acha kutamka maneno machafu na yasiyo na maana. Wako
Wakristo wengi – akina kaka, dada, Wainjilisti, Wamisionari, n.k., ambao
wanapenda kusema maneno machafu na yasiyo na maana. Niko hapa kukuhakikishia
juu ya kile ambacho Bwana alinionyesha ili maisha yako yabadilishwe. Ushuhuda
huu ni kwa ajili ya wewe kubadilika. Upendo wa Mungu na wa kwangu kwako ndio
ulioleta ushuhuda huu.
Ulimi wangu ulirudishiwa tena mahali pake na malaika na
ukawa umebadilishwa kabisa. Naweza kukuambia sasa, hakuna mtu anayeweza
kunikasirisha tena. Sasa naweza kufanya yale tu yanayompendeza Mungu.
Kisha, pua yangu nayo ilipitia mchakato huohuo. Maji
meusi yalitoka puani mwangu wakati wa kusafishwa na baadaye maji meupe. Pua
yangu ilipakwa mafuta na nilihisi maumivu makali sana wakati wa mchakato wa
kusafishwa. Nilisema: “Bwana, tafadhali niambie mambo niliyofanya kwa
kutumia pua yangu ambayo hayakukupendeza.”
Bwana akaniambia: “Baadhi ya wateja wako huvuta sigara na wewe
unavuta ule moshi kupitia pua zako maana
uliwahi kuwa mvutaji sigara na sasa wewe unajisikia vizuri kukaa nao wakati
wanapovuta.” Nikasema: “Bwana, najua. Nisamehe. Naomba
unirehemu.”
Bwana akaniambia: “Uko sawa tu na wale wote wanaovuta sigara na
wote wanaokunywa pombe pale unapokaa nao na kuvuta harufu ya sigara na pombe.”
Bwana akasema tena: “Hii ndiyo sababu yangu
ya kukusafisha wewe. Kwa hiyo, kuanzia leo kila utakapomwona mtu anavuta sigara
au anakunywa pombe, hautajisikia vizuri kukaa nao tena. Utajisikia kinyaa.”
Hakuna cha kujitetea mbele za Bwana. Mungu anafahamu fika
wewe ni nani na mimi ni nani. Libarikiwe Jina Takatifu la Bwana, Amina.
Niliendelea kumwomba Bwana rehema na nilipelekwa sehemu
nyingine. Pale, malaika walianza kuosha mwili wangu uliobakia kwa kutumia
sabuni nyeupe. Maji ya kijivu yalitoka kwenye mwili wangu.
Nikasema: “Bwana, nisaidie. Tafadhali, nisaidie.” Malaika
walikuwa wanasugua mwili wangu na ngozi ya juu iliondoka. Damu ilikuwa
inachuruzika kutoka kwenye ngozi yangu na nikamwuliza Bwana: “Kwa nini
unanifanyia hivi?”
Bwana akaniambia: “Ninakusafisha. Ni lazima uwe safi mwili wako
wote, nafsi yako, na roho yako. Roho yako, nafsi na mwili ni lazima viwe safi,
asema Bwana.”
Sabuni ilisuuzwa kutoka kwenye ngozi yangu kwa kutumia
maji ya thamani sana. Kisha malaika walipaka mafuta kila sehemu ya mwili wangu;
kila sehemu ya mwili wangu. Sehemu zote za mwili wangu zilipakwa mafuta.
Bwana akaniambia: “Usirudi tena kwenye njia zako za zamani,
binti yangu. Hivi sasa wewe ni Mtakatifu wangu aliyepakwa mafuta.”
Nikasema: “Bwana, nisamehe kwa mambo yote niliyokuwa
nikifanya zamani hata mbele za uwepo wako. Nisamehe Bwana kwa kuwa kila kitu
ambacho Mchungaji wangu alijaribu kunisahihisha mimi nilikuwa nikipingana naye.
Nilisema mambo mengi kwake ambayo sikutakiwa kusema.”
Mchungaji wangu mara nyingi alikuwa akiniambia kuwa
mavazi yangu kama Mkristo hayakuwa sawa. Nilishindana naye sana. Aliwahi
kuniambia kuwa nilisema uongo na mimi nikahuzunika. Pale mtu anapopotoka na
Mchungaji wake akamsahihisha, mtu huyo huhuzunika. Siku zote mimi nilikuwa
kinyume na Mchungaji wangu.
Kisha nilipelekwa kwenye idara nyingine ambako
nilipokelewa na malaika watatu. Malaika wale walitumia nguo nyeupe kufuta maji
kwenye mwili wangu. Kwenye nyuso za malaika wale, niliona kuwa walikuwa
wanajisikia huruma sana kwa ajili yangu kutokana na yote niliyopitia lakini
hawakusema kitu chochote, hata neno moja. Sikuweza kumwona Bwana kwenye sehemu
hizi. Nilikuwa nasikia tu sauti yake.
Malaika wengine watatu walinipokea kwenye idara nyingine.
Malaika hawa walinivika nguo nyeupe ya juu na sketi ndefu. Sketi ilikuwa ndefu
sana kiasi kwamba miguu yangu ilikuwa haionekani.
HATUA YA 4: Niliwaona Watakatifu Wengine Mbinguni
Nilipelekwa kwenye sehemu nyingine na mlango
ulifunguliwa. Niliona mwanga mkubwa ukimulika kupitia mlango ule. Ulikuwa ni mwanga
wa kuvutia sana. Bwana aliniambia nipite ndani. Nikasema, “Bwana, naogopa.”
Nilijua kuwa Mungu alikuwa ananiandaa kwa sababu anataka
niokoke. Upendo haupendi mtu yeyote apotee. Nilisema: “Bwana, unirehemu.” Moyo
wangu ulikumbuka vizuri sana kila kitu nilichoacha nyuma kule duniani; wanangu.
Nikasema: “Bwana, naikabidhi familia yangu mikononi mwako.”
Kwenye sehemu ile niliweza kuona vitu kama miji mikubwa
na watu wengi sana ambao walikuwa wananingojea. Walikuwa wananipungia mikono.
Walikuwa wanataka niende kwenye sehemu ile walikokuwa.
Bwana akaniambia: “Mtakatifu wangu, muda umeshafika. Muda
umefika wa kuwaona wote walio hapa ambao wanakungojea.” Watu wengi sana
walikuwa wananingojea. Nami nilimwuliza Bwana: “Kitu gani kinaendelea hapa?”
Bwana akaniambia: “Ni wakati wa wewe kwenda na kuwahubiria watu
wote. Ni wakati wa wewe kwenda na kuhubiria mataifa yote. Ni wakati umefika.
Yote ambayo nimekuambia, nenda kawaambie Kanisa langu maana nitalifanya Kanisa
langu kuwa kamilifu. Nitaifanya nyumba yangu kuwa kamilifu. Kisha Neno langu
litapelekwa sehemu zote duniani zilizobakia, asema Bwana. Lakini kwanza ni
Kanisa langu.”
Hatua Ya 5: Safari Yangu Kuzimu na Yote Niliyoyaona Kule
Malaika walinitoa pale na
tukawa tunaelekea chini. Nikawauliza malaika wale: “Mnanipeleka wapi?” Niliingiwa
na hofu kubwa sana na ghafla ardhi ilifunguka.
Nikauliza tena: “Mnanipeleka wapi? Kitu gani
kinachoendelea kwangu?” Tuliingia moja kwa moja kwenye ardhi. Ilikuwa
inatisha sana. Kila upande kulikuwa na giza, nami sikuelewa malaika wale
walikuwa wananipeleka wapi.
Tulifika mahali ambako niliweza kuona mwanga mkali.
Kulikuwa na mlango chini ya ardhi. Mlango ule ulikuwa mbaya sana. Hakuna kitu
kwenye dunia hii kinachoweza kufananishwa na mlango ule.
Bwana akaniambia: “Huu
ni mlango wa kuzimu.”
Nilifikiri labda ndio nilikuwa
nimehukumiwa kutupwa kuzimu kwa yale yote niliyotenda zamani. Kulikuwa na mtu
akiningoja pale. Bwana wetu Yesu Kristo ni mzuri sana. Bwana wetu Yesu Kristo
alinyosha mkono wake kwangu. Alikuwa akiningoja kwenye mlango wa kuzimu huku
akiwa na ufunguo. Na niliweza kuona wanyama wengi wa kutisha wakitokea kuzimu.
Nikasema: “Bwana, ni kitu
gani kinachotokea kwangu? Tafadhali Bwana, nihurumie.”
Bwana akaniambia: “Nitakuonyesha
kuzimu na kila kitu kilichomo ndani yake, ili uweze kuogopa na pia, kupitia
wewe, watu wengine waweze kujua kuwa kuzimu kweli kupo.”
Nikasema: “Bwana, hapana.
Sitaki kwenda humo!”
Bwana akasema: “Binti
yangu, fuatana nami. Njoo.”
Tulipofika pale, baadhi ya
mapepo yalinyosha mikono yao kujaribu kunikamata. Nikasema, “Bwana, siwezi kuona, tafadhali.” Nilijaribu kufunika uso wangu kwa mikono
yangu, lakini bado nilikuwa naona kila kitu waziwazi. Ukiwa pale, unasikia kila
kitu, unaona kila kitu na unagusa kila kitu, kama ilivyo kwa roho zingine
zilizoko humo kuzimu. Bwana aliwazuia mapepo kunikamata. Nilikuwa niko na
Bwana. Niliweza kuona jinsi roho zilizoko kuzimu zinavyoteseka.
KUNDI LA KWANZA LA ROHO
NILILOONA KUZIMU: MASHOGA NA WASAGAJI
Bwana alinipeleka mahali fulani. Watu waliokuwa pale
walikuwa ni Wakristo. Walimtumikia Bwana walipokuwa duniani lakini wakati
huohuo walikuwa wakitenda mambo yasiyompendeza Mungu. Walikufa na sasa wako
kuzimu.
Bwana alinionyesha mchungaji
ambaye alikuwa akitumia vibaya Neno la Mungu. Mchungaji huyu alikuwa anafanya
mapenzi na wanaume wenzake. Hakuwa mwana wa Mungu kwa sababu wana wa Mungu
hawatendi mambo kama hayo. Hapohapo, niliweza kuona jinsi mapepo yalivyokuwa
yanamtesa mchungaji yule ambaye alilinajisi Neno la Mungu. Mapepo yalimwingiza
kwenye tyubu fulani, na tyubu hiyo ikaanza kumzungusha na kumzungusha! Alikuwa
anateseka kweli! Alipokuwa duniani, alikuwa akinajisi watoto wadogo. Alinajisi
hata wanaume wenzake.
Kama ambavyo unasoma ushuhuda huu, huenda haya ndiyo
unayofanya. Kuzimu ni halisi na pia kuna adhabu inayowangoja wote wasiotii Neno
la Mungu.
Mungu alikuumba wewe
mwanamume. Pia, alimuumba mwanamke. Niliona jinsi mwanamume huyo alivyokuwa
anateswa kuzimu. Roho yake ililipuka kisha ikajikusanya tena na kuendelea na
mateso yale.
Bwana alimwambia: “Mwanangu,
ulikuwa na muda wa kutosha duniani wa kutubu na kurekebisha njia zako.”
Bwana alimwonyesha skrini na
kwenye skrini hiyo yalionekana maisha yake alipokuwa duniani. Alionekana mzee
ambaye alikuwa akimwambia asifuate njia mbaya; akimwambia atii Neno la Mungu.
Kila neno ambalo Bwana alimwambia kwa njia mbalimbali alionyeshwa kwenye skrini
ile. Alikataa kutubu na kurekebisha njia zake.
Na siku moja, alipata ajali na akafa. Hivi sasa yuko
kuzimu. Alijifanya kuwa yeye ni mchungaji kumbe hakuwa mchungaji.
Bwana alimgeuzia mgongo na yule mtu akaanza kutukana.
Hakuna upendo kuzimu. Hakuna kitu kabisa zaidi ya uchungu, huzuni, na maumivu
ya kutisha ambayo hakuna mtu anayeweza kustahimili.
Wakati niko pale, nilijihisi
kama nataka kufa. Nilisema: “Bwana, nataka kufa.”
Bwana akaniambia: “Binti
yangu umeshakufa. Ona kile ambacho roho zinateseka kuzimu binti yangu.”
Nikasema: “Bwana, siwezi
kuvumilia zaidi. Roho yangu inaungua. Joto ni kali sana. Bwana, siwezi!”
KUNDI LA PILI LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: MAKAHABA
Bwana alinipeleka sehemu nyingine. Niliona jinsi mapepo
yanavyoitesa roho ya mwanamke mmoja kuzimu. Mwanamke huyu alikuwa ni kahaba
wakati akiwa duniani. Aliwahi kuokoka. Bwana alimtoa kwenye ukahaba. Lakini
alianguka tena na kurudia ukahaba ule na akawa katika hali mbaya kuliko mwanzo.
Alikufa kwa kuuawa na sasa yuko kuzimu.
Niliona jinsi mapepo
yalivyokuwa yanamtesa kuzimu. Badala ya kuolewa na kufanya mapenzi na mume
mmoja tu, aliamua kufanya kinyume. Mungu anachukia mambo hayo yote. Hayo ni
machukizo mbele za Mungu. Mwanamke yule alikuwa uchi. Alilazwa chini na mapepo
walikuwa wanamteza. Nikasema: “Bwana, mhurumie.”
Bwana akasema: “Hapanaaa binti yangu. Alikuwa na muda wa
kutosha duniani wa kutubu.” Bwana alimwonyesha skrini na
wakaonekana Wainjilisti mbalimbali walioenda kumweleza juu ya kuyatoa maisha
yake kwa Yesu. Lakini hakutii sauti ya Mungu. Hivi sasa yuko kuzimu.
Ujumbe huu ni kwa wanawake wote wanaojiuza miili yao.
Labda unafanya hivyo kwa ajili ya kupata fedha za kulisha wanao; labda huna
mume. Mungu anakuambia leo urudi kwake. Mungu atakuhudumia wewe na familia
yako. Kwa wanawake wote wanaouza miili yao, nawaambia kwamba, tubuni leo na
kumrudia Mungu kupitia ushuhuda huu. Mungu ameleta ushuhuda huu kwa ajili ya
wokovu wa roho zenu ili kwamba msije kuishia kwenye sehemu ile ya mateso.
KUNDI LA TATU LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: WAONGO NA WASENGENYAJI
Bwana alinipeleka kwenye sehemu nyingine waliko waongo na
wasengenyaji. Niliona jinsi walivyokuwa wanateseka kuzimu. Ni hali ngumu mno.
Ni vigumu mno kuongelea kuhusu kuzimu.
Usengenyaji unaweza kukufanya upoteze wokovu wako.
Kuwasengenya majirani zako kunaweza kukupotezea wokovu. Kumsengenya mchungaji
wako kuwaweza kukupotezea wokovu wako. Tubu leo kupitia ushuhuda huu na umrudie
Mungu, na Mungu naye atakurudia wewe, asema Bwana.
Niliuliza: “Bwana, yaani hii ni kwa sababu ya
usengenyaji tu?”
Bwana akasema: “Ndiyo,
ni kwa usengenyaji tu.”
Nikauliza: “Bwana, lakini
si huwa tunaomba rehema tunapokutenda dhambi?”
Bwana akasema: “Hapana.
Watu hawa hawakuomba rehema; na sasa wanalipia dhambi zao.”
Kwa sababu hiyo, tunatakiwa
kupatanishwa na Mungu kila siku kwa sababu hakuna ajuaye ni lini atakufa.
Usiondoke uweponi mwa Mungu. Usengenyaji unaweza kukufanya upoteze wokovu wako.
KUNDI LA NNE LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: WAABUDU SANAMU
Mateso mahali pale yalikuwa makali sana. Kwa wanawake
wote wanaomtumikia Maria Lionza, je, mnamjua ni nani huyo? Huyo ni pepo. Bwana
alinionyesha Maria Lionza ni nani. Ni pepo
ambaye wachawi wengi wanapiga magoti kumwabudu kule kuzimu. Mapepo yaliwatesa
kupita kiasi. [Maelezo ya blogger: Maria Lionza ni
mzimu unaoabudiwa hasa kule Venezuela. Unaweza kusoma zaidi kwa kubofya HAPA.]
Miali ya moto wa kuzimu huwa haizimiki. Inawaka usiku na
mchana. Inawaka milele. Tafadhali ningependa utambue hili: waabudu sanamu
hawawezi kuuona uso wa Bwana.
Mungu anataka kubadili maisha yako. Mungu anataka uache
kuabudu sanamu. Mungu anataka umwabudu Yeye tu. Kuna Mungu mmoja tu na zaidi
yake hapana mwingine.
Roho za watu walio pale
wanalazimishwa kumwabudu pepo huyo hata kama hawataki. Wanateswa sana.
Wanalazimishwa kuvuta sigara kuzimu pale wanapomwabudu huyo pepo.
Shetani ni mwongo. Amekuja kuua na kuharibu. Lakini ni
lazima nikuambie hili: Yesu Kristo alikuja kuleta uzima na uzima tele. Mungu
Mwenyezi anakuita leo kupitia ushuhuda huu. Natamani uweze kuelewa ujumbe huu
na mipango aliyo nayo Mungu kwa ajili yako. Mungu ni halisi.
Nilikuwa kuzimu kwa saa 16 ili kuelewa makusudi ya ujumbe
huu; ili niweze kuuhubiri; ili niweze kusambaza ujumbe wa wokovu kwa kila mmoja
kwa moyo wote.
Nilimwona Barbara. Nilimwona Shango. Ninyi mnaomwabudu
Barbara, mtupeni nje ya nyumba zenu. Bwana anasema huyo ni pepola ukahaba.
Barbara hana upendo. Amejaa
uharibifu. Ziko nyumba nyingi ambazo hazina amani. Yeye ndiye anayehusika na
hilo. Pia, unaweza kuwa unashangaa ni nini kinachoendelea kwenye maisha yako –
labda una sanamu yake kwenye nyumba yako. Natamani sana ungeelewa ujumbe huu na
mpango wa Mungu kwa ajili yako. Pepo huyu alikuwa anawalazimisha watu kuzimu
wamwabudu yeye. Watu pale wanateseka sana. Ni moto tu kila mahali.
Nilimwuliza Bwana: “Je, hukuwapa watu hawa nafasi ya
kurekebisha njia zao?”
Bwana akasema: “Niliwapa.
Nilituma watakatifu wangu kwao.”
Palepale kuzimu skrini
inawekwa mbele yao nao wanaonyeshwa kila kitu. Roho zilizo kuzimu hazina cha
kujitetea mbele za Bwana. Bwana anawaonyesha kila fursa waliyopewa walipokuwa
duniani.
Kama hutatubu na kurekebisha
njia zako leo, utaona jinsi kifo kitakavyokushangaza nawe utaishia kuzimu.
KUNDI LA NNE LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: WALEVI
Bwana alinipeleka kwenye sehemu nyingine. Ilikuwa ni kama
klabu kubwa. Nilisikia watu humo wakipiga kelele, huku wakiomba kuhurumiwa na
kusaidiwa. Nikauliza: “Ni nini kinachoendelea humu?”
Bwana akasema: “Peleka ujumbe huu kwa wote wanaotumia vileo usiku na mchana; kwa wote
wale wanaoingiza miilini mwao vitu ambavyo haviwajengi; kwa wote ambao
wanatumia hata fedha za watoto wao kwa ajili ya kulewea; peleka ujumbe huu kwa
wanawake wale wote wanaolewa – waambie warekebishe njia zao kupitia ujumbe
huu.”
Pale kuzimu niliona meza imewekwa mbele yao ili wanywe.
Walilazimishwa kunywa bila kupenda. Wote walikuwa katikati ya moto. Kile
walichokuwa wakinywa ni asidi nami niliona jinsi roho zao zinavyolipuka baada
ya kunywa.
Nikasema: “Bwana, hapana. Siwezi kuvumilia zaidi ya
hapa, tafadhali Bwana.”
Kuna mwanamume kuzimu ambaye, wakati angali duniani,
Bwana alimpelekea Mwinjilisti baa akiwa analewa. Mwinjilisti yule alimwambia
atoe maisha yake kwa Bwana wetu Yesu Kristo, maana Mwinjilisti yule alihisi
kuwa mtu yule asingechukua muda mrefu kabla ya kufa. Mtu yule alimtukana
Mwinjilisti huyo. Alimwita kuwa ni mwanamke mwenye wazimu, jambo ambalo watu
wengi duniani wanawaambia Wakristo duniani. Siku ileile, mtu yule alitoka baa
akiwa amelewa. Alipata ajali na sasa yuko kuzimu.
Alikuwa analazimishwa kunywa vinywaji vya kule kuzimu.
Alijaribu kukimbia mateso lakini mapepo hayakumwachia. Anateswa pale kuzimu
milele.
WAVUTA SIGARA
Wavuta sigara nao wana idara
yao kule kuzimu. Wale wote wanaovuta bangi na wao pia wana idara yao kuzimu.
Wanateswa milele.
KUABUDU AU KUHESHIMU SANAMU
Huenda unajiita Mkristo au
vinginevyo, lakini bado unaheshimu au kuabudu sanamu. Ni lazima utubu leo na
kuyatoa maisha yako kwa Yesu Kristo.
Kule kuzimu kuna wanaume na
wanawake. Unaweza ukawa tajiri sana hapa duniani kama ukitaka. Utaenda kuzimu
usipotaka kuyatoa maisha yako kwa Yesu Kristo. Fedha zako haziwezi kukununulia
wokovu. Wokovu wako ulishanunuliwa na Bwana wetu, Yesu Kristo. Amina.
Alikuwapo mwanamume mwingine ambaye naye alikuwa
analazimishwa kunywa kinywaji cha kuzimu. Nikamwuliza Bwana kwamba yule alikuwa
nani.
Bwana akasema: “Mtu huyu alikuwa ni Mtakatifu wangu.
Aliniacha na kuziendea njia zake na hatimaye alikufa katika dhambi.”
Kila kitu ambacho Bwana alikisema kuhusiana na mtu yule
kilikuwa kinaonyeshwa kwenye skrini – ujumbe, siku na saa ambayo Bwana
alimpelekea ujumbe. Mtu huyo yuko kuzimu sasa kutokana na uasi wake.
Unaweza kuwa unasema kwamba hii si kweli. Lakini niko
hapa kukueleza kwamba Bwana wetu Yesu Kristo ni halisi.
KUNDI LA SITA LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: WANAWAKE WA MUNGU [WAHUBIRI]
Hawa ni wanawake waliomtumikia Mungu wakati wakiwa
duniani. Lakini hawakutaka kubadilika na kukubaliana na mafundisho ya Mungu.
Badala yake wao walipendelea kumtumikia Mungu kwa namna zao wenyewe. Mateso
niliyoyaona hapa yalikuwa mabaya zaidi ya yale niliyoyaona kabla.
Nilisikia huzuni kubwa sana
kwa ajili ya hawa wanawake wa Mungu walio kuzimu, maana walimtumikia Mungu
wangali duniani.
Bwana aliniambia: “Kila wakati niliongea nao. Nilijaribu kuwarekebisha
kupitia baadhi ya Watakatifu wangu lakini hawakutaka kuelewa makusudi.”
Bwana alinionyesha mmojawapo wa wanawake hawa. Alikuwa
amekaa kwenye kiti na kiti kile kilikuwa kimezungukwa na moto. Ghafla pepo
lilitokea na kummiminia maji fulani kichwani.
Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa
analia; Bwana wetu alikuwa analia.
Nikauliza: “Bwana, kwa nini unalia?”
Bwana akaniambia: “Niliteseka sana kwa ajili ya roho zilizoko
kuzimu. Alikuwa ni Mtakatifu wangu. Nilimrekebisha ili asiipende dunia wala
mambo ya dunia.” Bwana alikuwa anamsahihisha aache kupaka
nywele zake rangi.
Bwana aliniambia: “Alikuwa anaonea aibu mvi nilizompa. Alikuwa
anajaribu kujionyesha kwa mwonekano ambao si wa kwake.”
Nywele zangu zilikuwa nyeusi na mimi nilitaka ziwe
nyeusi. Bwana akaniambia: “Usionee aibu kile ambacho nimekupatia.” Pepo
liliendelea kumtesa. Alimlilia Bwana amsaidie. Bwana alimwambia kwamba
alishachelewa. Akaanza kutukana.
Hatuwezi kuishi kwa kujificha uhalisia wetu. Siku moja
sote tutakuwa na mvi.
Kadiri mapepo yalivyoendelea
kummimina yale maji kichwani mwake, shingo yake ilipinda upande mmoja. Nywele
zake zilikuwa zinadondoka. Alinyosha mikono yake ili kujaribu kuomba
msaada.
Nikasema: “Siwezi kuvumilia zaidi.”
Nilijaribu kufunika uso wangu
maana hata mimi nilikuwa ninabadili rangi ya nywele zangu lakini sikuweza
kuufunika uso wangu.
Bwana akaniambia: “Usionee aibu kile ambacho nimekupa.”
Mwanamke yule alikuwa na nywele ndefu sana. Alikuwa ni
mwanamke mrembo lakini alitaka kuwa mrembo zaidi ya alivyokuwa. Lakini aliishia
kutenda kosa kubwa sana. Kama Mungu ametupa mvi, ni lazima tuzikubali maana
zinatoka kwa Mungu. Jambo hilo ni lazima litimie kwenye maisha yetu.
Nikasema: “Bwana, sikujua
kuwa kubadili rangi ya nywele ni dhambi.” Kisha nikasema: “Bwana,
msaidie. Mrehemu.”
Bwana alipeleka Mchungaji kwa mwanamke huyu wakati
alipokuwa duniani. Alikuwa ni Mwinjilisti. Mwanamke huyu alikuwa akihubiri na
kufundisha. Kama ilivyo kwa baadhi, pale wanapohubiri, wanajaribu kujionyesha
wao kwanza kwenye kusanyiko ili wakubalike kwa jinsi walivyo, ili waweze
kuhubiri na kufundisha kile wakitakacho.
Mwanamke huyu hakuwahi kutaka kuelewa makusudi ya Mungu.
Hatimaye alikufa na sasa yuko kuzimu. Huyu alikuwa ni mwanamke aliyemtumikia
Bwana.
Bwana akasema: “Binti yangu, naenda kukuonyesha wanawake
wanaotumia vipodozi kwenye nyuso zao.”
Nikasema: “Bwana, hata mimi
natumia vipodozi pia. Natumia poda kwenye uso wangu ili nionekane mrembo zaidi,
ili kuziba mabakabaka kwenye uso wangu.”
Bwana akasema: “Vitu hivyo havinipendezi
mimi. Nafurahishwa na mwonekano wa asili wa Watakatifu wangu. Mwanamke
anatakiwa anifurahishe mimi na mume wake. Kwa hiyo, hahitaji vipodozi ili
kuonekana mrembo kwa mtu mwingine yeyote.”
Wakati huo ndipo nilipomwona mwanamke ambaye alikuwa ameshikilia
kioo mikononi mwake na mapepo yalikuwa yanamlazimisha kupaka vitu fulani usoni
mwake. Alipaka majimaji fulani usoni kisha ngozi ya uso wake ikabanduka na
kuanguka.
Huenda unasoma ushuhuda huu na unasema kwamba vipodozi si
dhambi. Nikwambie sasa – Mungu anaposema jambo, sote ni lazima tutii! Mwanamke
yule alikosa kutii alipokuwa duniani. Alikuwa akitumia vipodozi hapa duniani na
sasa yuko kuzimu. Kule analazimishwa kupodoa uso wake usiku na mchana.
Bwana akasema: “Vitu
hivyo havinipendezi mimi. Unakumbuka niliposema kuwa yule atakayeupenda
ulimwengu ni adui wa Mungu?”
Ni lazima tutii mstari huo wa
kwenye Biblia: Msiipende duni, wala mambo yaliyoko katika dunia. Mtu akiipenda dunia,
kumpenda Baba hakumo ndani yake. (1 Yohana 2:15).
Sote tutahukumiwa kwa neno hili. Aina zote za vipodozi
unazotumia hapa duniani, utavitumia na kuzimu pia. Nilikuwa nikitumia
“wet-lips” ili kufanya midomo yangu ing’ae na kuwafanya watu wengine wanione.
Nikasema: “Bwana, unisamehe
maana nilikuwa na hatia ya jambo hili.”
Bwana akasema: “Ninafanya
hivi kwa sababu ya upendo nilionao kwa roho yako. Ili kuleta hofu ya uzito wake
ndani yako; ili uweze kuelewa uzito wa matokeo; ili kwamba uweze kuwaeleza na
wengine waache kutumia vipodozi.”
Mwanamke yule alikuwa katikati ya moto huku akiendelea
kulazimishwa kujipodoa uso wake. Matokeo yake uso wake na midomo yake vilikuwa
vinadondoka chini.
Enyi wanawake wa Mungu; wanawake wa Mungu msiwatazame
majirani zenu. Yatazamani maisha yenu binafsi leo na kumwomba Mungu. Sema: “Bwana,
ni mambo gani ninayotenda ambayo hayakupendezi?” Muulize
Bwana naye atakujibu. Mungu huwa anajibu.
KUNDI LA SABA LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: WANAWAKE WANAOVAA MAPAMBO YA VITO
Bwana aliniambia: “Sasa nitaenda kukuonyesha waliko wanawake
wanaovaa mapambo ya vito.”
Hapo nilimwona mwanamke ambaye alikuwa akilazimishwa na
mapepo kuvaa hereni kwenye masikio yake. Joka kubwa lilikuja kwake naye alivaa
hereni masikioni mwake. Kisha lile joka lilijiviringisha kwenye shingo yake.
Bwana yuko kinyume kabisa na wanawake wanaotumia mapambo
ya vito. Nikasema: “Bwana, lakini mbona hili ni pambo la kawaida tu?”
Bwana akasema: “Binti yangu, vitu hivyo havinipendezi Mimi.”
KUNDI LA NANE LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: FAMILIA NA WAPENDWA
Bwana alinipeleka mahali ambako nilimwona mwanamke
akilia; akipiga kelele sana kuzimu. Nilimwuliza Bwana: “Bwana, mwanamke huyu
ni nani?” na Bwana akasema: “Nitakuonyesha huyu ni nani.”
Alikuwa ni mwanamke niliyemfahamu miaka mingi iliyopita.
Tangu nilipoyatoa maisha yangu kwa Bwana, sikuwahi kuhubiri ujumbe wa wokovu
kwa mwanamke huyu.
Bwana aliniambia: “Yuko hapa kuzimu kwa sababu yako. Nilitaka
kuiokoa roho yake kupitia wewe lakini hukuwahi kwenda kumweleza habari zangu.”
Nikasema: “Bwana, naomba
unihurumie!”
Mwanamke yule aliomba rehema
kwa Bwana nami nikasema: “Bwana, mhurumie.”
Mwanamke huyu alikuwa mlevi
wakati alipokuwa angali duniani. Bwana alimwonyesha kupitia skrini fursa zote
alizokuwa nazo wakati angali duniani za kuyatoa maisha yake kwa Bwana lakini
alikataa. Siku ambayo nilisukumwa kuongea na mwanamke huyu, sikusema naye kwa
sababu aliniambia kuwa angeniua kama ningemweleza habari za Bwana. Niliogopa na
sikuweza kumhubiria. Hivi sasa yuko kuzimu akiteseka. Jina lake ni Augustina.
KUNDI LA TISA LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: WATUMIA DAWA ZA KULEVYA
Nilimwona mwanamume ambaye
alikuwa akilazimishwa na mapepo kutumia dawa za kulevya kuzimu. Alipewa kitu
kama sigara ikiwa imejaa miali ya moto ili aivute. Nikasema: “Bwana, mwanamume huyu ni nani?”
Bwana akaniambia: “Njoo umwone ni nani.”
Nilimkaribia na nikashangaa kuona kuwa kumbe ni kaka
yangu Esau yuko kuzimu! Nilijawa na huzuni sana kumwona kaka yangu akiteseka
kuzimu. Nikasema: “Bwana, mhurume kaka yangu.”
Kaka yangu alinyoosha mkono wake ukiwa umejaa miali ya
moto na kuanza kumwomba Bwana rehema. Bwana akamwambia kaka yangu: “Mwanangu,
unakumbuka kuwa uliyatoa maisha yako kwangu wakati ulipokuwa gerezani na
ukaniomba nikutoe gerezani; na ukaahidi kwamba ungenitumikia katika maisha yako
yote?”
Kaka yangu akasema: “Bwana
najua; nakumbuka. Lakini tafadhali nisamehe. Nipe tu fursa ya kutoka mahali
hapa.”
Bwana alimwonyesha skrini na
tukaweza kuona wakati akiwa gerezani miaka mingi iliyopita. Bwana alimwonyesha
siku hiyo pamoja na ahadi zote alizoahidi kumtumikia Bwana.
Bwana alimtoa gerezani kwa ili
aweze kumtumikia lakini alipotoka, alikataa kutimiza ahadi yake ya kumtumikia
Bwana. Na miaka miwili baadaye aliuawa mikononi mwa mama yangu. Kaka yangu
alikufa kifo kibaya kwa sababu ya kutokutii kwake.
Huyu ni kaka yangu ambaye
ninakuambia habari zake. Kaka yangu mwenyewe yuko kuzimu! Inatisha! Sikutaka
kulisema hili waziwazi lakini Bwana aliniambia kuwa ni lazima niliseme. Nililia
sana nilipomwona kaka yangu akiwa kuzimu.
Huwezi kupata picha jinsi Bwana
wetu anavyolia kwa ajili ya roho zilizoko kuzimu, Bwana aliniambia.
Bwana alinionyesha mwanamke aliyekuwa Mchungaji wakati
alipokuwa duniani. Alikuwa amekalia kiti kilichozungukwa na miali ya moto.
Alikuwa anavalishwa wigi (nywele za bandia) kuzimu na jingine tena juu
yake.
Bwana aliniambia: “Alikuwa
ni Mtakatifu wangu wakati fulani uliopita. Alikuwa ni Mchungaji wangu. Alikuwa
ni mwanamke mkubwa wa Mungu. Nilimtumia kwa kiwango cha juu sana, lakini aliasi
Neno langu.”
Nikasema, “Bwana,
mhurumie.”
Alinyoosha mkono wake kwa
Bwana kuomba msaada. Najua kuwa hadithi ya mwanamke huyu itasababisha maumivu
makubwa sana ya kihisia.
Alikuwa ni mwanamke
aliyemtumikia Bwana. Alibadili mafundisho ya Bwana. Alimwacha Bwana kwa ajili
ya vitu vya dunia. Alikuwa akifanya vitu ambavyo vilikuwa havimpendezi Bwana.
Alikuwa akisema maneno yasiyo na maana kila wakati. Bwana alimwonyesha kwenye
skrini mambo yote aliyofanya wakati akiwa duniani.
Bwana alimwuliza: “Binti
yangu, unaweza kukumbuka pale nilipokuletea Neno langu kupitia Mtakatifu wangu,
Elma?”
Dada yangu, Elma alizungumza na mwanamke huyu wakati
akiwa duniani lakini yeye alimtukana dada yangu. Alikataa kutii na Bwana
akasema: “Hiyo ilikuwa ni fursa yako ya kurekebisha njia zako na kunirudia mimi
lakini ulikataa na hii ndiyo adhabu yako. Je, unakumbuka jinsi ambavyo binti
yako alikukumbatia na kusema, Mama rudi lakini hukutaka kusikiliza?”
Bwana alimgeuzia mgongo na
mwanamke yule akaanza kutukana.
Bwana wetu Yesu Kristo
alimgeuzia mgongo na kuanza kulia sana.
Nikauliza: “Bwana, kwa nini
unalia?”
Bwana akasema: “Huwezi
kujua jinsi ninavyojisikia kuona roho zikiwa hapa.”
NILIONA KITI CHA ENZI CHA
SHETANI KUZIMU
Bwana aliniambia: “Naenda kukuonyesha kitu binti yangu. Sikuwa
nimemwonyesha mtu yeyote kitu hiki kabla. Nataka ukione ili uweze kuelewa kuwa
shetani ni mwongo. Shetani huiga mambo.”
Nikasema: “Bwana, tafadhali
naomba unitoe mahali hapa. Siwezi tena kuvumilia zaidi.”
Bwana akanionyesha kiti cha
enzi kuzimu. Niliona kiti cha enzi cha shetani kuzimu! Shetani anamwiga Mungu
Mwenyezi huko kuzimu. Nilimwona akiwa amekaa kwenye hicho kiti chake cha enzi.
Shetani ni mbaya sana. Naye anajifanya ana ngazi za madaraka.
Niliweza kuona malaika wamemzunguka lakini wote ni
mapepo. Alikuwa amevaa joho jeupe likiwa limejaa madoadoa na ni chafu sana.
Niliona wazee ishirini na wanne wakimwabudu shetani kuzimu. Walidondosha taji
zao na kumwabudu. Niliweza kuona kuwa wote walikuwa ni mapepo.
Kiti cha enzi cha shetani
kimejaa mambo yaliyoigwa kutoka Mbinguni. Kila kitu kilionekana kibaya sana.
Nikauliza: “Bwana, hii ni
nini?”
Wakati huohuo, shetani aliita
mojawapo ya mapepo yake na akalituma kwenda kumleta mtu fulani kutoka kuzimu.
Mapepo yanafanya kila kitu ambacho shetani anayaambia yafanye. Kila wakati huwa
anayatuma duniani ili kufanya uharibifu.
KITABU CHA KUZIMU
Bwana akasema: “Nataka ufahamu kuwa shetani huiga mambo ya
mbinguni. Nataka ufahamu kuwa shetani ni halisi. Shetani anataka kuuharibu
ulimwengu.”
Mahali pale niliweza kuliona
pepo katika umbo la malaika wa kishetani likiwa na makucha marefu sana na
limeshikilia kitabu mkononi mwake. Pepo hili lilikuwa linaandika kitabuni
majina ya watu ambao wataenda motoni.
Nikauliza: “Bwana, kwa nini
wanafanya hivi?”
Bwana akasema: “Nenda
ukaiambie dunia kwamba watu wasio na Yesu Kristo maishani mwao, shetani
ameshaandika majina yao kwenye kitabu cha kuzimu.”
Bwana akaniambia tena: “Angalia,
pepo hili limetumwa kwenye barabara ili kusababisha ajali. Kuna ajali nyingi
zinazotokea kwenye maeneo mbalimbali. Shetani na mapepo yake ndio wanaohusika
na mambo haya.”
Nikasema: “Bwana, hali hii
ni mbaya sana.”
Bwana akasema: “Ni
muhimu uone mambo haya yote ili uwe na uwezo wa kuielezea dunia jinsi kuzimu
kulivyo, ili dunia iweze kujua na kuamini kuwa kuzimu kweli kupo.”
NILITESWA NA BAADHI YA MAPEPO
KUZIMU
Kisha Bwana alikuwa
akinipeleka kwenye sehemu nyingine. Nikasema: “Niondoe mahali hapa. Hapa ni
kubaya sana, tafadhali.”
Bwana alinishikilia mkono
wakati tukiwa bado tunaenda. Ghafla lilitokea pepo la kutisha, kubwa lenye
makucha marefu.
Pepo lile lilikamata nywele
zangu na likaruka na mimi. Wakati huu sikuweza kumwona Bwana. Bwana alipotea na
kuniacha peke yangu. Pepo lile lilinikokota hadi kwenye sehemu nyingine, kisha
mapepo mengine yalikuja na kuanza kunitesa kwa namna mbalimbali.
Sauti ikawa inaongea kwenye ufahamu wangu ikisema: “Utabakia
hapa kuzimu milele na utateswa, na utahisi maumivu na majonzi yote ambayo yako
hapa kuzimu.”
Nikasema: “Bwana, siwezi
kustahimili haya. Siwezi kustahimili haya!”
Pepo jingine lilikuja kwangu likiwa na mdomo mrefu sana,
likapanda juu yangu. Nilijaribu kulisukuma lakini sikuweza. Liliingiza domo
lake kwa nguvu kinywani mwangu na
nilihisi mate yake kwenye kinywa changu chote. Nikapiga kelele: “Bwana, kwa
nini unaruhusu haya yote yanipate?”
Bwana akasema: “Ni
muhimu; ni muhimu kwa wewe kuwaambia watu duniani jinsi kuzimu kulivyo hasa ili
waweze kuelewa makusudi.”
Bwana akasema: “MIMI
NI MUNGU MTAKATIFU, wako watu kanisani ambao wanafanya kila aina ya mambo
machafu kwa vinywa vyao.”
Nikauliza: “Bwana,
nitawezaje kusema mambo haya yote?”
Bwana akaniambia: “Sema
kila kitu nilichokuonyesha.”
Bwana alinionyesha skrini na
nikaweza kuona uchafu mwingi. Wako watu wengi kanisani leo ambao wanatenda aina
mbalimbali za dhambi za siri.
Nikauliza: “Bwana, hii ni
nini?”
Bwana akasema: “Waambie
wabadilike. Waambie kuwa MIMI NI MUNGU MTAKATIFU. Waambie kuwa vinywa vyao ni
kwa ajili ya kunitukuza mimi na si kwa ajili ya uchafu.”
Nikasema: “Bwana, ondoa pepo hili mwilini mwangu” maana
lile pepo lilikuwa linanyonya mwili wangu wote. Mate yake yalikuwa meusi sana
na yamefunika mwili wangu wote. Hali ilikuwa inatisha. Harufu ya kuzimu ni
mbaya mno kuliko hata mbwa aliyeoza. Sina maneno ya kuweza kuielezea. Nikasema:
“Bwana, nisaidie. Siwezi kustahimili zaidi.”
Bwana akaniambia: “Binti
yangu, tulia. Ni muhimu sana kwa wewe kupitia mambo yote haya.”
Nikauliza: “Bwana, kwa nini uliniacha peke yangu?”
Mara pepo jingine lilikuja.
Likanichukua hadi kwenye sehemu nyingine. Kule niliona roho zingine zikicheza.
Nikauliza: “Bwana, nini kinachofuata cha mimi kufanya sasa?”
Niliwekwa ili nicheze katikati
ya moto. Kulikuwa na vitu humo ndani vikinilazimisha kucheza. Nikauliza: “Bwana,
kwa nini haya yananipata?”
Bwana akasema: “Kwa
sababu wewe ni mchezaji. Huwa unacheza unaposikia kila muziki wa Kikristo na
miziki mingine inayokupendeza wewe.”
Bwana akaniambia tena: “Mambo
hayo hayanipendezi mimi.”
Nikasema: “Bwana, nisamehe.
Sitarudia tena.”
Bwana akasema: “Kama
ulivyo wewe, wako watu wengi miongoni mwa watu wangu ambao hucheza kama watu wa
dunia. Wanachezesha viuno vyao kama watu wa kidunia. Mambo hayo hayanipendezi
mimi.”
Nikasema: “Bwana, nisamehe.
Naomba unihurumie,” kwa sababu roho yangu ilikuwa inaungua. Nilikuwa
katikati ya miali ya moto. Ninaweza kukuambia jinsi kuzimu kunavyotisha kwa
sababu roho yangu ilikuwa pale. Sisemi uongo hata kidogo. Nawaambia kweli tupu.
Kuzimu ni halisi! Nilikuwa pale!!
Mapepo yalinitoa mahali pale na kunipeleka sehemu nyingine
tena. Kulikuwa na minyoo mingi sana hapo. Minyoo ile iliingia sehemu mbalimbali
za mwili wangu – kupitia masikioni, machoni.
Nikasema: “Bwana, tafadhali
nihurumie. Nitafanya kila ulichoniambia nifanye, lakini tafadhali naomba unitoe
hapa.”
Bwana akasema: “Hii
ni muhimu sana ili kila mtu aweze kuelewa kuwa kuzimu ni mahali halisi. Watu
wengi husema kuwa kuzimu hakupo. Nenda ukawaambie kuwa kuzimu kupo.”
Palepale
nilikumbuka kitabu cha Luka 16:19-31 kinachoongelea juu ya tajiri na Lazaro.
Pale kaka yangu aliponyoosha mkono alisema: “Bwana, peleka ujumbe huu kwa
familia yangu ili wasije kuja huku kuzimu.”
Bwana aliniambia: “Kumbuka
hadithi ya Tajiri na Lazaro. Tajiri alipoomba kwamba Lazaro atumwe duniani
kuiambia familia ya tajiri kwamba kuzimu kweli kupo.”
Niliondolewa kwenye sehemu
ambako nilikuwa nateswa na minyoo. Bwana akaniambia: “Ni muhimu sana ukaseme
mambo yote uliyoona ili roho ziokolewe. Ninafanya yote haya kwa sababu ya
upendo nilio nao kwa wanadamu. Kama
nisingekuleta hapa, ningekupoteza.”
Bwana akasema tena: “Roho
nyingi zitaokolewa kutokana na ushuhuda huu.”
Nikasema: “Tafadhali Bwana.
Niondoe huku kuzimu. Siwezi kuendelea kuwa hapa!”
Nilipitia mateso mengi sana kuzimu huku moto ukiwa
umefunika mwili wangu wote.
Hatimaye, ghafla nuru kali ilitokea na Bwana akanitokea.
Nilimkimbilia Bwana na kumkumbatia. Nikauliza: “Bwana, kwa nini uliniacha
peke yangu? Kwa nini uliniacha peke yangu? Kwa nini???”
Bwana akasema: “Ndiyo binti yangu. Binti, ilikuwa ni muhimu
sana uone maumivu ambayo roho zinayapata hapa kuzimu ili uwe na uwezo wa
kuuelezea ulimwengu uliobakia.”
Kisha Bwana alinitoa pale.
Bwana alinionyesha vitu vingine ambavyo sitaweza kuvisema kwa sasa. Mungu
ataniambia ni lini niviseme vitu hivyo. Hivi sasa nitakueleza tu vitu vile
ambavyo Bwana aliniambia niviseme.
SAFARI YANGU YA PILI KWENDA
MBINGUNI – KILA KITU KIKO TAYARI MBINGUNI
Bwana akasema: “Nitakuonyesha mahali ambako niliwaambia
mitume wangu kwamba naenda kuwaandalia mahali, ili mimi niliko na wao watakuwa
hapo pia, ili ukamwambie kila mtu kwamba mambo haya ni halisi.”
Bwana alikuwa ananipeleka moja
kwa moja hadi mbinguni. Kisha niliona mlango mkubwa ukiwa wazi.
Nikasema: “Bwana, kuzimu ni
kubaya sana. Lakini mahali hapa [mbinguni] ni kuzuri.”
Bwana akaniambia: “Binti
yangu, nitakuonyesha Mbinguni.”
Na niliona sehemu kama jiji
kubwa mbinguni. Ndiyo, napaita mahali pale jiji kubwa kwa sababu hicho ndicho
hasa nilichoona. Bwana alinipeleka kwenye mtaa mmoja mbinguni. Mitaa ya
mbinguni ni ya dhahabu tupu. Ni dhahabu halisi kabisa! Niliona maua mazuri pembeni ya mitaa ya mbinguni. Ni maua mazuri
mno kiasi kwamba hakuna maua hapa duniani yanayoweza kulinganishwa nayo!
Bwana alinipeleka mahali
fulani na akaniambia: “Ninaenda kukuonyesha mto. Nitakuingiza humo.”
Kulikuwa na mawemawe kwenye mto huo. Mto wenyewe ni kama
kioo. Mawe ya kwenye mto ule yanang’aa. Kulikuwa na samaki kwenye mto huo pia.
Bwana alimtoa samaki mmoja kwenye mto ule na kumshika mkononi; na samaki yule
alikuwa na furaha, huku akichezacheza mikononi mwa Bwana.
Nikasema: “Bwana, mrudishe
samaki majini, atakufa.”
Bwana akasema: “Hakuna
anayekufa hapa. Mauti haipo hapa. Mahali hapa kumejaa uzima tu. Kila kitu hapa
ni uzima.”
Nikasema: “Bwana, kuna watu
wengi sana kule wanaoteswa. Kwa nini hukuwapatia fursa ya kurekebisha njia zao
ili waje hapa Mbinguni?”
Bwana akasema: “Wako
pale kutokana na uasi wao.”
Bwana alinichukua kama mtoto
mdogo kutoka kwenye mto hadi mahali pengine. Mto huo ni mzuri sana. Kila kitu
kinachotungoja Mbinguni ni kizuri sana!
Kisha niliomba jambo kwa
Bwana. Nilimwambia Bwana: “Ziko wapi roho ulizoziokoa? Wako wapi hapa
mbinguni?”
Bwana akasema: “Nitakuonyesha.”
Bwana alinipeleka mahali
ambako alinionyesha mmojawapo wa dada zangu katika Kristo ambaye alishakufa.
Jina lake ni Aurora Esperanza. Bwana alinionyesha dada mwingine. Alikuwa ni
binti wa mmoja wa dada zangu, dada Grace. Alionekana akiwa mdogo na mzuri sana.
Bwana akasema: “HAWA
NI WATAKATIFU WANGU.”
Ana amani sana Mbinguni.
Watakatifu walioko Mbinguni ni kama malaika. Niliwaona Watakatifu wachanga
Mbinguni. Mavazi yao ni tofauti. Mahali ambako Bwana alinionyesha pamejaa maua
mazuri. Ni mahali pazuri sana penye harufu nzuri sana. Nilikuwa Mbinguni!
Nilipaona Mbinguni! Nilipagusa Mbinguni!
Bwana aliniambia: “Sasa nitakuonyesha yaliko mavazi ya
Watakatifu wangu.”
Nikamwuliza Bwana: “Je,
utanionyesha vazi langu?”
Bwana akasema: “Nitakuonyesha
mavazi ya Watakatifu Wangu.”
Bwana alionyesha baadhi ya
mavazi, mavazi meupe ambayo yamepambwa kwa dhahabu. Mavazi hayo yana mikanda ya
dhahabu na yote yameandikwa majina juu yake. Bwana alinionyesha pia mavazi
mengine. Mavazi haya ni ya baadhi ya watu ambao bado wako duniani ambao bado
hawajampokea Bwana wetu Yesu Kristo.
Bwana akaniambia: “Haya
ndiyo mavazi ya Watakatifu Wangu na haya ndiyo mavazi ya watu wengine ambao
bado wako duniani, ambao bado hawajanipokea mimi.”
Nikasema: “Bwana, nataka
kuona mataji. Nataka unionyeshe taji ya Mchungaji wangu, na taji yangu
mwenyewe. Bwana, nataka kuona taji yangu.”
Bwana akasema: “Nitakuonyesha.”
Bwana alinionyesha mataji hayo, ni mazuri sana. Nitakueleza juu ya taji
ya Mchungaji wangu. Nilimwomba Bwana anionyeshe taji yake maana nilitaka
kumletea Mchungaji wangu habari njema.
Bwana alinionyesha taji yangu.
Taji yangu haikuwa na vito. Haikuwa kama taji zingine ambazo zilinivutia sana
kama ile ya Mchungaji wangu.
Nikamwuliza Bwana: “Kwa
nini taji yangu haina vito?”
Bwana akasema: “Huwezi
kuelewa mambo aliyopitia hadi kufikia kuwa na taji yenye vito vingi kama hii.”
Malaika alichaguliwa kuweka
mataji na pia vito kwenye mataji. Watu wanapotubu na kuja kwa Yesu Kristo, unapoleta
roho kwenye Ufalme wa Mbinguni, malaika
ataweka kito kwenye taji yako. Unapowasaidia wenye shida, malaika
ataongeza kito kingine kwenye taji yako.
Unapowasaidia maskini na wasio na mahali pa kuishi, malaika
ataongeza vito zaidi kwenye taji yako.
Bwana alikuwa anaongea nami
kuhusu Mchungaji wangu. Alisema kuwa ameshateseka sana kwa ajili ya Ufalme wa
Mungu; na kwamba alipitia magumu mengi hadi kupata taji kama hiyo. Ana moyo
sana wa kuleta roho za watu kwa Kristo.
Bwana akasema: “Mwambie
ashikilie kwa nguvu kile alicho nacho ili mtu mwingine asije akachukua taji
yake.”
Nilimweleza Mchungaji wangu
yale yote ambayo Bwana aliniambia.
Halafu Bwana alinionyesha
mataji ya Watakatifu Wake wote.
Alinionyesha mataji ya watu ambao hawajayatoa maisha yao
kwake lakini bado wako duniani.
NILIONA KITI CHA ENZI CHA MUNGU
MBINGUNI
Bwana alisema: “Binti
yangu, nitakuonyesha kitu.”
Kutokea mbali, niliona kiti
cha enzi kikubwa sana; cha thamani sana.
Bwana akasema: “Hiki
ni kiti cha enzi cha Baba yangu.”
Bwana alikuwa amekaa pale.
Nuru kali ya kiti cha enzi ilinifanya nisiweze kuona mengi. Niliona baadhi ya
wazee wakitupa taji zao chini na kuinama ili kumwabudu Bwana. Hawaachi
kumwabudu Bwana Mbinguni.
Niliona malaika wengi sana
wakiwa wamesimama kuzunguka kiti cha enzi cha Mungu. Kitabu cha Ufunuo
kinaongelea kuhusu sehemu hii. Mbingu ni halisi. Niliona mbingu kwa sababu
nilifika pale.
Bwana akasema: “Binti,
kaiambie dunia kwamba mbingu ni halisi. Zungumza binti yangu.”
Nikauliza: “Bwana, unadhani
wataniamini?”
Bwana akasema: “NDIYO.”
Nilikuwa nazungumza na Bwana
kama ambavyo naweza kuzungumza na kaka yangu au na Mchungaji wangu.
Niliona malaika wengi sana Mbinguni; na kila walipomwona
Bwana, walivua mataji yao na kuinama na kumwabudu Bwana. Nilijawa na furaha
sana kuona mambo haya.
Bwana akasema: “Binti
yangu, UTUKUFU WOTE NI MALI YANGU. UTUKUFU WOTE NI WANGU.”
Hapa nilielewa kwamba Mungu
hashirikiani utukufu wake na yeyote. Malaika walikuwa wakiimba, wakimwabudu
Bwana muda wote. Hawaachi hata kidogo kumwabudu Bwana. Niliona jinsi kanisa
lenye wachungaji wazuri linavyomwabudu Bwana. Dada yangu, Yasmine, alikuwa akiwaongoza.
Bwana akasema: “Waambie
kwaya ya kanisa la wachungaji wazuri waniabudu Mimi na waache kufanya mambo
yasiyonipendeza. Waambie kuwa kila wanaponiabudu, malaika Mbinguni huabudu
pamoja nao.”
Ujumbe huu ni kwa wote
wanaoabudu. Bwana anataka mmwabudu zaidi.
“Waambie
waniabudu Mimi,” Bwana alisema.
Malaika walikuwa wakipiga
vyombo mbalimbali katika kumwabudu Bwana.
MUNGU WETU NI BABA MTAKATIFU,
AMINA
Malaika ni wazuri sana. Wanapomwabudu Bwana. Niliona
amani kubwa sana kati yao. Waliabudu kutoka moyoni.
Bwana alinipeleka sehemu
nyingine. Niliwaona malaika saba wameshikilia tarumbeta saba. Na karibu yao,
kulikuwa na malaika wengine saba wameshikilia vikombe mikononi mwao. Walikuwa
ni malaika wakubwa na warefu sana. Walivaa mavazi meupe sana; weupe ambao hata
hauelezeki!
Nikauliza: “Bwana, malaika
hawa ni akina nani?”
Bwana akasema: “Malaika
hawa wanasubiri kutumwa duniani ili kuiharibu dunia.”
Malaika wale tayari wana
tarumbeta mikononi mwao. Wanasubiri tu Bwana awaambie waanze kuzipiga.
Nikauliza: “Bwana, mbona ni
warefu hivyo?”
Bwana akasema: “Kwa
kuwa wao ni wana wa Mfalme.”
Nilikuwa nimekusudia kuuliza
maswali zaidi. Lakini Bwana akaniambia: “Usiwe mdadisi sana. Usiulizeulize maswali
mengi mno. Wewe onyesha tu yale ambayo nimekuonyesha; mambo ambayo nimekwambia
useme. Waambie kuwa kuna Mbingu moja tu na wala hakuna nyingine. Waambie kuwa
Mimi ni halisi, maana watu wengi hawazungumzi kuhusiana na Mimi. Waambie kuwa
Mungu yuko pale juu akiwangoja.”
Kisha Bwana akasema: “Sasa
nitakuonyesha kile kinachoendelea miongoni mwa watu wangu.”
Bwana alinionyesha sehemu
moja. Sehemu ile ilikuwa na pazia. Halafu akasema: “Ona kile kinachoendelea
kwenye Kanisa langu. Ndani ya Kanisa langu yapo mambo mengi ambayo
hayanipendezi. Nitaleta kwa Baba yangu taifa Takatifu tu. Kanisa langu haliko
tayari. Nenda kawaambie wajiweke tayari kwa sababu tarumbeta karibu italia.”
NILIONA MEZA YA BWANA
IMESHAANDALIWA TAYARI
Bwana akasema: “Sasa nitakuonyesha mahali ambako Watakatifu wangu
watakula pamoja na Mimi.”
Akanionyesha meza kubwa sana,
imepambwa vizuri kwa vitambaa vyeupe, vikombe vya dhahabu, huku kukiwa na viti
kila mahali, na viti vyote vina majina ya Watakatifu yameandikwa juu yake.
Sikuweza kuelewa majina yale. Nilimwomba Bwana anionyeshe kiti changu.
Bwana alinionyesha kiti changu
na kusema: “Liambie Kanisa langu lijiandae. Waambie watu wangu kwamba meza
imeshaandaliwa.”
Nikasema: “Bwana, hapa ni
pazuri sana.” Nilitaka kukaa
kwenye kiti kimojawapo.
Bwana akasema: “Usikae
kwenye kiti. Bado muda haujafika.”
Kisha niliona malaika wakienda
na kurudi, na mmoja wao alikuja na kuzungumza na Bwana moja kwa moja masikioni
mwake.
Nikamwuliza Bwana: “Amesema
nini?”
Bwana akasema: “Usiwe
mdadisi sana.”
Kisha malaika alikuja tena na
kuzungumza masikioni mwa Bwana. Bwana akasema: “Binti yangu, muda
umeshafika wa wewe kurudi. Kaliambie Kanisa langu wajiandae. Kawaambie kila
kitu nilichokuonyesha.”
Nikasema: “Bwana,
hapanaaaa! Sitaki kurudi.”
Bwana akasema: “Ndiyo,
ni lazima urudi ukawaambie kila kitu ulichoona. Waambie kuwa meza iko tayari,
inawangoja. Ni lazima mjiweke tayari.”
Wakati tukiwa tunaondoka, Bwana akasema: “Kanisa
langu liko namna hii: baadhi ya watu ni wa nia mbilimbili, baadhi ni wanafiki,
wengine hawako tayari, wengine hawanipendi Mimi kwa moyo wote, baadhi wanafanya
mambo kwenye nyumba yangu kwa sababu wanalazimika tu kufanya, wengine wanataka
waonwe na kusifiwa na wachungaji wao.”
Bwana alianza kulia!
WATOTO WASIO WATII, WANAOPOKEA
SIMU WAKIWA KANISANI
Bwana alinionyesha Kanisa. Nilimwona mhubiri akihubiri
madhabahuni na ghafla simu yake iliita. Mhubiri huyu aliacha kuhubiri. Alitoka
nje ili kwenda kusikiliza simu yake.
Bwana akasema: “Unaona jinsi wanavyopuuza uwepo wangu; ona
jinsi wanavyopuuza uwepo wangu. Mtu anapohubiri, anakuwa anahubiri Neno langu.
Wanaona bora kwenda kusikiliza simu kuliko kushughulika na Mimi.”
Kisha Bwana akaniambia: “Sema,
sema na Wachungaji waachane na mafundisho yao. Wanaweza kukuchukia kama
wakitaka, lakini watu wengi wataelewa makusudi ya Mimi kukuleta hapa na wengi
watatubu.”
Ujumbe kwenu wachungaji. Watu wanaweza kuwachukia pale
mnapoamua kuyafanya mapenzi ya Mungu. Haijalishi kama watawachukia. Sahauni
mafundisho yenu wenyewe. Fuateni kile ambacho Mungu amewapa. Msijaribu kumfurahisha
kila mtu. Msikubali kuridhia mambo asiyopenda Mungu.
Bwana akasema: “Nitaenda kuliunganisha Kanisa langu pamoja.
Mimi nina Kanisa moja tu. Sina Kanisa jingine duniani zaidi ya Kanisa moja tu.
Hili ndilo Kanisa nitakalolipeleka mbinguni. Hili ndilo Kanisa
nitakalolikabidhi kwa Baba yangu.”
Sisi tulio wa Huduma ya Kiinjilisti ndio Kanisa la Mungu.
Wale ambao wameyatoa maisha yao yote kwa Yesu Kristo. Wale ambao hawatendi
dhambi tena. Wale ambao wameziacha njia zao za zamani ili kuyafanya mapenzi ya Mungu.
Wale waliozaliwa upya. Hawa ndio watu watakaouona uso wa Mungu.
HITIMISHO
Ushuhuda wangu unakaribia mwishoni. Nimewaeleza kila kitu
ambacho Bwana aliniambia niseme, kwa utukufu wa Mungu. Utukufu wote, utukufu
wote ni wa Mungu.
Niko hapa kwa rehema za Mungu. Ni kwa rehema za Mungu tu
ninawaambia mambo haya ambayo Bwana alinitaka niyaseme. Ujumbe huu utakwenda
moyoni mwako na kubadili maisha yako ili kwamba uweze kutubu.
Mwulize Bwana: “Bwana, ni
eneo gani la maisha yangu ambako ninashindwa?” Bwana atakujibu.
Napenda kukuambia kwamba Yesu Kristo anakupenda wewe;
Yesu Kristo anakupenda wewe! Anataka kuyabadili maisha yako. Yesu Kristo hataki
uende jehanamu bali anataka uende Mbinguni. Mbingu ni halisi, na kuzimu nako ni
halisi pia. Tubu sasa na uyatoe maisha yako kwa Yesu Kristo. Wokovu unapatikana
kwa Yesu Kristo tu!
Yesu Kristo anagonga kwenye mlango wa moyo wako kupitia
ujumbe huu. Mtafute Bwana kwa moyo wako wote, naye atafanya mambo makubwa
kupitia wewe.
Bwana akasema: “Mambo yote haya niliyokuonyesha
yalishatabiriwa kwenye Kitabu cha Ezekieli, Kitabu cha Danieli na Kitabu cha
Ufunuo. Mafunuo yote haya yamo kwenye Biblia.”
Ninaomba kwamba ushuhuda huu ukabadilishe maisha yako kwa
ajili ya utukufu wa Mungu. AMINA.
MUNGU awabariki nyote.
**********
Ushuhuda huu nimeutafsiri
kutoka kwenye toleo lake la Kiingereza ambalo linaweza kupatikana kwa kubofya
kwenye kiungo kifuatacho: http://www.divinerevelations.info/Adelaida/index.htm
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni