Monday, September 2, 2013
Hatari ya Ndoto
![]() |
Na Mchungaji Kiongozi Josephat
Gwajima|Kawe Tanganyika
Packers|Dar es Salaam
|
1.0 Utangulizi
Leo nitafundisha kwa habari ya ndoto. Neno ndoto limeandikwa
ndani ya Biblia zaidi ya mara 86. Katika kitabu cha mwanzo pekee neno ndoto
limeandikwa zaidi ya mara 30. Katika kitabu cha Daniel neno ndoto limejitokeza
zaidi ya mara 22.Kwa kawaida kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa
mafundisho.
Nitafundisha hatari ya ndoto leo kwa mifano ya ndoto za
wafalme wawili. Mfalme wa kwanza Nebukadreza aliyekuwa mfalme katika mashariki
ya kati. (Danieli 2:1-6) Nebukadreza alitawala kipindi ambacho ufalme wake
ulikuwa mkubwa mashariki ya kati yote na dunia yote. Mfano wa pili ni mfalme wa
Misri Farao, huyu alikuwa mfalme katika Afrika (Mwanzo 41:1-8).
Daniel 2: 1-6, tunajifunza habari ya ndoto iliyootwa na
Mfalme Nebudkadreza. “ Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza,
Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi ukamwacha….”
1.1 Ndoto ni nini?
Ndoto ni jambo linalotakiwa kumpata mtu siku chache zijazo.
Ndoto ni kipimo cha hali ya rohoni ya mwotaji. Mfano mtu akiota anakimbizwa na
ng’ombe inaamanisha kuwa kiwango cha nguvu zako za rohoni kimeshuka. Endapo
utaota wewe ndio unamkimbiza adui inamaana nguvu zako za rohoni zipo juu. Ndoto
ni bayana.
2.0 Msisitizo wa Hatari ya ndoto
Ikiwa ndoto inamfadhaisha mfalme ambaye ni mkuu wan chi, je
nini mimi na wewe? Hii inatuonesha kuwa kitendo cha mfalme kutaka kufahamu
tafasiri ya ndoto inamaanisha kuwa ndoto ni bayana.
2.1 Mambo ya kufanya ukiota ndoto
(i) Jambo la kwanza la kufanya baada ya kuota ndoto ni kuindika
hiyo ndoto
Habakuki 2:2-3; BWANA akanijibu akasema, iandike njozi
ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili kila aisomaye apate kuisoma kama
maji.
(ii) Baini je ndoto uliyoota ni ya mema au ya mabaya
(iii) Ukiota ndoto ukabaini ni ya mabaya anza kuomba mara
baada ya kustuka toka ndotoni. Usisubirie kukuche. Omba kinyume cha hiyo ndoto.
Batilisha hiyo ndoto.
2.2 Maandiko yanayofanya baadhi ya watu wapuuzie ndoto
Mhubiri 5:3; “kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli
nyingi…”
Zekaria 10:2; “kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili
nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo…”
Yeremia 23:25; “Nimesikia waliyosema manabii wanaotabiri
uongo kwa jina langu, wakisema nimeota ndoto nimeota ndoto.”
Watu hupuunza ndoto kwa kuwa ndoto huja kwa shughuli nyingi
na pia hupuuza ndoto kwa kuwa zipo ndoto za uongo. Kimsingi kila andiko lenye
pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho. Uwepo wa maandiko mawili yanayofanya
baadhi ya watu wapuuzie ndoto hauwezi kupuuza ndoto zaidi ya 80 ambao zilikuwa
bayana, na Mungu alisema na watu katika ndoto.
3.0 Baadhi ya maandiko yanayotufanya tuzishughulikie ndoto
tunazoota
Mwanzo 20:3-5; “Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto
ya usiku…”
Mwanzo 28:12 Ndoto ya Yakobo “…akaota ndoto na tazama ngazi
imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena tazama malaika wa
Mungu wanapanda na kushuka juu yake….”
Mwanzo 31:11”Na malaika wa Mungu akiniambia katika ndoto…”
Mwanzo 31:23-24 “…Mungu akamjia Labani Mshami katika ndoto
ya usiku…”
Mwanzo 37:46; ndoto ya Yusuph
1 Falme 3:5-10; Ndoto ya Suleiman
Ayubu 7:14;
Ndoto ya Ayubu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni