Jumatano, 30 Oktoba 2013

VIFUNGO VYA MWILINI



Saturday, September 7, 2013

VIFUNGO VYA MWILINI

                                       
Na Mch. Josephat Gwajima                                              
Utangulizi:
Mungu anawapenda sana wanadamu na Biblia inasema wazi kuhusu hili katika kitabu cha Maombolezo 3:31; Ni raha yake kuona hatuna matatizo na tunaishi kwa amani. Mungu hakumuumba mwanadamu ateseke bali alimuumba afanikiwe akiwa duniani na kuishi kwa furaha.

Wakati huohuo, shetani kwa asili hapendi mtu aliyeumbwa na Mungu afanikiwe na ndio maana katika Luka 3:16 inasema, “…ambaye shetani amemfunga miaka kumi na minane…” (Matendo 10:38; 2Wathesalonike 2:18-19) kwa maandiko hayo tunaweza kujua kuwa shetani anaweza kufunga, kuzuia, kupinga na kushindana na mtu. Kwa asili shetani ni mshindani na furaha yake ni kuwatesa wanadamu ambao wanapendwa na Mungu. Yeye hufanya hivi ili kuumiza moyo wa Mungu kupitia wanadamu walioumbwa na Mungu.

SHETANI ANAWEZA KUMFUNGA MTU:
Kama tulivyoona kuwa shetani anapenda kuwatesa wanadamu na ili kutimiza lengo lake njia mojawapo anayotumia ni kuwafunga watu. Na tunapotaja vifungo, tunakuwa tunazungumzia vifungo vya aina kuu tatu, yaani, Vifungo vya mwilini, Vifungo vya rohoni na vifungo vya nafsini kwasababu mtu ni roho inayokaa ndani ya nyumba iitwayo mwili. Katika hatua hii ya kwanza tunaanza kuangalia kwa undani kuhusu vifungo vya mwilini:-

Mwili ni nini?
Hatuwezi kujua namna mwili unavyoweza kufungwa bila kujua asili ya mwili wa binadamu. Tuanze kwa kuangalia andiko hili Mwanzo 2:7 “BWANA Mungu akamfanya mtu kutoka katika mavumbi ya ardhi…” kumbe asili ya mwili wa mwanadamu ni mavumbi au udongo. Na ndio maana katika Isaya 64:8 Biblia inasema, “… sisi tu udongo nawe ni mfinyanzi wetu...” nabii Isaya ambaye aliwahi kumuona Mungu lakini alijua ukweli huu kuwa mwili ni mavumbi (Ayubu 7:21, 34:15). Kumbe pamoja na kuwa umevaa vizuri au umeupamba mwili vizuri lakini asili yake ni udongo na katika ulimwengu wa roho huonekana kuwa ni udongo kabisa. Kwa ufupi mwili wa mwanadamu ni udongo na mtu anapokufa mwili huirudia nchi (Mhubiri 12:7) yaani mavumbi.

Ndio maana hata watu wanapooana ni miili ndio ambayo inakuwa imeoana na si roho kwasababu mbinguni hakuna kuoa wala kuoana kule ni katika roho. Kwa kujua kuwa mwili ni udongo basi namna ambayo unaweza kuutendea udongo wa kawaida ndivyo vilevile waweza kuutendea mwili wa binadamu. Udongo wa ardhini waweza kuoteshwa mimea na kuchimbwa, vilevile na mwili wa binadamu waweza kufanyiwa hivyo.

TOFAUTI KATI YA MWILI NA UDONGO WA KAWAIDA:

Kuna mambo mawili makuu yanayosababisha mwili wa binadamu uwe tofauti na udongo wa kawaida.

1. Mwili uliwahi kushikwa na mikono ya Mungu maana hakuna kitu kilichowahi kushikwa na Mungu na kikabaki kama kilivyo.

2. Ndani ya mwili wa mwanadamu kuna roho ambayo huuisha mwili na kuupa uhai. Kwasababu hizo mwili wa mwanadamu hutofautina na udongo wa kawaida.

MWILI WA MWANADAMU UNAWEZA KUPANDIWA VITU:
Biblia iko wazi kuwa Mungu wa mbinguni anaweza kupanda, (Mwanzo 2:8); kumbe Mungu ambaye ni roho (Yohana 4:24) anaweza kupanda katika ardhi kabisa vivyo hivyo shetani naye ni roho naye ana uwezo wa kupanda katika mwili ambao kwa asili ni udongo. Hapa ndipo lile andiko la “KILA PANDO AMBALO BABA WA MBINGUNI HAKULIPANDA LITANG’OLEWA” linapoleta maana; Mapando ambayo hayajapandwa na Baba wa mbinguni ni lazima yatakuwa yamepandwa na shetani. Ndio maana ya mfano wa Yesu katika Mathayo 13:25 “lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.” Huyo ambaye Yesu anamwita adui ni shetani mwenyewe. Kumbe unapolala au kujisahau shetani huja na kupanda magugu, hili jambo linatendeka katika ulimwengu wa roho. Ni muhimu kujua siri hii kwamba kama vile udongo unavyopandwa vivyohivyo shetani naye anao uwezo wa kupanda juu ya mwili wa mwanadamu.

Unaweza kumsikia mtu analalamika kuwa mwili unachoma lakini kumbe katika ulimwengu wa roho mtu huyo amechomwa mkuki au kisu.  Kufikia hapa sasa twaweza kujua kwanini Mungu alikataza kupanda mbegu mbili za tofauti katika shamba moja (Mambo ya Walawi 19:19). Mungu alisema hivi akitufundisha kuwa mahali ambapo Mungu amepanda shetani hatakiwi kupanda mahali pale. Mtu anaweza kuhisi vitu vinatembea mwilini kumbe amepandiwa wanyama wanaotembea katika mwili wake.

PEPO ANAWEZA KUJIGEUZA NA KUWA CHOCHOTE:
Tulijifunza kuhusu sheria mbili za rohoni, hapo tuliona uwezo wa pepo wachafu kujigeuza na kuwa kitu kingine yaani kuvaa sura mbali mbali ili kutimiza kazi zao. Jambo hili twaweza kuliona katika (1Wafalme 22:19-23) huyu pepo kwa asili hakuwa wa uongo lakini aliweza akaenda na akawa pepo wa uongo. Yule pepo akaingia katika vinywa vya manabii wa Mfalme Ahabu na kuwafanya wamtabirie uongo. Kwa maana hiyo tunaona uwezekano wa pepo mchafu kujigeuza na kuwa kitu chochote ili kutimiza lengo alilokusudia.

Sasa twaweza jua kuwa mapando tuliyokuwa tunayazungumzia ni pepo wachafu ambao hujigeuza na kuwa kile kitu na hivi ndivyo vinavyoitwa “Vifungo vya mwilini”. Wakati mwingine pepo anaweza kujigeuza na kuwa kinywa cha mtu, kama pepo wa katika (1wafalme 22:19-23) alivyofanya. Hivyo; unaweza kumuona mtu anatukana matusi ya ajabu bila hata aibu, kumbe pepo kajigeuza na kuwa kinywa chake. Pepo anaweza kuwa uso wa simba, unamkuta baba mwenye nyumba mkali kwa watoto na mkewe kumbe ni uso wa simba. Kwahiyo; pepo wanaweza kujigeuza maumbo mbalimbali kama nyani, simba, paka hata bundi ili mradi kuharibu hatma ya mtu. Mnamkuta dada aolewi kumbe uso wake umefunikwa kwa sura ya simba, kila mwanaume anayetaka kumchumbia haoni sura nzuri bali anaona simba. Na ndio maana kuna baadhi ya wadada watumia muda mwingi kujipodoa lakini bado hawapendezi kwa kuwa uso sio wa kwake.

KUNG’OA KILA KILICHOPANDWA KATIKA MWILI WAKO:
Imeandikwa kila pando asilolipanda Baba wa mbinguni litang’olewa, hivyo Mungu ametupa mamlaka ya kung’oa kila pando la kishetani yaliyopandwa katika mwili. Miili yetu ni Hekalu la Roho Mtakatifu hivyo shetani hatakiwi kugusa sehemu yoyote ya mwili wako.

Tumia mamlaka yako kung’oa kila pando ambalo shetani amepanda katika maisha yako mapando ya magonjwa, homa zisizoisha, ukimwi, mwasho wa mwili na matatizo mbalimbali. Jina la Yesu lina mamlaka yote dhidi ya kazi zote za shetani katika maisha yako. 

ROBO YA WATU DAR NI MISUKULE



ROBO YA WATU DAR NI MISUKULE-12

ALINIPA bakuli akiniashiria nile lakini yeye akawa amesimama pale pale pembeni ya muuzaji akisubiri chombo hicho ili aondoke nacho. Nilikaa chini na kula kama nilivyoelekezwa. Muda wote wa kufanya hivyo, wateja walipungua na kutoingia dukani.

Hapa nataka kusema jambo moja ambalo mtalielewa kwani ni la kawaida sana na hutokea kwenye jamii yetu. Mara nyingi, muda wa mchana, biashara hazichanganyi sana, uongo kweli?
Unaijua sababu   SASA ENDELEA…

Naamini wengi mtajibu ni kweli. Sababu kubwa ni kwamba, biashara nyingi duniani zinaendeshwa kwa imani za kishirikina. Naweza kusema katika kila biashara mia moja, sitini na tano zinategemea ushirikina.

Ushirikina mwingi ni ule wa kuwepo kwa vitu, hasa misukule kwa ajili ya kuvuta wateja kwenye biashara hizo. Sasa kinachofanyika ni kwamba, hii misukule kazi yao kubwa ni kuita wateja kwa ishara kama niliyoisema.

Kazi hii hufanywa kwa muda mrefu kuanzia asubuhi hadi saa sita mchana ambapo hupumzika kula. Sasa katika kipindi hiki cha mlo, kwa sababu misukule huacha kuita, wateja nao hupunguza kasi ya kuingia kwenye maduka.
Hii hutokea hata kwenye maduka ya mtaani ambayo, wamiliki wake wanatumia misukule, ikifika wakati wa kula, utaona wateja ni wachache sana, hata wateja wenyewe kama wapo majumbani mwao hujisikia uvivu kutoka kwenda dukani.

Mara nyingi baada ya mlo hufuatiwa na mapumziko mafupi, lakini baada ya hapo shughuli uendelea. Ndiyo maana kuanzia saa nane na kuendelea biashara huchanganya tena kwa vile misukule mingi huwa imesimama ikiita wateja.
Sasa hili zoezi lina kitu kimoja cha ajabu, wamiliki ndiyo wanaojua kwamba yupo na msukule anayeitia wateja, lakini kuna wauzaji ambao huwa hawajui kama anauza akisaidiwa na misukule.

Ila kwa wale wauzaji ambao watataka kujua kuwa ndani ya duka analofanyia kazi kuna misukule atatakiwa kuangalia dalili hizi.
Mara nyingi akiwa ndani ya duka atakuwa anahisi kama kuna mtu anatembea, akishtuka anakuta hali ya utulivu.
Wakati mwingine akiwa amekaa atahisi damu zikimsisimka mwilini na nywele zikichachamaa. Hapo ina maana msukule umemfuata na kusimama nyuma yake kisha unamdhihaki kwa kumng’ong’a.

Akitoka kwenda chooni, akirudi na kuchunguza sana ndani ya duka ataona kuna mabadiliko. Lakini haya mabadiliko yanata kutumia akili sana kuyabaini. Mara nyingi mabadiliko haya ni mfano, gazeti liliwekwa likiwa limekunjwa ukurasa wa kwanza upo kwa ndani, lakini litakutwa ukurasa wa mwisho ndiyo uko kwa ndani wa kwanza upo nje.

Ndani ya duka ikipulizwa pafyumu ya aina yoyote, hata uchomwe udi, harufu yake haikai hata dakika tano. Wengi wamekuwa wakiamini pafyumu hiyo si nzuri lakini ukweli ni kwamba ni kwa sababu ya misukule. Wao humaliza harufu yoyote nzuri kwa uwepo wao tu.   

Uzuri ni kwamba, misukule inayowekwa ndani ya maduka hushindwa kuzuia kuibwa kwa fedha, mfano mmiliki wa duka amemwajiri kijana kuuza, halafu kijana huyo akawa anaiba fedha za mauzo, msukule hata ukiona, hautakuwa na uwezo wa kuzuia wizi huo.
Basi, nilipomaliza kula nilimpa bakuli yule aliyeniletea chakula, akapokea kisha akaondoka huku akimng’ong’a yule muuzaji ambaye naye hakuwa na hili wala lile.

Niliokota kipande cha karatasi nikajifuta mikono kisha nikakiachia, kikaanguka chini. Yule muuzaje alishtuka kwa karatasi hiyo kuanguka lakini hakufanya kitu, akaangalia juu kwenye feni akaamini ndilo lilisababisha kuanguka kwa karatasi hiyo lakini hakutaka kujua ilianguka kutokea wapi.

Nilikwenda kukaa pembeni kidogo jirani na mlango wa uani ili nipumzike kabla ya kuanza tena kazi ya kuita wateja.
Baada ya muda nilisimama, nikaanza tena kuita kwa staili ile ile ya kuinua mikono na kufanya ishara ya kuita ambayo kila mmoja wenu anaijua.

Nilifanya shughuli hiyo hadi saa kumi na mbili jioni alipokuja yule mzee kunichukua. Huyu mzee nilivyomjua alikuwa wakala, yaani kazi yake kubwa ni kuwatawanya misukule kwa wenye maduka wanaohitaji kwa malipo maalum ya fedha za kawaida. Hii ipo hata sasa, wapo wamiliki wa maduka ambao hawana misukule, kwa hiyo wanatafuta watu wanaomiliki misukule na kuongea nao kisha wakishapatana ndiyo inakuwa kama vile.

Hata hivyo, mmiliki wa duka anatakiwa aue mtu wake wa karibu ndiyo awe msukule, hii huleta faida kubwa kama una biashara kuliko kutumia misukule ya kukodi.
Kisheria, namaanisha mfumo wa kuua mtu wa karibu ili awe msukule, inatakiwa unayemuua awe yule aliyekukaa sana moyoni. Kama ni watoto, unatakiwa uchague unayempenda kuliko wote, ama mke, mume, baba au mama.

Basi, nje ya duka nilikuta misukule wengine kama tisa, wakiwemo ambao tuko wote kule kambini. Mnaweza kujiuliza nilijuaje wale ni misukule baada tu ya kutoka kwenye duka. Ni kwamba, hakuna msukule unaovaa nguo tofauti na shuka jeupe kwa kujifunga lubega. Pia, mashuka hayo huwa machafu sana kwa mwonekano.

Kingine, misukule ni myeusi kutokana na kuishi katika mazingira machafu, kutopaka mafuta na kutegemea uji ambao ni mchanganyiko wa unga na maji tu bila kupitia jikoni.
Nywele za misukule lazima ziwe ndefu na za kujisokota kwa sababu baada ya kuoga hakuna kuchana, unadhani hapo nini kitafuata?

Basi, tuliondoka wote, lakini si kwenda moja kwa moja kambini, kwani yule mzee aliwapitia misukule wengine ambao nao aliwatawanya katika maduka mbalimbali.

Kuna sehemu tulipita nikamwona mzee mmoja jirani na nyumbani kwangu, anaitwa Masakila, nikawaambia wenzangu kwa ishara kwamba namjua yule, wakakataa, nikaminya vidole viwili vya mkono wa kulia kisha nikavibetua, vikalia taa...

ROBO YA WATU DAR NI MISUKULE -13

NYWELE za misukule lazima ziwe ndefu na za kujisokota kwa sababu baada ya kuoga hakuna kuchana, unadhani hapo nini kitafuata?
Basi, tuliondoka wote, lakini sikwenda moja kwa moja kambini, kwani yule mzee aliwapitia misukule wengine ambao nao awali aliwatawanya katika maduka mbalimbali.

Kuna sehemu tulipita nikamwona mzee mmoja jirani na nyumbani kwangu, anaitwa Masakila, nikawaambia wenzangu kwa ishara kwamba namjua yule, wakakataa, nikaminya vidole viwili vya mkono wa kulia kisha nikavibetua, vikalia taa...   
SASA ENDELEA…

Mzee Masakila alishtuka na kugeuka kuangalia tulipokuwa tumesimama. Kule kugeuka nikawaambia wenzangu mmeona kwa ishara ya mikono. Wakaamini.

Tulitoka eneo lile na kwenda kuwapitia misukule wengine waliokuwa sehemu mbalimbali za katikati ya jiji. Si rahisi kuamini kuwa, wapo misukule waliokuwa kando  ya Bahari ya Hindi maeneo ya Posta ya zamani wakifanya shughuli mbalimbali za kijamii. Walipochukuliwa wote,   tulirudishwa kwenye maskani yetu.

Hapa nataka kusema kwamba, katikati ya jiji kuna misukule wengi ambao wapo kwa ajili ya kufanya kazi za watu, hasa biashara ndogo ndogo kama kuuza maji, juisi, vocha na pipi ambazo ni za kubeba mkononi.
Unaweza ukawa umeshanunua bidhaa kwa hawa misukule lakini bila kujijua. Ila kwa ishara ambazo ziko hapa utajua kuwa siku moja uliwahi kumuungisha msukule.

Ukiachilia mbali na ile dalili ya misukule wanaouza kahawa, hawa wana ishara au dalili nyingine kabisa. Ukiwa kwa miguu au kwenye basi, huja mpaka dirishani na kukukimbizia boksi lenye bidhaa, lakini sasa kama umewahi kuona kwa mwenzako au wewe mwenyewe kushuhudia unanunua kitu, halafu ukisharudishiwa chenji mbele ya safari unakuwa hujui ilipo, ujue ulifanya biashara na msukule.

Pia, misukule hawa wana tabia ya kuonesha ufundi mkubwa wawapo kazini kwani linaweza kuja gari nyuma kwa mwendo kasi, ukajua anagongwa, lakini atakavyolikwepa wewe mwenyewe hutaamini.

Kifupi wawapo kazini wamekuwa ni wa kupitia au kuashiria ajali ajali tu, mara waruke na kukwepa pikipiki, mara wapigiwe honi na madereva wanaokimbiza magari, lakini cha ajabu sasa, hakuna dereva atakayewapigia honi kisha akachanganya na kutukana matusi kama watu wengine wa kawaida.

Basi, usiku wa siku hiyo ulikuwa wa kipekee kwani tukiwa tumelala, alikuja mwanaume mmoja na kutuamsha, kisha akasema kuwa kila aliye na kucha hatakiwi kuzikata kwani imebainika kwamba wapo wanaokata kucha kwa kutumia meno.
Kumbe bwana, kila mtu duniani ana kazi yake na ujuzi wa kitu anachokijua yeye. Ni kwamba, misukule huwa haitakiwi kuwa na kucha fupi kwani zinawapa uwezo na ujuaji.

Yaani, msukule unapokuwa na kucha fupi unaweza kutoroka kutoka kwa bosi wake au bosi wake anaweza kukosa uwezo wa kumkontroo. Ndiyo maana sifa kubwa ya msukule ni kuwa na kucha ndefu sana zinazokaribia njiti ya kiberiti.

Basi, yule mtu akatutaka wote tusimame ili kukaguliwa kila mkono na kucha zake. Mimi nilibahatika kwani licha ya kutokatwa ulimi, lakini pia kucha zangu sikuwahi kuzikata iwe kwa meno au kwa njia nyingine yoyote.
Sasa nikawa najiuliza, wale watakaokutwa na kucha fupi kwamba wamezikata  watachukuliwa hatua gani? Nikasema moyoni ngoja nitaona hapo hapo.

Baada ya ukaguzi kumkuta msukule wa saba, wa nane akabainika amekuwa akikata kucha kwa meno, akachukuliwa na kupelekwa mahali pengine. Mpaka zoezi linakwisha, misukule waliobainika kukata kucha walikuwa wanne.
Wote walipelekwa kwenye chumba kimoja lakini hatukujua walichotendewa huko zaidi ya sisi kuamriwa tulale ili tuwahi kuamka eti kuna safari ya kwenda Kariakoo.

***
Ilikuwa asubuhi ya saa mbili na nusu ndipo tulipoanza safari ya kwenda Kariakoo, mkuu wa msafara wetu alikuwa mbele kama kawaida huku kila wakati akisimama pembeni na kuangalia usalama wetu.

Kabla sijaendelea mbele ya safari niseme ambalo sikuwahi kulifanyia kazi hata siku moja. Mpaka leo sijajua kama ni mimi tu au hata misukule wenzangu, ni kwamba nilikuwa nawaza nyumbani kwangu kama kawaida, namuwaza mke wangu, namuwaza mwanangu.

Lakini linapofika suala la hisia za kimapenzi, sikuwa nazo hata chembe. Nadhani ni eneo ambalo wachukuaji wa misukule hukimbilia kulifanyia kazi kwa sababu za kuogopa mimba maana tulikuwa wanawake kwa wanaume na kama si kuidhibiti hali hiyo kuna watoto wangekuwa wanazaliwa na misukule, sijui ingekuwa vipi maana kwenye maskani tulikuwa tunalala bila kujali mwanamke wapi, mwanaume wapi.

Kariakoo tulifikia kwenye kituo cha mafuta cha Msimbazi, tulisimama kwa dakika kumi na mkuu wetu, kwenye saa tatu akaja mzee mmoja wa Kiarabu akaongea na mkuu wetu kisha akaja kutuangalia sisi kama anayetukagua ili kujua tunaweza kukifanya alichotuitia au la!

“Lakini hawa ni wengi, mimi nataka nusu yake,” alisema yule Mwarabu. Pale tulikuwa kama kumi na tano.
“Sasa wengine nitawapeleka wapi muda huu, wenzao wengine kule wameshapangiwa majukumu,” alisema mkuu wetu.

ROBO YA WATU DAR NI MISUKULE-16

Mimi nilikimbia mpaka kwenye jengo moja ambalo nje kuna bustani kubwa, lakini hapaishi watu. Pembeni ya bustani palikuwa na bomba la maji, nikaenda kukaa pembeni ya bomba hilo huku nikihema kwa kasi.   
ENDELEA SASA…
Mara, mzee mmoja alikuja na kunikuta pale, akashtuka kwa hali niliyokuwa nayo na kuniuliza kulikoni?
Nilimsimulia kila kitu, nikamwambia ilivyotokea hadi kifo changu na maisha yangu nikiwa katika misukule.
Yule mzee alinichukua, akanipeleka kwake huku njiani akiwaambia watu mimi ni mgonjwa ameniokota, wengine walimpa pole.
Nilikaa kwa yule mzee kwa muda wa siku tatu, akaninunulia nguo, akanipeleka hospitali, siku hiyo ya tatu akanipandisha boti kurudi Dar huku akiniambia nimshukuru Mungu kwa bahati niliyoipata ya kuishi katikati ya misukule huku nikiwa sijakatwa ulimi kwani ningekatwa nisingekuwa na uwezo wa kuonekana kirahisi na kurudi duniani.

Nilitua Bandari ya Dar es Salaam saa kumi na mbili na nusu jioni. Nakumbuka ilikuwa siku ya Alhamisi. Nikapanda daladala hadi nyumbani kwangu ambapo wakati kigizagiza kinaingia, nikasimama nje ya mlango na kubisha hodi, akaja mke wangu.
Kwanza alianguka na kupoteza fahamu, ikabidi nimbebe hadi chumbani ambako nilimuweka kwenye kitanda na kuanza kumpepea. Alipopata fahamu, akataka kupiga kelele, nikamshika na kumzuia.

Nilimweleza kwa upole hali ilivyonitokea mwanzo mwisho na jinsi nilivyookotwa Zanzibar baada ya mkuu wa misukule kushtukia maisha yangu ya kuwa na wao bila kukatwa ulimi.
Awali mke wangu alionesha dalili ya kutoniamini, akaniomba akamwite mjumbe. Mjumbe alikuja akiwa ameongoza na wazee watatu na vijana wanne, walionesha dalili za kuja kwenye shari.
Waliniuliza maswali mengi na kwa muda mrefu hadi wakaanza kukubaliana na mimi. Lakini mjumbe akamuuliza mke wangu:
“Wewe mama si ulisema tangu kifo cha mumeo ulikuwa unahangaika kwa waganga ili mumeo arudi?”
Mke wangu akamjibu ndiyo mzee. Mjumbe akamuuuliza:
“Sasa ulitaka arudi kwa njia gani?”
Mke wangu akaja kunikumbatia, wale watu wakakaa sana na mimi wakiniuliza mambo mbalimbali kuhusu misukule,  mwisho wake waliondoka wakisema watarudi asubuhi.

Huo ndiyo mwisho wa maisha ya mimi kuwa msukule, bahati yangu ilikuwa moja tu, kutokatwa ulimi, basi.


HATARI YA KUSAHAU



Tuesday, July 30, 2013

HATARI YA KUSAHAU

Na Mch. Josephat Gwajima | SNP


Mungu katika Neno lake Mara nyingi anawaambia watu wake wakumbuke. Kuna uwezekano wa kusahau mambo ya nyuma na kuna hatari kubwa kusahau mambo fulani. Wana wa Israel walipokuwa wanatoka utumwani wakiwa njiani kuelekea nchi ya ahadi, Mungu alikuwa akiwalisha mana na baadae walipofika kwenye nchi ya Kanani. Mungu aliwambia watunze mana kwa ajili ya ukumbusho jinsi Mungu alivyowalisha jangwani. Kuna nguvu inayotokana na kukumbuka mambo makuu alikuyotendea Mungu.

KUMBUKUMBU LA TORATI 32:7
Kumbuka siku za kale, Tafakari miaka ya vizazi vingi; Mwulize baba yako, naye atakuonyesha; Wazee wako, nao watakuambia.

KUMBUKUMBU LA TORATI 7:18
19
Usiwaogope; kumbuka sana Bwana, Mungu wako, alivyomfanya Farao na Misri yote; uyakumbuke hayo majaribu makuu yaliyoyaona macho yako, na hizo ishara, na maajabu, na mkono wa nguvu, na mkono ulionyoka, aliokutolea nje Bwana, Mungu wako; ndivyo atakavyowafanya Bwana, Mungu wako, mataifa yote unaowaogopa.

KUMBUKUMBU LA TORATI 15:15
Nawe kumbuka kwamba ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, akakukomboa Bwana, Mungu wako; kwa hiyo mimi nakuamuru neno hili hivi leo.
Dhambi nyingi za watu hutokana na kusahau mambo waliyotendewa na Mungu. Na maranyingi Mafanikio katika maisha humfanya mtu asahau alikotoka. "Mafanikio yako ya leo ni adui wa kwanza wa mafanikio yako ya kesho"

KUMBUKUMBU LA TORATI 32:15
Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake. Mafanikio yaweza kukufanya usahau ulipotoka.

LUKA 16:25
Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.

Yesu anataka tukumbuke alivyojitoa na kufa kwa ajili yetu.

1kor 11:23-25

HATARI 15 ZA KUSAHAU

1. Mtu anayesahau ni dhalimu. Mungu si dhalimu maana hasahau kazi yetu.

WAEBRANIA 6:10
Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia.

Mungu anathibitisha kuwa wanadamu wanaweza kusahau hata mambo yanayoonekana.

JEREMIAH 2:32
Je! Mwanamwali aweza kusahau mapambo yake, au bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wangu wamenisahau mimi kwa muda wa siku zisizo na hesabu.

2. Wanaomsahau Mungu mwisho wao ni kunyauka na kuangamia - laana ya kunyauka

AYUBU 8:11
13
Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matope Na makangaga kumea pasipo maji? Yakiwa yakali mabichi bado, wala hayakukatwa, Hunyauka mbele ya majani mengine. Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu; Na matumaini yake huyo mbaya huangamia;

3. Ukisahau utarudi ulikotoka
Ukishahu kuwa ni dhambi iliyokufanya uishi maisha ya dhiki utatenda dhambi na kurudi ulikotoka.

4. Ukisahau kiburi kinaota - unasahau kuwa huko nyuma ulikuwa dhaifu. Ni muhimu kukumbuka ulikotoka ili umtukuze Bwana. Usahulifu humfanya mtu asikumbuke kuwa ni Mungu ampate nguvu ya kufanikiwa. Kukumbuka huleta unyenyekevu

KUMBUKUMBU LA TORATI 8:12
18
Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake; na makundi yako ya ng'ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka; basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa; aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu, aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako. Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo. Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

5. Kusahau humtia Mungu hasira - Kumb 9:7

KUMBUKUMBU LA TORATI 9:7
Kumbuka, usisahau ulivyomtia Bwana, Mungu wako, kasirani jangwani; tangu siku uliyotoka nchi ya Misri hata mlipofika mahali hapa, mmekuwa na uasi juu ya Bwana

6. Usahulifu huleta kuangamia - Kumb 8:19

KUMBUKUMBU LA TORATI 8:19
Lakini itakuwa, kama ukimsahau Bwana, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawashuhudia leo ya kuwa mtaangamia bila shaka.

7. Zaburi 88:10-12 - ukisahau unapoteza haki zako. Haki yetu inatokana na ahadi za Mungu maishani mwetu

ZABURI 88:10
12
Wafu je! Utawafanyia miujiza? Au waliofariki watasimama na kukuhimidi?Fadhili zako zitasimuliwa kaburini? Au uaminifu wako katika uharibifu?Miujiza yako itajulikana gizani? Au haki yako katika nchi ya usahaulifu?

8. Kumb 15:12-18 - kukumbuka kunaleta shukrani na kuwatendea wema wale katika hali duni ukiyokuwanayo huko nyuma

KUMBUKUMBU LA TORATI 15:12
18
Ikiwa nduguyo, mume wa Kiebrania, au mwanamke wa Kiebrania, akiuzwa kwako, naye amekutumikia miaka sita; basi mwaka wa saba mwache huru aondoke kwako. Nawe utakapomwacha huru aondoke kwako, usimwache aende zake mikono mitupu; umwangalie kwa wema katika kundi lako, na sakafu yako ya nafaka, na kinu chako cha divai; mpe kama alivyokubarikia Bwana, Mungu wako. Nawe kumbuka kwamba ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, akakukomboa Bwana, Mungu wako; kwa hiyo mimi nakuamuru neno hili hivi leo. Hata itakuwa, akikuambia, Siondoki kwako; kwa sababu akupenda wewe na nyumba yako, kwa kuwa yu hali njema kwako; ndipo utwae uma, uupenyeze katika sikio lake uingie katika ubao wa mlango, naye atakuwa mtumishi wako milele. Na kijakazi chako naye mfanye vivyo. Wala usione ugumu, utakapomwacha huru kuondoka kwako; kwani amekutumikia miaka sita kwa ujira mara mbili wa mwajiriwa; na Bwana, Mungu wako, atakubarikia kwa yote utakayofanya.

9. Kumb 4:9 - anayesahau hana la kuwaambia wanawe.

KUMBUKUMBU LA TORATI 4:9
Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;

10. Hosea 4:6 - ukimsahau Mungu yeye pia atasahau uzao wako.

HOSEA 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.

11. Hosea 8:14 - ukisahau Mungu atatuma moto uteketeze ulichokijenga. Unaweza kumsahau Mungu na kujishughulisha na kujenga vitu vingine lakini Mungu atatuma moto kuviharibu

HOSEA 8:14
Maana Israeli amemsahau Muumba wake, naye amejenga nyumba za enzi; na Yuda ameongeza miji yenye maboma; lakini nitapeleka moto juu ya miji yake, nao utaziteketeza ngome zake.

12. Zaburi 9:17 - Kumsahau Mungu kunaweza kumfanya mtu arejee kuzimu.

ZABURI 9:17
Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.

13. Ukikumbuka ulikotoka unajaa shukrani mbele za Mungu.

14. Kukumbuka ni silaha ya kushinda vita iliyo mbele yako -
Daudi alipokumbuka alivyomshinda dubu na simba alipata nguvu ya kumkabili Goliathi na kushinda vita

15. Kukumbuka ulikotoka ni nafasi ya kuudhihirisha utukufu wa Mungu. Unapoyasema mambo ya udhaifu uliyokuwanayo na jinsi mungu alivyokuvusha utukufu wa Mungu huwa dhahiri na Mungu hutukuzwa.


-Mch. Josephat Gwajima | SNP

Ufufuo na Uzima

VIFUNGO VYA MWILINI



Saturday, September 7, 2013

VIFUNGO VYA MWILINI

                                       
Na Mch. Josephat Gwajima                                              
Utangulizi:
Mungu anawapenda sana wanadamu na Biblia inasema wazi kuhusu hili katika kitabu cha Maombolezo 3:31; Ni raha yake kuona hatuna matatizo na tunaishi kwa amani. Mungu hakumuumba mwanadamu ateseke bali alimuumba afanikiwe akiwa duniani na kuishi kwa furaha.

Wakati huohuo, shetani kwa asili hapendi mtu aliyeumbwa na Mungu afanikiwe na ndio maana katika Luka 3:16 inasema, “…ambaye shetani amemfunga miaka kumi na minane…” (Matendo 10:38; 2Wathesalonike 2:18-19) kwa maandiko hayo tunaweza kujua kuwa shetani anaweza kufunga, kuzuia, kupinga na kushindana na mtu. Kwa asili shetani ni mshindani na furaha yake ni kuwatesa wanadamu ambao wanapendwa na Mungu. Yeye hufanya hivi ili kuumiza moyo wa Mungu kupitia wanadamu walioumbwa na Mungu.

SHETANI ANAWEZA KUMFUNGA MTU:
Kama tulivyoona kuwa shetani anapenda kuwatesa wanadamu na ili kutimiza lengo lake njia mojawapo anayotumia ni kuwafunga watu. Na tunapotaja vifungo, tunakuwa tunazungumzia vifungo vya aina kuu tatu, yaani, Vifungo vya mwilini, Vifungo vya rohoni na vifungo vya nafsini kwasababu mtu ni roho inayokaa ndani ya nyumba iitwayo mwili. Katika hatua hii ya kwanza tunaanza kuangalia kwa undani kuhusu vifungo vya mwilini:-

Mwili ni nini?
Hatuwezi kujua namna mwili unavyoweza kufungwa bila kujua asili ya mwili wa binadamu. Tuanze kwa kuangalia andiko hili Mwanzo 2:7 “BWANA Mungu akamfanya mtu kutoka katika mavumbi ya ardhi…” kumbe asili ya mwili wa mwanadamu ni mavumbi au udongo. Na ndio maana katika Isaya 64:8 Biblia inasema, “… sisi tu udongo nawe ni mfinyanzi wetu...” nabii Isaya ambaye aliwahi kumuona Mungu lakini alijua ukweli huu kuwa mwili ni mavumbi (Ayubu 7:21, 34:15). Kumbe pamoja na kuwa umevaa vizuri au umeupamba mwili vizuri lakini asili yake ni udongo na katika ulimwengu wa roho huonekana kuwa ni udongo kabisa. Kwa ufupi mwili wa mwanadamu ni udongo na mtu anapokufa mwili huirudia nchi (Mhubiri 12:7) yaani mavumbi.

Ndio maana hata watu wanapooana ni miili ndio ambayo inakuwa imeoana na si roho kwasababu mbinguni hakuna kuoa wala kuoana kule ni katika roho. Kwa kujua kuwa mwili ni udongo basi namna ambayo unaweza kuutendea udongo wa kawaida ndivyo vilevile waweza kuutendea mwili wa binadamu. Udongo wa ardhini waweza kuoteshwa mimea na kuchimbwa, vilevile na mwili wa binadamu waweza kufanyiwa hivyo.

TOFAUTI KATI YA MWILI NA UDONGO WA KAWAIDA:

Kuna mambo mawili makuu yanayosababisha mwili wa binadamu uwe tofauti na udongo wa kawaida.

1. Mwili uliwahi kushikwa na mikono ya Mungu maana hakuna kitu kilichowahi kushikwa na Mungu na kikabaki kama kilivyo.

2. Ndani ya mwili wa mwanadamu kuna roho ambayo huuisha mwili na kuupa uhai. Kwasababu hizo mwili wa mwanadamu hutofautina na udongo wa kawaida.

MWILI WA MWANADAMU UNAWEZA KUPANDIWA VITU:
Biblia iko wazi kuwa Mungu wa mbinguni anaweza kupanda, (Mwanzo 2:8); kumbe Mungu ambaye ni roho (Yohana 4:24) anaweza kupanda katika ardhi kabisa vivyo hivyo shetani naye ni roho naye ana uwezo wa kupanda katika mwili ambao kwa asili ni udongo. Hapa ndipo lile andiko la “KILA PANDO AMBALO BABA WA MBINGUNI HAKULIPANDA LITANG’OLEWA” linapoleta maana; Mapando ambayo hayajapandwa na Baba wa mbinguni ni lazima yatakuwa yamepandwa na shetani. Ndio maana ya mfano wa Yesu katika Mathayo 13:25 “lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.” Huyo ambaye Yesu anamwita adui ni shetani mwenyewe. Kumbe unapolala au kujisahau shetani huja na kupanda magugu, hili jambo linatendeka katika ulimwengu wa roho. Ni muhimu kujua siri hii kwamba kama vile udongo unavyopandwa vivyohivyo shetani naye anao uwezo wa kupanda juu ya mwili wa mwanadamu.

Unaweza kumsikia mtu analalamika kuwa mwili unachoma lakini kumbe katika ulimwengu wa roho mtu huyo amechomwa mkuki au kisu.  Kufikia hapa sasa twaweza kujua kwanini Mungu alikataza kupanda mbegu mbili za tofauti katika shamba moja (Mambo ya Walawi 19:19). Mungu alisema hivi akitufundisha kuwa mahali ambapo Mungu amepanda shetani hatakiwi kupanda mahali pale. Mtu anaweza kuhisi vitu vinatembea mwilini kumbe amepandiwa wanyama wanaotembea katika mwili wake.

PEPO ANAWEZA KUJIGEUZA NA KUWA CHOCHOTE:
Tulijifunza kuhusu sheria mbili za rohoni, hapo tuliona uwezo wa pepo wachafu kujigeuza na kuwa kitu kingine yaani kuvaa sura mbali mbali ili kutimiza kazi zao. Jambo hili twaweza kuliona katika (1Wafalme 22:19-23) huyu pepo kwa asili hakuwa wa uongo lakini aliweza akaenda na akawa pepo wa uongo. Yule pepo akaingia katika vinywa vya manabii wa Mfalme Ahabu na kuwafanya wamtabirie uongo. Kwa maana hiyo tunaona uwezekano wa pepo mchafu kujigeuza na kuwa kitu chochote ili kutimiza lengo alilokusudia.

Sasa twaweza jua kuwa mapando tuliyokuwa tunayazungumzia ni pepo wachafu ambao hujigeuza na kuwa kile kitu na hivi ndivyo vinavyoitwa “Vifungo vya mwilini”. Wakati mwingine pepo anaweza kujigeuza na kuwa kinywa cha mtu, kama pepo wa katika (1wafalme 22:19-23) alivyofanya. Hivyo; unaweza kumuona mtu anatukana matusi ya ajabu bila hata aibu, kumbe pepo kajigeuza na kuwa kinywa chake. Pepo anaweza kuwa uso wa simba, unamkuta baba mwenye nyumba mkali kwa watoto na mkewe kumbe ni uso wa simba. Kwahiyo; pepo wanaweza kujigeuza maumbo mbalimbali kama nyani, simba, paka hata bundi ili mradi kuharibu hatma ya mtu. Mnamkuta dada aolewi kumbe uso wake umefunikwa kwa sura ya simba, kila mwanaume anayetaka kumchumbia haoni sura nzuri bali anaona simba. Na ndio maana kuna baadhi ya wadada watumia muda mwingi kujipodoa lakini bado hawapendezi kwa kuwa uso sio wa kwake.

KUNG’OA KILA KILICHOPANDWA KATIKA MWILI WAKO:
Imeandikwa kila pando asilolipanda Baba wa mbinguni litang’olewa, hivyo Mungu ametupa mamlaka ya kung’oa kila pando la kishetani yaliyopandwa katika mwili. Miili yetu ni Hekalu la Roho Mtakatifu hivyo shetani hatakiwi kugusa sehemu yoyote ya mwili wako.

Tumia mamlaka yako kung’oa kila pando ambalo shetani amepanda katika maisha yako mapando ya magonjwa, homa zisizoisha, ukimwi, mwasho wa mwili na matatizo mbalimbali. Jina la Yesu lina mamlaka yote dhidi ya kazi zote za shetani katika maisha yako. 

SAFARI YA KUZIMU NA KUMBUKA NENO HILI ''MUDA UNAISHA HARAKA SANA''



Monday, December 17, 2012

SAFARI YA KUZIMU NA KUMBUKA NENO HILI ''MUDA UNAISHA HARAKA SANA''

Ushuhuda wa Victoria Juu ya Kuzimu


Muda Unaisha Haraka!
Huu ni ufupisho wa ushuhuda wa Victoria Nehale
Nilizaliwa na kuishi Namibia maisha yangu yote; na niliyatoa maisha yangu kwa Yesu tarehe 06 Februari 2005. Bwana Yesu Kristo ameshanifunulia mambo mengi katika ulimwengu wa roho ikiwa ni pamoja na safari za kuzimu. Bwana alinipa maelekezo kwamba niwashirikishe watu uzoefu wangu; pia alinionya kuwa nisiongeze wala kupunguza chochote katika vile alivyonionyesha na kuniambia. Wakati nikiandika kitabu hiki, mwishoni mwa 2006, nilishatembelewa mara 33 na Bwana Yesu Kristo. Kila aliponitembelea, Bwana alikuwa akiniambia kabla ya kuondoka: MUDA UNAISHA HARAKA!
Safari ya kwanza kuzimu
Katika wikiendi ya tarehe 23 Julai 2005, nilipanda taksi kwa ajili ya safari ya dakika thelathini kutokea mji wa Ondangwa ambako ndiko ninakofanya kazi na kuishi, hadi kijijini kwetu, kwa lengo la kwenda kuwa na wazazi wangu wakati wa wikiendi ile. Wakati nikielekea nyumbani, nilipata hisia kwamba kuna jambo lisilo la kawaida ambalo lingetokea jioni ile. Nilifika nyumbani kwenye saa 12 jioni; na hapo watu walikuwa wanaandaa chakula cha jioni. Nilikuwa jikoni pamoja na familia yetu, huku nikiwa nimelala kwenye mkeka. Watoto wa hapo nyumbani walikuwa wakiimba nyimbo zao za Shule ya Jumapili. Ghafla nilijisikia upako mzito ukinishukia; mwili wangu ukawa dhaifu sana; na nikawa nimetoka kwenye mwili kutokana na nguvu za Mungu. Nilimwona mwanamume amevaa joho jeupe refu likiwa limefungwa kwa kamba ya rangi ileile; akiwa anatembea kuelekea pale nilikokuwa nimelala. Kulikuwa na nuru imemzunguka kana kwamba ilikuwa ikitokea kwake. Alikuwa amevaa viatu vya wazi vya kahawia. Mwonekano wake ulikuwa kama wa watu wa Mashariki ya Kati, huku akiwa na ngozi nzuri ya hudhurungi. Uso wake ulikuwa mpole sana na umejaa utukufu lakini sikuweza kumtazama machoni. Alipoongea, sauti yake ilikuwa ya upole, na upendo, lakini pia  yenye mamlaka; mawimbi ya upendo yalikuwa yakitoka kwake.
Alinyoosha mkono wake kwangu na kuninyanyua kutokea pale nilipolala. Ghafla nilijiona nikiwa nina mwili mzuri sana. Nilijiona niko kama nilivyokuwa ningali na miaka kumi na nane. Nilikuwa nimevaa joho jeupe na kamba nyeupe. Japokuwa joho langu lilikuwa jeupe, lilitengenezwa kwa matirio tofauti na ya joho la yule mwanamume.  Joho lake lilikuwa la hariri huku liking’aa kiasi kwamba hata nashindwa namna ya kuelezea.
Alisema, kwa sauti ya upendo na upole sana: Victoria, nataka uende nami; nitakuonyesha mambo ya kuogopesha na ninakupekela mahali ambako haujawahi kufika katika maisha yako.” Alinishika mkono wa kulia na tukaondoka. Nilijiona kama vile tunatembea hewani na muda wote tulikuwa tukielekea tu juu. Baada ya muda, nikawa nimechoka sana, na nikamwambia kuwa nisingeweza kuendelea na safari. Hivyo nikamsihi aniruhusu nirudi. Hata hivyo, alinitazama kwa upendo na kusema, “Haujachoka – uko sawa tu. Kama ukichoka, nitakubeba, lakini kwa hivi sasa uko tu sawa. Amani iwe kwako. Tuendelee.”
Tulifika mahali ambako ni pakavu sana; pakavu kuliko jangwa lolote analojua binadamu; hakukuwa na dalili zozote za uhai. Hakukuwa hata na mti mmoja au hata jani au kiumbe chochote hai. Lilikuwa ni eneo linalofadhaisha sana.
Hatimaye tulifika kwenye geti moja na yule mwanamume alinigeukia na kusema: “Victoria, tutaingia kupitia geti hili na mambo ambayo utayaona yatakuogopesha na kukufadhaisha – lakini uwe na uhakika kuwa kokote nitakakokupeleka, utakuwa na ulinzi mkamilifu. Wewe fungua tu macho yako na kutazama kila nitakachokuonyesha.” Nilijawa na hofu na kuanza kulia. Nilikuwa nalalamika na kumwomba anirudishe. Nilimwambia kuwa sikutaka kuingia kwenye sehemu ile maana tayari nilikuwa naona kupitia getini kile kilichokuwa kikiendelea ndani. Aliniangalia na kusema,  “Amani iwe nawe; niko pamoja nawe. Ni lazima tuingie ndani, maana muda unakimbia haraka.”
Tuliingia kupitia getini. Siwezi kukusimulia utisho wa mahali pale. Nina uhakika kabisa kuwa hakuna sehemu yoyote ulimwenguni ambayo ni mbaya kama ile! Sehemu ile ilikuwa ni kubwa sana na nilipata hisia kuwa inaendelea kupanuka muda wote. Ilikuwa ni sehemu ya giza totoro na joto lake halipimiki; ilikuwa ni joto kuliko moto ulio mkali kabisa. Sikuona miali yoyote ya moto au chanzo cha joto lile lakini kulikuwa ni JOTO! Kulikuwa na wadudu wa kila ukubwa; wa kijani, weusi, na wa kijivu - ila aina ya wadudu unaoweza kuwafikiria. Zaidi ya hapo, kulikuwapo pia kila mahali funza wafupi, wanene, weusi, ambao wanapanda juu ya kila kitu. Walianza kupanda juu yetu na wadudu nao walikuwa wametuzunguka kila upande. Mahali pale kulikuwa na harufu mbaya mno; hakuna maneno ya kutosha kuelezea harufu ile. Harufu ilikuwa kama nyama iliyooza lakini ilikuwa ni mbaya mara mia zaidi ya nyama iliyooza  niliyowahi kunusa maishani mwangu mwote! Kulikuwa na kelele za vilio na kusaga meno, pamoja na vicheko vibaya vya mapepo.
Kibaya kabisa kwenye sehemu hii ni kuwa pamejaa watu. Walikuwa ni wengi sana kiasi kwamba hawahesabiki. Walikuwa ni mifupa tu. Ninaweza kusema kwa ujasiri na uhakika kabisa kwamba mifupa hii ilikuwa ni wanadamu kwa vile niliweza kuwatambua baadhi ya ndugu zangu wa karibu na watu kutoka kijijini kwangu. Mifupa yao ilikuwa ya kijivu cheusi na mikavu sana. Walikuwa na meno marefu makali kama wanyama wa porini. Midomo yao ilikuwa mikubwa na mipana na ndimi zao zilikuwa ndefu na nyekundu sana. Mikono na miguu yao ilikuwa na vidole vyembamba virefu, na kucha kali, ndefu. Baadhi yao walikuwa na mikia na pembe.
Kulikuwa na mapepo yakichanganyika na watu: mapepo yalionekana kama mamba na yalitembelea miguu minne. Yalionekana yanajisikia vizuri tu kwenye mazingira yale na mara zote yalikuwa yakiwachokoza na kuwatesa wanadamu. Kelele kutoka kwa yale mapepo zilikuwa ni kama vile yako kwenye sherehe; maana yalionekana yana furaha. Yalikuwa pia yakicheza na kurukaruka muda wote. Wanadamu kwa upande wao, walionekana wana mateso na fadhaa; walikuwa katika hali ya kukosa msaada. Kelele za wanadamu zilisababishwa na maumivu. Walikuwa wakilia, wakipaza sauti na kusaga meno yao; na walikuwa katika hali ya mateso makali yasiyo na mfano.
Watu katika sehemu ile, walikuwa ni wengi mno, lakini niliweza kuona kuwa wengi wao walikuwa wanawake. Waligawanyika katika makundi mbalimbali. Japokuwa walikuwa katika makundi, ilikuwa haiwezekani kukadiria idadi yao katika kundi lolote maana makundi yenyewe yalikuwa ni makubwa kupita kiasi!
Mwanamume yule alinipeleka hadi kwenye kundi mojawapo upande wa mashariki wa sehemu ile. Kisha alinitazama na kusema: “Victoria, hili ni kundi la watu ambao walikataa kuwasamehe wengine. Niliwaambia mara nyingi na kwa njia nyingi kuwa wawasamehe wengine lakini walinikataa; Mimi nimewasamehe wao dhambi zao zote lakini wao walikataa kuwasamehe wengine. Muda wao uliisha na wakajikuta wako hapa. Watabakia hapa milele yote; wanakula matunda ya kazi yao milele na milele. Hata hivyo, inaniuma sana kuwaona kwenye sehemu hii mbaya na katika sehemu hii ya milele – maana ninawapenda.”
Nilipelekwa kwenye kundi linalofuata, na mwanamume yule aIiniambia kuwa watu wa kundi lile la pili walikuwa ni wale waliokuwa na madeni: walikuwa na uwezo wa kulipa madeni yao lakini waliendelea kuahirisha. Walikuwa wakisema kuwa tutalipa kesho, wiki ijayo, mwaka ujao, hadi muda ukawaishia. Hapa ndipo watakaa milele; wanakula matunda ya kazi yao. 
Aina ya pili ilikuwa ni ya wale ambao walikuwa na madeni na walikuwa na uwezo wa kuyalipa; na walikuwa tayari kuyalipa, lakini walikuwa wakiogopa matokeo maana, labda, kama wangesema kweli, wangeishia kukataliwa, au wangefungwa, au labda kile ambacho walitenda kingejulikana duniani kote nao wangeaibika. Yule mwanamume akasema:  “Hakuna kati yao ambaye alinijia kuniomba njia ya kufanya. Kama wangeniomba, ningewaonyesha njia rahisi kabisa ya kutoka kwenye hali zilizowakabili. Muda wao uliisha na wakajikuta wako hapa ambako ndiko watakuwako milele. Wanakula matunda ya kazi zao.”
Kisha akasema: “Kundi la tatu walikuwa na madeni ambayo hawakuwa na uwezo wa kuyalipa, lakini pia, nao hakuna hata mmoja ambaye aliniambia kuwa ana deni asiloweza kulipa. Kama wangefanya hivyo, ningewalipia madeni yao. Pia, walijaribu kutumia ufahamu wao na hekima yao, kitu ambacho hakikuwasaidia kwa njia yoyote. Hivi sasa wamejikuta mahali hapa ambako ndiko watakakoku. Wanakula matunda ya kazi yao. Moyo wangu unauma kwa ajili ya watu hawa wote maana ninawapenda sana.”
Katika kundi la kwanza, niliwaona ndugu zangu wawili wa kike wa karibu sana pamoja na mtoto wa miaka kumi na mbili, naye pia akiwa ndugu yangu. Nilijua alikuwa na miaka kumi na mbili maana huo ndio ulikuwa umri wake wakati anakufa. Katika kundi la pili nako pia niliwaona baadhi ya ndugu zangu, pamoja na Mchungaji ambaye nilimfahamu vizuri sana. Rafiki yangu wa kiume, Jakes, ambaye alijiua kwa sababu mimi niliamua kumpa Kristo maisha yangu, naye alikuwa kwenye kundi la pili. Niliwaona baadhi ya majirani zangu kwenye makundi yote pia.
Niliwatambua watu niliowajua kabla ya kufa kwao; nao pia walinitambua. Ndugu zangu walijawa na hasira sana waliponiona na wakaanza kunitukana. Walikuwa wakitumia lugha chafu kabisa wakati wakinitukana. Mmoja wao alisema kuwa sikustahili kumfuata mwanamume yule ambaye nilikuwa naongozana naye; walikuwa wakiongelea mambo ambayo nilikuwa nikiyafanya kabla ya kutoa maisha yangu kwa Kristo. Hawakuwa wakisema uongo. Mambo waliyokuwa wakinituhumu nayo yalikuwa ya kweli. Jakes alikuwa akisema kuwa mimi nilikuwa wa kwake na kwamba nilitakiwa kwenda pale alipokuwa maana nilitenda dhambi zilezile kama alizotenda yeye. Mara ya kwanza, yule mchungaji alionekana amefurahi kuniona na akasema nimefanya vema kuja, lakini alibadilika ghafla pale alipomwona yule niliyekuwa nimeongozana naye; kisha naye akajiunga na wale waliokuwa wakinilaani kwa matusi. Mwanamume yule aliyekuwa nami akaniambia nisiwajali maana hawajui walitendalo.
Nilipigwa na bumbuazi na kujawa na huzuni kubwa sana. Mwili wangu ulikuwa ukitetemeka na sikuweza kusimama. Nilikuwa nikilia bila kuweza kujizuia. Mwanamume yule alinigeukia, akanikumbatia, na kusema: “Amani iwe nawe, Victoria.” Nguvu zangu zilinirejea na nikajisikia salama mikononi mwake. Kisha akaniambia kuwa tulitakiwa kuondoka pale na kurudi. Alinitazama na kusema: “Victoria, nimeshakuonyesha. Sasa inabidi uchague ni kundi lipi unataka kuingia; uchaguzi umo mikononi mwako. Ni lazima uwaeleze watu kila kitu ulichokiona lakini usiongeze au kupunguza chochote.”
Nakumbuka kuwa tuliondoka pamoja kwenye ile sehemu ya kutisha lakini sikujua nimemwacha wapi maana fahamu zangu za kawaida zilinirudia. Nilifungua macho yangu na kujikuta kwenye mwili wangu wa nyama, huku nikiwa nimelazwa kwenye Hospitali ya Oshakati. Nilikuwa nimetundikiwa dripu kwenye mkono wangu wa kushoto; na nilimwona mama yangu na ndugu zangu wengine wa kijijini kwenye kona moja ya chumba, ambako walikuwa wakiniangalia kwa mshangao. Niliona kwenye uso wa mama yangu kwamba alikuwa analia. Nilimwuliza nesi mmojawapo kama alikuwa anafahamu tatizo langu lilikuwa nini lakini alinifanyia tu mzaha na kusema: “Umerudishwa. Labda ulifanya kosa fulani na unatakiwa kutubu.” Nesi alikuwa anajaribu kuelezea kwa lugha nyepesi namna hali yangu ilivyokuwa, lakini nilibaini kuwa alikuwa anaogopa kunikaribia. Nilimwomba aniitie daktari aliyenihudumia. 
Daktari alipofika, alisema kuwa hakujua kulikuwa na tatizo gani kwangu. Mwanzoni, alidhani kuwa nilikuwa na malaria lakini vipimo vilionyesha kuwa sikuwa nayo. Aliendelea kunieleza kuwa joto langu, mapigo ya moyo, na shinikizo la damu vilikuwa chini sana kwa viwango vya hatari lakini hakuweza kujua sababu yake. Alisema kuwa hakuwa na cha kufanya tena kwa ajili yangu. Hakuweza hata kuniandikia kulazwa maana sikuwa na ugonjwa. Dripu waliyoniwekea ilikuwa haifanyi kazi mwanzoni, lakini nilipofungua tu macho yangu, ikaanza kufanya kazi. Alipendekeza kuwa nesi aniwekee dripu nyingine mara ile ya kwanza itakapoisha ili niweze kupata nguvu za kutosha kwenda nyumbani. 
Niliogepeshwa na kile nilichoona mahali pale na sikuweza kujizuia kulia. Harufu mbaya ya pale iliendelea kuwa halisi kama nilipokuwapo hapo. Taswira za pale ziliendelea kunijia wakati wote. Nilishindwa kulala na mwili wangu wote ulihisi maumivu makubwa. Nilijihisi kana kwamba miguu na mikono yangu ilinyofolewa na kurudishiwa tena. Ah, nilijisikia vibaya sana. Nilikuwa na tumbo la kuendesha na kichwa kiligonga kwa wiki nzima.
Niliamua moyoni mwangu kwamba nisingemweleza mtu yeyote juu ya kile nilichoona maana ni nani kwanza angeniamini? Watu watanielewaje? Niliendelea kujiambia kuwa sitamweleza kamwe mtu yeyote juu ya mambo hayo. Mmoja wa washauri wangu alinipigia simu siku tatu baadaye kuulizia kuhusu hali yangu maana nilikuwa nimemtumia meseji aniombee. Bila kujitambua, nilijikuta nikimsimulia kuhusu yaliyonikuta. Niliposhtuka, tayari nilishamweleza karibu kila kitu. Nilitamani kujipiga mateke. Nilikuwa nalia kwa kuwa niliamini kuwa nimefanya kosa kubwa kabisa maishani mwangu. Sasa hadithi nzima ilikuwa wazi; hakukuwa na uwezekano wa kuificha tena. Sasa najua kuwa kama Mungu akitaka jambo fulani lielezwe, lazima litaelezwa. Maana yeye si ni Mungu?
***********
Agosti 19, niliamka huku nikijisikia hali ya upako kwenye mwili wangu wa nyama. Nilikuwa dhaifu na kutetemeka, huku mawimbi ya umeme yakipita kwenye mwili wangu. Jioni, niliona mwanga mkali ukija chumbani kwangu, na katikati yake, alikuwa yuleyule mwanamume. Safari hii alikaa chini kwenye kiti karibu na kitanda changu. Hata sielewi kiti hiki kilitoka wapi lakini kilikuwa pale mara tu alipokuwa tayari kukaa. Kilikuwa ni kiti kizuri cha dhahabu tupu. Umbo lake lilikuwa la kiti cha kawaida, kikiwa na sehemu ya kuegemeza mgongo. Kwenye kila mguu kulikuwa na nyota ya madini ya fedha iliyopachikwa kwenye dhahabu ile; nyota ileile ilikuwa pia katikati ya sehemu ya nyuma ya kuegemeza mgongo. Kulikuwa na magurudumu kwenye kila mguu.
Baada ya kunisalimia, aliniambia kuwa alijua kuwa nina maswali mengi kuhusu yeye ni nani; hivyo alikuja kujitambulisha kwangu na kufafanua mambo kadhaa ambayo tayari nilikuwa nimeyapitia. Alisema: “Mimi ni Yesu Kristo, Mwokozi wako. Kama una mashaka yoyote, tazama mikono yangu. Mahali pale ambako tulienda, ni Kuzimu.” Nilipoangalia mikono yake, niliona makovu ambamo misumari ilimtoboa.
Rafiki, napenda nikueleze kuwa kuzimu si sehemu ya kufikirika tu mawazoni; lakini ni mahali halisi na si kuzuri hata kidogo. Ni mahali ambako hakukutengenezwa kwa ajili ya wanadamu bali kwa ajili ya shetani na mapepo yake. Sehemu inayotustahili ni Mbinguni pamoja na Yesu lakini inatubidi tumchague Yesu kabla hatujachelewa. Leo, unapoisikia sauti yake, usifanye moyo wako kuwa mgumu; mkubali Yesu awe Mwokozi wako binafsi kisha uishi kwa ajili yake. Kuzimu ni kubaya mno: ni sehemu ya hofu na huzuni; ni sehemu ya mateso na vilio vya milele na kusaga meno. Shetani anataka awachukue watu wengi kadiri iwezekanavyo ili aende kule pamoja nao. Usishirikiane naye; shirikiana na Yesu nawe, badala ya kufa, utaishi.
Sikuelewa kwa nini Bwana aliniambia nichague kati ya makundi mawili aliyonionyesha kule kuzimu ilhali mimi tayari nilikuwa Mkristo niliyeokoka. Nimeshamkubali maishani mwangu lakini bado alikuwa akiniambia nichague kama nataka kwenda kuzimu au la! Sikuweza kuelewa. Nilianza kuomba na kumwuliza Mungu anipatie ufunuo juu ya kile alichomaanisha na ni nini anataka nifanye. Bwana alinifunulia kuwa nilikuwa nimeficha roho ya kutosamehe na chuki moyoni mwangu kwa sababu ya dada yangu mmoja, pamoja na binamu yangu mmoja. Nilimwomba Bwana anisamehe kutokana na kutosamehe kwangu. Pia nilimwomba dada yangu anisamehe kwa kuweka hasira na uchungu moyoni mwangu kwa ajili yake. Bwana alinielekeza niende pia nikamwombe msamaha binamu yangu.
Bwana pia alinikumbusha kuwa kulikuwa na wakati ambapo nilipata kazi ya ualimu kwa kutumia cheti cha diploma cha uongo na alihesabu hilo kuwa ni deni na wizi. Nilikusudia kutenda kilicho sahihi na nilimwomba anisaidie kutoka kwenye tatizo hili na anionyeshe njia rahisi ya kutoka humo maana hili lilikuwa ni kosa kubwa na lingeweza kunifannya nifungwe. Alinielekeza niende kwenye Idara ya Elimu nikakiri kosa nililofanya. Nilikuwa tayari kwenda jela kama ingebidi. Nilipata upendeleo wa Bwana kwa kiasi kikubwa sana. Nilipofika kule, mhusika kwenye Idara ya Elimu aliniambia niamue kile ninachotaka kufanya: ama kulipa mshahara ambao nilipokea kutoka serikalini au la. Waliahidi kuwa hawatanishtaki maana walishangazwa na kitendo changu cha kwenda kukiri kosa lile. Mungu wetu ni Mungu mwaminifu ambaye analiheshimu Neno lake.
Kama uko kwenye hali inayofanana na niliyokuwa nayo, napenda nikutie moyo kuwa utende kile kilicho sahihi, bila kujali matokeo. Unaweza kufungwa kwenye jela ya kidunia lakini hiyo ni ya muda tu. Hakuna maumivu au aibu inaweza kulinganishwa na kutengwa na Mungu milele. Kuzimu si mahali pazuri: ni bora kumruhusu Mungu akuhukumu sasa kabla hujachelewa. Hatutakiwi kuogopa hukumu ya Mungu tungali bado kwenye kipindi cha Neema; ni lazima tumruhusu afunue chochote kisicho sawa kwenye maisha yetu tungali bado na muda wa kuweka mambo sawa naye, maana hakuna msamaha upande wa pili wa kaburi.
Safari ya pili kuzimu
Oktoba 18, 2005, niliamka saa 11:30 asubuhi lakini sikuweza kwenda kazini. Nilijisikia hali ya udhaifu sana na  kulewa; sikuweza kusogea au kugeuka kitandani kwangu; na uwepo wa Bwana ulikuwa mzito sana chumbani. Nilikuwa natetemeka na nikahisi kama umeme ukipita mwilini mwangu. Bwana alinijia kabla tu ya saa 2:00 maana kwa mara ya mwisho nilipotazama saa ilikuwa ni saa 1:48; na Yeye alifika muda mfupi tu baada ya hapo. Alinisalimia na kusema kuwa tunatakiwa kwenda tena maana muda unaisha haraka sana. Nilisimama na tulianza kutembea. Utembeaji wa safari hii ulikuwa tofauti kabisa na safari zingine zote. Japokuwa miguu yetu ilikuwa inafanya kitendo cha kutembea, tulikuwa kama vile tunaelea zaidi kuliko kutembea. Wakati tukiwa njiani, Yesu aliniambia kuwa dhambi zote ni mbaya na hakuna kitu kama dhambi ndogo au dhambi kubwa. Dhambi zote mwisho wake ni mauti - ziwe kubwa au ndogo. Bwana aliniambia kwamba tunaenda kutembelea kuzimu tena na akaniuliza iwapo nilikuwa nina hofu. Nilimjibu kuwa nilikuwa nayo.
Alisema, Roho ya woga haitoki kwa Baba yangu au kwangu; inatoka kwa Ibilisi. Woga utakusababisha utende mambo ambayo yatakupeleka kuzimu.” 
Bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu na hofu ni kinyume kabisa cha imani. Ni wazi kuwa hofu haimpendezi Mungu kwa kuwa inaharibu imani yetu. Muda wote tulipokuwa njiani, tulikuwa tunatembea kila mmoja peke yake. Lakini mara tu tulipofika kwenye lango la kuzimu, alinishika mkono wangu kwa mkono wake wa kulia kwa muda wote tuliokuwa kuzimu. Nilifurahi sana kwa Bwana kunishika mkono maana kwa namna alivyokuwa amenishikilia kwa nguvu, hofu yote ilitoweka. Sehemu ile ilikuwa bado iko vilevile: hakukuwa na tofauti na ilivyokuwa mwanzo. Kulikuwa na wadudu, funza, joto kali sana, harufu, mifupa, kelele: kila kitu kilikuwa kama mwanzo nilipoenda pale. Tulipita tena kwenye geti lilelile baya na Bwana akanipeleka kwenye kundi moja la watu. Kulikuwa na watu wengi niliowafahamu wakati wangali duniani. Maskini, walikuwa kwenye hali mbaya sana. Walionekana ni wenye taabu na maumivu makubwa; lakini baya zaidi ilikuwa ni nyuso zao zisizo na matumaini kabisa.  
Bwana alimwonyesha mwanamke mmoja wa makamo ambaye nilimfahamu kabla hajafa. Alikufa kwa ajali ya gari mwanzoni mwa mwaka 2005. Nilipigwa na butwaa kumwona pale maana sote tulimjua kuwa ni mtu aliyekuwa na hofu ya Mungu na aliyempenda Mungu. Bwana aliniambia kuwa mwanamke yule alimpenda na Yeye Bwana naye alimpenda; alimwokoa angali akiwa duniani; aliwashuhudia wengi ambao walimwijia Bwana na alifahamu Neno vizuri sana. Alikuwa mkarimmu kwa maskini na wahitaji; aliwapatia walichohitaji, na kuwasaidia kwa njia nyingi. Alikuwa ni mtumishi mzuri wa Bwana kwa namna nyingi.
Maneno hayo ya Bwana yalinishitua hata zaidi; nami nikamwuliza kwa nini amwache mtu kama huyo aliyemtumikia kwa kiasi kikubwa hivyo aingie kuzimu? Bwana alinitazama na kusema kuwa mwanamke yule aliamini uongo wa Ibilisi. Japokuwa aliyajua Maandiko vizuri, aliamini uongo wa ibilisi kwamba kuna dhambi ndogo na kubwa. Alidhani kuwa dhambi ‘ndogo’ zisingempeleka kuzimu, maana alikuwa Mkristo hata hivyo.
Bwana aliendelea kusema, “Nilimwendea mara nyingi na kumwambia aache kile alichokuwa anakifanya lakini mara nyingi alijenga hoja akilini mwake kuwa kile alichokuwa anakifanya kilikuwa ni kidogo sana na alichukulia kuwa yale maonyo yangu yalikuwa ni hisia zake tu za hatia. Kulikuwa na muda ambapo aliacha kwa muda lakini baadaye alijishawishi tena kuwa maonyo yale hayakuwa yanatoka kwangu, bali ni sauti yake tu kwa kuwa aliona kuwa dhambi ile ilikuwa ni ndogo sana kuweza kumhuzunisha Roho Mtakatifu.”
Nilimwuliza tena Bwana ili aniambie ni dhambi gani basi mwanamke yule alitenda. Alinijibu kwamba, “Mwanamke huyu alikuwa na rafiki ambaye alikuwa nesi kwenye Hospitali ya Oshakati. Kila mwanamke huyu alipoumwa, hakwenda hospitali na kulipa kwa ajili kadi yake kama inavyotakiwa kwenye taratibu za kawaida; badala yake yeyé alipiga tu simu na kumwambia rafiki yake amfanyie mipango ya dawa kutoka kwenye  Zahanati ya Hospitali. Na mara zote rafiki yake yule alikubali na kumwambia kuwa apite pale muda fulani kuchukua dawa. Kwanza, aliamua kukubali uongo wa ibilisi juu ya kuwapo kwa dhambi kubwa na ndogo na kuikataa kweli yangu; alimsababisha mtu mwingine atende dhambi na kuiba kwa niaba yake, lakini kibaya zaidi, ALIMHUZUNISHA ROHO MTAKATIFU. Hicho ndicho kilichomfanya afike kuzimu. Haijalishi kwamba utaleta mamilioni ya roho kwa Bwana; bado upo uwezekano wa kuingia kuzimu kutokana na kumhuzumisha Roho Mtakatifu. Si tu kwamba ni lazima ujali wokovu wa wengine lakini pia ni lazima uwe mwangalifu usije ukasahau roho yako. Kuwa makini na Roho Mtakatifu wakati wote.” Baada ya maneno hayo, Bwana alisema ni wakati wa kurudi.
************
Wakristo wengi waliosikia hadithi yangu hii huiona kama ina matatizo. Mara nyingi huwa wanniuliza, “Vipi kuhusu kuhesabiwa haki, rehema, na neema?” na pia “Inawezekana kweli kupoteza Wokovu wako baada ya kuwa umeupokea?” 
“Huko si kuvuka kiwango?”
“Mungu anaweza kuwa mkatili kiasi hicho?”
Kama nilivyosema kwingineko kwenye kitabu hiki, mimi siongei theolojia yangu hapa. Ninasema tu kile ambacho Bwana alinionyesha na kunifundisha – na kile alichoniruhusu kukishuhudia. Tafadhali someni Biblia zenu ili kupata majibu. Tazama aya zifuatazo, kisha uhukumu mwenyewe.
“…bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.” (1Wakorintho 9:27)
Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?
Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? (Warumi 6:1-2)
Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake.” (Warumi 6:12)
Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. (Waebrania 10:26 –27)
Unasema, “Je, naweza kwenda kuzimu baada ya kuwa nimemtumikia Bwana na kuwaleta wengi kwa Kristo?” Hukumu mwenyewe!
Kutokutii
Jumatatu ya tarehe 6 Machi 2006, niliamshwa na saa ya kengele saa 11:30. Nilianza kuomba na nikatambua kulikuwa na upako mzito juu yangu. Mwili wangu ulikuwa dhaifu na nilikuwa nikitetemeka; mawimbi ya umeme yalikuwa yanapita kwenye mwili wangu.
Wakati wa mchana, nikiwa nimelala kitandani, niliona nuru nyeupe ikijaza chumba changu. Niliona shanga ndogondogo, nyeupe, za duara, zenye ukubwa wa kichwa cha pini. Shanga hizi zilikuwa zikianguka kama mvua inavyonyesha na zilipogusa ngozi yangu, zilizama ndani. Zaidi ya hapo, niliona kama wingu linalofanana na ukungu mweupe likija kutokea juu. Nalo pia lilikijaza chumba na likawa likizama kwenye ngozi yangu kila liliponigusa. Baada ya hapo, nilimwona Yesu akitembea katikati ya lile wingu la ukungu kuelekea pale nilipokuwa. Alikaa kwenye kiti chake pembeni mwa kitanda changu. Hata sielewi kiti hiki kinatokea wapi; huwa kinatokea tu mara anapokuwa tayari kukaa.  Ni kiti kizuri kilichotengenezwa kwa dhahabu. Umbo lake ni kama la viti vingi tunavyovifahamu lakini kina sehemu ya kuegemeza mgongo. Kwenye kila mguu kuna nyota ya fedha; na nyota nyingine ya aina ileile, japo ni kubwa zaidi, iko kwenye sehemu ya kuegemea. Kuna magurudumu kwenye kila mguu.
Yesu alinisalimia na akaninyooshea mkono wake na kuniambia niamke maana muda unakimbia haraka sana. Alinivuta mkono wangu nami nikainuka na kukaa kitandani kwangu.
Kisha akaniambia, Victoria, tuombe.” Aliomba kwa lugha ambayo siielewi; nilielewa neno moja tu ‘Amen’. Kisha aliendelea kwa kuniuliza nilikuwa naona nini nami nilimwambia kuwa nilikuwa naona kundi la watu wakienda kazini kwao na wengine wakirudi kutoka kazini kwao. Nilikuwa pia naona vile vishanga vyeupe vikiwaangukia wale waliofika mwanzo kazini kwao. Baada ya kundi la kwanza, kundi jingine nalo lilifika baadaye.  Wakati huo, ile mvua ya vile vishanga iliacha kunyesha.
Niliona pia makundi mbalimbali ya watu, wakiwasili kwenye makanisa mbalimbali Jumapili asubuhi. Mvua ile ingeanza kunyesha mara tu watu wa mwanzo wanapoingia kwenye uwanja wa kanisa. Iliendelea kunyesha kwa muda kisha ikasimama. Wale wanaochelewa hawakuti chochote. 
Yesu aliniuliza iwapo nilikuwa naelewa maana ya maono yale, nami nilimwambia kuwa sikuelewa. Ndipo alinifafanulia kwa kusema kwamba: “Maono haya yanamaanisha kuwa kila mahali ambako unatakiwa kuwako kwa muda fulani na wewe unajua ni wakati gani unatakiwa kuwa pale, mara zote huwa kuna malaika wanagawa baraka kwa ajili ya muda huo. Kama ukifika mapema, utapokea baraka zako, lakini ukichelewa, unakosa baraka zako kwa siku ile maana malaika hugawa baraka kwa muda ule tu. Victoria, nataka kukuonya kwa sababu huwa unaenda kazini kwa kuchelewa, na hasa huwa unaenda kanisani kwa kuchelewa. Ni lazima ujue kuwa kwa nyakati zile huwa unachelewa bila kuwa na sababu za msingi; umekuwa ukikosa baraka zako kwa siku zile; hazitakurudia tena.  Victoria, ni lazima uache jambo hili na usilitende tena, isipokuwa pale unapokuwa na sababu ya msingi ya kuchelewa.” 
Bwana alipomaliza kusema maneno yale, kwa kweli nilitamani kutoweka au angalau nimpatie sababu inayokubalika kutokana na kukosa kwangu nidhamu. Nilimwambia kuwa wakati mwingine napitiliza kulala lakini alinitazama moja kwa moja machoni na kusema kuwa nilikuwa nasema uongo na kwamba nilikuwa nina tabia mbaya ya kurudi kitandani baada ya kuwa nimeamka, ili kutimiza ile shauku ya kusema ‘ngoja nilale kidogo tu.’
Baada ya Yesu kuwa amenionya. alisema, “Simama. Tuondoke sasa. Muda unakimbia haraka sana. Kuna mambo ambayo ni lazima tuyafanye.”
Safari hii Bwana alinipeleka mahali ambako sikuwahi kufika kabla. Ilikuwa pia ni mara ya kwanza kufuata barabara tuliyotembea siku ile. Tulifika kwenye bustani iliyojaa maua mazuri na miti mizuri ya kijani. Hakuna kitu duniani kinachoweza kulingana na mahali pale. Maua yalikuwa ya kila aina ya rangi za kung’aa.  Tulikaa kwenye benchi zuri la bustanini, ambalo lilitengenezwa kwa dhahabu safi huku likiwa na nyota ndogo za madini ya fedha ya kung’aa.
Tulipokaa, alionyesha kidole mbele na kusema, “Victoria, tazama, unaweza kuona mji ule? Nilipotazama, niliona jiji kubwa sana. Lilikuwa zuri kuliko maelezo. Jiji lile lilikuwa na geti la dhahabu inayong’aa, na kwenye geti lile kulikuwa na mwanamume amekaa, mwenye umri mkubwa. Alikuwa na ndevu ndefu nyeupe na nywele nyeupe. Nilishamwona mwanamume huyo kabla; na nilipomwuliza Yesu kuwa mwanamume yule ni nani, aliniambia kuwa alikuwa ni Ibrahimu, baba wa imani.
Niliona barabara nyingi kwenye mji ule, ambazo nazo ni za dhahabu. Kuna majengo marefu, ambayo nayo yalikuwa ya dhahabu inayong’aa. Mng’ao wa mji ule hata hauelezeki!
Yesu alinigeukia na kuniuliza, Unawaza nini juu ya jiji lile?”
Nilimjibu kuwa lilikuwa ni zuri sana na nilikuwa natamani kwenda pale. Yesu alisema: “Nitakupeleka pale kama ukiendelea kuwa mtii maana hapo pia ndiko nyumba yako itakakokuwako. Uendelee tu kuwa mtii – maana ukikosa utii, Victoria, kunguru wataruka kwenye nyumba yako. Nyumba yako itakuwa makao ya bundi na viwanja vya kuchezea vya mizimu. Hata hivyo, usiogope, maana mimi niko pamoja nawe. Wewe uwe mtii tu. Kwa kila mmoja ambaye si mtii, nyumba yake itakuwa na kunguru wakiruka pale; itakuwa ni makao ya bundi na mahali pa mizimu pa kuchezea.”
Yesu ni halisi na anatupenda kwa pendo lisiloweza kuelezeka. Shauku yake kubwa ni sisi tuchague uzima na kuishi milele naye. Moyo wake unauma kwa ajili ya wale watu ambao wanakufa na kuenda kuzimu kwa vile tu wanachagua kukataa Wokovu aliowapa na badala yake wanachagua mauti.
Uwe ni Mkristo uliyeokoka au la, tafadhali siku zote kumbuka jambo hili: Muda unakimbia haraka!