UJUMBE: MIKATABA INAYOTOKANA NA KAFARA Tar. 2.9.2012
Na Mchungaji Kiongozi Josephat
Gwajima
Utangulizi:
Wakristo
wengi huwa hawazungumzii neno kafara kwasababu wanahisi kuwa ni la waganga wa
kienyeji, lakini hili neno limeandikwa kwenye biblia mara nyingi sana. Hii ni kuonyesha
kuwa wapo watu wanatoa kafara.
KAFARA KWENYE BIBLIA:
Baada
ya Yoshua na wana wa Israeli kuangusha ukuta wa Yeriko, Yoshua aliweka agano
kuwa atakayeamua kujenga ukuta ataanza kwa kufiwa na mwanawe wa kwanza na
akasema akimaliza atafiwa na mwanae wa pili. Yoshua 6:20-27. Lakini miaka mingi baadaye mtu mmoja akatoa kafara
ya wanawe ili aweze kujenga ngome ya Yeriko kwa upya, Kumbe kafara yaweza
kutolewa kwa ajili ya kujenga kitu duniani. Imeandikwa katika 1Wafalme
16:38.
2Wafalme 3:20-27, Hapa tunaona habari ya Huyu Mfalme ambaye baada ya
kuona anashindwa vita dhidi ya wana wa Israeli, akaamua kumtoa kafara mwanaye
na hilo jambo
likawa hasira juu ya Israeli na kashinda vita. Kumbe kafara inaweza ikamwezesha
mtu kushinda vita. Ukisoma maandiko haya kwa haraka hutoweza kuelewa lakini
ukikaa ukatafakari utaona kuna jambo la muhimu
sana
hapo.
Kafara
ya mtu kwenye biblia; 2Wafalme17:17,“Wakawapitisha
watoto wao, waume na wake, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza
nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, hata kumkasirisha” kumpitisha mtoto motoni ni kumchoma moto kama kafara
yaani ukisoma biblia ya kingereza inatumia neno “sacrifices “ Ezekieli 16:20-21, kumbe jambo la
kafara lipo kwenye biblia,na hapa Ezekieli anasema wakawatoa kafara wanao kuwa
chakula; na pia neno hili limeoneka na pia katika kitabu cha Ezekieli 20:31-32.
KWELI KUHUSU KAFARA:
Mtoto
au mtu akitolewa kafara anakuwa ameuwawa Mwili na kupewa majini au mashetani,
katika biblia shetani anayehusika na mambo ya kafara, Mambo ya Walawi 18:21; ukisoma biblia ya Kiswahili unaweza
ukahisi moleki ni mtu lakini tuangalie kwenye biblia ya kingereza “do not give
out your children to be sacrifices..” Mambo
ya Walawi 20:2 “who sacrifices..
kumbe inawezekana unaumwa na upo kwenye ugonjwa kumbe ndio unatolewa
kafara hivyo..
Kumbe
sasa waweza kumwona mtu amekufa na
ugonjwa Fulani kumbe ni kafara, mwingine anatoa kafara kwa ajili ya utajiri. Mambo ya Walawi 20:3, pia tunaona kuwa
kumbe wachawi hawa wanatoa ndugu na si mtu ambaye hamjui. Yaani kama una ndugu
wa karibu au wa mbali ambaye ni mchawi, Yule ndiye anayeweza kukutoa kafara, na
kwenye kitabu cha Mambo ya walawi
shetani aliyekuwa anahusika na kafara aliitwa Moleki. Walawi 20:4,5 2Wafalme
20:10
Hayo
maandiko ni ya agano la kale lakini pia katika agano jipya jambo hili limetajwa
pia; 2Wakorintho 10:20 “.”
KWANINI WATU WANATOA KAFARA:
Ukiangalia
habari ya Nuhu baada ya kutoka kwenye safina nuhu alimtolea Mungu sadaka na ile
harufu ilipofika kwa Mungu; akasema hatailaani nchi tena kumbe ile harufu ina
maana sana
kwenye ulimwengu wa roho; vivyo hivyo wanapo mtolea shetani kafara wanalenga
kumpa ile harufu na ile harufu inamfanya shetani awa tekelezee wanayohitaji.
Mtu anamtoa mwanawe ili kuwapa kafara mashetani, wamtekelezee anacho hitaji kama utajiri n.k.
Mambo ya Walawi 2:12 “Vitu hivyo mtavisongeza kwa Bwana kuwa ni
malimbuko; lakini visifike juu ya madhabahu kuwa ni harufu ya kupendeza.”
Utajiuliza hii harufu na sadaka; hapa ni kafara inayotolewa kwa mashetani. Mambo ya Walawi 3:15, 16, Hesabu 5:17,
Sadaka ya vinywaji hii ni baadhi ya mila hapa kwetu ni pale mtu anakunywa pombe
alafu anawapulizia watu, hii ndio inaitwa sadaka ya vinywaji inayotolewa. Sasa
hii inapotolewa kwa mashetani kwenye ulimwengu wa roho wanakuja mahali pale. Hesabu 15:10; 17:24; 18:7
KUWA MAKINI
NA KAFARA ZILIZOTOLEWA KWA MASHETANI:
Kumbe shetani anaweza kutolewa kafaraza aina
mbalimbali inaweza kuwa ya vinywaji, uji, nafaka, harufu, watoto au watu
wazima; na ni muhimu kuwa makini sana
na kuhudhuria sherehe ambazo si za ki Mungu kwasababu waweza kujikuta
unashiriki kwenye sadaka hiyo. Kuna watu ambao matatizo yao yamewaanza baada ya kushiriki chakula cha
kafara jambo hili biblia imekataza kwasababu ya madhara yake.
Ufunuo 5:8;
8:3 hapa
biblia inataja sadaka ya harufu, na ndio maana ukienda kwenye maduka mengi
utakuta wameweka vitu vinaitwa ubani; Hii ni sadaka au kafala ya kuteketezwa
kwa majini, Isaya 43:23; Yeremia 6:20;
17:26, Ubani na Udi ni sadaka ya kuteketezwa, kimsingi; ile harufu ndiyo
inayoifanya iitwe sadaka ya kuteketezwa, kwahiyo mtu unayemuona anachoma ubani
ni anakuwa anatoa kafara ya ubani. Nehemia
13:9.. sadaka za unga na sadaka za ubani. Kimsingi watu tuliookolewa
hatutoi sadaka za ubani kwasababu biblia inasema maombi ya watakatifu ndio
sadaka ya harufu kwa Mungu. (Yohana 19:39)
Kumbe unapoona mahali au duka ukakuta wanachoma
udi kimsingi ni kwamba wanaita Mashetani ambayo yanawasaidia kuleta wateja. Na
ndio maana maduka mengi yana kuwa na vitu hivi ambavyo ni kafara au sadaka ya
harufu; ili majini yaite wateja. Na ndio maana watu wengi wenye majini
wanapenda ubani kwasababu kile ndio chakula chao.
KAFARA YA
NCHI:
Kuna uwezekano nchi ikawekewa kafara ili wananchi
wasiongee, yaani kunakuwa na matatizo katika nchi lakini kumbe ni kwasababu ya
kuwaita mashetani ili kufanya wananchi wasidai haki yao. Na ndio maana kuna vitu ambavyo
vinapitishwa kwenye nchi ambavyo kwa hakika ni kafara ya harufu kwa shetani.
Mambo kama mwenge unaopita ni sadaka kwa mashetani kwa ajili ya nchi, kama
unahitaji kujua ukweli wa jambo hili muombe Mungu akuonyeshe; katika ulimwengu
wa roho, utajua wazi kuwa ni kafara kabisa kwa ajili ya nchi nzima.
Biblia iko wazi kuhusu kafara inayotolewa kwa
ajili ya nchi; Katika biblia Kumbukumbu La
Torati 32:43 “Furahini, enyi mataifa, pamoja na
watu wake; Kwa maana atatwaa kisasi kwa damu ya watumwa wake, Atawatoza kisasi
adui zake, Tena atafanya kafara kwa nchi
yake, na watu wake.” Kumbe kuna uwezakano wa nchi kutolewa kafara yaani
mtu anatoa sadaka ili kuita mashetani kwenye nchi. Ni muhimu unapokuwa unaomba
uwe unavunja na kusambaratisha kafara zilizo tolewa katika nchi. Nchi ya Tanzania
inatakiwa ikombolewe kutoka kwenye kafala.
NGUVU YA
KAFARA:
Unaweza ukajiuliza kafara inafanyaje kazi; kimsingi;
sadaka au kafara ya vinywaji, damu au vyote tulivyoona ni chakula cha
mashetani. Na kimsingi mashetani yapo katika ngazi mbalimbali kuanzia majoka
mpaka kwenye majini majini madogo; kwahiyo wachawi au washirikina huita
mashetani kulingana na ukubwa wa kafara kama
ikitolewa kafara ya kuku anakuja shetani wa ngazi ndogo. Na ikitolewa kafara
kubwa kama ya mtu inaliita shetani la ngazi ya juu sana. Hivyo kama mtu hajaokoka ni rahisi
kutolewa kafara kwasababu anakuwa hana ulinzi wa Mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni