Ijumaa, 1 Novemba 2013

BINTI ALIYEFICHWA MSUKULE ARUDISHWA KWENYE MKUTANO WA GWAJIMA ARUSHA

BINTI ALIYEFICHWA MSUKULE ARUDISHWA KWENYE MKUTANO WA GWAJIMA ARUSHA

Binti aliyerudi kutoka msukuleni akiwa jukwaani.
Ikiwa hapo jana ilikuwa siku ya pili ya mkutano mkubwa wa injili chini ya Kanisa la Ufufuo na Uzima unaoendelea katika viwanja vya reli jijini Arusha, tayari miujiza mingi imeanza kutendeka ikiwemo binti aliyekuwa akishikiliwa kwa imani za kichawi katika moja ya nyumba jirani na viwanjani hapo yaani msukule kujikuta akifika mkutanoni hapo kwa maombi yaliyokuwa yakiongozwa na mchungaji Gwajima.

 Lakini pia watu walitimuliwa mapepo baada ya mchungaji kiongozi Josephat Gwajima kuwakabidhi malaika kazi ya kuwaleta mbele watu waliojazwa na mapepo kama alivyonukuliwa ambapo watu wengi walikimbilia mbele kwa maombi hadi kufanya idadi ya wahudumu kuwa ndogo.Inakisiwa watu zaidi ya 20,000 wanahudhuria mkutano huo ambao siku ya leo itakuwa siku ya tatu na mkutano huo unatarajiwa kumalizika siku ya tarehe 10 mwezi ujao.


Mchungaji Gwajima akizungumza na maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha hapo jana viwanja vya Reli.


Mchungaji Gwajima akimfanyia maombi binti huyo, huku pembeni mwimbaji wa nyimbo za injili Flora Mbasha akifuatilia kwa karibu.

Binti akianza kurejewa na fahamu baada ya kufanyiwa maombi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni