Monday, December 17, 2012
SAFARI YA KUZIMU NA KUMBUKA NENO HILI ''MUDA UNAISHA HARAKA SANA''
Ushuhuda wa Victoria Juu ya Kuzimu
Muda Unaisha Haraka!
Huu ni ufupisho wa ushuhuda wa Victoria Nehale
Nilizaliwa
na kuishi Namibia maisha yangu yote; na niliyatoa maisha yangu kwa Yesu tarehe
06 Februari 2005. Bwana Yesu Kristo ameshanifunulia mambo mengi katika
ulimwengu wa roho ikiwa ni pamoja na safari za kuzimu. Bwana alinipa maelekezo
kwamba niwashirikishe watu uzoefu wangu; pia alinionya kuwa nisiongeze wala
kupunguza chochote katika vile alivyonionyesha na kuniambia. Wakati nikiandika
kitabu hiki, mwishoni mwa 2006, nilishatembelewa mara 33 na Bwana Yesu Kristo.
Kila aliponitembelea, Bwana alikuwa akiniambia kabla ya kuondoka: MUDA UNAISHA HARAKA!
Safari ya kwanza kuzimu
Katika wikiendi ya tarehe 23 Julai 2005,
nilipanda taksi kwa ajili ya safari ya dakika thelathini kutokea mji wa
Ondangwa ambako ndiko ninakofanya kazi na kuishi, hadi kijijini kwetu, kwa
lengo la kwenda kuwa na wazazi wangu wakati wa wikiendi ile. Wakati nikielekea
nyumbani, nilipata hisia kwamba kuna jambo lisilo la kawaida ambalo lingetokea
jioni ile. Nilifika nyumbani kwenye saa 12 jioni; na hapo watu walikuwa
wanaandaa chakula cha jioni. Nilikuwa jikoni pamoja na familia yetu, huku
nikiwa nimelala kwenye mkeka. Watoto wa hapo nyumbani walikuwa wakiimba nyimbo
zao za Shule ya Jumapili. Ghafla nilijisikia upako mzito ukinishukia; mwili
wangu ukawa dhaifu sana; na nikawa nimetoka kwenye mwili kutokana na nguvu za
Mungu. Nilimwona mwanamume amevaa joho jeupe refu likiwa limefungwa kwa kamba
ya rangi ileile; akiwa anatembea kuelekea pale nilikokuwa nimelala. Kulikuwa na
nuru imemzunguka kana kwamba ilikuwa ikitokea kwake. Alikuwa amevaa viatu vya
wazi vya kahawia. Mwonekano wake ulikuwa kama wa watu wa Mashariki ya Kati,
huku akiwa na ngozi nzuri ya hudhurungi. Uso wake ulikuwa mpole sana na umejaa
utukufu lakini sikuweza kumtazama machoni. Alipoongea, sauti yake ilikuwa ya
upole, na upendo, lakini pia yenye
mamlaka; mawimbi ya upendo yalikuwa yakitoka kwake.
Alinyoosha mkono wake kwangu na kuninyanyua
kutokea pale nilipolala. Ghafla nilijiona nikiwa nina mwili mzuri sana.
Nilijiona niko kama nilivyokuwa ningali na miaka kumi na nane. Nilikuwa nimevaa
joho jeupe na kamba nyeupe. Japokuwa joho langu lilikuwa jeupe, lilitengenezwa
kwa matirio tofauti na ya joho la yule mwanamume. Joho lake lilikuwa la hariri huku liking’aa
kiasi kwamba hata nashindwa namna ya kuelezea.
Alisema, kwa sauti ya upendo na upole sana: “Victoria, nataka
uende nami; nitakuonyesha mambo ya kuogopesha na ninakupekela mahali ambako
haujawahi kufika katika maisha yako.” Alinishika
mkono wa kulia na tukaondoka. Nilijiona kama vile tunatembea hewani na muda wote
tulikuwa tukielekea tu juu. Baada ya muda, nikawa nimechoka sana, na
nikamwambia kuwa nisingeweza kuendelea na safari. Hivyo nikamsihi aniruhusu
nirudi. Hata hivyo, alinitazama kwa upendo na kusema, “Haujachoka
– uko sawa tu. Kama ukichoka, nitakubeba, lakini kwa hivi sasa uko tu sawa.
Amani iwe kwako. Tuendelee.”
Tulifika mahali ambako ni pakavu sana; pakavu
kuliko jangwa lolote analojua binadamu; hakukuwa na dalili zozote za uhai.
Hakukuwa hata na mti mmoja au hata jani au kiumbe chochote hai. Lilikuwa ni
eneo linalofadhaisha sana.
Hatimaye tulifika kwenye geti moja na yule
mwanamume alinigeukia na kusema: “Victoria, tutaingia kupitia geti hili na mambo ambayo utayaona
yatakuogopesha na kukufadhaisha – lakini uwe na uhakika kuwa kokote
nitakakokupeleka, utakuwa na ulinzi mkamilifu. Wewe fungua tu macho yako na
kutazama kila nitakachokuonyesha.” Nilijawa na hofu na kuanza kulia.
Nilikuwa nalalamika na kumwomba anirudishe. Nilimwambia kuwa sikutaka kuingia
kwenye sehemu ile maana tayari nilikuwa naona kupitia getini kile kilichokuwa
kikiendelea ndani. Aliniangalia na kusema,
“Amani iwe nawe; niko
pamoja nawe. Ni lazima tuingie ndani, maana muda unakimbia haraka.”
Tuliingia kupitia getini. Siwezi kukusimulia
utisho wa mahali pale. Nina uhakika kabisa kuwa hakuna sehemu yoyote
ulimwenguni ambayo ni mbaya kama ile! Sehemu ile ilikuwa ni kubwa sana na
nilipata hisia kuwa inaendelea kupanuka muda wote. Ilikuwa ni sehemu ya giza
totoro na joto lake halipimiki; ilikuwa ni joto kuliko moto ulio mkali kabisa.
Sikuona miali yoyote ya moto au chanzo cha joto lile lakini kulikuwa ni JOTO!
Kulikuwa na wadudu wa kila ukubwa; wa kijani, weusi, na wa kijivu - ila aina ya
wadudu unaoweza kuwafikiria. Zaidi ya hapo, kulikuwapo pia kila mahali funza
wafupi, wanene, weusi, ambao wanapanda juu ya kila kitu. Walianza kupanda juu
yetu na wadudu nao walikuwa wametuzunguka kila upande. Mahali pale kulikuwa na
harufu mbaya mno; hakuna maneno ya kutosha kuelezea harufu ile. Harufu ilikuwa
kama nyama iliyooza lakini ilikuwa ni mbaya mara mia zaidi ya nyama
iliyooza niliyowahi kunusa maishani
mwangu mwote! Kulikuwa na kelele za vilio na kusaga meno, pamoja na vicheko
vibaya vya mapepo.
Kibaya kabisa kwenye sehemu hii ni kuwa pamejaa
watu. Walikuwa ni wengi sana kiasi kwamba hawahesabiki. Walikuwa ni mifupa tu.
Ninaweza kusema kwa ujasiri na uhakika kabisa kwamba mifupa hii ilikuwa ni
wanadamu kwa vile niliweza kuwatambua baadhi ya ndugu zangu wa karibu na watu
kutoka kijijini kwangu. Mifupa yao ilikuwa ya kijivu cheusi na mikavu sana. Walikuwa
na meno marefu makali kama wanyama wa porini. Midomo yao ilikuwa mikubwa na
mipana na ndimi zao zilikuwa ndefu na nyekundu sana. Mikono na miguu yao
ilikuwa na vidole vyembamba virefu, na kucha kali, ndefu. Baadhi yao walikuwa
na mikia na pembe.
Kulikuwa na mapepo yakichanganyika na
watu: mapepo yalionekana kama mamba na yalitembelea miguu minne. Yalionekana
yanajisikia vizuri tu kwenye mazingira yale na mara zote yalikuwa yakiwachokoza
na kuwatesa wanadamu. Kelele kutoka kwa yale mapepo zilikuwa ni kama vile yako
kwenye sherehe; maana yalionekana yana furaha. Yalikuwa pia yakicheza na
kurukaruka muda wote. Wanadamu kwa upande wao, walionekana wana mateso na
fadhaa; walikuwa katika hali ya kukosa msaada. Kelele za wanadamu
zilisababishwa na maumivu. Walikuwa wakilia, wakipaza sauti na kusaga meno yao;
na walikuwa katika hali ya mateso makali yasiyo na mfano.
Watu katika sehemu ile, walikuwa ni wengi mno,
lakini niliweza kuona kuwa wengi wao walikuwa wanawake. Waligawanyika katika
makundi mbalimbali. Japokuwa walikuwa katika makundi, ilikuwa haiwezekani
kukadiria idadi yao katika kundi lolote maana makundi yenyewe yalikuwa ni
makubwa kupita kiasi!
Mwanamume yule alinipeleka hadi kwenye kundi
mojawapo upande wa mashariki wa sehemu ile. Kisha alinitazama na kusema: “Victoria, hili ni kundi la watu
ambao walikataa kuwasamehe wengine. Niliwaambia mara nyingi na kwa njia nyingi
kuwa wawasamehe wengine lakini walinikataa; Mimi nimewasamehe wao dhambi zao
zote lakini wao walikataa kuwasamehe wengine. Muda wao uliisha na wakajikuta
wako hapa. Watabakia hapa milele yote; wanakula matunda ya kazi yao milele na
milele. Hata hivyo, inaniuma sana kuwaona kwenye sehemu hii mbaya na katika
sehemu hii ya milele – maana ninawapenda.”
Nilipelekwa kwenye kundi linalofuata, na
mwanamume yule aIiniambia kuwa watu wa kundi lile la pili walikuwa ni wale
waliokuwa na madeni: walikuwa na uwezo wa kulipa madeni yao lakini waliendelea
kuahirisha. Walikuwa wakisema kuwa tutalipa kesho, wiki ijayo, mwaka ujao, hadi
muda ukawaishia. Hapa ndipo watakaa milele; wanakula matunda ya kazi yao.
Aina ya pili ilikuwa ni ya wale ambao walikuwa na
madeni na walikuwa na uwezo wa kuyalipa; na walikuwa tayari kuyalipa, lakini
walikuwa wakiogopa matokeo maana, labda, kama wangesema kweli, wangeishia
kukataliwa, au wangefungwa, au labda kile ambacho walitenda kingejulikana
duniani kote nao wangeaibika. Yule mwanamume akasema: “Hakuna kati yao ambaye alinijia kuniomba njia ya kufanya. Kama
wangeniomba, ningewaonyesha njia rahisi kabisa ya kutoka kwenye hali
zilizowakabili. Muda wao uliisha na wakajikuta wako hapa ambako ndiko
watakuwako milele. Wanakula matunda ya kazi zao.”
Kisha akasema: “Kundi la tatu walikuwa na madeni ambayo hawakuwa na uwezo wa kuyalipa,
lakini pia, nao hakuna hata mmoja ambaye aliniambia kuwa ana deni asiloweza
kulipa. Kama wangefanya hivyo, ningewalipia madeni yao. Pia, walijaribu kutumia
ufahamu wao na hekima yao, kitu ambacho hakikuwasaidia kwa njia yoyote. Hivi
sasa wamejikuta mahali hapa ambako ndiko watakakoku. Wanakula matunda ya kazi
yao. Moyo wangu unauma kwa ajili ya watu hawa wote maana ninawapenda sana.”
Katika kundi la kwanza, niliwaona ndugu zangu
wawili wa kike wa karibu sana pamoja na mtoto wa miaka kumi na mbili, naye pia
akiwa ndugu yangu. Nilijua alikuwa na miaka kumi na mbili maana huo ndio
ulikuwa umri wake wakati anakufa. Katika kundi la pili nako pia niliwaona
baadhi ya ndugu zangu, pamoja na Mchungaji ambaye nilimfahamu vizuri sana.
Rafiki yangu wa kiume, Jakes, ambaye alijiua kwa sababu mimi niliamua kumpa
Kristo maisha yangu, naye alikuwa kwenye kundi la pili. Niliwaona baadhi ya
majirani zangu kwenye makundi yote pia.
Niliwatambua watu niliowajua kabla ya kufa kwao;
nao pia walinitambua. Ndugu zangu walijawa na hasira sana waliponiona na
wakaanza kunitukana. Walikuwa wakitumia lugha chafu kabisa wakati wakinitukana.
Mmoja wao alisema kuwa sikustahili kumfuata mwanamume yule ambaye nilikuwa
naongozana naye; walikuwa wakiongelea mambo ambayo nilikuwa nikiyafanya kabla
ya kutoa maisha yangu kwa Kristo. Hawakuwa wakisema uongo. Mambo waliyokuwa
wakinituhumu nayo yalikuwa ya kweli. Jakes alikuwa akisema kuwa mimi nilikuwa
wa kwake na kwamba nilitakiwa kwenda pale alipokuwa maana nilitenda dhambi
zilezile kama alizotenda yeye. Mara ya kwanza, yule mchungaji alionekana
amefurahi kuniona na akasema nimefanya vema kuja, lakini alibadilika ghafla
pale alipomwona yule niliyekuwa nimeongozana naye; kisha naye akajiunga na wale
waliokuwa wakinilaani kwa matusi. Mwanamume yule aliyekuwa nami akaniambia
nisiwajali maana hawajui walitendalo.
Nilipigwa na bumbuazi na kujawa na huzuni kubwa
sana. Mwili wangu ulikuwa ukitetemeka na sikuweza kusimama. Nilikuwa nikilia
bila kuweza kujizuia. Mwanamume yule alinigeukia, akanikumbatia, na kusema: “Amani iwe nawe, Victoria.”
Nguvu zangu zilinirejea na nikajisikia salama mikononi mwake. Kisha akaniambia
kuwa tulitakiwa kuondoka pale na kurudi. Alinitazama na kusema: “Victoria, nimeshakuonyesha. Sasa
inabidi uchague ni kundi lipi unataka kuingia; uchaguzi umo mikononi mwako. Ni
lazima uwaeleze watu kila kitu ulichokiona lakini usiongeze au kupunguza
chochote.”
Nakumbuka kuwa tuliondoka pamoja kwenye ile
sehemu ya kutisha lakini sikujua nimemwacha wapi maana fahamu zangu za kawaida
zilinirudia. Nilifungua macho yangu na kujikuta kwenye mwili wangu wa nyama,
huku nikiwa nimelazwa kwenye Hospitali ya Oshakati. Nilikuwa nimetundikiwa
dripu kwenye mkono wangu wa kushoto; na nilimwona mama yangu na ndugu zangu
wengine wa kijijini kwenye kona moja ya chumba, ambako walikuwa wakiniangalia
kwa mshangao. Niliona kwenye uso wa mama yangu kwamba alikuwa analia.
Nilimwuliza nesi mmojawapo kama alikuwa anafahamu tatizo langu lilikuwa nini
lakini alinifanyia tu mzaha na kusema: “Umerudishwa. Labda ulifanya kosa fulani
na unatakiwa kutubu.” Nesi alikuwa anajaribu kuelezea kwa lugha nyepesi namna
hali yangu ilivyokuwa, lakini nilibaini kuwa alikuwa anaogopa kunikaribia.
Nilimwomba aniitie daktari aliyenihudumia.
Daktari alipofika, alisema kuwa hakujua kulikuwa
na tatizo gani kwangu. Mwanzoni, alidhani kuwa nilikuwa na malaria lakini
vipimo vilionyesha kuwa sikuwa nayo. Aliendelea kunieleza kuwa joto langu,
mapigo ya moyo, na shinikizo la damu vilikuwa chini sana kwa viwango vya hatari
lakini hakuweza kujua sababu yake. Alisema kuwa hakuwa na cha kufanya tena kwa
ajili yangu. Hakuweza hata kuniandikia kulazwa maana sikuwa na ugonjwa. Dripu
waliyoniwekea ilikuwa haifanyi kazi mwanzoni, lakini nilipofungua tu macho
yangu, ikaanza kufanya kazi. Alipendekeza kuwa nesi aniwekee dripu nyingine
mara ile ya kwanza itakapoisha ili niweze kupata nguvu za kutosha kwenda
nyumbani.
Niliogepeshwa na kile nilichoona mahali pale na
sikuweza kujizuia kulia. Harufu mbaya ya pale iliendelea kuwa halisi kama
nilipokuwapo hapo. Taswira za pale ziliendelea kunijia wakati wote. Nilishindwa
kulala na mwili wangu wote ulihisi maumivu makubwa. Nilijihisi kana kwamba
miguu na mikono yangu ilinyofolewa na kurudishiwa tena. Ah, nilijisikia vibaya
sana. Nilikuwa na tumbo la kuendesha na kichwa kiligonga kwa wiki nzima.
Niliamua moyoni mwangu kwamba nisingemweleza mtu
yeyote juu ya kile nilichoona maana ni nani kwanza angeniamini? Watu
watanielewaje? Niliendelea kujiambia kuwa sitamweleza kamwe mtu yeyote juu ya
mambo hayo. Mmoja wa washauri wangu alinipigia simu siku tatu baadaye kuulizia
kuhusu hali yangu maana nilikuwa nimemtumia meseji aniombee. Bila kujitambua,
nilijikuta nikimsimulia kuhusu yaliyonikuta. Niliposhtuka, tayari
nilishamweleza karibu kila kitu. Nilitamani kujipiga mateke. Nilikuwa nalia kwa
kuwa niliamini kuwa nimefanya kosa kubwa kabisa maishani mwangu. Sasa hadithi
nzima ilikuwa wazi; hakukuwa na uwezekano wa kuificha tena. Sasa najua kuwa
kama Mungu akitaka jambo fulani lielezwe, lazima litaelezwa. Maana yeye si ni
Mungu?
***********
Agosti 19, niliamka huku nikijisikia hali ya
upako kwenye mwili wangu wa nyama. Nilikuwa dhaifu na kutetemeka, huku mawimbi
ya umeme yakipita kwenye mwili wangu. Jioni, niliona mwanga mkali ukija
chumbani kwangu, na katikati yake, alikuwa yuleyule mwanamume. Safari hii
alikaa chini kwenye kiti karibu na kitanda changu. Hata sielewi kiti hiki
kilitoka wapi lakini kilikuwa pale mara tu alipokuwa tayari kukaa. Kilikuwa ni
kiti kizuri cha dhahabu tupu. Umbo lake lilikuwa la kiti cha kawaida, kikiwa na
sehemu ya kuegemeza mgongo. Kwenye kila mguu kulikuwa na nyota ya madini ya
fedha iliyopachikwa kwenye dhahabu ile; nyota ileile ilikuwa pia katikati ya
sehemu ya nyuma ya kuegemeza mgongo. Kulikuwa na magurudumu kwenye kila mguu.
Baada ya kunisalimia, aliniambia kuwa alijua kuwa
nina maswali mengi kuhusu yeye ni nani; hivyo alikuja kujitambulisha kwangu na
kufafanua mambo kadhaa ambayo tayari nilikuwa nimeyapitia. Alisema: “Mimi ni Yesu Kristo, Mwokozi
wako. Kama una mashaka yoyote, tazama mikono yangu. Mahali pale ambako
tulienda, ni Kuzimu.” Nilipoangalia
mikono yake, niliona makovu ambamo misumari ilimtoboa.
Rafiki, napenda nikueleze kuwa kuzimu si sehemu
ya kufikirika tu mawazoni; lakini ni mahali halisi na si kuzuri hata kidogo. Ni
mahali ambako hakukutengenezwa kwa ajili ya wanadamu bali kwa ajili ya shetani
na mapepo yake. Sehemu inayotustahili ni Mbinguni pamoja na Yesu lakini
inatubidi tumchague Yesu kabla hatujachelewa. Leo, unapoisikia sauti yake,
usifanye moyo wako kuwa mgumu; mkubali Yesu awe Mwokozi wako binafsi kisha
uishi kwa ajili yake. Kuzimu ni kubaya mno: ni sehemu ya hofu na huzuni; ni
sehemu ya mateso na vilio vya milele na kusaga meno. Shetani anataka awachukue
watu wengi kadiri iwezekanavyo ili aende kule pamoja nao. Usishirikiane naye;
shirikiana na Yesu nawe, badala ya kufa, utaishi.
Sikuelewa kwa nini Bwana aliniambia nichague kati
ya makundi mawili aliyonionyesha kule kuzimu ilhali mimi tayari nilikuwa
Mkristo niliyeokoka. Nimeshamkubali maishani mwangu lakini bado alikuwa
akiniambia nichague kama nataka kwenda kuzimu au la! Sikuweza kuelewa. Nilianza
kuomba na kumwuliza Mungu anipatie ufunuo juu ya kile alichomaanisha na ni nini
anataka nifanye. Bwana alinifunulia kuwa nilikuwa nimeficha roho ya kutosamehe
na chuki moyoni mwangu kwa sababu ya dada yangu mmoja, pamoja na binamu yangu
mmoja. Nilimwomba Bwana anisamehe kutokana na kutosamehe kwangu. Pia nilimwomba
dada yangu anisamehe kwa kuweka hasira na uchungu moyoni mwangu kwa ajili yake.
Bwana alinielekeza niende pia nikamwombe msamaha binamu yangu.
Bwana pia alinikumbusha kuwa kulikuwa na wakati
ambapo nilipata kazi ya ualimu kwa kutumia cheti cha diploma cha uongo na
alihesabu hilo kuwa ni deni na wizi. Nilikusudia kutenda kilicho sahihi na
nilimwomba anisaidie kutoka kwenye tatizo hili na anionyeshe njia rahisi ya
kutoka humo maana hili lilikuwa ni kosa kubwa na lingeweza kunifannya nifungwe.
Alinielekeza niende kwenye Idara ya Elimu nikakiri kosa nililofanya. Nilikuwa
tayari kwenda jela kama ingebidi. Nilipata upendeleo wa Bwana kwa kiasi kikubwa
sana. Nilipofika kule, mhusika kwenye Idara ya Elimu aliniambia niamue kile
ninachotaka kufanya: ama kulipa mshahara ambao nilipokea kutoka serikalini au
la. Waliahidi kuwa hawatanishtaki maana walishangazwa na kitendo changu cha
kwenda kukiri kosa lile. Mungu wetu ni Mungu mwaminifu ambaye analiheshimu Neno
lake.
Kama uko kwenye hali inayofanana na niliyokuwa
nayo, napenda nikutie moyo kuwa utende kile kilicho sahihi, bila kujali
matokeo. Unaweza kufungwa kwenye jela ya kidunia lakini hiyo ni ya muda tu.
Hakuna maumivu au aibu inaweza kulinganishwa na kutengwa na Mungu milele.
Kuzimu si mahali pazuri: ni bora kumruhusu Mungu akuhukumu sasa kabla
hujachelewa. Hatutakiwi kuogopa hukumu ya Mungu tungali bado kwenye kipindi cha
Neema; ni lazima tumruhusu afunue chochote kisicho sawa kwenye maisha yetu
tungali bado na muda wa kuweka mambo sawa naye, maana hakuna msamaha upande wa
pili wa kaburi.
Safari ya pili kuzimu
Oktoba 18, 2005, niliamka saa 11:30 asubuhi
lakini sikuweza kwenda kazini. Nilijisikia hali ya udhaifu sana na kulewa; sikuweza kusogea au kugeuka kitandani
kwangu; na uwepo wa Bwana ulikuwa mzito sana chumbani. Nilikuwa natetemeka na
nikahisi kama umeme ukipita mwilini mwangu. Bwana alinijia kabla tu ya saa 2:00
maana kwa mara ya mwisho nilipotazama saa ilikuwa ni saa 1:48; na Yeye alifika
muda mfupi tu baada ya hapo. Alinisalimia na kusema kuwa tunatakiwa kwenda tena
maana muda unaisha haraka sana. Nilisimama na tulianza kutembea. Utembeaji wa
safari hii ulikuwa tofauti kabisa na safari zingine zote. Japokuwa miguu yetu
ilikuwa inafanya kitendo cha kutembea, tulikuwa kama vile tunaelea zaidi kuliko
kutembea. Wakati tukiwa njiani, Yesu aliniambia kuwa
dhambi zote ni mbaya na hakuna kitu kama dhambi ndogo au dhambi kubwa. Dhambi
zote mwisho wake ni mauti - ziwe kubwa au ndogo. Bwana aliniambia kwamba
tunaenda kutembelea kuzimu tena na akaniuliza iwapo nilikuwa nina hofu. Nilimjibu kuwa nilikuwa nayo.
Alisema, “Roho ya woga haitoki kwa Baba yangu au kwangu; inatoka kwa
Ibilisi. Woga utakusababisha utende mambo ambayo yatakupeleka kuzimu.”
Bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu na hofu
ni kinyume kabisa cha imani. Ni wazi kuwa hofu haimpendezi Mungu kwa kuwa
inaharibu imani yetu. Muda wote tulipokuwa njiani, tulikuwa tunatembea kila
mmoja peke yake. Lakini mara tu tulipofika kwenye lango la kuzimu, alinishika
mkono wangu kwa mkono wake wa kulia kwa muda wote tuliokuwa kuzimu. Nilifurahi
sana kwa Bwana kunishika mkono maana kwa namna alivyokuwa amenishikilia kwa
nguvu, hofu yote ilitoweka. Sehemu ile ilikuwa bado iko vilevile: hakukuwa na
tofauti na ilivyokuwa mwanzo. Kulikuwa na wadudu, funza, joto kali sana,
harufu, mifupa, kelele: kila kitu kilikuwa kama mwanzo nilipoenda pale.
Tulipita tena kwenye geti lilelile baya na Bwana akanipeleka kwenye kundi moja
la watu. Kulikuwa na watu wengi niliowafahamu wakati wangali duniani. Maskini,
walikuwa kwenye hali mbaya sana. Walionekana ni wenye taabu na maumivu makubwa;
lakini baya zaidi ilikuwa ni nyuso zao zisizo na matumaini kabisa.
Bwana alimwonyesha mwanamke mmoja wa makamo
ambaye nilimfahamu kabla hajafa. Alikufa kwa ajali ya gari mwanzoni mwa mwaka
2005. Nilipigwa na butwaa kumwona pale maana sote tulimjua kuwa ni mtu
aliyekuwa na hofu ya Mungu na aliyempenda Mungu. Bwana
aliniambia kuwa mwanamke yule alimpenda na Yeye Bwana naye alimpenda; alimwokoa
angali akiwa duniani; aliwashuhudia wengi ambao walimwijia Bwana na alifahamu
Neno vizuri sana. Alikuwa mkarimmu kwa maskini na wahitaji; aliwapatia
walichohitaji, na kuwasaidia kwa njia nyingi. Alikuwa ni mtumishi mzuri wa
Bwana kwa namna nyingi.
Maneno hayo ya Bwana yalinishitua hata zaidi;
nami nikamwuliza kwa nini amwache mtu kama huyo aliyemtumikia kwa kiasi kikubwa
hivyo aingie kuzimu? Bwana alinitazama na kusema kuwa mwanamke yule aliamini
uongo wa Ibilisi. Japokuwa aliyajua Maandiko vizuri, aliamini uongo wa ibilisi
kwamba kuna dhambi ndogo na kubwa. Alidhani kuwa dhambi ‘ndogo’ zisingempeleka
kuzimu, maana alikuwa Mkristo hata hivyo.
Bwana aliendelea kusema, “Nilimwendea mara nyingi na kumwambia aache kile
alichokuwa anakifanya lakini mara nyingi alijenga hoja akilini mwake kuwa kile
alichokuwa anakifanya kilikuwa ni kidogo sana na alichukulia kuwa yale maonyo
yangu yalikuwa ni hisia zake tu za hatia. Kulikuwa na muda ambapo aliacha kwa
muda lakini baadaye alijishawishi tena kuwa maonyo yale hayakuwa yanatoka
kwangu, bali ni sauti yake tu kwa kuwa aliona kuwa dhambi ile ilikuwa ni ndogo
sana kuweza kumhuzunisha Roho Mtakatifu.”
Nilimwuliza tena Bwana ili aniambie ni dhambi
gani basi mwanamke yule alitenda. Alinijibu kwamba, “Mwanamke huyu alikuwa na rafiki ambaye alikuwa
nesi kwenye Hospitali ya Oshakati. Kila mwanamke huyu alipoumwa, hakwenda
hospitali na kulipa kwa ajili kadi yake kama inavyotakiwa kwenye taratibu za
kawaida; badala yake yeyé alipiga tu simu na kumwambia rafiki yake amfanyie
mipango ya dawa kutoka kwenye Zahanati
ya Hospitali. Na mara zote rafiki yake yule alikubali na kumwambia kuwa apite
pale muda fulani kuchukua dawa. Kwanza, aliamua kukubali uongo wa ibilisi juu
ya kuwapo kwa dhambi kubwa na ndogo na kuikataa kweli yangu; alimsababisha mtu
mwingine atende dhambi na kuiba kwa niaba yake, lakini kibaya zaidi,
ALIMHUZUNISHA ROHO MTAKATIFU. Hicho ndicho kilichomfanya afike kuzimu.
Haijalishi kwamba utaleta mamilioni ya roho kwa Bwana; bado upo uwezekano wa
kuingia kuzimu kutokana na kumhuzumisha Roho Mtakatifu. Si tu kwamba ni lazima
ujali wokovu wa wengine lakini pia ni lazima uwe mwangalifu usije ukasahau roho
yako. Kuwa makini na Roho Mtakatifu wakati wote.” Baada ya maneno
hayo, Bwana alisema ni wakati wa kurudi.
************
Wakristo wengi waliosikia hadithi yangu hii
huiona kama ina matatizo. Mara nyingi huwa wanniuliza, “Vipi kuhusu kuhesabiwa
haki, rehema, na neema?” na pia “Inawezekana kweli kupoteza Wokovu wako baada
ya kuwa umeupokea?”
“Huko si kuvuka kiwango?”
“Mungu anaweza kuwa mkatili kiasi hicho?”
Kama nilivyosema kwingineko kwenye kitabu hiki,
mimi siongei theolojia yangu hapa. Ninasema tu kile ambacho Bwana alinionyesha
na kunifundisha – na kile alichoniruhusu kukishuhudia. Tafadhali someni Biblia
zenu ili kupata majibu. Tazama aya zifuatazo, kisha uhukumu mwenyewe.
“…bali nautesa mwili wangu na
kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa
kukataliwa.” (1Wakorintho 9:27)
“Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema
izidi kuwa nyingi?
Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?” (Warumi 6:1-2)
“Basi, dhambi isitawale ndani
ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake.” (Warumi 6:12)
“Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya
kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali
kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao
wapingao.” (Waebrania 10:26 –27)
Unasema, “Je, naweza kwenda kuzimu baada ya kuwa
nimemtumikia Bwana na kuwaleta wengi kwa Kristo?” Hukumu mwenyewe!
Kutokutii
Jumatatu ya tarehe 6 Machi
2006, niliamshwa na saa ya kengele saa 11:30. Nilianza kuomba na nikatambua
kulikuwa na upako mzito juu yangu. Mwili wangu ulikuwa dhaifu na nilikuwa
nikitetemeka; mawimbi ya umeme yalikuwa yanapita kwenye mwili wangu.
Wakati wa mchana, nikiwa
nimelala kitandani, niliona nuru nyeupe ikijaza chumba changu. Niliona shanga
ndogondogo, nyeupe, za duara, zenye ukubwa wa kichwa cha pini. Shanga hizi
zilikuwa zikianguka kama mvua inavyonyesha na zilipogusa ngozi yangu, zilizama
ndani. Zaidi ya hapo, niliona kama wingu linalofanana na ukungu mweupe likija
kutokea juu. Nalo pia lilikijaza chumba na likawa likizama kwenye ngozi yangu
kila liliponigusa. Baada ya hapo, nilimwona Yesu akitembea katikati ya lile
wingu la ukungu kuelekea pale nilipokuwa. Alikaa kwenye kiti chake pembeni mwa
kitanda changu. Hata sielewi kiti hiki kinatokea wapi; huwa kinatokea tu mara
anapokuwa tayari kukaa. Ni kiti kizuri
kilichotengenezwa kwa dhahabu. Umbo lake ni kama la viti vingi tunavyovifahamu
lakini kina sehemu ya kuegemeza mgongo. Kwenye kila mguu kuna nyota ya fedha;
na nyota nyingine ya aina ileile, japo ni kubwa zaidi, iko kwenye sehemu ya
kuegemea. Kuna magurudumu kwenye kila mguu.
Yesu alinisalimia na
akaninyooshea mkono wake na kuniambia niamke maana muda unakimbia haraka sana.
Alinivuta mkono wangu nami nikainuka na kukaa kitandani kwangu.
Kisha akaniambia, “Victoria, tuombe.”
Aliomba kwa lugha ambayo siielewi; nilielewa neno moja tu ‘Amen’. Kisha
aliendelea kwa kuniuliza nilikuwa naona nini
nami nilimwambia kuwa nilikuwa naona kundi la watu wakienda kazini kwao na
wengine wakirudi kutoka kazini kwao. Nilikuwa pia naona vile vishanga vyeupe
vikiwaangukia wale waliofika mwanzo kazini kwao. Baada ya kundi la kwanza,
kundi jingine nalo lilifika baadaye.
Wakati huo, ile mvua ya vile vishanga iliacha kunyesha.
Niliona pia makundi mbalimbali
ya watu, wakiwasili kwenye makanisa mbalimbali Jumapili asubuhi. Mvua ile
ingeanza kunyesha mara tu watu wa mwanzo wanapoingia kwenye uwanja wa kanisa.
Iliendelea kunyesha kwa muda kisha ikasimama. Wale wanaochelewa hawakuti
chochote.
Yesu aliniuliza iwapo nilikuwa
naelewa maana ya maono yale, nami nilimwambia kuwa sikuelewa. Ndipo
alinifafanulia kwa kusema kwamba: “Maono haya yanamaanisha kuwa kila mahali ambako unatakiwa kuwako kwa
muda fulani na wewe unajua ni wakati gani unatakiwa kuwa pale, mara zote huwa
kuna malaika wanagawa baraka kwa ajili ya muda huo. Kama ukifika mapema,
utapokea baraka zako, lakini ukichelewa, unakosa baraka zako kwa siku ile maana
malaika hugawa baraka kwa muda ule tu. Victoria, nataka kukuonya kwa sababu
huwa unaenda kazini kwa kuchelewa, na hasa huwa unaenda kanisani kwa kuchelewa.
Ni lazima ujue kuwa kwa nyakati zile huwa unachelewa bila kuwa na sababu za
msingi; umekuwa ukikosa baraka zako kwa siku zile; hazitakurudia tena. Victoria, ni lazima uache jambo hili na
usilitende tena, isipokuwa pale unapokuwa na sababu ya msingi ya
kuchelewa.”
Bwana alipomaliza kusema
maneno yale, kwa kweli nilitamani kutoweka au angalau nimpatie sababu
inayokubalika kutokana na kukosa kwangu nidhamu. Nilimwambia kuwa wakati
mwingine napitiliza kulala lakini alinitazama moja kwa moja machoni na kusema
kuwa nilikuwa nasema uongo na kwamba nilikuwa nina tabia mbaya ya kurudi
kitandani baada ya kuwa nimeamka, ili kutimiza ile shauku ya kusema ‘ngoja
nilale kidogo tu.’
Baada ya Yesu kuwa amenionya.
alisema, “Simama. Tuondoke
sasa. Muda unakimbia haraka sana. Kuna mambo ambayo ni lazima tuyafanye.”
Safari hii Bwana alinipeleka
mahali ambako sikuwahi kufika kabla. Ilikuwa pia ni mara ya kwanza kufuata
barabara tuliyotembea siku ile. Tulifika kwenye bustani iliyojaa maua mazuri na
miti mizuri ya kijani. Hakuna kitu duniani kinachoweza kulingana na mahali
pale. Maua yalikuwa ya kila aina ya rangi za kung’aa. Tulikaa kwenye benchi zuri la bustanini,
ambalo lilitengenezwa kwa dhahabu safi huku likiwa na nyota ndogo za madini ya
fedha ya kung’aa.
Tulipokaa, alionyesha kidole
mbele na kusema, “Victoria,
tazama, unaweza kuona mji ule?”
Nilipotazama, niliona jiji kubwa
sana. Lilikuwa zuri kuliko maelezo. Jiji lile lilikuwa na geti la dhahabu
inayong’aa, na kwenye geti lile kulikuwa na mwanamume amekaa, mwenye umri
mkubwa. Alikuwa na ndevu ndefu nyeupe na nywele nyeupe. Nilishamwona mwanamume
huyo kabla; na nilipomwuliza Yesu kuwa mwanamume yule ni nani, aliniambia kuwa alikuwa ni Ibrahimu, baba wa imani.
Niliona barabara nyingi kwenye
mji ule, ambazo nazo ni za dhahabu. Kuna majengo marefu, ambayo nayo yalikuwa
ya dhahabu inayong’aa. Mng’ao wa mji ule hata hauelezeki!
Yesu alinigeukia na kuniuliza,
“Unawaza nini
juu ya jiji lile?”
Nilimjibu kuwa lilikuwa ni
zuri sana na nilikuwa natamani kwenda pale. Yesu alisema: “Nitakupeleka pale kama ukiendelea
kuwa mtii maana hapo pia ndiko nyumba yako itakakokuwako. Uendelee tu kuwa mtii
– maana ukikosa utii, Victoria, kunguru wataruka kwenye nyumba yako. Nyumba
yako itakuwa makao ya bundi na viwanja vya kuchezea vya mizimu. Hata hivyo,
usiogope, maana mimi niko pamoja nawe. Wewe uwe mtii tu. Kwa kila mmoja ambaye
si mtii, nyumba yake itakuwa na kunguru wakiruka pale; itakuwa ni makao ya
bundi na mahali pa mizimu pa kuchezea.”
Yesu ni halisi na anatupenda kwa pendo lisiloweza
kuelezeka. Shauku yake kubwa ni sisi tuchague uzima na kuishi milele naye. Moyo
wake unauma kwa ajili ya wale watu ambao wanakufa na kuenda kuzimu kwa vile tu
wanachagua kukataa Wokovu aliowapa na badala yake wanachagua mauti.
Uwe ni Mkristo uliyeokoka au la, tafadhali siku zote
kumbuka jambo hili: Muda unakimbia haraka!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni