Nitashindaje Dhambi Inayonisumbua?
Baba yangu mmoja wa kiroho
alipenda kusema, “Jiachie tu kwa Mungu naye atafanya.”
Neno hilo lilinisumbua kwa
muda mrefu sana kujua maana yake. Nilikuwa najiuliza, “Jiachie maana yake nini?
Mbona mimi najaribu kuishi maisha matakatifu lakini nashindwa? Ina maana mimi
sijaokoka?”
Kila tunaposikia au kusoma
Neno la Mungu, hapo ndipo tunapojiona jinsi ambavyo tumepunguka; tuko chini ya
viwango vya utakatifu wa Mungu!
Lakini wakati huohuo Biblia
inasema: Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu
wote, na huo utakatifu, ambao hakuna mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao.
(Waebrania 12:14).
Yaani nisipokuwa mtakatifu
siwezi kabisa kumwona Mungu? Utakatifu ni nini? Je, ni kuishi maisha ambayo
hayana dhambi nyingi na kubwakubwa? Hapana! Utakatifu ni kutokuwa na dhambi
kabisa – iwe kubwa au iwe ndogo.
Mungu ni mkamilifu na anasema
wazi kwamba mbinguni hakitaingia chochote kilicho kinyonge. (Ufunuo 21:27).
Sasa je, tunaweza kweli kuishi
humu duniani bila dhambi?
Sheria ya Mungu ina maagizo
mengi. Mungu anasema: Ombeni bila kukoma; mpende adui yako na umwombee;
usitamani vitu vya wengine; usiseme uongo; usiwaze mabaya; usichukie wengine;
ishi kwa imani, chochote kisichotokana na imani ni dhambi, n.k., n.k. Je, ni
kweli yupo mtu anayeweza kusema, “Mimi sina dhambi?”
Labda mara kwa mara umekuwa
ukijaribu kusimama lakini kila baada ya muda mfupi unaanguka tena. Matokeo yake
unaingiwa na hatia moyoni na hata hofu ya kuachwa siku ya mwisho au endapo
utakufa. Wengine pia wamekata tamaa kabisa na kusema tu, “Haiwezekani kuishi
maisha ya wokovu!” Wameamua kurudi nyuma kwenye dhambi kama zamani.
Lakini ni nini hasa ambacho
Mungu anategemea kutoka kwetu? Bwana anasema, Je,
Mkushi aweza kuibadili ngozi yake, au chui madoa-doa yake? Kama aweza ndipo na
ninyi mwaweza kutenda mema, ninyi mliozoea kutenda mabaya. (Yeremia
13:23).
Ngozi nyeusi ya Mkushi na
madoa ya chui ni asili yao. Dhambi ni asili yetu. Biblia inasema wazi, Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; mama yangu
alinichukua mimba hatiani. (Zaburi 51:5).
Ukianza kujitahiditahidi,
kujizuia, na kujilazimisha kuishi sawasawa na sheria ya Mungu, utapoteza muda
wako na utaishia kwenye kukata tamaa. Tukifanya hivyo, Mungu anasema kuwa hapo
ni kutaka kuithibitisha haki yetu wenyewe (Rum. 10:3). Yaani ni kama tunataka
kuja kusema, “Ah, nimepigana hadi nikashinda!” Isaya naye anasema, Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na
matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi. (Isaya
64:6).
Juhudi zetu zote ni kupoteza tu
muda kwa jambo ambalo halina faida bali hasara tupu. Bwana Yesu anasema, ... pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote.
(Yohana 15:5).
Ukianza kujitahidi kwa nguvu
zako mwenyewe, hicho ni kiburi. Huko ni kukataa kushuka chini ili usaidiwe.
Ukiona kwamba kuna dhambi
fulani inakusumbua maishani mwako, acha kujitahidi kuiacha. Ndiyo maana ni
muhimu sana kuishi kwa kufanya toba mbele za Mungu kila tunapokosa.
Kwa hiyo, acha kujitahidi
kumpendeza Mungu kwa juhudi zako, badala yake fanya mambo yafuatayo:
- Kiri kwamba kuna dhambi maishani mwako.
- Kusudia kuacha kutenda dhambi hiyo tena.
- Tubu dhambi hiyo mbele za Bwana.
- Piga magoti mbele za Bwana umwambie Roho Mtakatifu, “Siwezi peke yangu Bwana. Nisaidie kushinda dhambi hii.” Hakuna dhambi isiyosalimu amri chini ya neema ya Bwana – iwe ni ulevi, uasherati, dawa za kulevya, uchawi, n.k.
- Endelea kuomba rehema na neema za Bwana ili azidi kukutia nguvu hatimaye utatoka nje kabisa ya shimo hilo.
Huu ni unyenyekevu mbele za
Bwana. Maandiko yanasema, Basi nyenyekeeni chini ya
mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye
fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu.
(1Petro 5:6-7).
Utakatifu katika dunia hii
unawezekana, si kwa sababu ya juhudi zetu, bali kwa sababu iko damu ya Yesu
inayotusafisha na udhalimu wote (1Yoh.1:9) na yupo Roho Mtakatifu anayetupa
kushinda na zaidi ya kushinda!
Reactions:
|
|
10 comments:
AnonymousApril
28, 2012 at 10:45 AM
mtumishi mungu akubariki
usikate tamaa.songa mbele kufundisha neno la bwana katika mtandao
Amen ndugu yangu. Mungu
akubariki kwa kunitia moyo. Songa mbele pia kujitakasa kila kukicha.
NOEL SAWEJune
12, 2012 at 3:52 PM
KAZI UNAYOIFANYA MALIPO YAKE
NI MUNGU PEKEE ATAKAYEKULIPA. HONGERA NA MUNGU AENDELEE KUKUTIA NGUVU
asante
sana Noel.
Mungu akubariki na kuendelea kukupa nguvu katika safari yetu ya kiroho.
kuna kitu furani nahisi kuwa
kinapatikana katika huduma yako! na kitu hicho kinanifanya nisichoke kutembelea
blog yako! kwa ufupi unanitiamoyo sana
katika safari ndefu hii tuliyonayo.....ambayo kadri tunavyomkaribia inakuwa ni
fupi kuliko tulivyodhani!
Nakushukuru vilevile emback
kwa maoni ya kutia moyo. namshukuru pia Roho Mtakatifu kwa kutumia mafundisho
haya kusema nawe. Ubarikiwe na Bwana tunapokuwa tunamalizia safari hii tuliyo
nayo.
Franco SangaAugust
1, 2012 at 3:06 PM
Mtushi James MUngu pekee yake
Akubariki hadi ushangaee kwani umenigusa sanaa na umenitiaa moyo katika wakovu,pia
umeniapa kitu sasa nina kitu moyoni......naamu MUngu anasema imani huja kwa
kusikia au kusoma nami nimesoma neno la MUngu JAMES, almight God bless you.
naomba roho mtakatifu azidi kunena nawe zaidi,...
PIA NAKUOMBA
UTUFUNDISHE VIJA TULIO WENGI MAHUSIANO SAHIHI YA KIMUNGU KATIKA MAANDALIZI YA UCHUMBA NA KUOA.
Ubarikiwe sanaa.
naomba roho mtakatifu azidi kunena nawe zaidi,...
PIA NAKUOMBA
UTUFUNDISHE VIJA TULIO WENGI MAHUSIANO SAHIHI YA KIMUNGU KATIKA MAANDALIZI YA UCHUMBA NA KUOA.
Ubarikiwe sanaa.
Franco asante kwa maoni na kwa kunitia
moyo. Ashukuriwe Mungu wetu kwa kusema nawe kupitia masomo haya. Kuhusu masuala
ya uchumba kama ulivyosema, nitafanya hivyo.
unarikiwe.
Barikiwa James, nilikuwa
naomba ufundishe kuhusu kusikia sauti ya Mungu, jamani hili swala linanitatiza sana wapendwa, hasa jinsi ya kupambanua hii ni sauti ya
Mungu, shetani au mawazo binafsi hasa wakati mtu unaomba
Ningeshukuru sana kama una mafundisho kama hayo unitumie hata kwa email nahitaji sana kujua
Barikiwa sana mtumishi hata kuliko Abraham
Ningeshukuru sana kama una mafundisho kama hayo unitumie hata kwa email nahitaji sana kujua
Barikiwa sana mtumishi hata kuliko Abraham
Star, nitaangalia kuhusu hilo suala la kusikia
sauti ya Mungu, kisha nitajibu.
888 Casino | JtmHub
JibuFuta788 Casino. This 안성 출장안마 casino is offering 광명 출장샵 sports betting, bingo and poker as well 계룡 출장마사지 as 경주 출장안마 other casino games including blackjack, roulette and other 동해 출장안마 table games.