MIAKA KUMI NA TANO YA MATESO NA MAGONJWA YAKOMA BAADA YA MAOMBI
Mama Anna (kushoto) akiwa na Anna mwanaye ambaye alimleta mkutanoni |
Mama
Anna ambaye ameletwa na mtoto wake kutoka Babati ili apate kuombewa na
kupona tatizo ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda wa miaka 15; mtoto
wake anasimulia kuwa mama yao huyo aliumwa sana kwa kipindi cha miaka
kumi na mitano na hospitali zote wameshindwa kumtibu, ikefikia kipindi
inambidi awekewe mtungi wa oxygen kwa ajili ya kupumua.
Lakini
siku ya jumapili wakasikia kuwa kuna mkutano mkubwa wa injili
unafanyika jijini arusha ukiongozwa na mpakwa mafuta wa Bwana Yesu
Kristo, Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima pamoja na watendakazi wake,
na wakawa pia, wamesikia kupitia watu mbalimbali, matendo makuu ambayo
Mungu anayatenda kupitia mkono wa Mchungaji huyu.
Ndipo
wakafunga safari yakuja na kumkuta Ministry Pastor aitwaye Peter na
akamuombewa na kukemea magonjwa yote amabayo yalimsibu mama huyo na huyo
akohoa kwa sauti kubwa sana kwa mara saba na baada ya hapo akawa na
uwezo wakutabasamu na ndipo kila mtu pamoja na watoto wake walio mleta
walipomsifu Mungu kwa matendo makuu aliyowatendea.
MUNGU KWETU SISI NI MUNGU WA KUOKOA NA NJIA ZA KUTOKA MAUTINI ZINA YEYE!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni