MIKATABA YA DAMU
Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima. |
Na
Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima.
UTANGULIZI:
Katika
mfululizo wa masomo haya tayari tumekwisha kujifunza kuhusu kafara ya damu na
tukaona pia kuhusu Kafara ya mwanakondoo ambaye ni Yesu kristo. Leo tunaangalia
kuhusu mikataba inayoweza kusababishwa na damu iliyomwagika.
TABIA ZA DAMU KATIKA BIBLIA:
Mwanzo 4:10; Adamu alikuwa na watoto wawili mmoja aliitwa
Kaini na mwingine Habili; Kaini alipomuua Habili; Mungu akamwambia Kaini, Damu
ya ndugu yako inanililia. Kumbe damu yaweza kulia na inaweza kuongea pia.
Kumbukumbu 12:23 Mungu anasema kuwa “…damu ni uhai”. Kumbe
damu ina uhai; kwa namna hiyo kuna tabia kadhaa za damu:
i)
Damu ina sauti
ii)
Damu yaweza kulia
iii)
Damu inaleta
laana
Na ndio maana Mungu amekataza kula au kunywa
damu, hii ni kwasababu hizi tatu Kumbukumbu7:27;
Walawi 17:10,12
DAMU INA SAUTI (INANENA):
Damu
iliyomwagika chini inaweza kunena mema au yaweza kunena mabaya,damu inenayo
mema ni ya Yesu peke yake, Waebrania
12:24 inasema, “na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa,
inenayo mema kuliko ile ya Habili.” Kumbe kuna damu inayonena mema (damu
ya Yesu Kristo) na pia kuna damu inayonena mabaya (damu ya wanyama,ndege hata
watu)
Damu
yaweza kuongea mabaya juu ya mtu; damu ikimwagwa hunena na ndio maana hata nchi
yaweza kuingia kwenye matatizo kwasababu ya damu inenayo iliyomwagika.
Mambo ya Walawi 19:26 “Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye
kuloga, wala kutumia utambuzi.” Mungu amekataza kula nyama pamoja na
damu kwasababu damu ni uhai, na ina sauti. Na ukiangalia katika biblia kila
mahali ambapo damu imekatazwa na uchawi pia umetajwa. Kwa maana hiyo
tunajifunza kuwa uchawi upo na unaushirikiano wa karibu na matumizi ya damu.
MAFUNDO YA KICHAWI:
Ukisoma
Ayubu 15:26 “Humshambulia na shingo ngumu, Kwa mafundo makubwa ya ngao zake;” mafundo
yapo na wachawi ndio wanayo yafunga. Wachawi
wanaweza kuloga katika kufunga mafundo, hivi ni vifungo vya kichawi ambavyo
hutumia kudumisha maisha ya watu. Kumbukumbu
18:11 “wala
mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala
mtu awaombaye wafu.” Kuna mafundo ya aina mbalimbali mojawapo ni
mafundo ya maamuzi; yaani mtu anashindwa kuwa na maamuzi, na ndio maana watu
wengi wanashindwa kupiga hatua kwenye maisha kwasababu wamefungwa katika
maamuzi.
Wachawi
pia hutumia mafundo haya kufunga matumbo ya kina mama ili wasipate watoto; na
ndio maana ya maandiko yale yanayosema “Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa
yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa
mbinguni.” Mathayo 18:18.
Kwenye ulimwengu wa mwili mtu anaweza akaonekana anaumwa au ana matatizo lakini
katika ulimwengu wa roho anakuwa amefungwa. Luka 13:16 huyu mwanamke alionekana amepooza kumbe shetani alikuwa
amemfunga.
DAMU INAVYOTENDA KAZI:
Sasa
kwa kujua kuwa kila damu iliyomwagwa inauwezo wa kusema, wachawi hutumia tabia
hiyo ya damu kufunga maisha ya watu. kwahiyo wanachofanya wachawi au waganga ni
kuchukua mnyama na kumchinja yule mnyama na kuinuizia inene tatizo lako.
Kimsingi; hii damu iliyomwagwa ndiyo inayoitwa madhabahu ya tatizo lako. Na
ndio maana waganga wa kienyeji huagiza kuku, mbuzi au ng’ombe ile ni kwa ajili
ya kumwaga damu ili inene mabaya juu ya
mtu.
Damu
inapomwagwa inatoa sauti; yaani katika ulimwengu wa roho ni sauti kubwa ili mtu
akae katika tatizo; kinachotokea pale damu inaponena mashetani husikia rohoni
na kwa njia hiyo mashetani yanapata mlango wa kuingia kwenye maisha ya mtu. Hivyo
mashetani huja ili kutekeleza sauti ya ile damu inayonena. Kwa njia hiyo shetani
amefunga maisha ya watu na kifungo kinakuwa kikubwa kulingana na wingi wa damu
iliyomwagwa
DAMU INAYOTOKANA NA KUCHANJWA CHALE:
Biblia
iko wazi sana kuhusu kuchanja chale kwenye miili ya watu. Mambo ya Walawi 19:28 “Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa
ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana.”
Mambo ya Walawi 21:25; Yeremia 48:37 Yaani; mtu huyu sio
kwamba imemwagwa damu ya mnyama kwa ajili yake bali anakuwa amechanjwa mwenyewe
kwenye mwili na ameitoa damu yake mwenyewe. Kimsingi; mganga anapokuwa anachanja
chale huwa ananena maneno ambayo huwezi kuyaelewa. Yale maneno ndio sauti ya
ile damu iliyo mwagwa.
Utajiuliza
kwanini Mungu anakataza watu kupigwa chale; kimsingi damu inayomwagika ni uhai
wako, kwa lugha rahisi ni kwamba unapochanjwa chale unakuwa umeacha uhai wako kwa mganga wa
kienyeji. Hivyo mganga anaweza kukuona na kukufuatilia kirahisi, hivyo akiamua
kukufanya urudi kwake anaweza kukurudisha kirahisi kwasababu uhai wako umeuacha
kwake.
DAMU YA YESU KRISTO:
Unaweza
ukajifunza kwanini Yesu alipokuja duniani asingekufa kwa kuumwa au njia
nyingine ambayo haimwagi damu, Siri kuu ya kuja Yesu duniani ni kwa ajili yetu
sisi tufunguliwe na kutoka kwenye vifungo kwa damu ya Yesu ambayo yenyewe
hunena mema daima.
Yaani
Mungu alipoaamua kumkomboa mwanadamu ikamlazimu kuvaa mwili ili aje kuukomboa
ulimwengu. Na ndio maana aliitwa Immanuel yaani Mungu pamoja nasi, naye
alipokuja duniani akaenda msalabani ili atengeneze madhabahu yake kwa njia ya
kumwaga damu. Na nguvu ya damu ya Yesu ni kuwa hakutenda dhambi hivyo damu yake
ina nguvu dhidi ya madhabahu zote za giza.
Wakati
wao wanaitia damu za mafahari na mbuzi sisi tunanena damu ya Yesu, inayonena
mema. Kwa kutumia damu ya Yesu twaweza kunyamazisha damu nyingine za giza.
Ibada ilimalizika kwa maombi:
Baada
ya kujifunza somo hapo juu omba hivi;
Kamata
kuhani wa madhabahu:
Ninakamata
kuhani wa madhabahu kwa jina la Yesu.
Kila wachawi na waganga wote wanaosimama kama kuhani wa madhabahu, ninawakamata
kwa jina la Yesu. Ninaharibu kazi zao katika jina kuu la Yesu Kristo.
Imeandikwa mtakalolifunga duniani na mbinguni litakuwa limefungwa; ninawakamata
na kuwafunga wote Katika Jina La Yesu.
Bomoa
Madhabahu:
Katika
jina lenye Nguvu la Yesu Kristo ninaharibu kila madhabahu za kishetani kwa Jina
La Yesu. Ninabomoa madhabahu zinazoleta vifungo kwenye maisha yangu katika Jina
La Yesu. Madhabahu za magonjwa, mikosi na laana ninazibomoa na kuzisambaratisha
katika Jina la Yesu. Ninateketeza madhabahu zote katika Jina La Yesu.
Nyamazisha
damu yoyote iliyomwagwa inayonena mabaya kwa ajiliya maisha yako:
Nanyamazisha
damu zote zinazonena mabaya juu yangu katika Jina la Yesu, Nanyamazisha damu ya
mbuzi na damu zote za wanyama kwa Damu ya Mwanakondoo. Ninaamuru damu yoyote
inayonena mabaya juu yangu inyameze Kwa Damu ya Yesu Kristo. Imeandikwa Damu ya
Yesu inanena mema nami kwa Damu hiyo ninanyamazisha kila damu za mashetani na
damu ya Yesu inene mema kuanzia sasa.
UFUFUO
NA UZIMA {THE GLORY OF CHRIST (T) CHURCH}
TANGANYIKA
PACKERS,
KAWE,
DAR ES SALAAM.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni