WATU ZAIDI YA ISHIRINI WARUDISHWA KUTOKA MSUKULENI MKUTANONI ARUSHA
Mchungaji Josephat Gwajima akimwomba MUNGU |
Watu waliorudishwa walianza kuhojiwa mmoja baada ya mwingine.. |
WATU
WALIORUDISHWA MKUTANONI ARUSHA LEO HII HIZI NI BAADHI YA SHUHUDA
Ni siku nyingine
kubwa ambayo Mchungaji Josephat Gwajima ameendelea kutumiwa na Mungu katika
Mkutano Mkubwa wa Injili mkoani Arusha. Ikiwa ni siku ya sita leo hii kumetokea
mambo ya Ajabu kupita akili za watu kwani watu zaidi ya ishirini ambao walikuwa
wamechukuliwa msukule na kupelekwa mikoa mbali mbali kurudishwa.
Akiongozwa na Roho
Mtakatifu kuomba kwa kuita watu waliokuwa wamechukuliwa; Mchungaji Gwajima
aliomba maombi ya nguvu na kuamuru wote waliochukuliwa warudi. Zifuatazo ni
shuhuda mbalimbali za siku ya leo na mambo ambayo Mungu ametenda siku ya leo.
Wa kwanza kutoa
ushuhuda alisema kuwa yeye anaitwa Neema, alikua amechukuliwa na kupelekwa zanzibar
ametoka huko kwa kuruka na alichukuliwa na mke wa shemeji yake,
Mwingine ambaye
jina lake halikupatikana kwa haraka alidai kuwa yeye alichukuliwa na kupelekwa
Unga Limited.
Mtu wa tatu kutoa
ushuhuda; yeye alisema kuwa alikuwa amechukuliwa na bibi yake na kwa jina
anaitwa Mary. Kazi yake huko alikuwa analima viazi na walikuwa wanakunywa damu
za watu.
Ushuhuda mwingine
uliovuta hisia za wengi ni wa binti wa kiislam aliyeitwa Mwajuma; yeye alisema
kuwa alikuwa tabora, ghafla akiwa huko akasikia sauti ikimwita NJOOO akajiona
anapaa hadi uwanjani, Arusha. Wakati anasikia sauti hiyo alikuwa katika kazi za
kawaida huko za kulima na kazi nyingine aliyokuwa anafanya msukuleni ni
kusababisha ajali. Chakula cha huko kilikuwa ni nyama za watu na damu. Mwajuma
alisema hataki tena kuwa Muislamu na wachawi wapigwe kwakuwa wanatesa watu
wengi maana kuna wengine amewaacha huko wengi.
Ushuhuda mwingine
ni wa binti anayeitwa Husna; yeye alikuwa tanga na alichukuliwa msukule na
shangazi yake baada ya kulishwa sumu na kufa, ndugu zake waliona amekufa kumbe
yeye alikuwepo msukuleni.
Mwingine aliyepata
nafasi ya kutoa ushuhuda anaitwa Pendo; yeye alikuwa makaburini alichukuliwa na
mama mmoja ambaye hakumkumbuka kwa haraka bali alisema; mama huyo alikuwa
mrefu. Mama huyo alimwambia kuwa anampenda na akamchukua akawa anafanya kazi ya
kusafisha makaburi ndipo alipopata nafasi ya kumchukua na kumweka msukuleni
kwenye makaburi hayohayo aliyokuwa akisafisha.
Mwingine
aliyerudishwa alisema kuwa anaitwa Nipha na alichukuliwa akapelekwa Moshi.
Akiwa msukuleni akasikia sauti ikimwita NJOO akapaa kutoka moshi; ambapo huko
aliwekwa kwa mganga wa kienyeji kwenye kobe ya kuagua.
Msichana mwingine
pia alitoa ushuhuda wake kuwa alikuwa Tanga, na jina lake anaitwa Zerina; binti
huyo alisema huko Tanga alikuwa anakaa kwenye maji kwenye maji, huko alipelekwa
kwa babu mmoja anaitwa hussein alikua hali chakula na alikaa kwa mateso sana.
Mwingine aliyepata
nafasi ya kutoa ushuhuda alikuwa anaitwa Rose ambaye yeye alichukuliwa msukule
na kupelekwa kibosh. Jina lake ni Rose; alikuwa analishwa nyama za watoto
wadogo. Rose alichukuliwa na mke wa mwisho wa baba yake anaitwa Magreth,
alisikia sauti kutoka huko akajiona anapaa hadi mkutanoni.
Wa mwisho
kushuhudia alisema yeye alikuwa anaitwa Esther na alichukuliwa msukule na
kupelekwa sumbawanga. Yeye alichukuliwa na jirani yake hapo katika mtaa
anaoishi.
Mungu ametenda
mambo makuu mno katika siku hii ya sita.. picha na shuhuda kamili zitawajia
hivi punde….
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni